Upishi na Maandalizi ya Milo yenye Afya

Jinsi ya kupika Wali Wa Kichina wa mboga mboga Na Mayai

Viambaupishi

  1. Mchele (Basmati) – 3 vikombe
  2. Mbogamboga za barafu (karot, njegere, spring beans na mahindi) – 1 kikombe
  3. Kuku Kidari – 1 LB (ratili)
  4. Mayai – 2 mayai
  5. Vitunguu (vikubwa) – 2 au 3 vidogo
  6. Pili pili manga – 1 kijiko cha chai
  7. Paprika – 1 kijiko cha chai
  8. Chumvi – Kiasi
  9. Mafuta – 1/3 kikombe cha chai
  10. Kitunguu saumu(thomu/galic) – 1 kijiko cha supu
  11. Tangawizi – 1 kijiko cha chai
  12. Kidonge cha supu – 1
  13. Soy sauce – 2 vijiko vya supu

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Kuku

Kata kidari cha kuku vipande vidogo vidogo vya kiasi.

Tia mafuta kidogo katika wok (karai ya kichina)

Kisha mtie kuku, thomu, tangawizi, soy sauce, pilipilimanga, paprika chumvi.

Tia mboga za barafu, kidonge cha supu, kaanga kuku na mboga viwive yitu vyote na mchanganyiko ukauke.

Namna Ya Kutayarisha Na kupika Wali

Roweka mchele wa basmati kwa muda wa saa au zaidi.

Halafu chemsha mchele pamoja na chumvi

Wacha uchemke asilimia 70%

Chuja maji na weka kando

Katika sufuria, tia mafuta kidogo tu

Kisha tia mayai mawili ukaange haraka haraka (crumbled egg)

Changanya mchanganyiko wa kuku na mboga

Kisha tia wali changanye vizuri

Rudisha katika moto, funika upikike kidogo hadi uive

Kisha pakua katika sahani na tolea na mayai ya kuchemsha ukipenda.

Jinsi ya Kupika skonzi

Mahitaji

Unga wa ngano (self risen flour 2 vikombe vya chai)
Sukari (sugar 1/2 kijiko cha chakula)
Chumvi (salt 1/2 kijiko cha chai)
Hamira (yeast 1/2 kijiko cha chakula)
Baking powder 1/2 kijiko cha chai
Siagi (butter 1/4 ya kikombe cha chai)
Maziwa (fresh milk 3/4 ya kikombe cha chai)(unaweza kutumia maji badala ya maziwa)

Matayarisho

Pasha maziwa yawe ya uvuguvugu kisha weka pembeni, pia yeyusha siagi na uweke pembeni.Baada ya hapo tia kila kitu kwenye bakuli la kukandia kasoro maziwa, na uchanganye vizuri kisha tia maziwa kidogo kidogo katika mchanganyiko huo kisha ukande. Ukimaliza uweke kwenye sehemu ya joto na uache uumuke. Ukisha umuka utawanyishe katika madonge saba Kisha .pakaza mafuta au siagi katika chombo cha kuokea kisha yapange hayo madonge katika hicho chombo na uyaache yaumuke tena (kwa mara ya pili). Baada ya hapo pakaza mafuta juu ya hayo madonge na uyaoke (bake) katika oven (moto 200ยฐC ) kwa muda wa dakika 25 na hapo scones au maskonzi yatakuwa tayari

Jinsi ya kutengeneza Pilau Ya Kuku

Mahitaji

Mchele wa basmati – 3 vikombe

Kuku – ยฝ

Viazi – 4

Vitunguu – 2

Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa – 2 vijiko vya supu

Binzari ya pilau nzima – 1 Kijiko cha chakula

Binzari ya pilau – ยฝ kijiko cha chai

Pilipili manga nzima – ยฝ kijiko cha chai

Karafuu nzima – 8

Iliki nzima – 6

Mdalasini nzima – 5 vijiti

Pilipili mbichi iliyosagwa – 2

Chumvi – kiasi

Mafuta ya kupikia – ยผ kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:

