Upishi na Maandalizi ya Milo yenye Afya

Jinsi ya kupika Biskuti Nyembamba (Wafer Bar) Za Chokoleti Na Njugu

MAHITAJI

Wafer Powder/gram wafer (unga wa biskuti uliosagwa wa tayari) – vikombe 2

Maziwa ya Mgando Matamu ya Kopo – 2 vikombe

Nazi iliyokunwa – Β½ Kikombe

Chokoleti vipande vipande – 1 Kikombe

Njugu vipande vipande – Β½ Kikombe

Siagi – 227Β g

MAPISHI

Yeyusha siagi motoni kisha changanya na unga wa wafer acha kidogo motoni
Mimina katika treya unayochomea itandaze vizuri, kisha mimina maziwa juu yake pamoja na njugu vipande , nazi iliyokunwa na vipande vya chokoleti.
Choma (bake) kwenye oveni kwa moto wa 350ΒΊC kwa dakika 20.
Katakata tayari kwa kuliwa

Mapishi ya Pilau Ya Kuku Kwa Mchele Mpya

Mahitaji

Mchele – 1 kilo

Kuku – 1

Vitunguu – 3

Viazi/mbatata – 5

Jira/bizari ya pilau nzima – 3 vijiko vya supu

Mdalasini – 1 kijiti

Pilipili manga – 1 kijiko cha supu

Hiliki – 3 chembe

Karafuu – 5 chembe

Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa – 3 vijiko vya supu

Tangawizi mbichi ilosagwa – 3 vijiko vya supu

Mafuta ya kupikia – Β½ kikombe

Chumvi – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Baada ya kumsafisha kuku na kumkatakata, mchemshe kwa chumvi na ndimu, kijiko kimoja cha kitunguu thomu/somu na tangawizi yote..
Menya viazi, katakata vipande vya kiasi.
Katakata vitunguu maji kisha kaanga kwa mafuta katika sufuria ya kupikia pilau.
Tia bizari zote isipokuwa hiliki.
Saga hiliki kisha tia pamoja na kitunguu thomu/somu ukaange kidogo.
Mimina kuku na supu yake ikichemka kisha tia mchele na viazi.
Koroga kisha acha katika moto mdogomdogo wali uwive kama kawaida ya kupika pilau.

Mapishi na Viazi Vitamu: Vitamu na Vyenye Lishe

Mapishi ni kitu ambacho kinaweza kuwa raha na pia kuwa na manufaa kwa afya yetu. Na leo, kama AckySHINE, ningependa kuzungumzia kuhusu mapishi ya viazi vitamu na jinsi yanavyokuwa vitamu na vyenye lishe. Viazi vitamu ni chakula chenye lishe kubwa na ladha tamu ambacho kinaweza kuboresha mlo wako na kukupa nguvu na virutubisho muhimu.

Hapa chini nimeorodhesha pointi 15 ambazo zinaonyesha umuhimu wa kula viazi vitamu:

  1. Viazi vitamu ni chanzo kikubwa cha wanga ambacho kinaweza kukupa nishati ya kutosha kwa siku nzima. πŸ₯”

  2. Pia, viazi vitamu vina kiwango kikubwa cha nyuzinyuzi ambazo zinaweza kuboresha umeng’enyaji wa chakula na kusaidia katika mmeng’enyo wa chakula. 🍠

  3. Viazi vitamu vina kiwango kikubwa cha vitamini A ambayo inasaidia kuimarisha afya ya macho. 🌟

  4. Pia, viazi vitamu vina kiwango kikubwa cha vitamini C ambayo inasaidia kuimarisha kinga ya mwili. 🍊

  5. Kwa kuwa viazi vitamu ni chanzo cha wanga, yanaweza kuwa chaguo bora kwa watu wenye kisukari, kwani wanga wao hutolewa taratibu na kusaidia kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu. πŸ’ͺ🏽

  6. Viazi vitamu ni chakula chenye kalori chache ambacho kinaweza kusaidia katika kupunguza uzito. Kwa mfano, unaweza kuandaa chips za viazi vitamu zilizopikwa kwa kutumia mafuta kidogo badala ya kuzipika kwa kuzama kwenye mafuta. 🍟

