Jinsi ya kuongeza kiasi cha utokaji wa maziwa kwa kina mama wanaonyonyesha na kwa afya ya mtoto
Updated at: 2024-05-25 10:35:28 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Maziwa ni chakula kikuu cha mtoto punde anapozaliwa. Mama anahitaji kuwa na Maziwa ya kutosha ili mtoto aweze kuwa na afya. Zipo sababu mbalimbali zinazopelekea wakina mama wengi kushindwa kuzalisha maziwa mengi kwa ajili ya kuwanyonyesha watoto zao. Hata hivyo kama wewe ni mama na una tatizo hilo basi unatakiwa kufanya yafuatayio ili utengeneze maziwa kwa wingi;
Nyonyesha angalau mara nane kwa siku. Kadri unavyonyonyesha, ndivyo utatengeneza maziwa zaidi.
Epuka kukosa mlo wowote wa siku.
Iwapo baba na wanafamilia wengine watasaidia na kazi zingine za nyumbani, mama atamhudumia mtoto vizuri zaidi.
Usiache maziwa yako kujaa kwa muda mrefu. Hata kama uko mbali na mtoto hakikisha unakamua maziwa.
Updated at: 2024-05-25 10:35:00 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
NI muujiza! Pengine hivyo ndivyo yeyote anaweza kusema pindi akisikia kwa mara ya kwanza juu ya namna mihogo mibichi na nazi kavu maarufu kama mbata vinavyoweza kuwasaidia watu kiafya, na hasa wanaume.
Uchunguzi uliofanywa kwa siku kadhaa ukihusisha mahojiano na baadhi ya madaktari na pia maandiko yatokanayo na tafiti mbalimbali, umebaini kuwa mihogo na nazi mbata ambavyo huuzwa kwa wingi na kina mama jijini Dar es Salaam, vina uwezo mkubwa wa kurejesha heshima kwa kina baba mbele ya wenzi wao kwa kuimarisha uwezo wa kushiriki tendo la ndoa.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo, imebainika kuwa uwezo wa mihogo na nazi mbata katika kuwasaidia wanaume kwenye ushiriki wa tendo la ndoa hutokana na wingi wa virutubisho vilivyomo, hasa madini ya Zinc na Potassium (kwenye mihogo mibichi) na kiambata cha selenium kinachopatikana kwenye nazi mbata.
âVyakula hivi vina maajabu makubwa kwa afya ya kina baba⌠vinapoliwa kila mara na tena kwa kuzingatia usafi, huwasaidia wengi katika kuimarisha nguvu zao za tendo la ndoa na hivyo kuwapa heshima kwa wenzi wao,â mtaalamu mmoja wa masuala ya lishe jijini Dar es Salam aliiambia Nipashe.
Ofisa Utafiti wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Walbert Mgeni, alisema mihogo mibichi na nazi kavu (mbata) ni vyakula ambavyo vimethibitika kitaalamu kuwa husaidia kuiamrisha nguvu za tendo la ndoa kutokana na madini mbalimbali yanayopatikana, na hasa Zinc.
Alisema ni kwa sababu hiyo, anaamini ndiyo maana kuna kina baba wengi hutumia bidhaa hizo jijini Dar es Salaam na kwingineko nchini huku wauzaji wake wakubwa wakiwa ni kina mama.
âKuna uvumi mwingi kuhusu faida za mihogo mibichi na nazi kavu kwa wanaume. Wengi huhusisha na masuala ya tendo la ndoaâŚukweli ni kwamba wanaozungumzia suala hilo wako sahihi ingawa wanaweza kuwa siyo wataalamu.
Vitu hivyo vina madini mengi yakiwamo ya Zinki ambayo husaidia kurutubisha mbegu za kiume na kuongeza nguvu za kiume kwa mtu anayekula kwa usahihi na kwa muda mrefu,â alisema Mgeni.
Alisema zaidi ya kuimarisha mfumo wa uzazi kwa wanaume, mihogo mibichi na mbata vina faida nyingine nyingi mwilini mwa walaji ikiwa ni pamoja na kuimarisha milango ya fahamu, kusaidia uponaji wa vidonda vya ndani na nje ya mwili, kutunza ngozi na kuilinda, nywele na pia kusaidia uponaji wa matatizo mengi ya macho.
MUUJIZA ZAIDI
Dokta John Kimai wa Kituo cha Afya cha Arafa kilichopo Kimara jijini Dar es Salaam alisema ni kweli mihogo mibichi na nazi mbata husaidia kuiamrisha afya za walaji katika maeneo mengi ikiwamo via vya uzazi.
Aidha, alisema faida nyingine kiafya, hasa kwenye nazi mbata ni kuepusha matatizo ya moyo yatokanayo na wingi wa lehemu kwa kuwa nazi aina hiyo huwa na kiwango kikubwa cha kiambata kiitwacho âlauric acidâ.
Alisema faida nyingine ya nazi mbata ni kusaidia mlaji kuepukana na athari za kuvimbiwa, kuongeza nguvu za mwili kutokana na mafuta yake kuelea kwa kiasi kidogo kwenye damu (medium chain triglycerides â MCT) na hivyo huyafanya kusafirishwa moja kwa moja hadi kwenye ini ambako hutumika kama chanzo cha haraka cha nguvu.
