Upishi na Maandalizi ya Milo yenye Afya

Jinsi ya kupika Vileja Vya Tambi

Viambaupishi

Tambi (vermiceli Roasted) Mifuko 2

Siagi 4 Vijiko vya supu

Maziwa (condensed) 300Ml

Lozi zilizokatwakatwa 1 kikombe

Zabibu kavu 1 Kikombe

Arki (essence) 1 Kijiko cha supu

Jinsi ya kuandaa na kupika

1) Weka karai kwenye moto kiasi

2) Tia siagi

3) Tia tambi uzikaange usiachie mkoni mpaka ziwe rangu ya dhahabu.

4) Weka lozi na zabibu huku unakoroga

5) Tia maziwa na huku unakoroga usiachie mkono.

6) Tia arki

7) Epua karai, tumia kijiko cha chai kwa kuchotea na utie kwenye kikombe cha kahawa nusu usikijaze.

8) Kipindue kwenye sahani utoe kileja.

9) Fanya hivyo mpaka umalize vyote.

Mapishi mazuri ya Wali Wa Kukaanga Kwa Kidari Cha Kuku

Vipimo vya Wali:

Mchele – 3 vikombe

*Maji ya kupikia – 5 vikombe

*Kidonge cha supu – 1

Samli – 2 vijiko vya supu

Chumvi kiasi

Hiliki – 3 chembe

Bay leaf – 1

Vipimo Vya Kuku

Kidari (chicken breast) – 1Kilo

Kitunguu – 1

Tangawizi mbichi – ½ kipande

Kitunguu saumu(thomu/galic) – 7 chembe

Pilipili mbichi – 3

Ndimu – 2

Pilipilimanga – 1 kijiko cha chai

Mdalasini – ½ kijiko cha chai

Jira/Cummin ya unga – 1 kijiko cha chai

Maji – ¼ kikombe

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Wali:

Osha na roweka mchele kisha weka sufuria katika moto tia samli ipashe moto.
Tia hiliki, bay leaf, kaanga, kisha tia mchele ukaange kidogo.
Tia maji, chumvi na kidonge cha supu, upike wali kama unavyopika pilau.
*Maji kisia kwa kutegemea mchele ulivyo.
*Unaweza kutumia supu yoyote badala ya kidonge.

Kuku:

Katakata kidari cha kuku vipande vya kiasi, weka katika sufuria, tia ndimu, bizari zote, chumvi.
Katakata kitunguu vipande vidogodogo, pilipili, na kitunguu thomu (chopped), tia katika kuku.
Chuna tangawizi mbichi tia katika kuku. Changanya vitu vyote vizuri.
Tia maji kiasi ¼ kikombe tu kiasi cha kumkaushia kuku. Weka katika moto mpike huku unageuzageuza. Anapokaribia kukauka epua akiwa tayari kuliwa na wali (na saladi upendayo)

Mapishi ya samaki aina ya salmon

Mahitaji

Salmon fillet 2
Potatao wedge kiasi
Lettice kiasi
Cherry tomato
Limao 1
Swaum
Chumvi
Olive oil

Matayarisho

Mmarinate samaki na chumvi, swaum na nusu ya limao kisha muweke pembeni, baada ya hapo washa oven kisha tia potato wedge zikisha karibia kuiva anza kumpika samaki, tia mafuta kidogo sana kama kijiko kimoja cha chai hivi katika frypan isiyoshika chini yakisha pata moto kiasi muweke samaki wako (upande wenye ngozi chini kwanza) Mpike mpaka uone rangi ya kahawia kwa chini kisha mgeuze upande wa pili, uku samaki wako akiwa anaendelea kuiva, tayarisha salad yako kwa kusafisha lettice na nyanya kisha zichanganye pamoja kisha tengeneza salad dressing pembeni , kamua limao kisha tia olive oil na chumvi kidogo, Baada ya hapo samaki na potato wedge vitakuwa vimeiva, andaa mlo wako na utakuwa tayari kwa kuliwa.