  7. Pia, viazi vitamu vina kiwango cha juu cha potasiamu ambayo inasaidia kudumisha afya ya moyo na shinikizo la damu. πŸ’“

  8. Kwa kuwa viazi vitamu vina nyuzinyuzi nyingi, yanaweza kusaidia katika kusawazisha viwango vya kolesterolini mwilini na kusaidia katika afya ya moyo. 🌿

  9. Viazi vitamu ni chanzo kizuri cha madini ya chuma ambayo ni muhimu kwa afya ya damu na inaweza kusaidia katika kuzuia upungufu wa damu. 🌈

  10. Akishine anashauri kutumia viazi vitamu katika mapishi mbalimbali kama vile maini ya viazi vitamu, supu ya viazi vitamu au hata keki ya viazi vitamu. Unaweza kuchanganya na viungo mbalimbali kwa ladha tofauti. 🍲

  11. Viazi vitamu vinaweza kuwa chaguo bora kwa watoto, kwani ni chakula chenye ladha tamu ambacho kinaweza kuwafanya kuwa na hamu ya kula. Unaweza kuwafundisha watoto kula viazi vitamu kwa njia ya kuvutia kama kuandaa chips za viazi vitamu ambazo zimepikwa kwa njia ya afya. 🎈

  12. Pia, viazi vitamu ni chanzo kizuri cha asidi folic ambayo ni muhimu kwa afya ya wanawake wajawazito na inaweza kusaidia kuzuia kasoro za kuzaliwa kwa watoto. 🀰🏽

  13. Viazi vitamu ni chakula chenye mchango mkubwa kwa afya ya utumbo, kwani nyuzinyuzi zake zinasaidia katika kuimarisha utendaji kazi wa utumbo na kuzuia matatizo kama vile kuvimbiwa. 🚽

  14. Kwa kuwa viazi vitamu vina kiwango kikubwa cha vitamini E, vinaweza kusaidia katika kudumisha afya ya ngozi na kusaidia katika kupunguza madhara ya kuzeeka. 🌺

  15. Na mwisho kabisa, viazi vitamu vinaweza kuwa chaguo bora kwa watu wenye mlo wa mboga, kwani ni chakula chenye ladha nzuri na kinaweza kufanywa kuwa chakula kamili kwa kuongeza viungo mbalimbali kama vile mboga za majani, nyanya au hata kuku wa kukaanga. πŸ₯—

Kwa ufupi, viazi vitamu ni chakula chenye ladha tamu na muhimu kwa afya yetu. Kama AckySHINE, nakushauri kuwapa kipaumbele kwenye mlo wako na kujumuisha katika mapishi yako. Unaweza kujaribu mapishi mbalimbali na kubuni ladha tofauti kwa kutumia viazi vitamu. Je, unapenda viazi vitamu? Ni mapishi gani unayopenda kufanya na viazi vitamu? Napenda kusikia maoni yako! 🍽️😊

Jinsi ya kutengeneza juisi ya nyanya

Viamba upishi

Nyanya 1Β kg
Maji Iita Β½
Chumvi kijiko kidogo 1
Sukari

Hatua

β€’ Osha nyanya, katakata na chemsha na maji mpaka zilainike.
β€’ Chuja juisi.
β€’ Pima juisi – vikombe 2 vya juisi kwa kikombe 1 cha sukari, weka
kwenya sufuria safi .
β€’ Ongeza chumvi, chemsha ukikoroga mpaka ichemke.
β€’ Mara ikichemka epua, pozesha na weak kwenya chombo safi kwa
kunywa.

