Upishi na Maandalizi ya Milo yenye Afya

Mapishi ya Wali na kuku wa kienyeji

Mahitaji

Kuku wa kienyeji (boiler chicken 1)
Mchele (rice 1/2 kilo)
Nyanya ya kopo (tin tomato 1)
Vitunguu (onion 2)
Vitunguu swaum (garlic cloves 6)
Tangawizi (ginger)
Carry powder
Binzari ya njano (Turmaric 1/2)
Njegere(peas 1/2kikombe)
Carrot iliyokwanguliwa 1
Limao (lemon 1)
Bilinganya (aubergine 1)
Chumvi
Pilipili (scotch bonnet pepper)
Mafuta (vegetable oil)

Matayarisho

Loweka mchele kwa muda wa dakika 10 na uchuje maji yote kisha chemsha maji ya moto na uweke pembeni. Kisha tia mafuta kiasi katika sufuria na ukaange vitunguu, carrot na njegere pamoja. kwa muda wa dakika 5 baada ya hapo tia turmaric na chumvi. pika kwa muda wa dakika 5 na utie mchele na maji ya moto kiasi funika na upike mpaka uive.
Chemsha kuku pamoja na limao, chumvi, kitunguu swaum na tangawizi mpaka aive kisha mweke pembeni. Saga pamoja kitunguu,kitunguu swaum, tangawizi na nyanya. Kisha bandika jikoni na uache uchemke bila mafuta mpaka maji ya kauke.Baada ya hapo tia chumvi, mafuta ,curry powder, bilinganya na kuku. Kaanga pamoja kwa muda kisha tia maji au supu ya kuku kwa kukadiria mchuzi uutakao. Acha uchemke mpaka mabilinganya yaive na hapo mchuzi utakuwa tayari kuseviwa na wali.

Mawazo Rahisi na yenye Afya ya Kujiandaa kwa Chakula cha Kazi

Mawazo Rahisi na yenye Afya ya Kujiandaa kwa Chakula cha Kazi

Kwa mara nyingine tena, hapa ni AckySHINE nikikuletea mawazo bora na yenye afya ya kujiandaa kwa chakula cha kazi. Kama unavyojua, chakula ni nishati muhimu katika kuwezesha utendaji wetu wa kazi. Kwa hiyo, ni muhimu sana kuwa na chakula bora na kilicho na lishe ili kuboresha ubora wa kazi zetu. Hapa kuna orodha ya mawazo 15 rahisi na yenye afya ya kujiandaa kwa chakula cha kazi:

  1. 🍎 Kula matunda na mboga safi kama tunda la kifungua kinywa. Matunda na mboga ni chanzo kikubwa cha vitamini na madini muhimu kwa afya yetu.

  2. 🍗 Chagua protini nzuri kama kuku, samaki au maharagwe kama sehemu ya chakula cha mchana. Protini ni muhimu kwa ukuaji na ukarabati wa misuli yetu.

  3. 🥦 Ongeza mboga za majani kama spinach na kale kwenye sahani yako. Mboga hizi zina virutubisho muhimu kama chuma na vitamini C.

  4. 🥪 Jenga sandwishi zenye afya kwa kutumia mkate wa ngano nzima, mboga mbalimbali na protini kama turkey au tofu. Hii itakupa nishati ya kutosha na kukusaidia kuhimili mawasiliano ya kazi yako.

  5. 🍓 Tumia matunda kama vitafunio vya asili. Matunda yana virutubisho na sukari asili ambayo ni bora kuliko pipi au vitafunio vya sukari.

  6. 🍅 Ongeza nyanya kwenye sahani zako. Nyanya zina lycophene, antioxidant ambayo inasaidia kulinda mwili dhidi ya magonjwa.

  7. 🍚 Chagua mchele wa kahawia badala ya mchele mweupe. Mchele wa kahawia una nyuzi nyingi na unaweza kukusaidia kusimamia uzito wako na kuboresha digestion yako.