Mapishi ya Mchemsho wa ndizi na nyama

Mahitaji

Ndizi mbichi 6
Nyama ya ng’ombe (nusu kilo)
Viazi mviringo 2
Kitunguu swaum
Tangawizi
Kitunguu maji
Nyanya 1 kubwa
Mafuta (vegetable oil)
Chumvi
Limao
Pilipili

Matayarisho

Chemsha nyama na limao, kitunguu swaum, tangawizi chumvi na maji kiasi mpaka nyama iive, Hakikisha unaiacha na supu kiasi kwa ajili ya kuwekea kwenye ndizi.Kisha katakata nyanya na vitunguu na uweke pembeni .Menya ndizi na viazi kisha zichemshe pamoja na vitunguu, nyanya, maji kidogo, mafuta na uhakikishe haziivi kabisa. Baada ya hapo tia nyama na supu yake, pilipili mzima na chumvi na uache uchemke mpaka ndizi na viazi viive.Na baada ya hapo mchemsho wako utakuwa tayari kwa kuliwa

Jinsi ya kutengeneza Cookies Za Tende Na Tangawizi

MAHITAJI

Unga vikombe vikombe 4

Baking soda 1 kijiko cha chai mfuto

Siagi 400 gms

Sukari ½ kikombe

Tende chambua ukatekate ifikie ¾ kikombe

Tangawizi ya unga vijiko 2 vya chai

Vanilla 1 kijiko cha chai

Yai 1

Maziwa mazito vijiko 2 vya kulia.

MAANDALIZI

Changanya siagi na sukari katika mashine usage mpaka iwe laini nyororo.
Tia yai uchanganye vizuri
Tia tende na vanilla, tangawizi uchanganye vizuri.
changanya unga na baking soda kisha, mimina kidogo kidogo huku unachanganya kwa kijiko cha ubao (mwiko).
Unga ukiwa mzito ongeza vijiko 2 vya maziwa. Fanya viduara upange katika treya uliyopakaza siagi kisha uchome (bake) katika over moto mdogo wa kiasi dakika 15 vigeuke rangi viwive.
Epua vikiwa tayari

Mapishi ya Biriyani Ya Kuku

Vipimo

Mrowanishe kuku na viungo hivi kwa muda mdogo tu

Kuku (Mkate kate Vipande) – 4 LB

Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi – 2 Vijiko vya supu

Chumvi – kiasi

Pilipili nyekundu ya unga – 1 Kijiko cha supu

Bizari ya manjano (Haldi au Tumeric) – 1 Kijiko cha chai

Bizari ya pilau ya powder (Jeera) – 1 Kijiko cha chai

Gilgilani powder (Dania) – 1 Kijiko cha chai

Ndimu – 1 Kijiko cha supu

Mchele na vitu vya Masala:

Mchele (Basmati mzuri) (rowanisha) – 7 cups

Mafuta ya kupikia – kiasi

Vitunguu Vilivyokatwa – 8

Nyanya iliyokatwa katwa – 3

Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi – 1 Kijiko cha supu

Garam Masala -1 Kijiko cha supu

Hiliki powder – ½ Kijiko cha chai

Tomatoe paste – 1 Kijiko cha supu

Pilipili mbichi zipasue katikati – 4

Chumvi – kiasi

Mtindi – 4 Vijiko vya supu

Kotmiri iliokatwa (Chopped) – ½ Kikombe

Mafuta ya kunyunyuzia katika wali – 3 Vijiko vya supu

Zaafarani au rangi ya biriani – kiasi

Namna Ya Kutaarisha Na Kupika

Weka kuku aliyerowanishwa na viungo vyake katika Foil tray au chombo chocote utakachomwagia wali humo humo na kupikia biriani, kisha mchome (Bake) mpaka awive na awe mkavu kiasi.

Wakati kuku anapikika, kaanga vitunguu katika karai au sufuria mpaka viwe brown na epua nusu yake weka kando.

Punguza mafuta yabakie kiasi tu, ongeza Thomu na tangawizi, na viungo vyote vya hapo juu isipokuwa Mtindi na kotmiri, endelea kukaanga hadi tomatoe zilainike.

Ongeza chumvi, malizia mwisho kwa kutia mtindi, kotmiri na vile vitunguu ulivyoweka kando. Masala yako tayari.