Jinsi ya kupika Mchuzi Wa Ngogwe Na Bamia

Viamba upishi

Ngogwe Β½ kg
Kitunguu 2
Bamia ΒΌ kg
Karoti 2
Mafuta vijiko vikubwa 8
Maji vikombe 3 Mayai 2
Nyanya 2
Chumvi

Hatua

β€’ Osha, menya na katakata nyanya na vitunguu.
β€’ Osha, menya na kata karoti virefu virefu.
β€’ Osha, kata ncha za bamia pande zote na kama ndefu sana kata
vipande viwili.
β€’ Osha, kata vikonyo vya ngongwe, kama ni kubwa kata vipande viwili.
β€’ Kaanga vitunguu, ongeza nyanya, korogoa mpaka zilainike.
β€’ Ongeza ngogwe, karoti, bamia na chumvi, koroga mpaka
zionekane kukolea rojo.
β€’ Ongeza maji vikombe 2 koroga na funikia kwa dakika 10-15 au
mpaka ziive. Punguza moto.
β€’ Koroga mayai kwenye maji mpaka iwe kama maziwa, ongeza
kwenye mboga na koroga polepole usiponde ngogwe wala bamia
kwa dakika 5.
β€’ Onya chumvi, pakua za moto kama kitoweo.

Jinsi ya kupika Mishkaki ya kuku

Kidali cha kuku 1 kikubwa
Swaum,tangawizi 1 kijiko cha chai
Limao 1/2
Pilipili ya unga 1/2 kijiko cha chai
Curry powder 1/2 kijiko
Paprika 1/2 kijiko cha chai
Hoho jekundu 1/2
Hoho la njano 1/2
Kitunguu 1/2
Chumvi
Olive oil

Matayarisho

Katakata kuku ktk vipande vya mishkaki ya kawaida kisha vimarinate na vitu vyote, kasoro hoho na kitunguu.Ni vizuri kuziacha either usiku mzima au kwa masaa machache ili spice ziingie vizuri. Baada ya hapo katakata hoho na vitunguu vipande vya wastani kiasi. Baada ya hapo Taarisha vijiti vya mishkaki kisha tunga nyama pamoja na hoho na vitunguu kisha nyunyuzia mafuta na kisha uzichome kama mishkaki ya kawaida. Itakapoiva itakuwa tayari kwa kuliwa na chochote upendacho kama ndizi za kuchoma, viazi na n.k.

Mapishi ya wali wa hoho nyekundu

Mahitaji

Pilipili hoho (Red pepper 3)
Cougette 1
Kitunguu (onion 1)
Uyoga (mashroom 1 kikombe cha chai)
Carrot 1
Nyanya (fresh tomato 1)
Nyanya ya kopo iliyosagwa (tomato paste 3 vijiko vya chai)
Giligilani (fresh coriander)
Binzari manjano (Turmaric 1/2 ya kijiko cha chai)
Curry powder 1/2 ya kijiko cha chai
Chumvi (salt)
Mafuta (vegetable oil)

Matayarisho

Kata hoho kati na utoe moyo wake kisha ziweke pembeni, Kisha katakata cougette, kitunguu, uyoga, carrot, nyanya katika vipande vidogo vidogo, Weka sufuria jikoni na uanze kupika uyoga kwa muda wa dakika 5, kisha weka curry powder, turmaric na chumvi na kaanga kidogo kisha weka vegetable zilizobakia pamoja na nyanya ya kusaga pamoja na giligilani. Zikaange kwa muda wa dakika 5 kisha zitie kwenye hoho na kisha uzibake kwa muda wa dakika 20 na hapo zitakuwa tayari kuseviwa na wali.
Wali: angalia katika recipe zilizopita

