Updated at: 2024-05-25 10:23:10 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga - 6 vikombe
Samli - ½kikombe
Baking Powder - ½kijiko cha chai
Maziwa- 1 kikombe
Maji -Kisia kiasi kama unga bado mzito
VIAMBAUPISHI VYA SHIRA
Sukari - 5 vikombe
Maji - 2 1/2 vikombe
Vanilla - 2 vijiko vya chai
Rangi ya orange - 1 kijiko cha chai
Iliki ya unga - 1 Kijiko cha chai
MAANDALIZI
Changanya unga wa dengu, samli, baking powder pamoja na maziwa katika mashine ya keki (cake mixer). Ukisha changanya angalia kama mchanganyiko wako umekua mwepesi kidogo kuliko wa keki, kama bado mzito basi ongeza maji kiasi. Kisha weka mafuta kiasi kwenye karai,weka na samli kikombe kimoja, weka kwenye moto wa kiasi. Mafuta yakisha pata moto, chukua kijiko kikubwa cha matundu chota mchanganyiko wako na kijiko cha kawaida tia kwenye kijiko cha matundu. Hakikisha kijiko cha matundu kiwe juu ya karai ili mchanganyiko wako uchuruzike ndani ya mafuta yalio pata moto. Pika ndani ya mafuta mpaka iwive, ila usiache ikawa brown. Toa mchanganyiko ulowiva tia ndani ya shira uliyo pika. Hakikisha shira iwe imepoa kabla ya kutia mchanganyiko huo. Endelea kupika mchanganyiko wako mpaka uishe, kila ukitoa katika mafuta hakikisha unatia ndani ya shira. Ukishamaliza wote kanda huo mchanganyiko ulokua ndani ya shira mpaka uone shira yote imekauka (yaani iwe imeingia ndani ya mchanganyiko). Tupia zabibu kavu na lozi zilizo katwa, changanya na mkono. Wacha mchanganyiko katika bakuli, funika na foil mpaka siku ya pili. Siku ya pili chukua mchanganyiko kiasi katika mkono tengeneza mviringo (round).
MAANDALIZI YA SHIRA
Katika sufuria, tia sukari, maji, iliki, vanilla na rangi. weka kwenye moto wacha ichemke mpaka itowe povu (bubbles) juu. Kisha toa povu, wacha shira kwenye moto kama dakika 3. Hakikisha shira yako iwe inanata kiasi kwenye vidole, lakini iwe nyepesi kidogo kuliko shira ya kaimati.
Updated at: 2024-05-25 10:37:56 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kuna nyama za aina mbili, nazo ni nyama nyeupe na nyama nyekundu.
Nyama nyeupe
Hizi ni nyama zitokanazo na samaki, kuku, ndege wa aina zote, bata, wadudu
Nyama nyekundu
Hutokana na ng’ombe, mbuzi, kondoo,nguruwe na wanyama wa porini.
Nyama ina virutubishi vingi muhimu kwa afya ya binadamu kama protini, vitamini na madini. Madini ya chuma yanayopatikana kwenye nyama ni rahisi sana kusharabiwa (kufyonzwa) mwilini na ni muhimu kwa kuongeza wekundu wa damu. Uwezo wa miili ya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI kuyeyusha chakula na kusharabu (kufyonza) virutubishi hupungua. Utumiaji wa nyama nyekundu kwa wingi unaweza kuwaletea matatizo hasa katika uyeyushwaji tumboni kwani nyama nyekundu si rahisi kuyeyushwa ukilinganisha na nyama nyeupe.
Hata hivyo katika nchi yetu watu walio wengi wanatumia nyama kwa kiasi kidogo sana na mara chache. Si vyema watu hawa waache kabisa nyama nyekundu. Jambo la muhimu ni kutumia njia mbalimbali ili kuifanya nyama hii iyeyushwe kwa urahisi tumboni.
Namna ya kusaidia uyeyushwaji ni pamoja n a : -
• Kutafuna vizuri au kutumia nyama ya kusaga (kwa wanaoipata). • Kupika nyama na viungo vinavyosaidia kulainisha kama vile papai bichi, limao, vitunguu saumu n.k. • Kula nyama pamoja na papai
Kwa hiyo, kwa anayepata nyama nyekundu kwa wingi, kupunguza kiasi cha nyama hiyo na kuongeza kiasi cha nyama nyeupe. Na kwa yule asiyepata nyama nyeupe, apatapo nyama nyekundu asiache kutumia kwani ina umuhimu mwilini mwake.