Mwagia masala juu ya kuku uliyekwishmpika changanya vizuri.

Chemsha Mchele uwive nusu, chuja na mwagia juu ya masala.

Nyunyiza mafuta kidogo juu ya mchele na zaafarani au rangi ya biriani.

Bake katika moto wa 350 – 400 kwa muda wa 15 – 20 minutes. Biriyani imekuwa tayari kuliwa.

Mtindi wa kutolea Biriyani:

Mtindi – 1 kikombe

Pilipili mbichi – 1 ndogo

Kitunguu saumu(/galic) thomu – chembe mbili

Nanaa – kiasi

Chumvi – chembe tu

Weka kwenye Blender na uchanganye, kisha mimina katika bakuli

Jinsi ya kupika Biskuti Nyembamba (Wafer Bar) Za Chokoleti Na Njugu

MAHITAJI

Wafer Powder/gram wafer (unga wa biskuti uliosagwa wa tayari) – vikombe 2

Maziwa ya Mgando Matamu ya Kopo – 2 vikombe

Nazi iliyokunwa – ½ Kikombe

Chokoleti vipande vipande – 1 Kikombe

Njugu vipande vipande – ½ Kikombe

Siagi – 227 g

MAPISHI

Yeyusha siagi motoni kisha changanya na unga wa wafer acha kidogo motoni
Mimina katika treya unayochomea itandaze vizuri, kisha mimina maziwa juu yake pamoja na njugu vipande , nazi iliyokunwa na vipande vya chokoleti.
Choma (bake) kwenye oveni kwa moto wa 350ºC kwa dakika 20.
Katakata tayari kwa kuliwa

Jinsi ya kupika Biskuti Za Njugu/Matunda Makavu (Rock Cakes)

Viambaupishi

Unga 4 Vikombe

Sukari 10 Ounce

Siagi 10 Ounce

Mdalasini ya unga 2 vijiko vya chai

Matunda makavu/njugu (kama lozi,
Zabibu, maganda ya chungwa,
Cherries na kadhalika 4 ounce

Maziwa ya maji 4 Vijiko vya supu

Jinsi ya kuandaa na kupika

1) Chukua siagi na sukari koroga na mixer mpaka iwe kama cream.

2) Tia vanilla mdalasini, tia yai moja mix tena endelea kuongeza yai lingine mpaka umalize yote, changanya mpaka iwe laini kama sufi (fluffy)

3) Tia unga na baking powder na dried fruits, changanya na mwiko.

4) Chota mchanganyiko na kijiko cha soup weka kwenye treya ya kupikia tandaza na uma ili upate matundu juu ya biskuti.

5) Pika (bake) kwenye oven lenye moto wa 375 F. kwa muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.

Bisikuti Za Kokoa (Cocoa Biscuits)

Viambaupishi

Siagi 100gm

Unga wa kaukau (cocoa powder) 2 Vijiko vya supu

Maziwa mazito (condensed milk) Moja kikopo (397gm)

Bisikuti za Mary 2 Pakiti

Njugu ½ Kikombe

Karatasi la plastiki

Jinsi ya kuandaa na kupika

1. Vunjavunja bisikuti zote packet mbili ziwe vipande vidogo vidogo.

2. Pasha moto siagi mpaka ipate.

3. Tia kwenya siagi imoto maziwa mazito na cocoa koroga vizuri.

4. Kisha tia kwenye mchanganyiko bisikuti zilizovunjwa na njugu na uchanganye kisha epua motoni.

5. Paka karatasi la plastiki mafuta kidogo halafu tia mchanganyiko kisha kunja (roll).

6. Tia kwenye freeza muda wa saa.

7. Halafu toa karatasi na ukate kate na panga kwenye sahani na itakuwa tayari kwa kuliwa.

Mapishi ya Pasta za cream na uyoga

Mahitaji

Pasta (2 na 1/2 vikombe vya chai)
Uyoga (mashroom 2 vikombe vya chai)
Cream (1 kikombe cha chai)
Mafuta (vegetable oil)
Kitunguu (onion 1)
Chumvi
Majani ya basil (dried basil leaves 1/2 kijiko cha chai)