Aidha, kwa mujibu wa Dk. Kimai, mbata husaidia pia kuimarisha kinga dhidi ya maradhi mbalimbali kutokana na uthibitisho wa tafiti mbalimbali kuthibitisha kuwa âlauric acidâ hubadilishwa kuwa acid inayojulikana kama âmonolaurinâ. Aidha, nazi kavu husaidia pia kuzisisimua seli na shughuli za ubongo na kwa kufanya hivyo husaidia kuzuia matatizo ya akili (dementia) na upotezaji wa kumbukumbu (Alzheimer).
Akielezea kuhusu faida za mihogo mibichi, daktari mwingine alisema kuwa ina madini mengi pia yakiwamo ya calcium, phosphorus, chuma na potassium ambayo kwa pamoja husaidia ukuaji wa tishu za mwili wa binadamu.
âKwa mfano, calcium ni muhimu kwa ajili ya kuimarisha mifupa na meno kwa mwanadamu na hivyo mtu anayekula kwa wingi mihogo mibichi huimarisha meno yake na kuyafanya kuwa na nguvu,âalisema.
Katika mbata, baadhi ya virutubisho vingine vilivyomo ni Folates, Niacin, Pantothenic acid,
Pyridoxine, Riboflavin, Thiamin, Sodium na Copper
Updated at: 2024-05-25 10:35:09 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Fenesi ni miongoni mwa matunda ya msimu yenye umbo la kipekee huku likiwa na ladha tamu isiyomithilika. Licha ya sifa hii, tunda hili linatajwa kuwa na faida lukuki endapo litaliwa na mwanadamu.
Kwanza, linatajwa kuwa na virutubisho kadha wa kadha vyenye kazi mbalimbali mwilini. Baadhi ya virutub
isho hivyo ni pamoja na vitamini za aina mbalimbali, madini, protini, mafuta, uwanga na nyuzinyuzi.
Fenesi pia linatajwa kuwa chanzo kizuri cha nishati kisichokuwa na lehemu. Si hivyo tu, bali pia ni chakula chenye virutubisho vya kuondosha sumu mwilini vinavyoweza kuukinga mwili dhidi ya saratani na magonjwa mengine kadha wa kadha.
Uwepo wa viondosha sumu ndani ya tunda hili kunasaidia pia kuongeza uwezo wa kuona. Tunda hili pia linatajwa kuwa na kiasi kikubwa cha madini ya potassium yanayosaidia kuimarisha mifupa na afya ya ngozi.
Fenesi ni chanzo kizuri cha vitamini C. Uwepo wa kiasi kikubwa cha vitamini hiyo pamoja na viondosha sumu kunaongeza ufanisi wa mfumo wa kinga mwilini. Husaidia kuongeza kinga dhidi ya kifua, mafua na kikohozi.
Ni tunda salama kiafya, halina lehemu licha ya kuwa na kiasi kikubwa cha mafuta. Pia, lina wanga na kalori kwa kiasi kikubwa. Sukari iliyomo ndani yake huchangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha mwili.
Hurekebisha msukumo wa damu na pia husaidia kurahisisha mmengâenyo wa chakula tumboni pamoja na kuukinga mwili dhidi ya magonjwa ya moyo na kupooza.
Inasadikika pia kuwa tunda hili lina uwezo wa kuukinga mwili dhidi ya ugonjwa wa pumu.
Si hivyo tu, fenesi lina vitamini muhimu katika utengenezaji wa damu mwilini.
Updated at: 2024-05-25 10:34:59 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Upungufu wa maji ni pale mwili unapopoteza kiasi kingi cha maji kwa njia mbalimbali, ikiwemo jasho na mkojo, mwili hupungukiwa maji na hivyo mtu huyo huambiwa ana upungufu wa maji. Tunaelezwa kuwa karibu theluthi mbili ya miili yetu imejaa maji. Ili mwili uweze kufanya kazi yake vizuri, kiwango cha maji mwilini hakipaswi kupungua hata kidogo, hivyo kila mtu ana wajibu wa kunywa maji ya kutosha kila siku ili kulinda kiwago chake cha maji kisipungue na kinapopungua ndipo hapo mwili huanza kuonesha dalili za kukaukiwa maji (dehydration).
Updated at: 2024-05-25 10:35:07 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Hakuna mtu anayependa kupata majeraha au kuchelewa kupona majeraha. Kwa kuwa uhai na uzima wetu haupo mikononi mwetu, ni vyema tukafahamu kuwa kuna wakati tunaweza kuumia.
Kwa kutambua hili karibu nikufahamishe mambo matano unayoweza kuyafanya ili kuharakisha kupona majeraha.
Lishe bora ni muhimu wakati wote, lakini ni muhimu zaidi mara unapokuwa na majeraha. Ili uweze kupona majeraha mapema unahitaji ule matunda na vyakula vyenye protini, vitamini C, B12 pamoja na madini ya chuma kwa wingi.