Jinsi ya kupika Biriani Ya Nyama Mbuzi Ya Mtindi Na Zaafaraan

Vipimo – Nyama

Nyama mbuzi – 1 kilo

Kitunguu menya katakata – 1

Nyanya/tungule – 2

Thomu (kitunguu saumu/garlic) saga – 5 chembe

Tangawizi mbichi – kuna/grate au saga – 1 kipande

Pilipili mbichi saga – 2

Bizari ya pilau nzima (cumin seeds) – Β½ kikombe cha kahawa

Mdalasini – 1 kijiti

Karafuu nzima – 5 chembe

Gilgilani/dania (coriander seeds) – Β½ kikombe cha kahawa

Bizari ya mchuzi – 1 Kijiko cha supi

Chumvi – Kiasi

Mtindi – 1 glass

Hiliki ilopondwa – 2 vijiko vya chai

Vitunguu – menya katakata slices kwa ajili ya kukaanga- 7- 9

Mafuta – Kiasi ya kukaangai vitunguu

Vipimo – Wali

Mchele wa pishori/basmati – 4 glass

Zaafarani roweka katika kikombe cha kahawa – Kiasi

Mafuta – Kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Katika sufuria, changanya nyama pamoja, kitunguu kimoja, tangawizi, thomu, nyanya, na viungo vyake isipokuwa mtindi, hiliki na vitunguu vilobakia.

Tia maji kisha funika ichemke mpaka iwive nyama na ikauke supu.

Tia mtindi na hiliki changanya pamoja.

Weka mafuta katika karai, kaanga vitunguu mpaka viwe rangi ya hudhurungi. Toa uchuje mafuta. Kisha viponde ponde kwa mkono uchanganye na nyama.

Chemsha mchele uive nusu kiini, mwaga maji.

Mimina katika nyama utie zaafarani, funika upike wali hadi uwive.

Epua ukiwa tayari.

Mapishi ya Maini ya kuku

Mahitaji

Maini ya kuku 1/2 kilo
Vitunguu vikubwa 2
Hoho 1
Pilipil 1
Limao 1/2
Swaum/tangawizi 1 kijiko cha chai
Curry powder 1/2 kijiko cha chai
Mafuta ya kupikia

Matayarisho

Safisha maini weka pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu,swaum na tangawizi pamoja (hakikisha vitunguu visiwe vya brown), kisha tia maini, curry powder, pilipili, chumvi ,hoho na limao kisha changanya vizuri na ufunike. Pika mpaka maini yaive na hakikisha yanakuwa na rojo kidogo. Baada ya hapo ipua na yatakuwa tayari kwa kuliwa na chochote upendacho kama vile chapati, chips, ugali, wali.

Mapishi ya Pilau Ya Samaki Wa Tuna Na Mboga

Mahitaji

Mchele – 2 Mugs

Mboga mchanganyiko za barafu (Frozen veg) – Mug

Tuna (samaki/jodari) – 2 kopo

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi -2 vijiko vya supu

Garam masala – 1 kijiko cha supu

Nyanya – 2

Kitungu maji – 1

Mdalasini nzima – 2 vijiti

Karafuu – 6 chembe

Pilipili mbichi – 1

Chumvi – kiasi

Viazi – 3

Maji – 2 Β½ Mugs

Mafuta – 3 vijiko vya supu

Maandalizi

Osha mchele na uroweke kwa muda wa dakika 20
Tia mafuta katika sufuria, kaanga kitunguu maji mpaka kigeuke rangi ya hudhurungi (brown).
Mimina viazi, thomu na tangawizi, bizari zote na kaanga.
Tia nyanya uliyokatakata ikaange mpaka iwive.
Tia tuna endelea kukaanga kidogo tu.
Tia maji, yatakapochemka tia mchele.
Punguza moto uwe mdogo funika kwa muda wa Β½ saa hadi wali ukauke na uwive. Utakuwa tayari kuliwa.

Mapishi ya Wali Wa Tambi Na Kuku Wa Sosi Ya Mtindi

Vipimo Vya Wali

Mchele – 3 vikombe

Tambi – 2 vikombe

Mafuta – ΒΌ kikombe

Chumvi

Vipimo Vya Kuku

Kuku kidari (boneless) aliyekatwa katwa vipande – 1 Kilo

Kitunguu maji kilichokatwa katwa – 2

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi iliyosagwa – 1 kijiko cha supu

Pilipili mbichi iliyosagwa – 1 kijiko cha chai

Chumvi – kiasi

Paprika – 1 kijiko cha supu

Masala ya kuku (tanduri au yoyote) – 1 kijiko cha supu

Ndimu – 2 vijiko vya supu

Mtindi (yoghurt) au malai (cream) – 1 kikombe

Mafuta – ΒΌ kikombe

Majani ya kotmiri (coriander) – Β½ kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Wali:

Osha Mchele, uroweke.
Tia mafuta katika sufuria, kaanga tambi zilizokatwakatwa hadi zigeuke rangi kuwa nyekundu.
Tia mchele endelea kukaanga kidogo.
Tia maji kiasi cha wali kupikika kama unavyopika pilau. Kiasi cha maji kinategemea aina ya mchele
Funika katika moto mdogo mdogo hadi uive ukiwa tayari.