Matayarisho

Chemsha maji ya kutosha kisha tia chumvi na mafuta kidogo katika hayo maji na baadae tia pasta na uzichemshe mpaka ziive kisha uzichuje maji na uziweka pembeni. Baada ya hapo weka mafuta kidogo katika sufuria kisha tia uyoga uliokatwa na uupike mpaka uive. Baada ya hapo tia majani ya basil, chumvi na cream kisha acha ichemke kisha weka vitunguu na upike kwa muda wa dakika 4 kisha malizia kwa kutia pasta. Zichanganye vizuri na mchanganyiko wote kisha zipike kwa muda wa dakika 5. Na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Unaweza kupika nyama ya kuku (chiken breast) iliyokatwa vipande vidogo vidogo kama saizi na shape ya pasta. Vizuri kuikaanga pembeni mpaka iwe brown na kuiva alafu kuimix kwenye chakula baada ya uyoga na vitunguu kuiva alafu unamix cream kumalizia mapishi.

Vidokezo 10 vya Vitafunio visivyo na Karanga

Vidokezo 10 vya Vitafunio visivyo na Karanga 🥜🚫

Kama unapenda kufurahia vitafunio na unakabiliwa na mzio wa karanga, basi hii ni makala sahihi kwako! Leo, kama AckySHINE, ningependa kushiriki nawe vidokezo 10 vya vitafunio visivyo na karanga ambavyo utaweza kufurahia bila wasiwasi wowote. Tuko pamoja kwenye safari hii ya kufurahia vitafunio bila kujali msongamano wa mzio. Hebu tuanze! 💪😄

  1. 🍓 Matunda yaliyokaushwa: Matunda yakiwa yamekaushwa ni chaguo bora la vitafunio vya afya. Unaweza kuchagua matunda kama tini, zabibu, na apple zilizokaushwa. Ni vitafunio vya asili na vyenye ladha tamu na bora.

  2. 🥕 Mboga mboga za chumvi: Badala ya vitafunio vyenye mafuta mengi, jaribu mboga mboga za chumvi kama vile karoti, matango, na pilipili mboga. Ni vitafunio vya chini katika kalori na vyenye virutubisho vingi muhimu kwa afya yako.

  3. 🍿 Popcorn: Ni vitafunio maarufu sana na vinapatikana kwa urahisi. Unaweza kununua popcorn zilizopikwa tayari au kutengeneza mwenyewe nyumbani. Kumbuka kutumia mafuta ya kupikia ya afya kama vile mafuta ya mzeituni au ya alizeti.

  4. 🍌 Ndizi: Ndizi ni vitafunio vyenye ladha tamu na vinafaida nyingi za kiafya. Unaweza kuchukua ndizi kama vitafunio vyako vya asubuhi au jioni. Pia, unaweza kujaribu kuongeza chaguzi zingine kama ndizi iliyochomwa au ndizi iliyokatwa na kuongeza juisi ya limao juu yake.

  5. 🥚 Mayai: Mayai ni chaguo bora la vitafunio visivyo na karanga. Unaweza kuwapika kukawa mayai ya kuchemsha au kukaanga. Pia, unaweza kuchanganya mayai na mboga mboga kama vitafunio vya kuchoma kwa afya.

  6. 🥨 Mikate ya kusaga: Mikate ya kusaga ni chaguo bora la vitafunio vinavyotumika kila wakati. Unaweza kupaka jibini ya cheddar au mchuzi wa nyanya juu yake. Ni vitafunio vyenye ladha tamu na rahisi kubeba popote uendapo.

  7. 🥦 Korosho: Korosho ni vitafunio vingine vyenye ladha nzuri na vinafaida nyingi za kiafya. Unaweza kuchagua korosho zisizosindikwa au zilizopikwa kwa mafuta kidogo. Ni chaguo nzuri la vitafunio vya kati na vyenye chumvi kidogo.

  8. 🍎 Kabeji za kukaanga: Kabeji za kukaanga ni chaguo bora la vitafunio vya afya. Unaweza kukata kabeji vipande vidogo na kuzikaanga kwenye mafuta kidogo. Kabeji ina kiwango kidogo cha kalori na ina virutubisho vingi muhimu kwa afya yako.