Vyakula na matunda hayo ni kama vile machungwa, mapapai, mayai, maziwa, samaki, maharage, n.k. Kwa kula vyakula hivi mwili utaweza kutibu majeraha kwa haraka zaidi.
Kupumzika ni njia ya kuupa mwili nafasi ya kujijenga na kujitibu wakati wa majeraha. Kutokana na mtindo wa maisha au changamoto za kiuchumi, baadhi ya watu hawapati muda wa kupumzika wapatapo majeraha.
Hivi leo utamkuta mtu akiendelea na shughuli zake huku akiwa na plasta, au bandeji bila hata kujali. Ili uweze kupona mapema unahitaji kuupumzisha mwili kwa kiasi cha kutosha ili upone vyema.
Kutokana na majeraha uliyoyapata daktari anaweza kukataza usile au sifanye kitu fulani lakini wewe hutaki; je unafikiri utaweza kupona mapema?
Watu wengi hukatazwa vitu kama vile pombe au kazi ngumu mara wapatapo majeraha, lakini ni wachache ndiyo wanaoheshimu hili.
Ni lazima ufuate ushauri wa daktari ikiwa unataka kupona mapema.
Maji huchukua takriban asilimia 70 ya mwili wa binadamu. Kunywa maji mengi uwapo na majeraha kutakuwezesha kupona majeraha yako mapema.
Maji huboresha kinga mwili, huboresha misuli pamoja na viungio (joints) mbalimbali hivyo kukuwezesha kupona majeraha mapema.
Tafiti mbalimbali zilizofanywa zimeonyesha kuwa kuna manufaa makubwa ya kuogea maji ya baridi. Manufaa haya pia yapo kwa mtu aliyepata majeraha.
Kuogea maji ya baridi kutasababisha mzunguko mzuri wa damu, hivyo viini lishe na tiba vitasafirishwa vyema kwenda kuponya majeraha; pia maji baridi hupunguza maumivu ya vidonda au majeraha.
Kwa hakika lishe bora ni tiba ya maradhi takriban yote. Katika makala hii umeona jinsi lishe bora pamoja na kuzingatia kanuni chache za msingi za afya kunaweza kukusaidia kupona majeraha mapema.
Updated at: 2024-05-25 10:35:14 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kukosa choo ni tatizo kubwa katika jamii zetu japo huwa halionekani kama ni tatizo. Hata hivyo kuna vyakula ambavyo vinapatikana kwa urahisi na vinasaidia kutibu tatizo la kukosa choo kwa njia rahisi kabisa.
Kwa kawaida mtu mwenye afya njema anatakiwa kwenda chooni angalau mara tatu kwa siku, lakini si ajabu kusikia mtu hajaenda chooni siku tatu na tunaona ni kawaida sana kwenda chooni mara moja kwa siku.
Tatizo la kukosa choo (Constipation) linatokana na chakula tunachokula kuchelewa kuunguzwa tumboni hivyo kuchukua muda mrefu katika mfumo wa usagaji.
Tatizo hili linasababishwa na mfumo wa chakula kukosa baadhi ya mahitaji ili kufanya kazi yake ya usagaji. Vitu hivi ni maji na vyakula vya fiba(Vyakula vyenye nyuzinyuzi) ambavyo ni muhimu sana kuharakisha zoezi la usagaji wa chakula tumboni.
Tende zikiwa kavu au kama juisi inasaidia kuondoa tatizo la kukosa choo. Tende zina fiba kwa wingi hivyo kusaidia zoezi la usagaji chakula tumboni. Pia Tende zina kemikali ya sorbitolâaina ya sukari ambayo inatajwa kusaidia usagaji chakula.
Kunywa maji kwa wing kunasaidia kutibu tatizo la kukosa choo kwa kuwa maji yanahochea usagaji wa chakula na kufanya choo kuwa laini. Fiba zinahitaji maji ili kufanya kazi ya kufagia uchafu tumboni na maji yanapokosekana hunyonya toka katika uchafu tumboni na kufanya choo kuwa kikavu na kusababisha ugumu wa kutoka.
Wataalamu wa afya wanashauri kunywa glasi 6 mpaka 8 za maji kila siku( Lita 1-2 kwa siku)
Kama kunywa maji ni ngumu kwako basi jaribu kuweka vipande vya matunda kama ndimu ,limao,tikiti maji na aina nyingine ya matunda.
Kahawa na vinywaji vingine vya moto husaidia kusukumwa kwa chakula tumboni na kupata choo.
Matumizi ya muda mrefu ya kahawa yanaweza pia yakaongezea tatizo. Kama unatumia kahawa kwa wingi unashauriwa kunywa maji mengi pia,vinginevyo itaongezea tatizo la kukosa choo
Matunda yanasaidia kutibu tatizo la kukosa choo kwa vile yana fiba kwa wingi. Lakini matunda yanasaidia kuongeza maji maji hasa matunda kama matikiti.
Pia ulaji wa matunda ni muhimu kuzingatia muda wa kula, ni vyema kula matunda saa moja au dakika 30 kabla au baada ya chakula. Kula matunda mara baada ya kula kama wengi wanavyofanya ni makosa na kunakukosesha faida zinazotarajiwa.
