Maisha ya ndoa yanahitaji maandalizi mazuri, kama waswahili wasemavyo nyote njema huonekana asubuhi, asubuhi ya maisha ya ndoa ni kipindi cha uchumba. Ndugu zangu, kipindi cha uchumba ni lazima tukitumie vizuri na kwa makini na kila jambo, ukitambua hakuna jambo dogo wa kubwa, kila jambo uliangalie katika mapana yake na katika uzito wake.
Hivyo basi huyo anayetaka kuwa na wewe jiulize maswali haya juu yake;
1. Je anamtambua Mungu na kuishi maisa ya kumpendeza Mungu, katika matendo yake na maneno yake?
2. Je huyo mchumba wako yupo tayari kukusaidia wewe kufikia malengo yako katika maisha?
3. Je huyo mchumba wako anakuheshimu na kukusikiliza au mtu anayekudharau?
4. Je mchumba wako anakushirikisha kila jambo kuhusu maisha yake na pia kuwa na utayari wa kupokea mawazo yako?
5. Je mchumba wako ana mawasiliano na wewe kwa kiasi kikubwa na kukujulia hali mara kwa mara?
6. Je mchumba wako yupo tayari kujitoa kwa ajili yako kwa hali na mali ili kufikia malengo yenu ya pamoja?
7. Je unatambua mazuri na mapungufu ya mchumba wako, hasa tukitambua hakuna mtu ambaye ni mkamilifu na namna gani mnasaidiana katika madhaifu yenu
8. Je mchumba wako ni msikivu au ni mtu ambaye anapoamua jambo ndilo analotaka hawezi kukusikiliza wala kupokea mapendekezo yako?
9. Je mchumba wako ni mwaminifu na anajitunza kwa ajili yako wewe tu au ni mtu ambaye haeleweki heleweki?
10. Je mchumba wako yupo tayari kukusamehe unapomkosea au kuomba msamaha anapokosea, au ni mtu mbishi
Haya ni mambo machache ambayo ni lazima kuyatafakari kuhu mchumba wako kama anakufaa kuunga naye NDOA? Usikurupuke.
Editor: Melkisedeck Leon Shine. About Me | Contact Me | LinkedIn | TikTok | WhatsApp
Read and Write Comments
Recommended Posts
Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu uzazi na mipango ya familia
Jinsi ya Kujenga na kudumisha urafiki na marafiki wa mpenzi wako
Kujenga Mazingira ya Amani na Furaha katika Familia Yako
Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya kisheria na mikataba
Utunzaji wa Afya ya Uzazi katika Kufanya Mapenzi: Kujifunza na Kuzungumza
Kuunda Mazingira ya Ushirikiano na Kuhamasisha Kujali katika Familia Yako
Je, kuna umuhimu wa kujadili maoni na mitazamo yako kuhusu ngono/kufanya mapenzi?
Tofauti kati ya mwanamke na mwanamme katika Kufanya Mapenzi