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Kuku

Katika bakuli, changanya vitu vyote isipokuwa mtindi na kitunguu.
Tia mafuta katika karai, kisha tia kitunguu ukaange muda mdogo tu, usikiache kugeuka rangi.
Tia kuku na masala yake, endelea kukaanga, kisha tia mtindi au malai ufunike apikike na kuiva vizuri.
Nyunyuzia kotmiri iliyokatwakatwa ikiwa tayari kuliwa na wali wa tambi.

Mapishi ya samaki aina ya salmon

Wakati mwingine mtu unakuwa umechoka na usingependa kupoteza muda jikoni, so mlo wa chapchap unakuwa ni wazo zuri, Mlo huu ni rahisi kuuanda na hata haikuchukui zaidi ya dakika ishirini chakula kinakuwa tayari mezani.

Mahitaji

Salmon fillet 2
Potatao wedge kiasi
Lettice kiasi
Cherry tomato
Limao 1
Swaum
Chumvi
Olive oil

Matayarisho

Mmarinate samaki na chumvi, swaum na nusu ya limao kisha muweke pembeni, baada ya hapo washa oven kisha tia potato wedge zikisha karibia kuiva anza kumpika samaki, tia mafuta kidogo sana kama kijiko kimoja cha chai hivi katika frypan isiyoshika chini yakisha pata moto kiasi muweke samaki wako (upande wenye ngozi chini kwanza) Mpike mpaka uone rangi ya kahawia kwa chini kisha mgeuze upande wa pili, uku samaki wako akiwa anaendelea kuiva, tayarisha salad yako kwa kusafisha lettice na nyanya kisha zichanganye pamoja kisha tengeneza salad dressing pembeni , kamua limao kisha tia olive oil na chumvi kidogo, Baada ya hapo samaki na potato wedge vitakuwa vimeiva, andaa mlo wako na utakuwa tayari kwa kuliwa.

Namna ya kupika Vitumbua

Vitumbua ni aina ya vitafunwa vya chai ambavyo hutengenezwa kwa kutumia unga wa mchele. Kiasili vitumbua ni chakula ambacho hupendelewa sana na watu wa pwani. Na mara nyingi wamekuwa wakipika kwa kuchanganya na nazi ili kuvifanya view na ladha nzuri zaidi

Mahitaji:

Unga wa mchele Β½ kg
Sukari vijiko 4 vya mezani
Tui bubu la nazi
Mafuta ya kupikia
Unga wa hiliki Β½ kijiko cha chai
Hamira kijiko 1 cha chai
Chuma cha vitumbua

Maandalizi:

Chukua unga wa mchele na weka kwenye bakuli au sufuria ya kilo moja
Weka hamira kisha weka sukari kisha miminia tui katika mchanganyiko wako
Weka hiliki koroga hadi view uji mzito
Acha uji huo kwa muda wa saa moja hadi uumuke, mara nyingi kuumuka kunategemea na hali ya hewa,
Baada ya hapo weka mafuta kijiko kimoja cha chakula kila kishimo acha yapate moto Kisha kaanga virumbua vyako

Mapishi ya Biskuti Za Mayai

VIAMBAUPISHI

Unga 3 Vikombe

Sukari ya unga (icing sugar) 1 Kikombe

Siagi 250 gm

Mayai 3

Vanilla 2 Vijiko vya chai

Baking powder 1 Kijiko cha chai

JINSI YA KUPIKA

Koroga siagi na sukari katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy).
Tia mayai na vanilla koroga mpaka mchanganyiko uwe laini.
Tia unga na baking powder changanya na mwiko.
Tengeneza round upange kwenye tray utie nukta ya rangi.
Nyunyuzia sukari juu ya hizo round ulizotengeneza kabla huja choma.
Pika (bake) katika oven moto wa 350Β°F kama muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.

