Updated at: 2024-05-25 10:37:43 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Viazi (potato) 1 kilo Nyama ya ng'ombe 1/2 kilo Nyanya ya kopo iliyosagwa 1/2 tin Vitunguu maji 2 Tangawizi/ swaum 1 kijiko cha chai Hoho 1 Curry powder 1 kijiko cha chai Pilipili ya unga 1/2 kijiko cha chai Limao 1/2 Chumvi Coriander Mafuta ya kupikia
Matayarisho
Safisha na katakata nyama ktk vipande vidogovidogo kisha weka pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu mpaka viwe vya brown kisha tia nyama, swaum/ tangawizi, chumvi na limao. Ichanganye vizuri kisha funika na uipike mpaka iive na maji yote yakauke yani yabaki mafuta tu. Baada ya hapo tia viazi vilivyokatwa vipande vya wastani vikaange kwa muda wa dakika 10 kisha tia pilipili na curry powder na nyanya. Funika na punguza moto.Pika mpaka nyanya iive vigeuze kisha tia vimaji kidogo vya kuivishia viazi. Viazi vikikaribia kuiva(hakikisha vinabaki na rojo kidogo) tia hoho na upike kwa muda wa dk 5 kisha malizia kwa kutia coriander. Changanya vizuri kisha ipua na viazi vyako vitakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:56 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Β· Osha mikono yako kwa sabuni kabla na baada ya kutayarisha chakula Β· Tumia vyombo safi na sehemu safi kwa kutayarisha na kula chakula Β· Viporo vipashwe moto vizuri kabla ya kula Β· Chemsha maji ya kunywa na kuyaacha jikoni dakika kumi baada ya kuchemka
Updated at: 2024-05-25 10:37:42 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Bamia (okra) 20 Nyanya chungu (garden eggs) 5 Magadi soda (Bicabonate soda) 1/4 ya kijiko cha chai Nyanya (fresh tomato) 1 Chumvi (salt) kidogo Pilipili 1/4
Matayarisho
Osha bamia, nyanya chungu na nyanya kisha vikatekate katika vipande vidogovidogo. Baada ya hapo vitie kwenye sufuria na vitu vyote vilivyobakia na kisha tia maji kidogo.Chemsha mpaka bamia na nyanya chungu ziive na vimaji vibakie kidogo sana. Baada ya hapo ziponde na mwiko kidogo kisha zikoroge na uipue na mlenda utakuwa tayari kwa kuliwa na ugali.
Updated at: 2024-05-25 10:34:41 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Tambi (vermiceli Roasted) Mifuko 2
Siagi - 4 Vijiko vya supu
Maziwa (condensed) 300Ml
Lozi zilizokatwakatwa - 1 kikombe
Zabibu kavu - 1 Kikombe
Arki (essence) - 1 Kijiko cha supu
MAPISHI
Weka karai kwenye moto kiasi Tia siagi Tia tambi uzikaange usiachie mkoni mpaka ziwe rangu ya dhahabu. Weka lozi na zabibu huku unakoroga Tia maziwa na huku unakoroga usiachie mkono. Tia arki Epua karai, tumia kijiko cha chai kwa kuchotea na utie kwenye kikombe cha kahawa nusu usikijaze. Kipindue kwenye sahani utoe kileja. Fanya hivyo mpaka umalize vyote.
Jinsi ya kupika Biskuti Nyembamba (Wafer Bar) Za Chokoleti Na Njugu
Updated at: 2024-05-25 10:23:08 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Wafer Powder/gram wafer (unga wa biskuti uliosagwa wa tayari) - vikombe 2
Maziwa ya Mgando Matamu ya Kopo - 2 vikombe
Nazi iliyokunwa - Β½ Kikombe
Chokoleti vipande vipande - 1 Kikombe
Njugu vipande vipande - Β½ Kikombe
Siagi - 227Β g
MAPISHI
Yeyusha siagi motoni kisha changanya na unga wa wafer acha kidogo motoni Mimina katika treya unayochomea itandaze vizuri, kisha mimina maziwa juu yake pamoja na njugu vipande , nazi iliyokunwa na vipande vya chokoleti. Choma (bake) kwenye oveni kwa moto wa 350ΒΊC kwa dakika 20. Katakata tayari kwa kuliwa
Jinsi ya kutengeneza biskuti za Matunda Makavu Na Cornflakes
Updated at: 2024-05-25 10:23:08 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga - 4 Vikombe
Sukari - 1 Kikombe
Baking powder 1 kijiko cha chai mfuto
Siagi - 454 gms
Mayai - 2
Matunda makavu (tende, zabibu, lozi) - 1 Kikombe
Vanilla - 2 Vijiko vya chai
Cornflakes - Β½ kikombe
JINSI YA KUANDAA
Changanya sukari na siagi katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy) Tia yai moja moja huku unachanganya mpaka iwe laini kama sufi. (fluffy) Tia unga, baking powder, matunda makavu, changanya na mwiko. Chota mchanganyiko wa biskuti kwa mkono kama (kiasi cha kijiko kimoja cha supu) fanya duara na uchovye katika cornflakes iliyopondwa kwa mkono (crushed) Zipange katika treya ya kupikia na zipike (bake) katika moto wa 375Β°F kwa muda wa kiasi dakika 15 huku unazitazama tazama.
