Updated at: 2024-05-25 10:37:56 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Β· Osha mikono yako kwa sabuni kabla na baada ya kutayarisha chakula Β· Tumia vyombo safi na sehemu safi kwa kutayarisha na kula chakula Β· Viporo vipashwe moto vizuri kabla ya kula Β· Chemsha maji ya kunywa na kuyaacha jikoni dakika kumi baada ya kuchemka
Updated at: 2024-05-25 10:23:00 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga wa ngano (self risen flour) vikombe 2 na1/2 Sukari (sugar) 1/2 kikombe Hamira (yeast) 1/2 kijiko cha chai Hiliki (cardamon powder) 1/4 kijiko cha chai Tui la nazi (coconut milk) kiasi Baking powder 1/4 kijiko cha chai Siagi (butter)1 kijiko cha chakula Mafuta ya kukaagia
Matayarisho
Changanya unga na vitu vyote kasoro tui la nazi na mafuta ya kukaangia. Ukisha changanyika vizuri tia tui la nazi na uanze kuukanda mpaka uwe mlaini. Baada ya hapo usukume na ukate mandazi katika shape uipendayo, Kisha uyawe katika sehemu yenye joto (warm place) ili yapate kuumuka. Yakisha uumuka yakaange katika mafuta mpaka yaive kisha ipua na uyaache yapoe tayari kwa kuliwa. (Mafuta ya kukaangia yasiwe yamoto sana kwani yatayababua mandazi na hivyo ndani hayataiva vizuri.
Updated at: 2024-05-25 10:23:14 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele - 1 kilo
Kuku - 1
Vitunguu - 3
Viazi/mbatata - 5
Jira/bizari ya pilau nzima - 3 vijiko vya supu
Mdalasini - 1 kijiti
Pilipili manga - 1 kijiko cha supu
Hiliki - 3 chembe
Karafuu - 5 chembe
Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa - 3 vijiko vya supu
Tangawizi mbichi ilosagwa - 3 vijiko vya supu
Mafuta ya kupikia - Β½ kikombe
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Baada ya kumsafisha kuku na kumkatakata, mchemshe kwa chumvi na ndimu, kijiko kimoja cha kitunguu thomu/somu na tangawizi yote.. Menya viazi, katakata vipande vya kiasi. Katakata vitunguu maji kisha kaanga kwa mafuta katika sufuria ya kupikia pilau. Tia bizari zote isipokuwa hiliki. Saga hiliki kisha tia pamoja na kitunguu thomu/somu ukaange kidogo. Mimina kuku na supu yake ikichemka kisha tia mchele na viazi. Koroga kisha acha katika moto mdogomdogo wali uwive kama kawaida ya kupika pilau.
Jinsi ya kupika Visheti Vya Kastadi Vya Shepu Ya Kombe
Updated at: 2024-05-25 10:34:51 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Unga wa ngano 1 Kilo
Siagi ΒΌ kilo
Mayai 2
Kastadi (custard) 3 vijiko vya supu
Baking powder 1 kijiko cha chai
Maziwa 1 Β½ gilasi
Mafuta Ya kukaangia kiasi katika karai
Maandalizi na upikaji
Weka unga katika bakuli kubwa kisha changanya na unga wa kastadi na baking powder. Tia siagi uchanganye vizuri. Tia mayai, kisha maziwa ya baridi uchanganye vizuri usiukande sana. Fanya madonge kisha kata vipande vidogovidogo kisha ubonyeze kwa kidole uvikwaruze kwenye chujio lenye tundu itokee shepu (design) yake.
5- Tia mafuta katika karai yakipata moto, kaanga visheti hadi viive. Usiache hadi vikageuka rangi sana.
6- Eupua, weka katika sufuria au chombo kikubwa kusubiri shira.
Vipimo Vya Shira
Sukari Β½ kilo
Hiliki ilosagwa 1 kijiko cha chai
βarki (rose flavor) 5 matone
Maji 1 gilasi
Namna Ya Kutyarisha
Changanya sukari na maji uipike hadi iwe nzito. Ukiona mapovu yanatoka tia hilik na βarki . Mwagia katika visheti uchanganye vizuri hadi vishike na sukari.