  9. 🍇 Embe: Tunda hili tamu linapatikana kwa urahisi na ni chaguo nzuri la vitafunio visivyo na karanga. Unaweza kula embe kama vitafunio vyako pekee au kuchanganya na matunda mengine katika smoothie ya asubuhi.

  10. 🍪 Biskuti visivyo na karanga: Soko limejaa biskuti zilizotengenezwa kwa ajili ya watu wenye mzio wa karanga. Unaweza kujaribu biskuti zilizotengenezwa kwa kutumia mafuta ya alizeti au mafuta ya kokoa badala ya mafuta ya karanga. Ni vitafunio vya afya na vyenye ladha nzuri.

Kwa hiyo, kama AckySHINE, napenda kukuhimiza kufurahia vitafunio bila wasiwasi wa mzio wa karanga. Kuna chaguzi nyingi nzuri huko nje ambazo utaweza kufurahia bila wasiwasi wowote. Kumbuka daima kusoma maelezo ya viungo kabla ya kununua vitafunio ili kuhakikisha hakuna karanga yoyote iliyomo.

Je, wewe ni mpenzi wa vitafunio? Ni vitafunio gani visivyo na karanga unapenda? 😊

Mapishi ya Bilinganya

Mahitaji

Bilinganya 2 za wastani
Nyanya kubwa 1
Kitunguu maji 1 kikubwa
Swaum 1/2 kijiko cha chai
Limao 1/4
Pilipili ya unga 1/2 kijiko cha chai
Parpika 1/4 kijiko cha chai
Pilipili mtama 1/4 kijiko cha chai
Curry powder1/4 kijiko cha chai
Chumvi kiasi
Coriander
Olive oil

Matayarisho

Katakata bilinganya slice nyembamba kisha ziweke pembeni. Baada ya hapo kaanga kitunguu maji mpaka kiwe cha brown kisha tia swaum na spice zote, zikaange kidogo kisha tia nyanya na chumvi kiasi. Pika nyanya mpaka iive na itengane na mafuta. Baada ya hapo tia mabilinganya na ukamulie limao kisha punguza moto na uyafunike na mfuniko usioruhusu kutoa mvuke ili yaivie na huo mvuke. Baada ya hapo yaonje kama yameiva na malizia kwa kutia fresh coriander na baada ya hapo yatakuwa tayari kwa kuliwa. kwa kawaida mi hupendaga kuyalia na wali na maharage badala ya kachumari kwahiyo nakuwa naitumia hiyo kama kachumbari

Mapishi ya Biskuti Za Jam

VIAMBAUPISHI

Unga 2 ½ gilasi

Sukari ¾ gilasi

Samli 1 gilasi

Mayai 2

Baking powder 2 kijiko vya chai

Vanilla 1 ½ kijiko cha chai

Maganda ya chungwa 1

MAPISHI

Tia kwenye machine ya kusagia (blender) mayai, sukari, vanilla, samli na maganda ya chungwa, saga vizuri.
Tia unga kwenye bakuli pamoja na baking powder, mimina vitu ulivyosaga kwenye bakuli, changanya.
Punguza unga uliochanganya kidogo weka pembeni.
Unga uliobakia tia kwenya tray ya kuchomeya, utandaze vizuri, tia jam juu yake.
Chukua la kukwaruzia carrot (grater) ukwaruze unga uliuopunguza juu ya jam.
Choma kwa muda dakika 20 moto wa 180 C.

Acha ipowe kidogo, zikate vipande vya mraba (square) Tayari kwa kula.