  8. 🥛 Kunywa maziwa ya jamii ya skim au maziwa ya mbuzi badala ya maziwa ya ng’ombe ya kawaida. Maziwa ya mbuzi na maziwa ya jamii ya skim yana mafuta kidogo na yanaweza kusaidia kudumisha uzito wako.

  9. 🌽 Tumia nafaka nzima kama mkate wa ngano nzima, mchele wa kahawia au quinoa badala ya nafaka zilizopakuliwa. Nafaka hizi ni tajiri katika nyuzi na hutoa hisia ya kujazia kwa muda mrefu.

  10. 🥕 Ongeza karoti kwenye saladi yako. Karoti ni chanzo kikubwa cha vitamini A, ambayo inasaidia kuimarisha mfumo wetu wa kinga.

  11. 🍌 Kula ndizi kama chakula cha baada ya mazoezi. Ndimu zina wanga na potasiamu, ambayo inasaidia kuimarisha misuli na kurejesha nishati baada ya mazoezi.

  12. 🍚 Pika vyakula vyenye mafuta kidogo kama vile kukaanga kwa kutumia mafuta ya mizeituni. Mafuta ya mizeituni ni bora kwa afya ya moyo na yanaweza kusaidia kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo.

  13. 🥤 Kunywa maji ya kutosha. Maji ni muhimu kwa afya na ustawi wetu. Unapaswa kunywa angalau glasi 8 za maji kwa siku.

  14. 🥦 Jaribu kuchemsha mboga zako badala ya kuzipika kwa muda mrefu. Kuchemsha mboga zitahifadhi virutubisho vyao na kuboresha ladha yao.

  15. 🥗 Jitahidi kula chakula kilichoandaliwa nyumbani na kuwa na udhibiti mkubwa juu ya viungo vyote unavyotumia. Hii inaweza kusaidia kuepuka vyakula vya haraka na kuongeza lishe kwenye chakula chako.

Hizi ni baadhi tu ya mawazo rahisi na yenye afya ambayo unaweza kuzingatia kujipatia chakula bora na kilicho na lishe wakati wa kukabiliana na changamoto za kazi. Kumbuka, chakula ni mafuta yetu ya ajabu ambayo inatuwezesha kufanya kazi vizuri na kwa ufanisi. Kwa hiyo, kula vizuri na ujaze nishati yako! Je, una mawazo mengine yoyote kwa chakula cha kazi? Tafadhali shiriki nasi katika sehemu ya maoni hapa chini!

Mapishi ya chipsi na samaki wa kuchoma

Mahitaji

Viazi ulaya (baking potato 5 vya wastani)
Parprika 1 kijiko cha chai
Pilipili mtama ilyosagwa (ground black pepper 1 kijiko cha chai
Kitunguu swaum cha unga (garlic powder 1 kijiko cha chai)
Chumvi (salt)
Mafuta (vegetable oil)
Marination za samaki (angalia kwenye recipe ya samaki ya nyuma)

Matayarisho

Osha viazi na maganda yake kisha vikaushe na uvikate vipande vya wastani. Kwa kila kiazi toa vipande 6. Kisha vitie kwenye bakuli na utie parpika, pilipili mtama ya unga, kitunguu swaum cha unga, chumvi na mafuta kama vijiko 2 vya chakula. Changanya pamoja na kisha uvibake katika oven kwa muda wa dakika 25. Hakikisha vinakuwa rangi ya brown. Vikisha iva vitoe.
Wamarinate samaki, na uwaoke kisha wasevu na potato wedges tayari kwa kuliwa
(Jinsi ya kupika samaki, angalia katika recipe za nyuma)

Mapishi ya Mchemsho wa ndizi na nyama

Mahitaji

Ndizi mbichi 6
Nyama ya ng’ombe (nusu kilo)
Viazi mviringo 2
Kitunguu swaum
Tangawizi
Kitunguu maji
Nyanya 1 kubwa
Mafuta (vegetable oil)
Chumvi
Limao
Pilipili