Updated at: 2024-05-25 10:23:05 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mayai yaliochemshwa 4 Nyama ya kusaga robo kilo Kitunguu swaum Tangawizi Limao Chumvi Pilipili Breadcrambs Carry powder Binzari nyembamba ya unga Yai moja bichi Mafuta
Matayarisho
Marinate nyama na pilipili, kitunguu swaum, tangawizi, limao, chumvi, carry powder, binzari nyembamba na breadcrambs pamoja. Kisha vunja yai moja bichi kwenye kibakuli na ulikoroge kisha tia kwenye mchanganyiko wa nyama.Gawanisha matonge manne kwa ajili ya kuzungushia kwenye mayai .Chemsha mayai kwa muda wa dakika 20. Yakisha iva acha yapoe na kisha yamenye maganda na uyaweke pembeni. Baada ya hapo chukua yai moja lililochemshwa na ulizungushie donge moja la mchanganyiko wa nyama. fanya hivyo kwa mayai yote yaliobakia. Baada ya hapo paka mafuta kwa nje ya hizo eggchop na kisha paka mafuta kwenye sinia la kuokea na uziokee kwenye oven kwa moto wa kawaida, kwa muda wa dakika 20.Na eggchop zako zitakuwa tayari kwa kuliwa
Updated at: 2024-05-25 10:23:07 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga 6 Vikombe
Sukari ya kusaga 2 vikombe
Siagi 500 gm
Baking powder 1 Kijiko cha chai
Kastadi Β½kikombe
MAPISHI
Koroga siagi na sukari katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy). Mimina mchanganyiko uliopiga kwa mashine kwenye bakuli. Tia unga na baking powder na Kastadi. Kata usanifu (design) unaopenda halafu panga kwenye sahani ya kupikia (baking tray). Pika (bake) katika oven moto wa 350Β° F kama muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.
Updated at: 2024-05-25 10:22:22 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Upishi wa Afya kwa Ajili ya Afya ya Moyo: Kitamu na Kilainishi πππ½
Leo, tutazungumzia juu ya jambo muhimu sana katika maisha yetu - afya ya moyo. Kama AckySHINE, ninapenda kushiriki na wewe njia ambazo unaweza kula chakula kitamu na cha kufurahisha wakati huo huo kuhakikisha kuwa unalinda afya yako ya moyo. Sasa twende tukashiriki njia hizi kumi na tano za upishi wa afya kwa ajili ya afya ya moyo wako! πͺβ€οΈ
Kula Matunda na Mboga: Matunda na mboga mboga ni chanzo kizuri cha vitamini, madini, na nyuzi ambazo zinaweza kusaidia kudumisha afya bora ya moyo. ππ₯¦
Kupunguza Matumizi ya Chumvi: Chumvi nyingi inaweza kuongeza shinikizo la damu na hatari ya magonjwa ya moyo. Jaribu kutumia viungo vingine vya kitamu kama vile pilipili, tangawizi, au vitunguu. πΆοΈπ§
Kula Nafaka Zisizochakatwa: Nafaka zisizochakatwa kama vile mchele mzuri, ngano nzima, na tambi za ngano nzima zina nyuzi nyingi na virutubisho vingine muhimu kwa afya ya moyo wako. πΎπ
Punguza Matumizi ya Mafuta Yasiyo na Lishe: Mafuta mengi ya wanyama na ya nazi ni mafuta yenye mafuta mengi ambayo yanaweza kuathiri afya ya moyo wako. Badala yake, tumia mafuta yenye afya kama vile mafuta ya zeituni au ya alizeti. π₯₯π«
Kupunguza Matumizi ya Sukari: Sukari nyingi inaweza kuongeza hatari ya kisukari na shida ya moyo. Badala yake, tumia asali au matunda kuongeza ladha tamu kwenye vyakula vyako. π―π
Ongeza Samaki kwenye Lishe yako: Samaki kama vile samaki wa maji baridi na mafuta kama vile samaki wa tuna, salmoni, na sardini, ni matajiri katika asidi ya mafuta omega-3 ambayo inaweza kusaidia kudumisha afya ya moyo. ππ
Kula Vyakula vya Lishe: Kula vyakula vyenye lishe kama vile karanga, maharage, na mbegu za chia ambazo zina protini, nyuzi, na viinilishe vingine muhimu kwa afya ya moyo wako. π₯
Kuepuka Vyakula Vyenye Mafuta Mengi: Vyakula vyenye mafuta mengi kama vile nyama ya nguruwe, nyama ya ng'ombe, na bidhaa za maziwa zilizochakatwa zina mafuta mengi ya wanyama ambayo yanaweza kuathiri afya ya moyo wako. Chagua nyama nyepesi kama vile kuku au nyama ya ng'ombe iliyokatwa mafuta. ππ·
