Updated at: 2024-05-25 10:23:14 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo Vya Wali
Mchele wa Basmati/Pishori - 1 kilo moja
Vitunguu maji - 3
Karoti - 2
Siagi - 3 vijiko vya supu
Kidonge cha supu (stock) - 1 kimoja
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Ósha mchele uroweke kama saa moja au mbili Katakata vitunguu vipande vidogodogo (chopped) weka kando. Kwaruza karoti (grate) weka kando. Tia siagi katika sufuria ya kupikia wali, weka katika moto iyayuke Kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi kiasi tu. Tia maji kiasi ya kupikia wali, changanya na kidonge cha supu. Yakichemka tia mchele, koroga, funika uweke moto mdogo mdogo. Kabla ya maji kukauka tia karoti changanya wali kisha funika uive kama unavyopika pilau.
Vipimo Vya Kuku Wa Kukaanga
Kuku alokatwakatwa - 1
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi ilosagwa - 2 vijiko vya supu
Bizari ya mchanganyiko/garam masala - kijiko cha supu
Mtindi/Yoghurt - 1 kijiko cha supu
Ndimu - 1
Chumvi - kiasi
Mafuta ya kukaangia - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Ukishamuosha kuku, mchuje atoke maji yote. Changanya viungo vyote katika kibakuli kidogo. Changanya pamoja na kuku kisha acha akolee viungo (marinate) kwa muda wa masaa mawili takriban. Weka mafuta katika karai na kaanga kuku, akiwiva yu tayari kuliwa na wali.
Updated at: 2024-05-25 10:23:09 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Unga wa mchele - 500g
Samli - 250g
Sukari - 250g
Hiliki iliyosagwa - 1/2 kijiko cha chai
Arki (rose flavour) - 1/2 kijiko cha chai
Baking powder - 1 kijiko cha chai
Mayai - 4
Maji ya baridi - 1/2 kikombe cha chai
MAANDALIZI
Saga sukari iwe laini kiasi, changanya unga wa mchele, baking powder, hiliki na sukari. Pasha moto samli mpaka iwe nyepesi kama maji mimina kwenye ule mchanganyiko wa unga wa mchele, kisha uchanganye pamoja na arki. Ongeza mayai yaliopigwa endelea kuchanganya mpaka unga umeanza kuchanganyika vizuri. Ongeza maji ya baridi sana kama nusu kikombe tu ili uchanganyike vizuri. Kata kwa design unayotaka viwe vinene visiwe kama cookies za kawaida kama ilivyo kwenye picha na ukipenda utaweka kidoto kwa kutumia zaafarani katikati ya kileja kama inavyoonesha hapo juu. Choma kwa moto wa baina ya 300F na 350F kwa dakika 15 mpaka 20 visiwe vyekundu toa na tayari kwa kuliwa.
Mapishi ya Biriani Ya Samaki Nguru, Njegere Na Snuwbar (UAE)
Updated at: 2024-05-25 10:23:13 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele wa basmati - 4 cups
Samaki nguru (king fish) - 7 vipande au zaidi
Kitunguu - 5
Nyanya/tungule - 3
Njegere - 1 kikombe
Snuwbar (njugu za pine) - 1 kikombe
Viazi - 2 kata kata mapande makubwa
Tangawizi mbichi - 1 kijiko cha supu
Kitunguu saumu - 1 kijiko cha supu
Pilipili nyekundu - 1 kijiko cha chai
Bizari ya biriani/garama masala - 1 kijiko cha supu
Namna Ya Kupika:
Kaanga samaki mbali kwa viungo upendavyo umkoleze vizuri. Au choma (bake/grill) katika oveni ukipenda. Weka mafuta katika sufuria, tia vitunguu kaanga hadi vigeuka rangi. Gawa sehemu mbili. Sehemu moja bakisha katika sufuria kisha tia tangawizi mbichi na kitunguu thomu ukaange. Tia nyanya kaanga kisha tia bizari zote endelea kukaanga, tia njegere, njugu za snuwbar na ndimu kavu. Tia viazi ulivyokwishakaanga, na vitunguu vilobakia. Tia mapande ya samaki, changanya na masala bila ya kumvuruga samaki. Chemsha wali kisha mwagia juu yake, funika upike ndani ya oveni au mkaa hadi wali uive kama unavyopika kawaida ya biriani. Epua pakua huku ukichanganya na masala ya samaki.
Updated at: 2024-05-25 10:34:44 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
• Maziwa ya mama pekee ndio chakula na kinywaji cha mtoto bora zaidi kwa watoto kwa miezi sita ya kwanza. • Ni jambo la muhimu sana kunyonyesha watoto wachanga kwa muda wa miezi minne na uendelee kunyonyesha hadi mtoto atakapofikisha mwaka mmoja na kuendelea.
• Mtoto akifikisha miezi sita ndio wakati muafaka wa kumpa vyakula vya nyongeza vilivyotayarishwakatika hali ya usafi.
• Onana na mnasihi akushauri kuhusu muda na jinsi ya kumuanzishia mtoto wako vyakula vya nyongeza
• Vyakula vya ngogeza viwe ni vya mchanganyiko wa makundi yafuatayo ya chakula:- vyakula vya nafaka, venye asili ya nyama, mbogamboga na matunda, mafuta na sukari (kiasi). Lisha kila chakula kwa siku kadhaa kwa kufuatanisha kabla hujaaza chakula chengine kipya.
• Usimuachilie mtoto alale kama chupa ya maziwa ingali mdomoni, ili kuepukana na kuoza kwa meno na madhara ya.
• Watoto wanaopewa maziwa ya mama pekee hawaugui mara kwa mara, na wakiugua, makali ya ugonjwa hupungua na hupona mapema kwa sababu yale maziwa ya mwanzo ya njano yenye viini vingi vya kumkinga dhidi ya magonjwa.
Updated at: 2024-05-25 10:34:42 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Unga wa ngano - 2 - 2 ¼ Vikombe
Siagi - 1 ½ Kikombe
Sukari - 1 Kikombe
Yai - 1
Vanilla -Tone moja
Baking Powder -kijiko 1 cha chai
Chumvi - Kiasi kidogo (pinch)
Unga wa Kastadi - 2 Vijiko vya supu
MATAYARISHO
Changanya vitu vyote isipokuwa unga. Tia unga kidogo kidogo mpaka mchanganyiko uwe sawa. Kisha fanya duara ndogo ndogo uzipange kwenye treya na utie rangi katikati. Halafu zichome katika moto wa 300°F kwa muda wa dakika 20 - 25 na zisiwe browni . Kisha panga kwenye sahani tayari kuliwa na chai.
Updated at: 2024-05-25 10:37:49 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Slice za mkate 6 Mayai 3 Chumvi Olive oil
Matayarisho
Vunja mayai yote katika sahani kisha tia chumvi kidogo sana na uyapige mpaka chumvi ichanganyike. Kisha chukua frying pan na utie vimafuta kidogo na uweke jikoni. Mafuta yakishapata moto kiasi,chovya slice za mkate katika hayo mayai na uzipike pande zote zikishaiva zitoe na uziweke katika kitchen towel ili kukausha mafuta.Na baada ya hapo mikate yako itakuwa tayari kwa kuliwa na chai.