Mboga za majani kama ilivyo matunda ni chanzo kizuri cha faiba ambazo ni muhimu sana katika usagazi na usukumaji wa chakula.
Mchicha, Spinachi,karoti na mboga mboga nyingine ni muhimu kuwepo katika chakula cha kila siku.
Maharage na aina nyingine za kunde kunde pia zina fiba kwa wingi na zinasaidia kupunguza tatizo.
Ukiachia vyakula,ufanyaji mazoezi au kazi zinazoshughulisha mwili zinazaidia kuzuia na kutibu tatizo la kukosa choo.
Kufanya mazoezi kila siku angalau kwa dakika 30 ni jambo linalowezekana kama utalipa muda na kuweka katika ratiba zako. Mazoezi rahisi kabisa ni kukimbia (jogging) na pia hushughulisha mwili mzima(Total Body Exercise).
Ukiachia kutibu tatizo la kukosa choo pia mazoezi yanasaidia kuzuia magonjwa mengine mengi kama presha na kisukari.
Kama unasumbuliwa na tatizo la kukosa choo au unamfahamu mtu mwenye shida hii basi mshilikishe na ajaribu kufuta maelekezo kama yalivyotolewa hapa ili kuweza kutibu tatizo la kukosa choo kwa kupangilia vyakula tu unavyokula kila siku.
Updated at: 2024-05-25 10:35:30 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Wakati mafuta ya nazi yakiwa yamemengâenywa na mwili huhamasisha uundwaji wa nguvu mpya za ubongo zijulikanazo kama âketonesâ.
Ketones zina uwezo wa kusambaza nguvu katika ubongo hata kama insulin itakuwa chini ya kiwango kama matokeo ya ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).
Insulin kazi yake kubwa ni kuishughulikia sukari (glucose) na hivyo kuzipa nguvu seli za ubongo.
Ubongo wa mtu mwenye ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu hauwezi kujitengenezea insulin yake kwa usahihi na vya kutosha. Kwa hiyo inashauriwa kutumia mafuta haya.
Mafuta ya nazi yanao uwezo wa kupigana na seli za kansa. Tafiti za karibuni zinasema kitu chochote chenye uwezo wa kuuongezea nguvu ubongo husaidia pia kuzuia kusambaa kwa seli za kansa katika mwili.
Zaidi ni kuwa mafuta haya yana uwezo wa kumdhibiti bakteria ajulikanaye kama âhelicobacter pyloriâ ambaye husababisha vidonda vya tumbo.
Kuongeza kinga ya mwili ni moja ya faida za mafuta ya nazi sababu ni mafuta ambayo hupigana dhidi ya bakteria, fangasi na virusi mbalimbali.
Paka moja kwa moja juu ya ngozi au kuyanywa pia kuchanganya kwenye vyakula mbalimbali kwa ajili ya kuongeza kinga yako ya mwili.
Mafuta ya nazi yana asidi mafuta nzuri zenye uwezo wa kusaidia na kuzilinda seli za ubongo na kuziwezesha kufanya kazi kwa ufasaha zaidi.
Mafuta ya nazi yanajulikana vizuri kwa uwezo wake wa kukuongezea uvumilivu yaani stamina.
Mafuta ya nazi ni dawa ya mba na mara nyingine hutumika kwa kuchanganywa na mafuta mengine
Ni mazuri kwa ngozi na yanatibu magonjwa mbalimbali ya ngozi.
Mfuta ya nazi yanaweza kuzuia mpaka asilimia 20 ya miale ya jua kushindwa kukufikia moja kwa moja kwenye ngozi yako kama utayafanya kuwa ndiyo mafuta yako ya kupakaa.
Wengi mnapenda kufanya scrub hasa usoni (facial). Kwa lugha nyepesi ni kitendo cha kusugua ngozi kwa dawa maalumu ili kuondoa uchafu wote na kuifanya ionekane nyororo na yenye kupendeza.
Sasa huhitaji dawa zenye kemikali kwa ajili hiyo wakati mafuta ya nazi yanaweza kukusaidia hilo bila madhara yoyote mabaya.
Fanya hivi changanya nusu kikombe (mln125) cha mafuta ya nazi na sukari kikombe kimoja na ufanye dawa ya kusugua na kusafisha uso wako.
Unaweza pia kutumia nazi yenyewe moja kwa moja kabla hujapata mafuta yake.
Tumezoea kutumia nazi jikoni kwenye mapishi, lakini nazi pia inaweza kutumika kama scrub ya asili ya ngozi yako.
Fuata hatua hizi zifuatazo ili kufanya ngozi ya uso wako iwe laini, nyororo na kufanya uso wako uwe laini, nyororo na wenye mvuto.
Scrub hii unaweza pia kuitumia kwa mwili mzima, lakini hapa nitaelezea namna ya kutumia kwa uso wako.
*Safisha uso wako kwa maji safi na sabuni ya kawaida isiwe sabuni ya dawa (medicated)
*Ukishamaliza hapo, utakaa hivyo bila kuuosha uso wako kwa muda wa dakika 15 mpaka 20.