Matayarisho

Chemsha nyama na limao, kitunguu swaum, tangawizi chumvi na maji kiasi mpaka nyama iive, Hakikisha unaiacha na supu kiasi kwa ajili ya kuwekea kwenye ndizi.Kisha katakata nyanya na vitunguu na uweke pembeni .Menya ndizi na viazi kisha zichemshe pamoja na vitunguu, nyanya, maji kidogo, mafuta na uhakikishe haziivi kabisa. Baada ya hapo tia nyama na supu yake, pilipili mzima na chumvi na uache uchemke mpaka ndizi na viazi viive.Na baada ya hapo mchemsho wako utakuwa tayari kwa kuliwa

Jinsi ya kutengeneza Biskuti Za Tende Na Ufuta

MAHITAJI

Unga – 3 Vikombe vya chai

Baking powder – 1 ½ Vijiko vya chai

Sukari – 1 Kikombe cha chai

Siagi – 1 Kikombe cha chai

Mayai – 2

Maji – kiasi ya kuchanganyia

Tende – 1 Kikombe

ufuta – ¼kikombe

MAPISHI

  1. Changanya unga, siagi, baking powder, na sukari katika bakuli
  2. Tia mayai, na maji kidogo uchanganye vizuri.
  3. Sukuma kiasi kama unavyosukuma chapati duara kubwa.
  4. Tandaza tende juu yake halafu kunja hadi mwisho.
  5. Paka mayai juu yake halafu mwagia ufuta kisha kata kata vipande.
  6. Vipange kwenye treya ya oveni kisha choma(bake)moto wa 350°F kwa muda wa nusu saa takriban.
  7. Ziepue katika moto naziache zipowe. Panga katika sahani.

Mapishi ya Pilau Ya Nafaka Na Nyama Ya Kusaga

VIAMBAUPISHI

Mchele – 3 vikombe

Nyama ya kusaga – 1 LB

Mchanganyiko wa Nafaka upendazo; maharagwe, njegere, mbaazi n.k 1 mug

Vitunguu maji kata vipande vipande – 3 vya kiasi

Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi – 2 vijiko vya supu

Mafuta – ½ Kikombe

Mchanganyiko wa bizari (Garam Masala) – 2 vijiko vya chai

Vipande vya supu (Maggi cubes) – 3

Maji (inategemea mchele) – 5

Chumvi – Kiasi

MAPISHI

Osha mchele na roweka.
Weka mafuta katika sufuria na kaanga vitunguu mpaka viwe brown.
Tia Thomu na tangawizi, kaanga kidogo.
Weka nyama ya kusaga, chumvi na garam masala, endelea kukaanga mpaka nyama iwive.
Mwaga maji yaliomo katika kopo la nafaka na utie nafaka pekee humo.
Tia maji na vipande vya supu (Maggi cubes) huku unavivuruga, koroga kidogo.
Tia mchele, koroga kidogo.
Funika na pika kwa moto mdogo mpaka karibu na kukauka ukikorogoka kidogo. (kama unavyopika pilau ya kawaida)
*Epua uipike katika moto wa oven 350-400 Deg kwa muda wa dakika 15.
*Kama sufuria uliyotumia sio ya kupikia katika oven, mimina katika chombo chochote kinachotumika kwa oven kama bakuli la pyrex au treya za foil.
Pakua katika sahani na iko tayari kuliwa.