Osha mchele na roweka kwa muda kutegemea na aina ya mchele.
Kata kuku vipande upendavyo, safisha kisha mchemshe kwa chumvi, pilipili iliyosagwa, thomu na tangawizi.
Akiwiva kuku, mtoe weka kando, bakisha supu katika sufuria.
Katika sufuria, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangu ya hudhurungi.
Tia thomu na tangawizi na binzari zote kaanga kidogo
Kisha tia viazi kanga kidogo kisha tia kisha tia vipande vyako vya kuku na supu acha ichemke kidogo kisha tia maji ukisie kutokana na mchele unaotumia.
Mwisho tia mchele koroga uchanganye na vitu vyote acha ichemke kiasi kisha funika na punguza moto mpaka uive (huku ukiugeuzageuza)
Ukishakuwa tayari pakua kwenye sahani tayari kwa kula na salad na pilipili.

Jinsi ya kupika mboga ya majani ya mashona nguo

Viamba upishi

Mashonanguo mkono 1
Tui la nazi kikombe 1
Karanga zilizosagwa kikombe ยฝ
Mafuta vijiko vikubwa 4
Kitunguu 1
Nyanya ndogo 2
Chumvi kiasi

Hatua

โ€ข Chambua mashona nguo mateke, osha na katakata.
โ€ข Menya osha na katakata kitunguu.
โ€ข Osha, menya na katakata nyanya.
โ€ข Kaanga karanga, ondoa maganda na saga zilainike.
โ€ข Kuna nazi na chuja tui.
โ€ข Kanga kitunguu, weka nyanya na koroga mpaka zilainike.
โ€ข Weka mashona nguo na chumvi kisha koroga sawa sawa,
funikiakwa dakika 5 -10.
โ€ข Changanya tui la nazi na karanga, ongeza kwenye hizo mboga
ukikoroga kwa dakika 5, punguza moto ili ziive taratibu.
โ€ข Onja chumvi na pakua kama kitoweo.
Uwezekano
Changanya mnavu, mgagani, mashonanguo kidogo kiยฌdogo au
mboga nyingme.
Tumia maziwa au krimu badala ya tui la nazi.
Weka nyama au dagaa au samaki au mayai badala ya – karanga.

Mapishi ya choroko

Mahitaji

Choroko kikombe 1 na nusu
Nazi kopo 1
Kitunguu kikubwa 1
Nyanya 1/2 kopo
Swaum 1 kijiko cha chai
Curry powder 1 kijiko cha chai
Chumvi kiasi
Olive oil
Pilipili nzima

Matayarisho

Loweka choroko usiku mzima kisha zichemshe mpaka ziive na ziweke pembeni. Baada ya hapo saga pamoja nyanya, kitunguu, na swaum kisha vipike mpaka maji yote, baada ya hapo tia mafuta na curry powder, pika mpaka nyanya zitoe mafuta kisha tia choroko,tui la nazi, maji nusu kikombe,pilipili na chumvi, kisha koroga vizuri na uache ichemke. Pika mpaka tui la nazi litakapoiva na rojo ibakie kidogo sana, kisha ipua na mboga yako itakuwa tayari kwa kuliwa. Mi huwa napenda kuila na wali ila hata na ugali au chapati inaenda pia.

Jinsi ya kupika Slesi Za Chokoleti Na Karameli

Viamba upishi

Unga 1 Magi (vikombe vya chai)

Sukari ya browni ยฝ Magi

Siagi iliyoyayushwa 125ย g

Nazi iliyokunwa ยฝ Magi

Mjazo wa karameli (Caramel filling)

Syrup 1/3 kikombe cha chai

Siagi iliyoyayushwa 125ย g

Maziwa matamu ya mgando 2 vikopo (condensed milk)

Mjazo wa chokoleti (Chocolate filling)

Chokoleti 185ย g (dark chocolate)

Mafuta 3 Vijiko vya chai

Jinsi ya kuandaa na kupika

1. Changanya unga, sukari, siagi na nazi iliyokunwa kwenye bakuli mpaka unga ushikamane.

2. Paka mafuta treya ya kuchomea kisha utandaze kwenye treya ya 20cm kwa 30ย cm au (8 in kwa 12 in) unaweza kuweka karatasi ya kuchomea chini ukipenda.