Ili kupata matokeo mazuri fanya hivi kwa muda wa siku 5 mfululizo bila kuacha, yaani mara moja kwa siku.
Amini nakuambia utapata matokeo mazuri mpaka mwenyewe utaifurahia ngozi yako na hata vocha utaninunulia kunipongeza.
Unatakiwa kupakaa tu sehemu yenye tatizo moja kwa moja huku ukinywa kijiko kidogo kimoja kila siku na hutakawia kupona hivyo vidonda.
Yanangarisha kucha na kuzikinga na wadudu.
Mafuta ya nazi Yanaweza kutumika kama dawa ya asili ya kufukuza wadudu (insect repellent) wakiwemo mbu. Unachohitaji ni kuchanganya pamoja na kiasi kidogo cha mafuta ya karafuu au ya mnanaa (mint) na ujipake juu ya ngozi yako na hakuna mdudu yoyote akiwemo mbu atakayekusogelea.
Mafuta ya nazi yana viondoa sumu vyenye nguvu zaidi ambavyo vinaweza kuulinda mwili wako dhidi ya vijidudu nyemelezi.
Zaidi, matumizi ya mafuta ya nazi yanaweza kurahisisha umengâenywaji wa madini ya kalsiamu tumboni mwako.
Upungufu wa madini ya kalsiamu mwilini husababisha mifupa kuwa hafifu jambo linaloishia kuleta ugonjwa wa mifupa (osteoporosis).
Kuzuia ugonjwa wa mifupa unahitaji kuongeza mafuta ya nazi kuwa sehemu ya chakula chako. Hii ndiyo faida ya mafuta ya nazi ambayo niliona si vema kama sitakuambia.
Watu wenye vitambi au unene uliozidi wanatakiwa kuongeza mafuta ya nazi kwenye milo yao na miili yao itakaa sawa yenyewe.
Matumizi ya mafuta ya nazi yanaweza kusaidia mafuta kuchomwa zaidi mwilini huku kiasi chako cha njaa kikishuka.
Mifadhaiko ni jambo lisiloweza kuepukika katika maisha yetu. Kazi ya mfadhaiko au stress ni kukufanya uwe imara zaidi, mpole na unayejiamini zaidi.
Unapofadhaishwa mwili wako huwa unajiongeza na kuwa na shauku ya kufanikiwa zaidi. Hata hivyo mfadhaiko unapodumu kwa muda mrefu unaweza kuleta madhara makubwa kwa mhusika kihisia na hata kimwili pia.
Mfadhaiko wa muda mrefu unaweza kupelekea huzuni mbaya na hatimaye kuathiri muonekano wako.
Watu wenye mifadhaiko (stress) ya muda mrefu huonekana ni wenye umri mkubwa hata kama umri wao bado ni mdogo.
Tafiti za karibuni zimeonyesha uhusiano wa karibu uliopo kati ya matumizi ya mafuta ya nazi na kupungua kwa mfadhaiko wa akili.
Tunaweza kusema kuwa, kitendo hiki cha kuondoa mfadhaiko au stress ni moja ya kazi ya kustajaabisha kabisa ya mafuta ya nazi. Asidi mafuta zilizomo ndani ya mafuta haya ndizo zinazohusika na kazi hii mhimu.
Ili mwili wako ubaki ni wenye afya na kuzuia usipatwe na magonjwa unahitaji kuwa na mfumo mzuri wa mmengâenyo wa chakula na wakati huo huo mfumo imara wa uchukuwaji wa viinilishe, madini na vitamini mbalimbali kutoka kwenye chakula unachokula.
Kwa bahati nzuri, kuuongezea nguvu mfumo wa mmengâenyo wa chakula ni kazi nyingine ambayo mafuta ya nazi yanaweza kukusaidia bila madhara mengine mabaya.
Matumizi ya mafuta ya nazi yatakuwezesha kuongeza uchukuwaji wa viinilishe mhimu kutoka kwenye chakula sababu mafuta haya yana madini ambayo huweza kuyeyuka kwenye mafuta kama kalsiamu na magnesiamu.
Zaidi, mafuta haya yanaweza kusaidia umengâenywaji wa mafuta mengine magumu ndani ya mwili kama matokeo ya kuimarishwa kwa vimengâenya vinavyohusiana na mmengâenyo wa chakula.
Kama unapata maumivu au matatizo yoyote katika kongosho au kibofu cha mkojo unahitaji kuongeza matumizi ya mafuta ya nazi.
Ukiendelea kutumia mafuta ya nazi kila mara utaweza kujitibu pia tatizo la mawe katika kibofu cha mkojo na kuondoa hali ya kutojisikia vizuri kutokana na magonjwa katika kongosho au kibofu cha mkojo.
Faida kubwa ya mafuta ya nazi haiishii katika uwezo wake wa kuchoma mafuta, bali yana kazi nyingine ya kushangaza zaidi nayo ni kutengeneza misuli ya mwili.
Kwenye bidhaa nyingi zinazouzwa zaidi duniani za kutengeneza virutubishi vya kutengeneza misuli ya mwili mafuta ya nazi lazima yawemo.