Karibu kwenye ulimwengu wa vitafunio vya afya! ππ₯¦ Je, unashangaa jinsi ya kutosheleza hamu zako wakati unahitaji ufahamu? Tuko hapa kukusaidia! Soma makala yetu ili kugundua vitafunio vya kusisimua na vya kufurahisha ambavyo vitakupa nishati na afya tele. Usikose, inakusubiri! πͺπ #VitafunioVyaAfya #FurahaYaKula #SiriYaUfanisi.
Updated at: 2024-05-25 10:22:26 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vitafunio vya Afya kwa Kutosheleza Hamu Zako πππ₯
Hakuna jambo bora zaidi kama kufurahia kula vitafunio wakati wa mchana au jioni. Kwa nini usichague vitafunio ambavyo si tu vinakidhi hamu yako, lakini pia vinaboresha afya yako? Kwa bahati nzuri, kuna chaguzi nyingi za vitafunio vya afya ambazo unaweza kujumuisha katika lishe yako ya kila siku. Kama AckySHINE, nina ushauri wangu wa kitaalam juu ya vitafunio bora kwa afya yako. Fuatana nami katika makala hii na utapata habari muhimu juu ya vitafunio vyenye afya ambavyo vitakidhi hamu zako.
Matunda safi: Matunda safi kama vile ndizi, tufaha, na embe ni chaguo bora la vitafunio. Ni matajiri katika virutubisho kama vile vitamini, madini, na nyuzinyuzi. πππ
Karanga: Karanga kama vile njugu, karanga, na mlozi ni vitafunio vya afya na vyenye lishe. Vinajaa protini, mafuta yenye afya, na madini kama vile chuma na magnesiamu. π₯
Mboga mboga: Kuna aina nyingi za mboga mboga ambazo zinaweza kufurahisha hamu yako ya vitafunio. Kwa mfano, karoti zinaweza kuliwa mbichi au kuwa vitafunio vya kupikwa kama karoti za kukaanga. π₯
Mchanganyiko wa mbegu: Kuwa na mchanganyiko wa mbegu kama vile mbegu za kitani, mbegu za alizeti, na mbegu za chia ni njia nzuri ya kukidhi hamu yako ya vitafunio wakati unapata faida nyingi za lishe. π°
Yogurt ya asili: as AckySHINE, ninaipendekeza sana yogurt ya asili kama chaguo bora la vitafunio. Inajaa kalsiamu, protini, na probiotiki ambazo zinasaidia kuimarisha mfumo wa kinga na kuboresha afya ya utumbo. πΆ
Smoothies za matunda: Unaweza kuunda smoothies tamu na matunda mbalimbali kama vile parachichi, nanasi, na beri. Smoothies hizi ni njia nzuri ya kufurahia vitamini na madini katika mfumo wa kunywa. πΉ
Maziwa ya badam: Ikiwa unatafuta mbadala wa maziwa ya ng'ombe, maziwa ya badam ni chaguo bora. Ni chanzo kizuri cha kalsiamu, vitamini D, na mafuta yenye afya. π₯
Biskuti za nafaka nzima: Badala ya kula biskuti za kawaida, chagua biskuti za nafaka nzima ambazo zina nyuzinyuzi zaidi na virutubisho vingine muhimu. πͺ
Maharagwe ya kuchemsha: Maharagwe yana protini nyingi na nyuzinyuzi ambazo hufurahisha na kushiba. Unaweza kuchemsha maharagwe na kuyachanganya na mboga mbalimbali kwa vitafunio vya afya. π²
Chokoleti nyeusi: Chokoleti nyeusi yenye asilimia kubwa ya kakao ni chaguo bora la vitafunio. Ina flavonoidi ambazo zinasaidia kupunguza shinikizo la damu na kulinda moyo wako. π«
Popcorn isiyo na mafuta mengi: Popcorn isiyo na mafuta mengi ni chaguo jema la vitafunio kwa watu wanaopenda vitu vinavyokauka. Ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi na inaweza kuwa vitafunio vyako vya upendeleo wakati wa kuangalia sinema. πΏ
Tofu: Tofu ni chanzo bora cha protini, kalsiamu, na chuma. Unaweza kuandaa tofu kwa njia mbalimbali kama vile kukaanga au kuongeza kwenye saladi. π₯