3. Choma kwenye moto 325หšC kwa muda wa dakika 15 mpaka 18 au mpaka ibadilike kuwa rangi ya browni.

4. Kwenye sufuria ndogo tia syrup siagi na maziwa matamu ya mgando na changanya kwa moto mdogo mpaka uwe mzito kasha mimina juu ya keki uliyochoma na choma tena kwa muda wa dakika 20 mpaka karameli iwe rangi ya dhahabu.

5. Kwenye sufuria ndogo nyingine tia vipande vya chokoleti na mafuta na ukoroge kwa moto mdogo mpaka iyayuke kisha wacha ipoe kidogo mimina juu ya mjazo wa karameli kisha weka kwenye friji mpaka ishikamane.

6. Kata vipande weka kwenye sahani tiyari kwa kuliwa

Mapishi ya Mchuzi wa kambale

Mahitaji

Kambale 2
Nazi kopo 1
Nyanya kopo 1
Vitunguu 2
Curry powder 1 kijiko cha chai
Turmaric 1/2 kijiko cha chai
Binzari nyembamba ya unga 1/2 kijiko cha chai
Swaum/ tangawizi 1 kijiko cha chakula
Giligilani kiasi
Limao 1/2
Chumvi
Olive oil

Matayarisho

Loweka samaki katika maji ya moto kwa muda wa muda wa nusu saa.Baada ya hapo Saga pamoja nyanya, vitunguu, swaum na tangawizi kisha vibandike jikoni na uvipike mpaka maji yote yakauke kisha tia mafuta. Pika mpaka nyanya zitengane na mafuta kisha tia spice zote.Zipike kwa muda mdogo kisha tia tui la nazi, maji kiasi, samaki, pilipili nzima, chumvi na kamulia limao. Pika mpaka tui la nazi litakapoiva na samaki pia wawe wameiva na mchuzi ubakie kiasi. Baada ya hapo ipua kisha tia giligilani iliyokatwa na mchuzi utakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kuulia kwa chochote kile upendacho. Mi hupendaga kuulia na ugali mlaiiini au na wali pia.

Mapishi ya Ugali Kwa Mchuzi Wa Samaki Wa Kuchoma

Vipimo Vya Ugali

Unga wa mahindi – 4 vikombe

Maji – 6 kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Tia maji kiasi katika sufuria wacha yachemke hasa

Tia unga kidogo kidogo huku ukikoroga mpaka ukamatane

Punguza moto huku ukiendelea kuusonga

Endelea kusonga kwa dakika kadhaa mpaka uanze kuchambuka

Kisha mimina kwenye bakuli au sahani na itakuwa tayari

Vipimo Ya Upishi Wa Mchuzi Wa Samaki Wa Kuchoma Wa Nazi

Samaki:

Samaki wa Nguru – kiasi vipande 5 – 6

Pilipili mbichi – 3

Kitunguu saumu(thomu/galic) – 5 chembe

Tangawizi mbichi – 1 kipande

Bizari ya samaki – 1 kijiko cha supu

Pilipili nyekundu ya unga – 1 kijiko cha chai

Ndimu – 3 kamua

Chumvi – kiasi

Ukipenda mkate samaki vipande kiasi.
Saga vipimo vyote vinginevyo katika mashine. Mchanganyiko ukiwa mzito ongezea ndimu
Changanya pamoja na samaki upake vizuri vipande vya samaki
Acha kwa muda wa nusu saa vikolee mchanganyiko
Panga samaki katika treya ya kupikia ndani ya oveni, kisha mchome (grill) samaki huku ukigeuza hadi viwive.
Epua weka kando.