Kama unataka kuongeza misuli mingi mwilini kirahisi zaidi changanya tui zito la nazi kikombe kimoja (robo lita), ongeza vanilla vijiko vikubwa vitatu, ongeza maji maji ya chungwa vijiko vikuwa viwili na ndizi zilizoiva mbili.
Saga na mashine ya kusagia matunda jikoni (blender) mchanganyiko huu kwa pamoja na ule wote kutwa mara 1 kila siku.
Kuzuia kuoza kwa jino na magonjwa ya fizi ni moja ya kazi nyingine nzuri ya kushangaza ya mafuta ya nazi ambayo nimependa kukufahamisha kupitia makala hii.
Mafuta ya nazi ni dawa inayoweza kudhibiti bakteria wabaya na hivyo kuzuia kuoza kwa jino na maumivu mengine katika fizi. Ili kuzuia haya unahitaji tu kutumia mafuta yako ya nazi kama dawa yako ya mswaki kila siku.
Unaweza pia kuongeza kijiko kidogo kimoja cha mafuta ya nazi ndani ya kikombe kimoja cha maji ya moto ili kutengeneza dawa ya kusafisha mdomo (mouthwash).
Kwa mjibu wa madaktari wengi, kuna uhusiano wa karibu kati ya madhara ya figo na kushindwa kufanya kazi kwa ogani hii mhimu.
Kama tatizo la kufeli kwa figo halitapatiwa ufumbuzi linaweza kupelekea kifo. Figo na Ini ni ogani mhimu zaidi katika mwili ambazo zinatakiwa kupewa uangalizi wa karibu kila mara zisipatwe na madhara yoyote.
Kwa bahati nzuri, mafuta ya nazi yanayo uwezo wa kulinda figo na Ini visipatwe na madhara yoyote mabaya moja ya kazi ya mafuta ya nazi mwilini ulikuwa huijuwi bado.
Wanasayansi wameviona viinilishe katika mafuta ya nazi ambavyo ni mhimu sana kwa afya ya Ini na figo katika mwili wa binadamu.
Nazi pamoja na mafuta ya nazi huwa na asidi mafuta mhimu sana ambazo huhamasisha uundwaji wa âMonooctanoinâ ambayo hufanya kazi ya kuyeyusha mawe katika kibofu cha mkojo na figo.
Wagonjwa ambao hawawezi kumudu gharama za upasuwaji kuondoa mawe katika figo na katika kibofu cha mkojo wanaweza kujitibu hilo kwa kutumia mafuta ya nazi kama dawa mbadala.
Unachohitaji kufanya ni kunywa tu kijiko kidogo kimoja cha mafuta ya nazi kila siku kutwa mara 1 mpaka utakapokuwa umepona.
Mafuta ya nazi hudhibiti uvimbe na kuondoa sumu mwilini, kazi hizi mbili zinayafanya kuwa dawa bora ya kutibu ugonjwa wa baridi yabisi.
Unahitaji kijiko kidogo kimoja cha mafuta haya kila siku ili kujitibu na ugonjwa wa baridi yabisi.
Faida za mafuta ya nazi zinahusu pia kurekebisha kazi za ogani za mwili kama kuweka sawa mapigo ya moyo, kupumua na kuzalisha homoni mhimu.
Tezi koromeo huzalisha homoni mbili ambazo huwa na msaada mkubwa katika kuongeza nguvu katika mfumo wa mmengâenyo wa chakula.
Ufanisi mzuri wa tezi hii huweza kuhakikisha mapigo ya moyo ni sawa, uzito sawa wa mwili, na usawa ulio sawa wa homoni.
Kutibu kisukari aina ya kwanza ni moja ya kazi nyingine nzuri za mafuta ya nazi sababu mafuta haya yanao uwezo wa kuiweka sawa damu sukari (blood glucose) ndani ya mwili.
Mafuta ya nazi yamethibitika siyo katika kushusha kisukari aina ya kwanza tu bali pia katika kuweka sawa aina mbalimbali za homoni mwilini.
Kijiko kidogo kimoja cha mafuta ya nazi kwa siku kinatosha kwa kazi hii.
Mafuta ya nazi ni moja ya dawa nyingine nzuri kwa ajili ya kutibu maambukizi ya fangasi kwa sababu moja kuu kwamba ni mafuta yanayoweza kuua bakteria na virusi mbalimbali.
Hii ni kazi ya mafuta haya ambayo isingekuwa vema kama nisingekujulisha kupitia makala hii. Hii ni matokeo ya kuwa na âlauric acidâ na âcapric acidâ.
Tafiti mbalimbali zimeonyesha uhusiano uliopo baina ya matumizi ya mafuta yenye afya na kushuka kwa maambukizi ya fangasi.
Kwa fangasi yoyote juu ya ngozi unaweza kutumia mafuta haya kama mafuta yako ya kupakaa kila siku pia unaweza kunywa kijiko kidogo kimoja kila siku kuongeza kinga zaidi ya mwili.
Maradhi mengi mwilini huja kama sababu ya homoni zako kutokuwa sawa. Ni bahati kufahamu kuwa mafuta ya nazi ni moja ya dawa za asili nzuri katika kuziweka sawa homoni zako.
