Mafundisho ya Msingi ya Kanisa Katoliki: Makala za Katoliki

Ishi kama Penseli ili uwe mtu bora

Muumbaji wa penseli alipomaliza kuiumba penseli yake aliiambia mambo muhimu ya kuzingatia ili iweze kuwa penseli bora kabla hajaituma kuingia kazini kwa matumizi.

“Kuna vitu sita unatakiwa uvitambue, “ Aliiambia penseli,

“Kabla sijakutuma kwenda kutumika, unatakiwa uviweke akilini vitu hivyo na usivisahau kamwe. Vitakusaidia siku zote na utakuwa penseli bora maisha yako yote.”

Alisema muumbaji wa penseli.

Read More »
Kanisa Katoliki La Roma

Siri ya kamba nyekundu

Miaka zaidi ya 3000 iliyopita katika mji wa Yeriko alikuwepo mwanamke mmoja kahaba, jina lake Rahabu. Huyu mwanamke aliwaokoa wapelelezi wa Israel waliotumwa kwenda kufanya uchunguzi ktk nchi yao.

Wakati wana wa Israel wanatoka Misri kuelekea nchi ya Kaanani, Mungu aliwaahidi kuwapa mji wa Yeriko. Kwahiyo walipofika ng’ambo ya mto Yordani, Yoshua akatuma wapelezi wawili kwenda kuipeleleza Yeriko kabla wana wa Israel kuivamia na kuitwaa. 

Read More »

Kilichowapata Watu 8 waliowahi kumdhihaki Mungu

1. JOHN LENNON (MUIMBAJI)

Wakati alipokuwa akihojiwa na Mwandishi wa habari wa gazeti la #American alinukuliwa akisema hivi “Ukristo utakufa na kutoweka duniani, siwezi kuwa na wasiwasi na hilo kwa kuwa nina uhakika nalo. Mafundisho ya #Yesu yalikuwa sahihi na wala sipingi hilo ila mafundisho yale yalikuwa mepesi sana ambayo mtu yeyote anaweza kuyafundisha. Hebu angalia leo, tumekuwa maarufu hata zaidi yake (Hapo alilitaja kundi lake la The Bettle). Ilikuwa mwaka 1966.
Wiki moja baada ya kutamba kwamba yeye na kundi lake lilikuwa maarufu hata zaidi ya Yesu, akapigwa risasi sita na kufariki.

Read More »
Shopping Cart