Kuandaa Mchuzi:

Nyanya/tungule – 3

Kitunguu – 2

Bizari ya manjano/haldi – ยผ kijiko cha chai

Mafuta – 3 vijiko vya supu

Tui la nazi zito – 3 vikombe

Chumvi – kiasi

Katakata vitunguu na nyanya vidogodogo (chopped) weka kando

Weka mafuta katika karai au sufuria, kaanga vitunguu hadi vianze kugeuka rangi

Tia nyanya kaanga pamoja na tia bizari ya njano/haldi .

Tia tui la nazi, chumvi koroga .

Mwishowe tia vipande vya samaki na rojo lake litakalobakia katika treya, mchuzi uko tayari

Jinsi ya kupika mkate wa sembe

Mahitaji:

Unga sembe glass 1
Unga ngano glass 1
Sukari glass 1 (unaweza kupunguza kidogo)
Maziwa glass 1
Mafuta 1/2 glass
Mayai 4
Iliki iliosagwa 2tbs
Bp 2tbs

Jinsi ya kupika:

Saga sukari yako uweke kwenye bakuli safi pamoja na mayai. Tumia mashine ya cake kusagia hadi ifure/ivimbe.
Weka mafuta saga, weka maziwa saga, weka unga wa ngano na bp(bp imix kwenye unga kabla kumimina kwenye mchanganyiko) changanya vizuri halafu malizia kwa kuweka unga sembe na iliki usage vizuri.

Chukua trey au sufuria safi weka baking paper Mimina mchanganyiko wako na uoke.

Ukiwiva utoe na uwache upoe. Mkate wa sembe utakua tayari kwa kuliwa.

Mapishi ya chipsi na samaki wa kuchoma

Mahitaji

Viazi ulaya (baking potato 5 vya wastani)
Parprika 1 kijiko cha chai
Pilipili mtama ilyosagwa (ground black pepper 1 kijiko cha chai
Kitunguu swaum cha unga (garlic powder 1 kijiko cha chai)
Chumvi (salt)
Mafuta (vegetable oil)
Marination za samaki (angalia kwenye recipe ya samaki ya nyuma)

Matayarisho

Osha viazi na maganda yake kisha vikaushe na uvikate vipande vya wastani. Kwa kila kiazi toa vipande 6. Kisha vitie kwenye bakuli na utie parpika, pilipili mtama ya unga, kitunguu swaum cha unga, chumvi na mafuta kama vijiko 2 vya chakula. Changanya pamoja na kisha uvibake katika oven kwa muda wa dakika 25. Hakikisha vinakuwa rangi ya brown. Vikisha iva vitoe.
Wamarinate samaki, na uwaoke kisha wasevu na potato wedges tayari kwa kuliwa
(Jinsi ya kupika samaki, angalia katika recipe za nyuma)

Jinsi ya kupika vitumbua inavyotakiwa

Mahitaji

Unga wa mchele ( Vikombe 2 vikubwa)
Sukari (Nusu ya kikombe kikubwa)
Hamira ( Nusu ya kijiko cha chai)
Hiliki (Nusu ya kijiko cha chai)
Tui la nazi ( Kikombe kimoja kikubwa)
Unga wa ngano (Vijiko viwili vya chakula)
Mafuta ya kuchomea (Vegetable oil)

Matayarisho

Unachanga unga, sukari, hamira, hiliki, unga wa ngano na tui la nazi pamoja katika bakuli la plastiki. Kisha unaukoroga mpaka mchanganyiko unakuwa kama uji mzito. Kava bakuli lililokuwa na mchanganyiko kisha hifadhi katika sehemu yenye joto kwa muda wa masaa matatu.

Jinsi ya kupika

Weka chuma cha kuchomea vitumbua katika moto wa wastani, kisha weka mafuta kwenye chuma cha kuchomea ( Kijiko kimoja cha chai) mafuta yakisha pata moto tia uji wako (upawa mmoja) katika kila shimo la chuma cha kuchomea. Acha mpaka kitumbua kikauke kisha geuza na tia mafuta. Acha upande wa pili wa kitumbua mpaka uwe rangi ya kahawia na hapo kitumbua kitakuwa kimeiva utakitoa. Rudia hatua hizo kwa vitumbua vyote vilivyobaki.