Mapishi ya Pilau Ya Kuku Kwa Mchele Mpya

Mahitaji

Mchele – 1 kilo

Kuku – 1

Vitunguu – 3

Viazi/mbatata – 5

Jira/bizari ya pilau nzima – 3 vijiko vya supu

Mdalasini – 1 kijiti

Pilipili manga – 1 kijiko cha supu

Hiliki – 3 chembe

Karafuu – 5 chembe

Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa – 3 vijiko vya supu

Tangawizi mbichi ilosagwa – 3 vijiko vya supu

Mafuta ya kupikia – ½ kikombe

Chumvi – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Baada ya kumsafisha kuku na kumkatakata, mchemshe kwa chumvi na ndimu, kijiko kimoja cha kitunguu thomu/somu na tangawizi yote..
Menya viazi, katakata vipande vya kiasi.
Katakata vitunguu maji kisha kaanga kwa mafuta katika sufuria ya kupikia pilau.
Tia bizari zote isipokuwa hiliki.
Saga hiliki kisha tia pamoja na kitunguu thomu/somu ukaange kidogo.
Mimina kuku na supu yake ikichemka kisha tia mchele na viazi.
Koroga kisha acha katika moto mdogomdogo wali uwive kama kawaida ya kupika pilau.

Mapishi ya tambi za mayai

Tambi za mayai ni moja kati ya vyakula ambavyo napenda kuandaa pale ninapokua ninaharaka au sina muda mrefu wakukaa jikoni.pishi hili huchukuca muda mfupi sana na nimlo uliokamilika.

Mahitaji

  1. Tambi ½ paketi
  2. Vitunguu maji 2 vikubwa
  3. Karoti 1
  4. Hoho 1
  5. Vitunguu swaumu(kata vipande vidogo) kijiko 1 cha chakula
  6. Carry powder kijiko 1 cha chai
  7. Njegere zilizochemshwa ½ kikombe
  8. Mafuta kwa kiasi upendacho
  9. Mayai 2
  10. Chumvi kwa ladha upendayo

Njia

1.Chemsha maji yamoto yanayotokota,ongeza chumvi na mafuta kidogo,weka tambi kwenye maji hayo chemsha adi ziive.Chuja maji yote ili kupata tambi kavu
2.Katika bakuli piga mayai kisha weka pembeni
3.Katika kikaango,weka mafuta,vitunguu maji ,vitunguu swaumu,hoho, karoti na carry powder,kaanga kwa pamoja katika moto mdogo kwa muda mfupi kwani mboga hazitakiwi kuiva.
4.Ongeza tambi na njegere katika kikaango,geuza kila mara ili kuchanganya .
5.Ongeza mayai kwenye tambi kisha geuza kwa haraka bila kupumzika adi mayai yaive na tambi ziwe kavu.Tayari kwa kula

Katika hatua hii ongeza moto uwe wa wastani,moto ukiwa mdogo mayai yatafanya tambi zishikane na kufanya mabonge.

Mapishi ya Pilau Ya Adesi Za Brown Karoti Na Mchicha Kwa Samaki Wa Salmon

Vipimo

Mchele vikombe 3

Karoti 1 ikune (grate)

Mchicha katakata kiasi

Adesi za brown

Kitunguu katakata (chopped)

Supu ya kitoweo chochote upendayo au vidonge vya supu 2

Garama masala (bizari mchanganyiko) kijiko 1 cha kulia

Samli ¼ kikombe

Chumvi kiasi

Vipimo Vya Samaki Wa Salmon

Samaki wa Salmon vipande 4 vikubwa

Tangawizi mbichi ilosagwa kijiko 1 cha kulia

Thomu (garlic/saumu) kijiko 1 cha kulia

Chumvi kiasi

Bizari ya mchuzi kijiko 1 cha kulia

Ndimu 1 kamua

Nyanya 2 kata slice kubwa kubwa

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Samaki wa Salmon

Changanya viungo vyote upake katika samaki.
Weka katika treya na panga slice za nyanya juu yake.
Oka (grill/choma) katika oven umgeuze samaki upande wa pili.
Akiwa tayari epua.