Upishi na Matunda ya Mzabibu: Vitamu vyenye Antioxidants

Upishi na Matunda ya Mzabibu: Vitamu vyenye Antioxidants πŸ‡

Habari za leo wapenzi wa chakula na afya! Leo nataka kuzungumzia faida ya upishi na matunda ya mzabibu. Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni, matunda haya matamu yanajulikana kuwa na virutubisho na antioxidants nyingi ambazo zinaweza kuleta manufaa makubwa kwa afya yetu. Kama AckySHINE, nina ushauri muhimu na maelezo kuhusu jinsi ya kufurahia vitu hivi vyenye faida ya ajabu. Soma makala hii ili kujua zaidi!

  1. πŸ‡ Faida ya kwanza ya matunda ya mzabibu ni kwamba yana antioxidants nyingi ambazo husaidia kupambana na athari za radicals huru katika mwili wetu. Hii husaidia kulinda seli zetu dhidi ya uharibifu na kuimarisha mfumo wetu wa kinga.

  2. πŸ‡ Kula matunda ya mzabibu kunaweza kusaidia kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo. Antioxidants zilizopo katika matunda haya husaidia kupunguza viwango vya cholesterol mbaya na kuboresha afya ya moyo.

  3. πŸ‡ Matunda ya mzabibu yana kiwango kizuri cha vitamini C, ambayo ni muhimu kwa afya ya ngozi yetu. Vitamini C husaidia kujenga collagen, ambayo ina jukumu kubwa katika kuifanya ngozi yetu ionekane nzuri na yenye afya.

  4. πŸ‡ Kwa kuwa na kiwango cha juu cha maji, matunda ya mzabibu yanaweza kusaidia katika kudumisha afya ya figo. Maji ya kutosha mwilini ni muhimu kwa kazi nzuri ya figo.

  5. πŸ‡ Pia, matunda haya yana kiwango kikubwa cha resveratrol, ambayo inajulikana kwa uwezo wake wa kupambana na uchochezi. Hii inaweza kuwa na manufaa sana kwa watu wenye matatizo ya uchochezi kama vile ugonjwa wa arthritis.

  6. πŸ‡ Kwa kuwa ni chanzo kizuri cha nyuzi za chakula, kula matunda ya mzabibu kunaweza kusaidia katika kudumisha afya njema ya utumbo wetu. Nyuzi hizi husaidia katika kuzuia matatizo ya kuvuja kwa utumbo na kuboresha mwendo wa utumbo.

  7. πŸ‡ Je, umewahi kusikia kuhusu mafuta ya mbegu za mzabibu? Mafuta haya yana virutubisho muhimu kama vile asidi ya linoleiki na vitamini E ambavyo husaidia kulinda ngozi yetu dhidi ya madhara ya mazingira na kuifanya iwe laini na yenye afya.

  8. πŸ‡ Kulingana na utafiti, matunda ya mzabibu yameonyeshwa kuwa na uwezo wa kuboresha kumbukumbu na afya ya ubongo. Polyphenols katika matunda haya yana jukumu katika kuboresha afya ya ubongo na kuzuia uharibifu wa seli za ubongo.

  9. πŸ‡ Matunda ya mzabibu ni chanzo kizuri cha nishati. Kwa sababu ya sukari asili iliyomo, matunda haya yanaweza kutoa nguvu na kuongeza kiwango chako cha nishati katika siku yako.

  10. πŸ‡ Kwa wale wanaopenda kupunguza uzito, matunda ya mzabibu yanaweza kuwa msaada mzuri. Kwa kuwa yana kiwango cha chini cha kalori na mafuta, yanaweza kusaidia katika kudhibiti hamu ya kula na kusaidia katika kupunguza uzito.