Hii ni kwa sababu mafuta ya nazi yana mafuta mazuri yajulikanayo kama âlauric acidâ. Mafuta ya nazi huiweka sawa homoni mhimu sana kwa upande wa uzazi kwa mwanamke homoni ijulikanayo kama âestrogenâ. Chanzo kingine kizuri cha homoni hii ni pamoja na tunda la parachichi.
Kuzeeka mapema ni jambo lisilopendwa karibu na watu wote. Kuzeeka mapema hakuathiri muonekano wako tu bali huathiri pia afya yako.
Tunapozungumzia juu ya faida za kushangaza zilizomo katika mafuta ya nazi lazima ujuwe kuwa mojawapo ni hili la kukufanya usizeeke mapema.
Viuajivijasumu vilivyomo kwenye mafuta ya nazi hufanya kazi mhimu katika kupunguza vijidudu nyemelezi na matatizo mengine katika ini.
Kuzuia magonjwa ya ubongo ni faida nyingine ya mafuta ya nazi ambayo unapaswa kuijua.
Asidi mafuta zilizomo kwenye mafuta ya nazi hubadilishwa na kuwa âketonesâ ambazo huzuia kutokea tatizo la kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).
Kupoteza kumbukumbu ni matokeo ya kuongezeka kwa kemikali ijulikanayo kwa kitaalamu kama âamyloid beta peptidesâ.
Kwenye mafuta ya nazi kuna kitu mhimu sana kijulikanacho kama âPhenolic compoundsâ ambacho hudhibiti ile kemikali ya âamyloid beta peptidesâ na hivyo kukuondolea tatizo la kupoteza kumbukumbu kirahisi zaidi.
Mafuta ya nazi yanaweza kukupunguzia hitaji lako la kutaka kula chakula kila mara kwa kuwa hufanya kazi ya kupunguza njaa ndani ya mwili.
Kutumia mafuta ya nazi kutakufanya ujisikie umeshiba kwa kipindi kirefu na kama matokeo yake kutakusaidia kupunguza kiasi cha nishati unaingiza ndani ya mwili wako kila siku.
Kuna uhusiano wa karibu kati ya mafuta safi kwa afya na kuwa na njaa ya wastani.
Tafiti mbalimbali Zimeonyesha kwamba Msongamano wa juu wa lipoprotini kolesto (high-density lipoproteins -HDL) unao uwezo wa kulinda moyo wako.
Hivyo mafuta ya nazi yanaweza kupunguza hatari kwako ya kupatwa na ugonjwa wa moyo moja ya kazi nyingine mhimu sana ya mafuta haya.
Mafuta ya nazi yana asidi mhimu sana kwa afya ya moyo iitwayo âlauric acidâ ambayo ina uwezo mkubwa kuuweka moyo wako katika hali ya afya na furaha kwa kuidhibiti kolesteroli/lehemu mbaya katika moyo na mwili kwa ujumla.
Lauric acid huongeza uwepo wa kolesteroli nzuri mwilini ijulikanayo kwa kitaalamu kama High Density Lipoprotein (HDL) huku ikiishusha ile kolesteroli mbaya ijulikanayo pia kwa kitaalamu kama Low Density Lipoprotein (LDL) jambo ambalo ni mhimu kwa afya ya moyo kama anavyosema Lovisa Nilsson, mtaalamu wa lishe wa Lifesum.
Tafiti zimeendelea kuonyesha uhusiano uliopo kati ya matumizi ya mafuta ya nazi na kuimarika kwa mfumo mzuri wa mmengâenyo wa chakula.
Mafuta ya nazi yanapokuwa yamemengâenywa ndani ya mwili wako hutumika kama nguvu yako moja kwa moja.
Watu wanaotumia mara kwa mara mafuta ya nazi kwenye vyakula vyao kila siku wanakuwa na mfumo mzuri wa mmengâenyo wa chakula jambo ambalo ni mhimu katika kuchoma mafuta na nishati ndani ya mwili.
Mafuta ya nazi yanasaidia kuimarisha kinga yako ya mwili kwani mafuta ya nazi yana kiasi cha kutosha cha viuajivijasumu (antioxidants) dhidi ya vijidudu mbalimbali nyemelezi.
Tafiti zimeonyesha kwamba matumizi ya mafuta ya nazi yanaweza kuwa msaada mkubwa katika kuotesha na kukuza nywele.
Mafuta ya nazi ni mazuri kwa kupaka mdomoni. Vilevile kama una tatizo la midomo kukauka basi uwe unapakaa mafuta ya asili ya nazi kila mara.
Mafuta ya nazi yana uwezo mkubwa wa kuungua na bado yakabaki na viinilishe vyake kama kawaida hata baada ya kuunguzwa au kuchomwa katika moto.
Mafuta ya nazi hubaki katika hali yake hata katika joto la kawaida tofauti na mafuta mengine.
Mafuta ya nazi ni mafuta mazuri kwa ajili ya masaji na kukupatia hali ya utulivu unaouhitaji kupitia masaji.