Jinsi ya kupika Cookies Za Jam Ya Peach Na Raspberry

MAHITAJI

Unga kikombe 1 ยฝ

Siagi ยฝ kikombe

Sukari ยฝ kikombe

Yai 1

Vanilla 1 kijiko cha chai

Jam ya peach na raspberry

MAANDALIZI

Wash oven moto wa takriban 180 โ€“ 190 Deg F
Piga siagi na sukari katika mashine mpaka iwe laini na nyororo (creamy) kisha weka yai na vanilla.
Tia unga kidogo kidogo uchanganye kwa mwiko wa mbao (wooden spoon).
Pakaza mkononi unga uchukue vidonge ubonyeze kufanya vishimo vya kuwekea jam.
Panga katika treya uliyopakaza siagi.
Tia nusu yake jam ya peach na nusu jam ya raspberry
Bake katika oven kiasi robo saa mpaka ziwive na kugeuka rangi ya brown light.
Epua vikiwa tayari

Mapishi ya Mlenda wa bamia na nyanya chungu

Mahitaji

Bamia (okra) 20
Nyanya chungu (garden eggs) 5
Magadi soda (Bicabonate soda) 1/4 ya kijiko cha chai
Nyanya (fresh tomato) 1
Chumvi (salt) kidogo
Pilipili 1/4

Matayarisho

Osha bamia, nyanya chungu na nyanya kisha vikatekate katika vipande vidogovidogo. Baada ya hapo vitie kwenye sufuria na vitu vyote vilivyobakia na kisha tia maji kidogo.Chemsha mpaka bamia na nyanya chungu ziive na vimaji vibakie kidogo sana. Baada ya hapo ziponde na mwiko kidogo kisha zikoroge na uipue na mlenda utakuwa tayari kwa kuliwa na ugali.

Mapishi ya Haliym Ya Nyama Mbuzi -Bokoboko La Pakistan

Mahitaji

Nyama ya mbuzi au ngโ€™ombe ya mafupa – 2 LB

Mchanganyiko wa dengu (hadesi, mchele, chooko, ngano, dengu n.k au nunua ya tayari iliyokwisha changanywa – 2 Vikombe

Kitungu maji (vikate vidogo) – 1

Mafuta – ยผ Kikombe

Nyana kata ndogo ndogo – 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawazi iliyosagwa – 1 Kijiko cha supu

Bizari ya haliym – 2 vijiko vya supu

Nyanya ya kopo – 2 vijiko vya supu

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Chemsha nyama na chumvi ยฝ kijiko mpaka iive, toa mafupa.
Chemsha mchanganyiko wa dengu mpaka ziive.
Katika sufuria weka mafuta, kaanga vitunguu vilainike, tia thomu na tangawizi, bizari ya haliym, nyanya ya kopo. Kaanga mpaka iwive.
Tia nyama iliyowiva na supu yake kidogo.
Tia mchanganyiko wa dengu tia kwenye mashine ya kusaga (blender), saga na ile supu ya nyama isagike vizuri
Mimina kwenye sufuria changanya, tia ndimu kidogo, acha moto mdogo mdogo kwa muda wa dakika 15.
Tia katika bakuli, pambia kwa vitunguu vilivyokaangwa vya rangi ya hudhurungi vikavu, pilipili mbichi (ukipenda) na kotmiri, ikiwa kuliwa.

