Maisha ya ndoa yanahitaji maandalizi mazuri, kama waswahili wasemavyo nyote njema huonekana asubuhi, asubuhi ya maisha ya ndoa ni kipindi cha uchumba. Ndugu zangu, kipindi cha uchumba ni lazima tukitumie vizuri na kwa makini na kila jambo, ukitambua hakuna jambo dogo wa kubwa, kila jambo uliangalie katika mapana yake na katika uzito wake.
Hivyo basi huyo anayetaka kuwa na wewe jiulize maswali haya juu yake;
1. Je anamtambua Mungu na kuishi maisa ya kumpendeza Mungu, katika matendo yake na maneno yake?
2. Je huyo mchumba wako yupo tayari kukusaidia wewe kufikia malengo yako katika maisha?
3. Je huyo mchumba wako anakuheshimu na kukusikiliza au mtu anayekudharau?
4. Je mchumba wako anakushirikisha kila jambo kuhusu maisha yake na pia kuwa na utayari wa kupokea mawazo yako?
5. Je mchumba wako ana mawasiliano na wewe kwa kiasi kikubwa na kukujulia hali mara kwa mara?
6. Je mchumba wako yupo tayari kujitoa kwa ajili yako kwa hali na mali ili kufikia malengo yenu ya pamoja?
7. Je unatambua mazuri na mapungufu ya mchumba wako, hasa tukitambua hakuna mtu ambaye ni mkamilifu na namna gani mnasaidiana katika madhaifu yenu
8. Je mchumba wako ni msikivu au ni mtu ambaye anapoamua jambo ndilo analotaka hawezi kukusikiliza wala kupokea mapendekezo yako?
9. Je mchumba wako ni mwaminifu na anajitunza kwa ajili yako wewe tu au ni mtu ambaye haeleweki heleweki?
10. Je mchumba wako yupo tayari kukusamehe unapomkosea au kuomba msamaha anapokosea, au ni mtu mbishi
Haya ni mambo machache ambayo ni lazima kuyatafakari kuhu mchumba wako kama anakufaa kuunga naye NDOA? Usikurupuke.
Editor: Melkisedeck Leon Shine. About Me | Contact Me | LinkedIn | TikTok | WhatsApp
Read and Write Comments
Recommended Posts
Je, kuna vitu fulani ambavyo hupendezwa nayo katika ngono/kufanya mapenzi?
Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Heshima na Uadilifu katika Familia: Kuunda Tabia ya Uaminifu
Kusawazisha Kazi na Mahusiano: Kujenga Usawa na Utulivu
Jinsi ya Kuelewa na Kujibu Mahitaji ya Mapenzi ya mke wako
Kujenga Mazingira ya Upendo na Ukarimu katika Familia
Jinsi ya Kuelewa na kukidhi mahitaji ya kihisia ya mpenzi wako
Jinsi ya Kuwa Msaada katika Safari ya Kiroho ya mke wako
Kuweka Kipaumbele cha Uhusiano wa Karibu na Kuweka Nafasi ya Wakati wa Familia