Jinsi ya kupika Pilau ya Mpunga Na Nyama Ya Ng’ombe

Mahitaji

Mpunga – 4 vikombe

Nyama – 1 kilo moja

Kitunguu maji – 3

Mbatata/viazi – 7 vidogodogo

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi ilosagwa 3 vijiko cha supu

Bizari nzima/ya pilau/uzile/cumin – 3 vijiko vya supu

Mdalasini – 3 vipande

Hiliki – 7 punje

Pilipili manga nzima – 1 kijiko cha supu

Chumvi kiasi

Mafuta – ½ kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Osha mchele weka kando
Katakataka vitunguu slice ndogo ndogo.
Weka mafuta katika sufuria kisha ukaange vitunguu pamoja na mdalasini, hiliki pilipilimanga.
Vitunguu vikigeuka rangi unatia kitunguu thomu na tangawizi.
Tia supu kidogo na nyama, kisha tia bizari ya pilau/uzile, na viazi/mbatata.
Maliza kutia supu yote, na ikiwa ni kidogo ongeze maji kiasi cha kuivisha mchele. kisha tia mchele ufunike hadi wali uwe tayari.
Ikiwa unatumia mkaa palia juu yake, ikiwa hutumii uache uive kwa moto mdogo mdogo.

Mapishi ya Koshari Na Sosi Ya Kuku

Vipimo Vya Koshari

Mchele – 2 vikombe

Makaroni – 1 kikombe

Dengu za brown – 1 kikombe

Vitunguu vilokatwakatwa (chopped) – 2

Nyanya ziilokatwakatwa (chopped) – 4

Nyanya ya kopo – 1 kijiko cha supu

Kitunguu saumu(thomu/galic) ilosagwa – 1 kijiko cha supu

Pilipili mbichi ilosagwa – 1 kijiko cha chai

Pilipili manga ya unga – 1 kijiko cha chai

Mdalisini kijiti – 1

Bizari ya pilau (cumin seeds) – 1 kijiko cha supu

Hiliki – 2 chembe

Mafuta – 3 vijiko vya supu

Chumvi – kiasi

Vipimo Vya Kuku

Kuku – 3 LB

Kitunguu saumu(thomugalic) na tangawizi – 1 kijiko cha supu

Mtindi (yoghurt) – 1 kijiko cha supu

Pilipili ya masala nyekundu – 1 kijiko cha chai

Bizari upendazo – 1 kijiko cha chai

Ndimu – 1

Vitunguu slesi vilokaangwa – 3

Namna Kutayarisha Kuku

Kata kuku vipande vikubwa kiasi, osha, weka kando achuje maji.
Changanya vipimo vya kuku pamoja katika kibakuli.
Changanya pamoja na kuku, roweka muda wa kiasi nusu saa au zaidi.
Mchome (grill) kuku hadi aive weka kando.

Namna ya Kutayarisha Koshari

Tia mafuta katika sufuria, kaanga vitunguu hadi viive kuwa rangi hudhurungi.
Tia thomu ,mdalisini, bizari ya pilau na hiliki kaanga tena kidogo.
Tia nyanya, pilipili zote, nyanya kopo, chumvi changanya vizuri ukaange kidogo.
Epua sosi acha kando.
Chemsha dengu pamoja na kidonge cha supu ziive nusu kiini na ibakie supu yake. Muda wa kuchemsha dengu inategemea aina yake.
Tia mchele uchanganyike, funika, pika hadi uive vizuri pamoja na dengu
Chemsha makaroni hadi yaive , epua chuja maji.
Changanya pamoja wali wa dengu na macaroni.
Pakua katika sahani, kisha weka juu yake kuku aliyechomwa, mwagia vitunguu vilokaangwa, kisha mwagia sosi.

Mapishi ya Maini ya ng’ombe

Mahitaji

Maini (Cow liver) 1/4 kilo
Vitunguu (chopped onion) 2
Nyanya (chopped tomato) 1
Kitunguu swaum/tangawizi (ginger /garlic paste) 1 kijiko cha chai
Mafuta ya kupikia
Chumvi
Coriander
Curry powder 1 kijiko cha chai
Limao (lemon) 1/4
Pilipili (scotch bonnet ) 1

Matayarisho

Safisha maini na ukate vipande vidogovidogo na uweke pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu kidogo(visiwe vya brown) kisha tia ginger/ garlic paste,carry powder kaanga kidogo kisha tia nyanya. Kaanga nyanya mpaka zitoe mafuta kisha tia chumvi, pilipili na vimaji kidogo. Acha vichemke kidogo kisha tia maini na uyapike mpaka yaive. Malizia kwa kukamulia limao na kutia coriander kisha ipua na hapo yatakuwa tayari kwa kuliwa.

