Ishara ya msalaba ni nini?
Ishara ya Msalaba ni tendo la mtu kugusa panda la uso, kifua na mabega kwa kutumia mkono wa kulia na kutamka “Kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina”
Kwa kugusa paji la uso tuna maana gani?
Kwa kugusa paji la uso tuna maana ya kukubali kwa akili
Kwa kugusa kifua tuna maana gani?
Kwa kugusa kifua maana yake ni kuupokea na kuukubali msalaba moyoni.
Kwa kugusa mabega tuna maana gani?
Kwa kugusa mabega maana yake ni kuwa tayari kuubeba msalaba kwa nguvu zetu zote
Kwa nini tunafanya Ishara ya Msalaba?
Tunafanya Ishara ya Msalaba kwa nia ya kumkiri Mungu mmoja katika Nafsi Tatu. Pia msalaba ni Ishara ya Ukombozi wetu
Ishara ndogo ya Msalaba juu ya panda la uso, mdomo, na kifua kabla ya Injili ina maana gani?
Maana yake ni kama Ahadi kuwa, Niko tayari kulifahamu Neno la Mungu kwa akili yangu, Nitalitangaza kishujaa kwa Midomo yangu, Nitalipenda na kulishika kwa Moyo wangu wote.
References:
Google ScholarResearchGateSemantic ScholarAckySHINE
Hauko peke yako; Mungu yuko nawe
Endelea kuamini, hata ikiwa ni vigumu kuona njia
Imani ni kuwa na uhakika wa kile tunachotarajia na kujua kwa hakika kile ambacho hatuoni
Imani inakua imara zaidi wakati wa majaribu
Katika rehema zake, Mungu husamehe na kurejesha