Updated at: 2024-05-25 10:37:42 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Maharage (beans 2 vikombe vya chai) Nazi (coconut milk kiasi) Vitunguu maji (onion 1kikubwa) Nyanya (fresh tomato 1) Kitunguu swaum (garlic paste 1/4 kijiko cha chai) Chumvi (salt kiasi) Curry powder 1 kijiko cha chai Mafuta (vegetable oil)
Matayarisho
Chemsha maharage mpaka yaive kisha yaweke pembeni. Kaanga vitunguu maji na mafuta mpaka vianze kuwa vya brown kisha weka kitunguu swaum,nyanya na curry powder. kaanga mpaka nyanya iive kisha tia maharage na chumvi kiasi. Geuza mpaka mchanganyiko uchanganyike vizuri. Baada ya hapo tia tui la nazi na ukoroge vizuri na uache lichemke mpaka liive. Baada ya hapo ipua na maharage yatakuwa tayari kwa kuliwa
Updated at: 2024-05-25 10:34:52 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Maziwa ya unga 2 vikombe
Sukari 3 vikombe
Maji 3 vikombe
Unga wa ngano ½ kikombe
Mafuta ½ kikombe
Iliki kiasi
Jinsi ya kuandaa na kupika
Paka sinia mafuta kabla ya kupika labania Katika sufuria chemsha maji na sukari pamoja na iliki mpaka inate vizuri Kisha mimina mafuta koroga Halafu mimina unga wa ngano na ukoroge haraka haraka Kisha tia unga wa maziwa, endelea kukoroga usiwe na madonge mpaka uwe rangi ya browni isiokoleza. Kisha mimina mchanganyiko kweye sinia uliyoipaka mafuta, iwache ipoe na kata kata upendavo na itakuwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:37:40 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Viazi ulaya 4 vya wastani Hoho jekundu 1/2 Hoho la njano 1/2 Hoho la kiajani 1/2 Njegere 1 kikombe cha chai Carrot 1 kubwa Broccoli kidogo Cauliflower kidogo Kitunguu 1 Nyanya 1/2 kopo Swaum/tangawizi 1 kijiko cha chakula Curry power 1 kijiko cha chakula Coriander powder 1 kijiko cha chai Tarmaric 1/2 kijiko cha chai Olive oil Chumvi 1/4 ya limao
Matayarisho
Katika sufuria isiyoshika chini kaanga vitunguu mpaka viwe vya brown kisha tia swaum/tangawizi na spice zote kaanga kwa muda mfupi kisha tia nyanya na chumvi. pika mpaka nyanya ziive kisha tia vegetable zote na vimaji kidogo sana na kisha kamulia limao, baada ya hapo punguza moto na kisha funika na zipike mpaka vegetable zote ziive na rojo ibakie kidogo. Baada ya hapo mboga yako itakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:56 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Ngogwe ½ kg Kitunguu 2 Bamia ¼ kg Karoti 2 Mafuta vijiko vikubwa 8 Maji vikombe 3 Mayai 2 Nyanya 2 Chumvi
Hatua
• Osha, menya na katakata nyanya na vitunguu. • Osha, menya na kata karoti virefu virefu. • Osha, kata ncha za bamia pande zote na kama ndefu sana kata vipande viwili. • Osha, kata vikonyo vya ngongwe, kama ni kubwa kata vipande viwili. • Kaanga vitunguu, ongeza nyanya, korogoa mpaka zilainike. • Ongeza ngogwe, karoti, bamia na chumvi, koroga mpaka zionekane kukolea rojo. • Ongeza maji vikombe 2 koroga na funikia kwa dakika 10-15 au mpaka ziive. Punguza moto. • Koroga mayai kwenye maji mpaka iwe kama maziwa, ongeza kwenye mboga na koroga polepole usiponde ngogwe wala bamia kwa dakika 5. • Onya chumvi, pakua za moto kama kitoweo.
1) Weka karai kwenye moto kiasi
2) Tia siagi
3) Tia tambi uzikaange usiachie mkoni mpaka ziwe rangu ya dhahabu.
4) Weka lozi na zabibu huku unakoroga
5) Tia maziwa na huku unakoroga usiachie mkono.
6) Tia arki
7) Epua karai, tumia kijiko cha chai kwa kuchotea na utie kwenye kikombe cha kahawa nusu usikijaze.
8) Kipindue kwenye sahani utoe kileja.
9) Fanya hivyo mpaka umalize vyote.
Updated at: 2024-05-25 10:37:48 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Tango 1/2 Kitunguu 1/2 Cherry tomato 8 Lettice kiasi Green olives kidogo Black olives kidogo Hoho jekundu 1 Carrot Giligilani kidogo
Salad dressing Yogurt 1/2 kikombe Swaum 1/2 kijiko cha chai Limao 1/2 Pilipili ya unga 1/4 kijiko cha chai Chumvi kidogo Olive oil kiasi
Matayarisho
Osha vitu vyote kisha vikaushe maji. Baada ya hapo ktk bakuli kubwa katakata, lettice, tango,hoho, kitunguu,giligilani na kisha ikwangue carrot na utie bila kusahau nyanya zote pamoja na olives.Baada ya hapo ichanganye vizuri, kisha tengeneza salad dressing kwa kuchanganya vitu vyote vilivyo (kwenye list ya salad dressing) kisha koroga vizuri.Baada ya hapo ichanganye na salad.Na hapo salad yako itakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuila na chochote upendacho kama vile chips, nyama choma au au chakula kikuu.
Updated at: 2024-05-25 10:34:41 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Maziwa ya unga - 2 vikombe
Sukari - 3 vikombe
Maji - 3 vikombe
Unga wa ngano - ½ kikombe
Mafuta - ½ kikombe
Iliki - kiasi
MAPISHI
Paka sinia mafuta kabla ya kupika labania Katika sufuria chemsha maji na sukari pamoja na iliki mpaka inate vizuri Kisha mimina mafuta koroga Halafu mimina unga wa ngano na ukoroge haraka haraka Kisha tia unga wa maziwa, endelea kukoroga usiwe na madonge mpaka uwe rangi ya browni isiokoleza. Kisha mimina mchanganyiko kweye sinia uliyoipaka mafuta, iwache ipoe na kata kata upendavo na itakuwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:34:41 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga - 3 Vikombe vya chai
Siagi - 250 gms
Baking powder - 3 Vijiko vya chai
Mayai - 2
Chumvi - 1 kijiko cha chai
Maziwa - 1/2 Kikombe
Pilipili manga ya unga 1 Kijiko cha chai
MAANDALIZI
Katika bakuli la kusagia (blender) au mashine ya keki, tia siagi, chumvi na mayai, piga mpaka iwe kama malai (cream). Tia Unga, baking powder, pilipili manga. Tia maziwa. Kata usanifu (design) unayotaka na sokota au kunja kwa usanifu unaopenda. Pika (bake) katika moto wa 350º C – usiviache vikawa rangu ya udongo (brown) sana.