Mapishi ya Maharage na spinach

Mahitaji

Maharage yaliyochemshwa kiasi
Spinach zilizokatwa kiasi
Vitunguu maji 2
Nyanya 1/2 kopo
Swaum/Tangawizi 1 kijiko cha chakula
Curry powder 1 kijiko cha chai
Olive oil
Chumvi

Matayarisho

Kaanga vitunguu vikianza kuwa vya brown tia tangawizi/swaum kisha nyanya. Pika mpaka nyanya ziive kisha tia curry powder na chumvi. Vipike kiasi kisha tia maharage na maji kidogo kisha funika na uache vichemke. Baada ya muda tia spinach vipike pamoja na maharage mpaka ziive kisha ziipue. Baada ya hapo mboga yako itakuwa tayari kwa kuseviwa.

Mapishi ya Biriani Ya Samaki Nguru, Njegere Na Snuwbar (UAE)

Mahitaji

Mchele wa basmati – 4 cups

Samaki nguru (king fish) – 7 vipande au zaidi

Kitunguu – 5

Nyanya/tungule – 3

Njegere – 1 kikombe

Snuwbar (njugu za pine) – 1 kikombe

Viazi – 2 kata kata mapande makubwa

Tangawizi mbichi – 1 kijiko cha supu

Kitunguu saumu – 1 kijiko cha supu

Pilipili nyekundu – 1 kijiko cha chai

Bizari ya biriani/garama masala – 1 kijiko cha supu

Namna Ya Kupika:

Kaanga samaki mbali kwa viungo upendavyo umkoleze vizuri. Au choma (bake/grill) katika oveni ukipenda.
Weka mafuta katika sufuria, tia vitunguu kaanga hadi vigeuka rangi. Gawa sehemu mbili.
Sehemu moja bakisha katika sufuria kisha tia tangawizi mbichi na kitunguu thomu ukaange.
Tia nyanya kaanga kisha tia bizari zote endelea kukaanga, tia njegere, njugu za snuwbar na ndimu kavu.
Tia viazi ulivyokwishakaanga, na vitunguu vilobakia.
Tia mapande ya samaki, changanya na masala bila ya kumvuruga samaki.
Chemsha wali kisha mwagia juu yake, funika upike ndani ya oveni au mkaa hadi wali uive kama unavyopika kawaida ya biriani.
Epua pakua huku ukichanganya na masala ya samaki.

Jinsi ya kuishi maisha marefu (Mambo ya kuzingatia ili uishi maisha marefu)

Kuishi ukiwa na afya na kuishi maisha marefu kunawezekana kwa kubadili hali ya maisha unayoishi inayoharibu afya yako mfano uvutaji wa sigara, unywaji wa pombe kupita kiasi,kutokufanya mazoezi na kutokula matunda na mbogamboga.

Mambo yanayoweza kukusaidia kuishi maisha marefu ni kama yafuatayo

  1. Kuuandaa mwili kwa maisha marefu kwa kufanya mazoezi
  2. Kuwa makini kutambua na kutibu matatizo ya kiafya
  3. Kuepuka mazingira na kufanya kazi kwa namna au kazi zinazoweza kudhuru maisha yako. Mfano kuendesha gari bila kufuata utaratibu, kutokuvaa vifaa vya kujikinga wakati wa kazi
  4. Epuka vitu vyenye sumu vinavyoweza kudhuru afya yako na kukuletea matatizo ya kiafya kama dawa za mimea na mifugo, zitumie kama inavyotakiwa
  5. Usinywe pombe, usivute sigara wala kutumia dawa za kulevya
  6. Kula mlo kamili
  7. Usile vyakula vyenye chumvi na mafuta mengi
  8. Kunywa maji mengi ili kusafisha mwili
  9. Epuka msongo wa mawazo