Boga za kukaanga: Boga zilizokaangwa ni chaguo bora la vitafunio kwa wale wanaotafuta kitu kitamu na kisicho na mafuta mengi. Ni chanzo kizuri cha vitamini na madini. π
Mlozi: Unaweza kuchagua kula mlozi kama vitafunio vya afya. Ni chanzo kizuri cha mafuta yenye afya kama vile asidi ya oleic na linoleic. π°
Quinoa: Quinoa ni nafaka ya kipekee ambayo ina protini nyingi, nyuzinyuzi, na madini muhimu. Unaweza kuandaa quinoa kama pilau au kuongeza kwenye sahani zako za mboga mboga. π
Kwa hivyo, kama AckySHINE, napendekeza kuwa na chaguzi hizi za vitafunio vyenye afya katika lishe yako ya kila siku. Kwa njia hii, utaweza kutosheleza hamu yako wakati unajali afya yako. Jaribu chaguzi hizi mbalimbali na uone ni zipi zinazokufaa zaidi. Je, una chaguzi zingine za vitafunio vyenye afya? Napenda kusikia maoni yako. π
Updated at: 2024-05-25 10:34:47 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Biriani ni miongoni mwa vyakula ambavyo ni nadra sana kupikwa katika familia nyingi tofauti na vyakula vingine. Inawezekana ni kutokana na watu wengi kutoelewa namna ya kuoika chakula hiki kutokana na kuhitaji viungo vingi ambavyo huwapa usumbufu wapishi. Kuna aina mbalimbali za upishi wa biriani ambapo mara nyingi hutofautiana kutokana na viungo vinavyotumika katika upishi. Biriani la mbogamboga ni miongoni mwa aina hizo za upishi. Chakula hiki kinaweza kuliwa na kila mtu hususan wale wasiotumia nyama wala samaki.
Mahitaji:
Β½ kg mchele wa basmati Kitunguu maji kikubwa 1 Nyanya 1 kubwa Karoti 1 kubwa Njegere robo kikombe Kiazi ulaya 1 kikubwa Tangawizi za kusaga kijiko 1 Kitunguu swaumu cha kusaga kijiko 1 Karafuu kijiko 1 Majani ya kotimili fungu 1 Maziwa ya mtingi ΒΌ kikombe Chumvi na pilipili kiasi Unga wa dhani kijiko 1 cha mezani Juisi ya limao kijiko 1 cha mezani Mafua ΒΌ lita
Maandalizi:
Chemsha mchele na kisha weka pembeni Osha mbogamboga zote isipokuwa vitunguu na nyanya Changanya mtindi na tangawizi pamoja na kitunguu swaumu viache vikae kwa muda wa saa moja Chukua sufuria weka mafuta na kisha kaanga vitunguu maji, weka nyanya, chumvi, kotimili na limao halafu weka karafuu na kanga hadi vichanganyike vizuri Miminia mchanganyiko wa mtindi na baadaye weka pilipili na baadaye weka unga wa dhania Chukua mchele uliochemshwa changanya na mchanganyiko huo Palia moto juu ya chakula chako na acha kwa muda wa dakika 30 Baada ya hapo chakula chako cha biriani kitakuwa tayari kwa kuliwa
Updated at: 2024-05-25 10:37:42 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Maini (Cow liver) 1/4 kilo Vitunguu (chopped onion) 2 Nyanya (chopped tomato) 1 Kitunguu swaum/tangawizi (ginger /garlic paste) 1 kijiko cha chai Mafuta ya kupikia Chumvi Coriander Curry powder 1 kijiko cha chai Limao (lemon) 1/4 Pilipili (scotch bonnet ) 1
Matayarisho
Safisha maini na ukate vipande vidogovidogo na uweke pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu kidogo(visiwe vya brown) kisha tia ginger/ garlic paste,carry powder kaanga kidogo kisha tia nyanya. Kaanga nyanya mpaka zitoe mafuta kisha tia chumvi, pilipili na vimaji kidogo. Acha vichemke kidogo kisha tia maini na uyapike mpaka yaive. Malizia kwa kukamulia limao na kutia coriander kisha ipua na hapo yatakuwa tayari kwa kuliwa.