Viambaupishi
Unga 4 Vikombe
Sukari 10 Ounce
Siagi 10 Ounce
Mdalasini ya unga 2 vijiko vya chai
Matunda makavu/njugu (kama lozi,
Zabibu, maganda ya chungwa,
Cherries na kadhalika 4 ounce
Maziwa ya maji 4 Vijiko vya supu
Jinsi ya kuandaa na kupika
1) Chukua siagi na sukari koroga na mixer mpaka iwe kama cream.
2) Tia vanilla mdalasini, tia yai moja mix tena endelea kuongeza yai lingine mpaka umalize yote, changanya mpaka iwe laini kama sufi (fluffy)
3) Tia unga na baking powder na dried fruits, changanya na mwiko.
4) Chota mchanganyiko na kijiko cha soup weka kwenye treya ya kupikia tandaza na uma ili upate matundu juu ya biskuti.
5) Pika (bake) kwenye oven lenye moto wa 375ย F. kwa muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.