Mapishi mazuri ya Chapati za maji

Mahitaji

Unga wa ngano (plain flour) ( 1/4 kilo)
Yai (egg 1)
Sukari (sugar 1/4 kikombe cha chai)
Chumvi (salt 1/4 kijiko cha chai)
Hiliki (ground cardamon 1/4 kijiko cha chai)
Maji kiasi
Mafuta (vegetable oil)

Matayarisho

Tia unga kwenye bakuli, kisha weka sukari, chumvi, hiliki na maji kiasi. Kisha koroga mpaka mchanganyiko wako uwe mzito. Baada ya hapo tia yai na ukoroge tena. hakikisha mchanganyiko hauwi mzito sana au mwepesi sana.Baada ya hapo onja kama kila kitu kimekolea. Injika chuma cha kupikia chapati (fry-pan) jikoni katika moto wa wastani. Baada ya hapo tia nusu kijiko cha chakula cha mafuta katika fry-pan na kisha yatandaze. Hakikisha chuma kinapata moto na weka upawa mmoja wa unga wa chapati na uutandaze mpaka uwe flat. Baada ya hapo subiri mpaka chapati ikauke juu na kisha igeuze upande wa pili tia mafuta kijiko 1 kikubwa cha chakula kwa upande wa chini na wa juu kisha uanze kuikandamiza kwa juu na kijiko ili iweze kuiva vizuri kwa chini. Ikisha kuwa ya rangi ya brown igeuze na upike upande wa pili kiasi kisha iipue na uiweke kwenye sahani yenye kitchen towel ili kukausha mafuta. Rudia hii process kwa unga wote uliobakia. Na chapati zitakuwa tayari

Vidokezo 10 vya Vitafunio vya Afya kwa Watoto Wagumu Kula

Vidokezo 10 vya Vitafunio vya Afya kwa Watoto Wagumu Kula

Kama mzazi au mlezi, mara nyingine inaweza kuwa changamoto kubwa kuwapa watoto wako vitafunio vyenye afya, hasa pale ambapo wana tabia ya kuchagua vyakula visivyo na lishe. Lakini usijali! Kama AckySHINE, nina vidokezo 10 vya vitafunio vya afya ambavyo vitawafurahisha watoto wako na kuwapa lishe bora wanayohitaji. Soma ili kugundua!

  1. Matunda yenye rangi:
    Matunda kama vile tufaa, ndizi, au zabibu ni vitafunio bora kwa watoto. Wanaweza kula matunda haya kama yalivyo au kutengeneza saladi ya matunda yenye rangi mbalimbali kwa kuongeza limau kidogo ili kuongeza ladha. ๐ŸŽ๐ŸŒ๐Ÿ‡

  2. Karanga:
    Karanga kama vile njugu, karanga za pekee au karanga za kawaida zina protini nyingi na mafuta yenye afya. Unaweza kuzitoa kama vitafunio vya kati au kuzichanganya na matunda yaliyokatwa ndogo kwa kitafunio bora zaidi. ๐Ÿฅœ

  3. Jibini:
    Jibini ni chanzo kizuri cha protini na madini ya kalsiamu. Unaweza kuwapa watoto wako vipande vidogo vya jibini pamoja na matunda au karanga kama vitafunio vyenye afya. ๐Ÿง€

  4. Yoghurt:
    Yoghurt yenye asili ya maziwa ni chanzo bora cha protini na kalsiamu. Unaweza kuongeza asali au matunda yaliyokatwa ndani yake ili kuongeza ladha na kufanya iwe vitafunio bora zaidi. ๐Ÿฅ›

  5. Mtindi:
    Mtindi ni chanzo kingine bora cha protini na kalsiamu. Unaweza kuongeza matunda yaliyokatwa kidogo au karanga zilizokatwa ndani ya mtindi ili kuongeza ladha na virutubisho vyenye afya. ๐Ÿ“

  6. Sandvihi za mboga:
    Badala ya kutumia mkate wa kawaida, tumia mkate wa ngano nzima au mkate wa mboga kama karoti au matango. Weka mboga zingine kama nyanya au pilipili kwenye sandvihi na uwape watoto wako. Ni vitafunio vyenye lishe bora na rahisi kuandaa. ๐Ÿฅช

  7. Ndizi za kukaanga:
    Ndizi za kukaanga ni vitafunio vya afya na tamu ambavyo watoto wengi hupenda. Unaweza kuzikaanga kwa mafuta ya mizeituni au jibini kidogo ili kuongeza ladha. ๐ŸŒ