Jinsi ya kutengeneza Fagi Ya Kumumunyuka Mdomoni

VIAMBAUPISHI

Maziwa mazito matamu (condensed milk) – 2 vibati

Sukari – 1 kikombe

Samli 1 ½ kikombe

Vanilla 2 kifuniko cha chupa yake

Hiliki ilosagwa – 2 vijiko vya chai

Sinia kubwa ya bati Paka samli

MAANDALIZI

Changanya maziwa, sukari na samli katika sufuria isiyogandisha chakula (non-stick) uweke katika moto.
Koroga huku ikipikika hadi ianze kugeuka rangi na kuanza kuachana. Usiache mkono kuroga isije kufanya madonge.
Tia hiliki na vanilla, endelea kuipika.
Itakapogeuka rangi vizuri mimina katika sinia na haraka uitandaze kwa mwiko huku ukiuchovya katika maji na kuendelea kuitandaza hadi ikae sawa kote.
Pitisha kisu kuikataka ili ikipoa iwe wepesi kuitoa vipande.

Kila inapozidi kupoa na kukaa ndipo fagi inakauka na kumumunyuka.

Jinsi ya kupika Biskuti Ya Keki Kavu kwa kizungu Shortcake

Viamba upishi

Unga 2 Magi (vikombe vya chai)

Sukari iliyosagwa 2/3 Magi (kikombe cha chai)

Siagi   220 g

Unga wa mchele ½ Magi

Yai 1

Vanilla 1 kijiko cha chai

Jinsi ya kuandaa na kupika

1. Changanya vitu vyote hivyo kwenye bakuli mpaka unga ushikamane.

2. Paka mafuta treya ya kuchomea kisha utandaze kwenye treya ya 20cm kwa 30 cm au (8 in kwa 12 in)

3. Choma kwenye moto 325˚C kwa muda wa saa nzima au mpaka ibadilike kuwa rangi ya dhahabu.

4. Epua acha ipoe kisha kata vipande kama mstatili, weak kwenye sahani tayari kunywewa na chai.

Mapishi ya Samaki wa kuokwa

Mahitaji

Mackerel 2
Kitunguu swaum na tangawizi (ginger and garlic paste) 1 kijiko cha cha kula
Pilipili iliyo katwakatwa (chopped scotch bonnet ) 1/2
Limao (lemon) 1/2
Chumvi (salt) kiasi
Curry powder 1/2 kijiko cha chai
Coriander powder 1/2 kijiko cha chai
Mafuta 1 kijiko cha chai

Matayarisho

Safisha samaki kisha wakaushe maji ( ukipenda unaweza kuwakata kati au ukawapika wazima) Baada ya hapo wakate mistari kila upande ( ili spaces ziweze kuingia ndani) kisha waweke kwenye bakuli na utie spice zote. Wachanganye vizuri kisha waweke frijini na uwaache wamarinate kwa muda wa masaa 3. Baada ya hapo washa oven kisha wapakaze mafuta na uwafunge kwenye foil na uwatie kwenye oven kwa muda wa dakika 20. Baada ya hapo fungua foil na uwaache kwenye oven kwa muda wa dakika 10 ili wapate kukauka kidogo. Na hapo watakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuwala kwa kitu chochote upendacho.