  11. πŸ‡ Kumbuka, ingawa matunda ya mzabibu ni yenye manufaa kwa afya, ni muhimu kula kwa kiasi. Kula matunda mengi sana ya mzabibu kunaweza kuwa na athari hasi kama vile kuongeza uzito na kuathiri viwango vya sukari mwilini.

  12. πŸ‡ Kwa upande mwingine, unaweza pia kufurahia faida za matunda ya mzabibu kupitia juisi yake. Juisi ya mzabibu inaweza kuwa chaguo nzuri kwa wale ambao hawapendi kula matunda yenyewe.

  13. πŸ‡ Je, umewahi kufikiria kutumia matunda ya mzabibu kwenye sahani yako ya salad? Matunda haya yanaweza kuongeza ladha na ladha ya kipekee kwenye saladi yako na pia kuongeza faida ya kiafya.

  14. πŸ‡ Unaweza pia kuongeza matunda ya mzabibu kwenye smoothie yako ya asubuhi. Itakupa ladha tamu na virutubisho muhimu kwa mwili wako.

  15. πŸ‡ Kwa kuhitimisha, matunda ya mzabibu ni chakula kizuri sana kwa afya yetu na inaweza kuongeza ladha katika milo yetu ya kila siku. Kama AckySHINE, napendekeza kujumuisha matunda haya matamu katika lishe yako na kufurahia faida zake nyingi!

Je, umewahi kula matunda ya mzabibu? Una maoni gani kuhusu faida zake? Tuambie katika sehemu ya maoni hapa chini! πŸ‡πŸ˜Š

Mapishi ya Mchemsho wa ndizi na nyama

Mahitaji

Ndizi mbichi 6
Nyama ya ng’ombe (nusu kilo)
Viazi mviringo 2
Kitunguu swaum
Tangawizi
Kitunguu maji
Nyanya 1 kubwa
Mafuta (vegetable oil)
Chumvi
Limao
Pilipili

Matayarisho

Chemsha nyama na limao, kitunguu swaum, tangawizi chumvi na maji kiasi mpaka nyama iive, Hakikisha unaiacha na supu kiasi kwa ajili ya kuwekea kwenye ndizi.Kisha katakata nyanya na vitunguu na uweke pembeni .Menya ndizi na viazi kisha zichemshe pamoja na vitunguu, nyanya, maji kidogo, mafuta na uhakikishe haziivi kabisa. Baada ya hapo tia nyama na supu yake, pilipili mzima na chumvi na uache uchemke mpaka ndizi na viazi viive.Na baada ya hapo mchemsho wako utakuwa tayari kwa kuliwa

Jinsi ya kupika Viazi Vya Nazi Kwa Nyama

Mahitaji

Viazi – 3lb

Nyama – 1lb

Kitunguu – 1

Nyanya – 2

Kitunguu saumu(thomu/galic) – 1 kijiko cha chai

Manjano – Β½ kijiko cha chai

Curry powder – Β½ kijiko chai

Nyanya kopo – 1 kijiko cha chai

Pilipili ya unga – kiasi upendavyo

Chumvi – kiasi

Kidonge cha supu – 1

Tui la nazi – 1 kopoau zaidi

Mtindi ukipenda – 3 vijiko vya supu

Kotmiri – kiasi ya kupambia

Nazi ya unga – 4 vijiko vya supu

Mafuta – 2 vijiko vya supu

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Kata nyama vipande vipande kisha chemsha na chumvi mpaka iive.
Menya maganda viazi na ukate slice kubwa weka pembeni
Kata kata kitunguu kisha kaanga na mafuta mpaka vibadilike rangi
Tia thomu, bizari ya manjano, pilipili ya unga, nyanya kopo
Kata kata nyanya nzima vipande vidogo tia na kidonge cha supu.
Kisha tia viazi, nyama na tui la nazi finika mpaka viazi viwive lakini visiwe vikavu.
Tia mtindi na nazi ya unga kama vijiko 4 vya supu iache motoni kidogo kisha pakua, tupia kotmiri juu na itakuwa tayari kuliwa.