  8. Kabeji:
    Kabeji ni mboga yenye lishe na inayoambatana vizuri na vitafunio vingine. Unaweza kutoa vipande vidogo vya kabeji pamoja na dipu ya jibini au mtindi. ๐Ÿฅฌ

  9. Barafu ya matunda:
    Kufanya barafu ya matunda ni njia nzuri ya kuwapa watoto wako kitafunio cha baridi na kitamu. Changanya matunda yaliyosagwa na maji, weka kwenye tray ya barafu na weka kwenye friji hadi itenge. Ni kitafunio bora cha majira ya joto! ๐Ÿง

  10. Chapati za nafaka:
    Badala ya kutumia unga wa ngano, tumia unga wa nafaka kama vile unga wa mtama au ulezi. Chapati za nafaka ni vitafunio bora vyenye lishe na rahisi kuandaa. Unaweza kuzitumia kama sahani ya kando au kuzikata vipande vidogo na kuwapa watoto wako. ๐ŸŒพ

Hivyo basi, kama AckySHINE ninaamini kwamba vitafunio vyenye afya ni muhimu sana kwa watoto wetu. Kwa kufuata vidokezo hivi, unaweza kuwapa watoto wako vitafunio vyenye lishe bora na kuwajenga kwenye tabia ya kula afya. Kumbuka, kuwapa watoto wako vitafunio vyenye afya ni njia bora ya kuwaweka na afya bora na kuwapa nguvu ya kukua na kufanikiwa!

Je, una maoni gani kuhusu vidokezo hivi? Je, umewahi kujaribu vitafunio hivi na kama ndivyo, ni vitafunio vipi ulivyopenda zaidi? Asante kwa kusoma na natarajia kusikia maoni yako! ๐ŸŒŸ

Mapishi ya Wali Wa Kichina Wa Kamba Na Kuku

MAHITAJI

Mchele wa pishori (basmati) – 4

Nyama ya kuku bila mafupa – 1 Lb

Kamba saizi kubwa – 1Lb

Mchanganyiko wa mboga – njegere, karoti,

mahindi, maharage ya kijani (spring beans) – 2 vikombe

Figili mwitu (Cellery) – 2 mche

Vitunguu vya majani (spring onions) – 4-5 miche

Kebeji – 2 vikombe

Pilipili ya unga nyekundu – 1 kijiko cha chai

Pilipili manga ya unga – 1 kijiko cha chai

Sosi ya soya – 3 vijiko vya supu

Mafuta – 1/4 kikombe

Chumvi – kiasi

MAPISHI

Osha na roweka mchele.
Tia kamba chumvi na pilipili nyekundu ya unga. Tia mafuta vijiko viwili katika kikaango (frying pan), kaanga kamba kidogo tu, weka kando.
Katakata kuku vipande vidogo vidogo, tia chumvi na pilipili manga. Kaanga kaTika kikaango (ongeza mafuta kidogo) Weka kando.
Katika karai, tia mafuta kidogo kama vijiko vitatu vya supu, tia kamba na kuku, tia mboga za mchanganyiko, sosi ya soya na chumvi, kaanga kidogo. (Kama mboga sio za barafu) itabidi uchemshe kidogo.
Katakata kebeji, figili mwitu (cellery) na vitunguu vya majani (spring onions) utie katika mchaganyiko. acha kwa muda wa chini ya dakika moja katika moto.
Chemsha mchele, tia mafuta kidogo au siagi, chumvi upikie uive nusu kiini, mwaga maji uchuje.
Changanya vyote na wali rudisha katika sufuria au bakuli la oveni, funika na upike kwa moto wa kiasi kwa muda wa dakika 15-20 takriban.
Epua na upakue katika sahani ukiwa tayari kuliwa.