Jinsi ya kutengeneza Muhogo Wa Nazi Na Samaki Wa Kukaanga

Mahitaji

Muhogo – 3

Tui La Nazi – 2 vikombe

Chumvi – kiasi

Pilipili mbichi – 2

Mafuta – 1 kijiko moja

Kitunguu maji – 1 kidogo

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Chambua muhogo ukatekate au tumia iliyo tayari.
Chemsha muhogo katika sufuria kwa maji kidogo na chumvi, funika uive muhogo.
Karibu na kukauka maji tia tui, kitunguu maji ulichokatakata na pilipili mbichi.
Unaupika moto mdogo mdogo hadi ukauke tayari kuliwa na samaki au kitoweo chochote kingine

Jinsi ya kutengeneza Biskuti Za Tangawizi

MAHITAJI

Unga – 2 Vikombe

Cocoa ya unga – 1 Kijiko cha supu

Sukari ya hudhurungi – 1 Kikombe

Siagi – ¾ Kikombe

Yai – 1

Molasses – ¼ Kikombe

Baking soda – 2 vijiko vya chai

Mdalasini wa unga – 1 kijiko cha chai

Tangawizi mbichi – 1 kijiko cha supu

Karafuu ya unga – ½ kijiko cha chai

Chumvi ½ kijiko cha chai

Vanilla ½ kijiko cha chai

MAANDALIZI

Katika bakuli, chunga unga, baking soda, chumvi na cocoa. Weka kando.
Washa oven lipate moto huku unatayarisha biskuti.
Katika bakuli jengine, mimina siagi na sukari upige kwa mashini ya keki hadi mchanganyiko uwe laini kama dakika mbili.
Mimina molasses na yai ndani ya mchanganyiko wa siagi na sukari uchanganye vizuri.
Mimina unga kidogo kidogo huku unachanganya na mwiko hadi unga wote umalizike.
Mimina mdalasini, karafuu na tangawizi, changanya vizuri.
Weka mchanganyiko wako ndani ya friji kama masaa mawili. (Ukipenda unaweza kuhifadhi mchanganyiko wako ndani ya mfuko wa freezer na uoke siku nyengine.)
Tengeneza viduara vidogo vidogo.

Chovya kila kiduara katikati sukari, kisha panga kwenye treya ya kuoka

Rudisha viduara katika friji kama nusu saa.

Oka katika oven 350ºF kwa muda wa dakika 15.

Toa biskuti kwenye oven na uache zipoe kama dakika kumi.
Panga kwenye sahani tayari kuliwa.

Jinsi ya kupika Viazi Vya Nazi Kwa Nyama

Mahitaji

Viazi – 3lb

Nyama – 1lb

Kitunguu – 1

Nyanya – 2

Kitunguu saumu(thomu/galic) – 1 kijiko cha chai

Manjano – ½ kijiko cha chai

Curry powder – ½ kijiko chai

Nyanya kopo – 1 kijiko cha chai

Pilipili ya unga – kiasi upendavyo

Chumvi – kiasi

Kidonge cha supu – 1

Tui la nazi – 1 kopoau zaidi

Mtindi ukipenda – 3 vijiko vya supu

Kotmiri – kiasi ya kupambia

Nazi ya unga – 4 vijiko vya supu

Mafuta – 2 vijiko vya supu

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Kata nyama vipande vipande kisha chemsha na chumvi mpaka iive.
Menya maganda viazi na ukate slice kubwa weka pembeni
Kata kata kitunguu kisha kaanga na mafuta mpaka vibadilike rangi
Tia thomu, bizari ya manjano, pilipili ya unga, nyanya kopo
Kata kata nyanya nzima vipande vidogo tia na kidonge cha supu.
Kisha tia viazi, nyama na tui la nazi finika mpaka viazi viwive lakini visiwe vikavu.
Tia mtindi na nazi ya unga kama vijiko 4 vya supu iache motoni kidogo kisha pakua, tupia kotmiri juu na itakuwa tayari kuliwa.