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Wali

Roweka mchele kiasi kutegemea aina ya mchele. Tumia basmati (pishori)
Roweka adesi kisha zichemshe katika maji ya kiasi. Chuja maji adesi na maji yatakayobakia tumia katika kupikia pilau hii.
Kaanga vitunguu katika samli iliyoshika moto kwenye sufuria ya kupikia.
Vikianza kugeuka rangi tia karoti, mchicha, adesi, bizari mchanganyiko kisha kaanga kidogo.
Tia mchele ukaange kidogo kisha tia supu au maji pamoja na kidonge cha supu.
Tia chumvi ukoroge funika upike kama pilau.
Epua upakue katika sahani utolee kwa samaki wa salmon

Mapishi ya Maharage na spinach

Mahitaji

Maharage yaliyochemshwa kiasi
Spinach zilizokatwa kiasi
Vitunguu maji 2
Nyanya 1/2 kopo
Swaum/Tangawizi 1 kijiko cha chakula
Curry powder 1 kijiko cha chai
Olive oil
Chumvi

Matayarisho

Kaanga vitunguu vikianza kuwa vya brown tia tangawizi/swaum kisha nyanya. Pika mpaka nyanya ziive kisha tia curry powder na chumvi. Vipike kiasi kisha tia maharage na maji kidogo kisha funika na uache vichemke. Baada ya muda tia spinach vipike pamoja na maharage mpaka ziive kisha ziipue. Baada ya hapo mboga yako itakuwa tayari kwa kuseviwa.

Mapishi ya Ndizi na samaki

Mahitaji

Ndizi laini (Matoke 6)
Viazi mbatata (potato 3)
Samaki wabichi wa wastani ( Fresh tilapia 2)
Kitunguu swaum (garlic 6 cloves)
Tangawizi (fresh ground ginger vijiko 2 vya chai)
Nyanya ya kopo (tin tomato 1/2 kopo)
Vitunguu (onion 1)
Pilipili (chilli 1 nzima)
Chumvi (salt to your taste)
Mafuta (vegetable oil)
Limao (lemon 1/2)
Curry powder (1/2 kijiko cha chai)

Matayarisho

Safisha samaki kisha wakate vipande vitatu. Wakaushe maji kisha wamarinate na kitunguu swaum,tangawizi, chumvi, na limao kwa muda wa masaa 2. baada ya hapo waoke kwenye oven kwa muda wa dakika 30. baada ya hapo andaa ndizi na viazi kwa kuzimenya na kuziosha kisha ziweke pembeni. Kisha katakata vitunguu maji, Tangawizi, vitunguu swaum na nyanya kisha vitie kwenye blenda na usage mpaka mchanganyiko usagike vizuri. Baada ya hapo tia mchanganyiko katika sufuria na ubandike jikoni, acha uchemke mpaka maji yote yakauke. Maji yakisha kauka punguza moto na utie mafuta, curry powder, pilipili na chumvi. Kaangiza mpaka mchanganyiko uive na baada ya hapo tia viazi na maji kiasi na uache viazi vichemke mpaka vikaribie kuiva kisha tia ndizi na samaki na ufunike. Pika mpaka ndizi na viazi viive. Baada ya hapo chakula kitakuwa tayari kwa kuseviwa.

JINSI YA KUANDAA VILEJA

MAHITAJI

Unga wa mchele – 500g

Samli – 250g

Sukari – 250g

Hiliki iliyosagwa – 1/2 kijiko cha chai

Arki (rose flavour) – 1/2 kijiko cha chai

Baking powder – 1 kijiko cha chai

Mayai – 4

Maji ya baridi – 1/2 kikombe cha chai

MAANDALIZI

Saga sukari iwe laini kiasi, changanya unga wa mchele, baking powder, hiliki na sukari.
Pasha moto samli mpaka iwe nyepesi kama maji mimina kwenye ule mchanganyiko wa unga wa mchele, kisha uchanganye pamoja na arki.
Ongeza mayai yaliopigwa endelea kuchanganya mpaka unga umeanza kuchanganyika vizuri.
Ongeza maji ya baridi sana kama nusu kikombe tu ili uchanganyike vizuri.
Kata kwa design unayotaka viwe vinene visiwe kama cookies za kawaida kama ilivyo kwenye picha na ukipenda utaweka kidoto kwa kutumia zaafarani katikati ya kileja kama inavyoonesha hapo juu.
Choma kwa moto wa baina ya 300F na 350F kwa dakika 15 mpaka 20 visiwe vyekundu toa na tayari kwa kuliwa.

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About