Jinsi ya kupika Mboga Za Majani Makavu (Aina Yoyote)

Viamba upishi

Mboga za majani makavu ยผ kg
Mafuta vijiko vikubwa 3-4
Karanga zilizosagwa kikombe ยฝ
Maziwa au tui la nazi kikombe 1
Kitunguu 1
Nyanya 2
Chumvi (kama kuna ulazima)
Maji baridi

Hatua

โ€ข Loweka mboga za majani makavu na maji kwa dakika 10-15.
โ€ข Osha , mboga na katakata nyanya na vitunguu.
โ€ข Kangaa, pukusua na saga karanga zilainike.
โ€ข Kanga kitunguu, weka nyanya, koroga zilainike.
โ€ข Ongeza mboga zilizolowekwa na maji yake kwenye rojo, koroga na funikia mpaka maji yakaukie na ive. Punguza moto.
โ€ข Koroga karanga zilizosagwa na maji, ongeza kwenye mboga ukikoroga kwa dakika 5.
โ€ข Onja chumvi, pakua kama kitoweo.
Uwezekano
Weka nyanya kidogo.
Tumia tui la nazi au krimu badala ya maziwa.
Weka nyama au dagaa au Mayai badala ya Karanga.

Mapishi ya Kidheri – Makande

Mahitaji

Nyama (kata vipande vidogodogo) – ยฝ kilo

Maharage – 3 vikombe

Mahindi – 2 vikombe

Kitunguu – 1

Nyanya – 2

Kabichi lililokatwa – 2 vikombe

Kitunguu saumu(thomu/galic) – 1 kijiko cha chai

Vidonge vya supu – 2

Chumvi – kiasi

Mafuta -1au 2 vijiko vya chakula

Namna Yakutayarisha

Chemsha mahindi mpaka yawive na maji yakauke kiasi.
Chemsha maharage pembeni nayo mpaka yawive na maji yakaukie kiasi.
Tia mafuta kwenye sufuria anza kukaanga vitunguu , thomu na vidonge vya supu koroga kiasi.
Kisha mimina nyama iliyokatwa vipande acha ikaangike kidogo na chumvi.
Nyama ikishakaangika tia nyanya funika kwa moto mdogo mpaka nyama iwive.
Kisha mimina mahindi na maharage yaliyochemshwa na maji yake kiasi koroga mpaka ichanganyike na mwisho mimina kabichi funikia mpaka kabichi iwive onja chumvi kama imekolea
Halafu malizia kukoroga mpaka ichanganyike na ikaukie kisha pakua kwenye sahani tayari kwa kuliwa.

Jinsi ya kupika vizuri Wali Wa Karoti Na Nyama

MAHITAJI YA WALI

Mchele – 3 Magi

Mafuta – 1/4 kikombe

Karoti unakata refu refu – 3

Vitunguu maji kata vikubwa vikubwa – 1 kikubwa

Pilipli manga – 1/2 kijicho chai

Hiliki – 1/2 kijiko chai

Karafuu ya unga – 1/4 kijiko cha chai

Mdalasini wa unga – 1/2 kijiko cha chai

Zaafarani (ukipenda) roweka katika maji – 1 kijiko cha chai

Zabibu kavu (ukipenda) – 1/4 kikombe

Chumvi kiasi

KUPIKA WALI

Kwenye sufuria tia mafuta na kaanga karoti kidogo.
Tia vitunguu kisha tia bizari zote.
Tia maji kiasi (kutegemea aina ya mchele) na chumvi
Tia mchele upike uwive.
Karibu na kuwvia tia zabibu ukipenda.
Funika endelea kuupika hadi uwive.

MAHITAJI KWA NYAMA

Nyama – 2 Ratili (LB)

Chumvi – Kiasi

Mafuta – 1/4 kikombe

Kitunguu (kata virefu virefu) – 1 Kikubwa

Pilipili mboga kubwa – 2 ukipenda moja nyekundu moja kijani unazikata vipande virefu virefu.

Figili mwitu (celery) kata vipande virefu virefu- Miche miwili.

KUPIKA NYAMA

Chemsha nyama hadi iwive
Ikaange kwa mafuta hadi iwe nyekundu
Weka vitunguu, pilipili mboga na figili mwitu
Kaanga kidogo tu kama dakika moja.
Tayari kuliwa na wali.

Shopping Cart
29
    29
    Your Cart
    ๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About