Yatupasa kuwaombea wengine, watu wote wenye shida wakosefu na hata maadui zetu, vilevile tumtolee Mungu shukrani kila wakati na hasa kwa kuadhimisha Ekaristi Takatifu.
Sababu za kusali
1. Kumuabudu Mungu
2. Kumshukuru Mungu
3. Kuomba Neema na Baraka kwa ajili yetu na wenzetu
4. Kuomba msamaha
Namna za sala
1. Sala ya sauti : Sala asaliyo mtu au kikundi kwa kutumia maneno
2. Sala ya fikra : Sala asaliyo mtu akiwa peke yake au na wengine kimya kimya akimuwaza Mungu.
3. Sala ya Taamuli: Kumtazama tuu Mungu kwa upendo Mkubwa Moyoni.
Nyakati zote zinafaa kwa sala hasa
1. Asubuhi na jioni
2. Kabla na baada ya kula
3. Kila dominika
4. Sikukuu za amri
5. Kabla na baada ya kazi
6. Katika kishawishi
Vyanzo vya sala za Kikristo
1. Neno la Mungu
2. Liturujia ya Kanisa
3. Fadhila za Kimungu
4. Matukio ya kila siku
Aidha Roho Mtakatifu ndiye mlezi wa ndani wa sala ya Kikristo akitufundisha kusali na kusali ndani mwetu.
Sala Muhimu kwa Mkristo
Sala kubwa ya kanisa ni Misa Takatifu na sala Bora kwa Bikira Maria ni Rozari Takatifu.
Sala nyingine Muhimu kwa Mkristu ni:
1. Baraka ya Sakramenti kuu
2. Andamo la Ekaristi
3. Litania Takatifu
4. Njia ya Msalaba
5. Rozari takatifu
6. Novena
Mtu anaweza kusali popote lakini kanisani ndio mahali rasmi pa sala, Aidha familia ni shule ya kwanza ya sala ambapo mtu hujifunza na kujizoesha kusali anapokua katika familia.
Changamoto na majaribu wakati wa kusali
1. Mtawanyiko wa mawazo
2. Ukavu wa Moyo
3. Uvivu na uregevu
1. Zinaleta neema nyingi
2. Zinatuimarisha ili tushinde vishawishi na dhambi
3. Zinatuunganisha na Mungu
4. Zinatudumisha katika kutenda mema
References:
Google ScholarResearchGate
Semantic Scholar
AckySHINE
Imani inaweza kusogeza milima
Mungu ni kimbilio letu na nguvu zetu, siku zote tayari kusaidia wakati wa shida
Kupitia Kristo, tunapokea rehema za Mungu kwa wingi
Kwa Mungu, yote yanawezekana
Mwamini Bwana; anajua njia