Kupika Kwa Kutumia Njia za Kupikia Zisizo za Mafuta Mengi: Jaribu kupika kwa kutumia njia kama kupika kwa mvuke, kuchemsha, au kupika kwenye grill badala ya kukaanga au kuchoma moto. Hii itapunguza matumizi ya mafuta mengi na kuifanya chakula chako kiwe afya zaidi. π³π₯¦
Punguza Matumizi ya Vyakula Vilivyosindikwa: Vyakula vilivyosindikwa mara nyingi huwa na viungo vingi vya kemikali na mafuta mengi ambayo yanaweza kuwa na athari mbaya kwa afya ya moyo. Chagua vyakula vya asili na visindikwe kwa wingi. ππ
Kula Chakula kidogo mara kwa mara: Badala ya kula milo mikubwa mara chache, jaribu kula milo midogo mara kwa mara. Hii itasaidia kudumisha kiwango cha sukari na cholesterol kwenye damu yako. π½οΈβ°
Kunywa Maji ya Kutosha: Maji ni muhimu kwa afya ya moyo wako. Kunywa angalau lita mbili za maji kwa siku ili kudumisha mwili wako vizuri. π§π¦
Kufanya Mazoezi: Mazoezi ni muhimu kwa afya ya moyo wako. Fanya mazoezi angalau dakika 30 kwa siku, kama vile kutembea au kukimbia ili kuweka moyo wako mwenye nguvu. πββοΈποΈββοΈ
Kupunguza Mafadhaiko: Mafadhaiko yanaweza kuathiri afya ya moyo wako. Jaribu kufanya mazoezi ya kupumua, yoga, au kutafakari ili kupunguza mafadhaiko yako na kuweka akili yako na moyo wako vizuri. π§ββοΈπ
Kwa kumalizia, kula chakula kitamu na cha kufurahisha haimaanishi kuwa unapaswa kuhatarisha afya yako ya moyo. Kwa kufuata kanuni hizi za upishi wa afya, unaweza kufurahia chakula chenye ladha nzuri wakati ukihakikisha kuwa moyo wako unaendelea kuwa na afya bora. Kumbuka, afya ya moyo ni muhimu sana kwa maisha yetu ya kila siku, na kula vyakula vyenye afya ni hatua ya kwanza ya kuhakikisha tunadumisha moyo mzuri. Kwa hivyo, jiunge nami katika safari hii ya kusisimua ya upishi wa afya kwa moyo wako! π₯β€οΈ
Na wewe je, una maoni gani kuhusu njia hizi za upishi wa afya kwa ajili ya afya ya moyo? Je, umewahi kujaribu njia hizi au una njia nyingine za kuongeza kitamu na kilainishi kwenye lishe yako ya moyo? Nimependa kusikia maoni yako! π¬π
Jinsi ya kuandaa Ndizi Mbichi Za Supu Ya Nyama Ngβombe
Updated at: 2024-05-25 10:37:39 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Ndizi mbichi - Kisia
Nyama ngβombe - Β½ kilo
Pilipili ya kusaga - 1 kijiko cha chai
Tangawizi ya kusaga - 2 vijiko vya supu
Thomu (garlic/saumu) - 1 kijiko cha supu
Bizari mchuzi - 1 kijiko cha chai
Nazi ya unga (ukipenda kuongezea) - 2 vijiko cha supu
Chumvi - Kiasi
Ndimu - 1 kamua
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Weka nyama ngβombe katika sufuria, tia tangawizi, thomu, pilipili mbichi, bizari, chumvi. Roweka kidogo ukipenda kisha ikaushe yenyewe kwa maji yake Ongezea maji ya kiasi yasizidi mno, kisha funika na chemsha. Menya ndizi, ukatekate. Nyama ikikaribia kuiva, weka ndizi uendelee kupika mpaka viive vyote. Tia nazi ya unga kidogo tu ukipenda. Koleza kwa bizari mchuzi, pilipili, na ndimu Epua mimina katika chombo cha kupakulia zikiwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:37:49 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Slice za mkate 6 Mayai 3 Chumvi Olive oil
Matayarisho
Vunja mayai yote katika sahani kisha tia chumvi kidogo sana na uyapige mpaka chumvi ichanganyike. Kisha chukua frying pan na utie vimafuta kidogo na uweke jikoni. Mafuta yakishapata moto kiasi,chovya slice za mkate katika hayo mayai na uzipike pande zote zikishaiva zitoe na uziweke katika kitchen towel ili kukausha mafuta.Na baada ya hapo mikate yako itakuwa tayari kwa kuliwa na chai.