Pakaa mafuta ya nazi katika uke kulainisha. Faida nyingine unapopaka mafuta haya ukeni ni kutibu fangasi na bakteria tena bila madhara.
Mafuta ya nazi yanaweza kudhibiti dalili za ugonjwa wa aleji. Kila siku pakaa mafuta ya nazi ndani ya pua zako na hauta piga chafya unapokuwa karibu na kile kinachokuletea aleji/mzio.
Updated at: 2024-05-25 10:35:34 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Zabibu huweza kutumika kama tiba ya shinikizo la chini la damu kama ifuatavyo
Updated at: 2024-05-25 10:37:31 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Maganda ya ndizi ni dawa nyingine nzuri ya kuondoa chunusi. Unachohitaji ni kuwa tu na maganda ya ndizi kwa ajili hii.
Hatua kwa hatua namna ya kutumia dawa hii:
a)Menya ndizi na ule
b)Chukua ganda la ndizi uliyokula na ukandamizekandamize sehemu ya ndani ya ganda hilo sehemu yenye chunusi
c)Subiri kwa dakika 30 kisha jisafishe na maji safi
Updated at: 2024-05-25 10:35:05 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kukoroma ni tatizo linalowapata watu wengi wakati wanapolala ambalo linaweza kuwatokea watu wa kila umri ingawa hutokea mara nyingi kwa wanaume au watu wanene. Kukoroma huzidi kwa kadri umri unavyoongezeka na asilimia 54 ya watu wazima hukoroma baadhi ya wakati huku asilimia 25 ya wengine wakiwa na tabia ya kukoroma kila wakati. Kukoroma baadhi ya wakati kwa kawaida sio tatizo kubwa na mara nyingi huleta tu karaha kwa mtu anayelala karibu na mkoromaji. Hata hivyo kukoroma huko sio tu kwamba huharibu usingizi wa anayekoroma bali pia huwasumbua na kuwakeresha wanaolala karibu na mkoromaji. Wale wenye tabia ya kukoroma, hukoroma kila wanapolala na mara nyingi huchoka wanapoamka, na watu wa aina hii hushauriwa kumuona daktari na kushauriwa kuhusiana na tatizo hilo. Lakini kabla hatujaendela mbele ni bora tujue kukoroma hasa ni nini au hutokea vipi? Mtu huwa anakoroma pale kunapokuwa na kitu au sababu yoyote itakayoziba kuingia au kutoka kwa hewa mdomoni na katika pua. Kuta za koo hutikisika wakati wa kupumua na matokeo yake ni sauti inayosikika ya kukoroma. Kuingia au kutoka kwa hewa huweza kuzuiwa na sababu mbalimbali kama vile: ⢠Kuziba tundu za pua kusiko kamili ambako husababisha nguvu zaidi zitumike katika kupitisha hewa kwenye pua wakati mtu akiwa amelala. Kitendo hicho hupelekea nyama laini za pua na koo zijikusanye na kusababisha mkoromo. Kuna baadhi ya watu wanakoroma tu kipindi cha allergy (allergy season) au wanapatwa na matatizo ya sinus. Baadhi ya matatizo kama vile kupinda pua (deviated septum) au ukuta unaotenganisha tundu za pua na polyps za pua pia huweza kufanya pua zizibe na kusababisha kukoroma. Watu wengi wanaofanya operesheni za pua pia hupatwa na tatizo la kukoroma. ⢠Kuwa na misuli dhaifu katika koo na ulimi. Misuli au nyama za koo na ulimi zinapokuwa dhaifu sana hulegea na kuanguka upande wa nyuma wa sehemu inayopita hewa. Suala hilo hutokea pale mtu anapolala fofofo au kuwa na usingizi mzito na kusababisha kukoroma. ⢠Kuwa na misuli minene ya koo. Hii ni kwa wale watu wanene ambao hata nyama zao za koo pia hunenepa na kupanuka na suala hilo husababisha kukoroma, Pia watoto wenye tonsesi kubwa na adenoids baadhi ya wakati hukoroma. ⢠Kuwa na kilimi kikubwa ni mojawapo ya sababu zinazosababisha kukoroma. Kilimi kirefu kinaweza kuzuia koo na pale kinapotikisika wakati hewa inapita kwa msukumo husababisha kukoroma. ⢠Sababu nyinginezo zinazoweza kumsababishia mtu akorome anapolala ni kuwa na umri mkubwa au uzee, imeshuhudiwa kuwa watu wa makamo na wazee hukoroma, kwani misuli na nyama za koo huanza kuzeeka na kulegea kadri umri unayoongezeka. Vilevile wanaume wanakoroma zaidi kuliko wanawake hii ni kutokana na wanaume kuwa na njia nyembamba zaidi ya hewa kuliko wanawake. Kukoroma pia kunaweza kuwa ni tatizo la kurithi. Pombe, kuvuta sigara na matumizi ya baadhi ya dawa pia husababisha misuli ya koo ilegee na hivyo hupelekea mtu akorome. Kulala vibaya pia husababisha kukoroka kama vile kulala kichalichali, kwani hufanya nyama za koo zilegee na kuziba hewa.