Jinsi ya kutengeneza Rock-cakes Za Njugu Na Matunda Makavu

Mahitaji

Unga – 4 Vikombe

Sukari -10 Ounce

Siagi – 10 Ounce

Mdalasini ya unga – 2 vijiko vya chai

Matunda makavu/njugu (kama lozi, Zabibu, maganda ya chungwa, Cherries na kadhalika – 4 ounce

Maziwa ya maji – 4 Vijiko vya supu

Maandalizi

Chukua siagi na sukari koroga na mixer mpaka iwe kama cream.
Tia vanilla mdalasini, tia yai moja mix tena endelea kuongeza yai lingine mpaka umalize yote, changanya mpaka iwe laini kama sufi (fluffy)
Tia unga na baking powder na dried fruits, changanya na mwiko.
Chota mchanganyiko na kijiko cha soup weka kwenye treya ya kupikia tandaza na uma ili upate matundu juu ya biskuti.
Pika (bake) kwenye oven lenye moto wa 375Β F. kwa muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.

Jinsi ya kupika Mboga Za Majani Makavu (Aina Yoyote)

Viamba upishi

Mboga za majani makavu ΒΌ kg
Mafuta vijiko vikubwa 3-4
Karanga zilizosagwa kikombe Β½
Maziwa au tui la nazi kikombe 1
Kitunguu 1
Nyanya 2
Chumvi (kama kuna ulazima)
Maji baridi

Hatua

β€’ Loweka mboga za majani makavu na maji kwa dakika 10-15.
β€’ Osha , mboga na katakata nyanya na vitunguu.
β€’ Kangaa, pukusua na saga karanga zilainike.
β€’ Kanga kitunguu, weka nyanya, koroga zilainike.
β€’ Ongeza mboga zilizolowekwa na maji yake kwenye rojo, koroga na funikia mpaka maji yakaukie na ive. Punguza moto.
β€’ Koroga karanga zilizosagwa na maji, ongeza kwenye mboga ukikoroga kwa dakika 5.
β€’ Onja chumvi, pakua kama kitoweo.
Uwezekano
Weka nyanya kidogo.
Tumia tui la nazi au krimu badala ya maziwa.
Weka nyama au dagaa au Mayai badala ya Karanga.

Mapishi ya Ndizi Mbichi Za Nyama Ng’ombe

Vipimo

Ndizi mbichi – 10

Nyama – kilo 1

Nazi ya kopo – 1

Chumvi – 1 Kijiko cha chakula

Ndimu – 1

Bizari ya manjano – 1 Kijiko cha chai

Pili pili mbichi – 3

Nyanya (tomatoes) – 2

Kitunguu maji – 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi iliyosagwa – 1 Kijiko cha chakula

Namna ya Kutayarisha Na Kupika

Kata nyama vipande vipande na uisafishe.
Chemsha nyama weka chumvi, thomu, tangawizi na ndimu. Iache iwive.
Kata kata nyanya na kitunguu, kisha mimina kwenye nyama inayochemka, weka na bizari nusu kijiko. Wacha supu iwive kisha weka pembeni. Ukumbusho: Hakikisha supu inakuwa kiasi na si nyingi.
Menya maganda ndizi na uzikate vipande vipande vya kiasi.
Zikoshe ndizi na uziweke ndani ya sufuria.
Weka maji ndani ya sufuria kisha zichemshe ndizi mpaka ziwe laini kidogo.
Zimwage maji ndizi kisha mimina supu na nyama ndani ya ndizi.
Mimina nazi pili pili na bizari nusu kijiko ndani ya ndizi na uziweke kwenye jiko zichemke mpaka zibakie na urojo kiasi. Onja chumvi na uongeze kadri utakavyopenda.
Weka pembeni zipoe.
Pakua ndizi kwenye sahani au bakuli tayari kwa kuliwa.

Shopping Cart
35
    35
    Your Cart
    Kitabu cha SMS Maalumu kwa Umpendaye
    Kitabu cha SMS Maalumu kwa Umpendaye
    1 X Sh2,500 = Sh2,500
    🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About