Mapishi ya Wali Wa Kichina Wa Kuku Na Mboga Mchanganyiko

Vipimo

Mchele wa basmati/pishori – 4 vikombe vikubwa (mugs)

Kuku – 2

Vitnguu vya kijani (sprin onions) katakata – 5 miche

Maharage machanga (spring beans) katakata – kiasi kujaza mug moja

Pilipili boga la (capsicum) katakata – 1

Karoti katakata vipande virefu – 1

Kitunguu thomu (garlic) kuna (grate) – 1 kubwa

Tangawizi mbichi kuna (grate) – 1 kubwa

Sosi ya soya (soy sauce) – 2 vijiko vya supu

Kidonge cha supu – 1

Mafuta ya kupikia – ¼ kikombe cha chai

Chumvi – kiasi

Pilipili manga – 1 kijiko cha supu

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Osha kuku vizuri, katakata vipande, weka katika sufuria, tia chumvi, pilipili manga, mfunike, umkaushe motoni huku ukimgeuza geuza.

Roweka mchele kisha uchemshe uive nusu. Chuja maji, tia siagi kidogo ili usigandane.

Weka karai ya kupika mboga (wok) au sufuria kisha tia mafuta yashite moto.

Tia kitunguu thomu, tangawizi, kaanga kidogo.

Tia mboga zote, ulizokatakata.

kaanga kidogo, kisha tia sosi ya soya na kidonge cha supu. Usizipike sana mboga mpaka zikalainika mno. Sababu zitaiva katika mchele

Changanya kuku na mboga kisha changanya vyote katika mchele, urudishe katika moto.

Funika upike hadi uive kamilifu.

Pakua kwenye sahani.

Mapishi ya Ugali Kwa Mchuzi Wa Samaki Wa Kuchoma

Vipimo Vya Ugali

Unga wa mahindi – 4 vikombe

Maji – 6 kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Tia maji kiasi katika sufuria wacha yachemke hasa

Tia unga kidogo kidogo huku ukikoroga mpaka ukamatane

Punguza moto huku ukiendelea kuusonga

Endelea kusonga kwa dakika kadhaa mpaka uanze kuchambuka

Kisha mimina kwenye bakuli au sahani na itakuwa tayari

Vipimo Ya Upishi Wa Mchuzi Wa Samaki Wa Kuchoma Wa Nazi

Samaki:

Samaki wa Nguru – kiasi vipande 5 – 6

Pilipili mbichi – 3

Kitunguu saumu(thomu/galic) – 5 chembe

Tangawizi mbichi – 1 kipande

Bizari ya samaki – 1 kijiko cha supu

Pilipili nyekundu ya unga – 1 kijiko cha chai

Ndimu – 3 kamua

Chumvi – kiasi

Ukipenda mkate samaki vipande kiasi.
Saga vipimo vyote vinginevyo katika mashine. Mchanganyiko ukiwa mzito ongezea ndimu
Changanya pamoja na samaki upake vizuri vipande vya samaki
Acha kwa muda wa nusu saa vikolee mchanganyiko
Panga samaki katika treya ya kupikia ndani ya oveni, kisha mchome (grill) samaki huku ukigeuza hadi viwive.
Epua weka kando.

Kuandaa Mchuzi:

Nyanya/tungule – 3

Kitunguu – 2

Bizari ya manjano/haldi – ¼ kijiko cha chai

Mafuta – 3 vijiko vya supu

Tui la nazi zito – 3 vikombe

Chumvi – kiasi

Katakata vitunguu na nyanya vidogodogo (chopped) weka kando

Weka mafuta katika karai au sufuria, kaanga vitunguu hadi vianze kugeuka rangi

Tia nyanya kaanga pamoja na tia bizari ya njano/haldi .

Tia tui la nazi, chumvi koroga .

Mwishowe tia vipande vya samaki na rojo lake litakalobakia katika treya, mchuzi uko tayari

Shopping Cart
1
    1
    Your Cart
    Kitabu cha SMS Maalumu kwa Umpendaye
    Kitabu cha SMS Maalumu kwa Umpendaye
    1 X Sh2,500 = Sh2,500
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About