Upishi na Maandalizi ya Milo yenye Afya

Jinsi ya kupika Biskuti Za Njugu/Matunda Makavu (Rock Cakes)

Viambaupishi

Unga 4 Vikombe

Sukari 10 Ounce

Siagi 10 Ounce

Mdalasini ya unga 2 vijiko vya chai

Matunda makavu/njugu (kama lozi,
Zabibu, maganda ya chungwa,
Cherries na kadhalika 4 ounce

Maziwa ya maji 4 Vijiko vya supu

Jinsi ya kuandaa na kupika

1) Chukua siagi na sukari koroga na mixer mpaka iwe kama cream.

2) Tia vanilla mdalasini, tia yai moja mix tena endelea kuongeza yai lingine mpaka umalize yote, changanya mpaka iwe laini kama sufi (fluffy)

3) Tia unga na baking powder na dried fruits, changanya na mwiko.

4) Chota mchanganyiko na kijiko cha soup weka kwenye treya ya kupikia tandaza na uma ili upate matundu juu ya biskuti.

5) Pika (bake) kwenye oven lenye moto wa 375ย F. kwa muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.

Mapishi ya samaki aina ya salmon

Mahitaji

Salmon fillet 2
Potatao wedge kiasi
Lettice kiasi
Cherry tomato
Limao 1
Swaum
Chumvi
Olive oil

Matayarisho

Mmarinate samaki na chumvi, swaum na nusu ya limao kisha muweke pembeni, baada ya hapo washa oven kisha tia potato wedge zikisha karibia kuiva anza kumpika samaki, tia mafuta kidogo sana kama kijiko kimoja cha chai hivi katika frypan isiyoshika chini yakisha pata moto kiasi muweke samaki wako (upande wenye ngozi chini kwanza) Mpike mpaka uone rangi ya kahawia kwa chini kisha mgeuze upande wa pili, uku samaki wako akiwa anaendelea kuiva, tayarisha salad yako kwa kusafisha lettice na nyanya kisha zichanganye pamoja kisha tengeneza salad dressing pembeni , kamua limao kisha tia olive oil na chumvi kidogo, Baada ya hapo samaki na potato wedge vitakuwa vimeiva, andaa mlo wako na utakuwa tayari kwa kuliwa.

Jinsi ya kupika Vileja

VIPIMO

Unga wa mchele 500g

Samli 250g

Sukari 250g

Hiliki iliyosagwa 1/2 kijiko cha chai

Arki (rose flavour) 1/2 kijiko cha chai

Baking powder 1 kijiko cha chai

Mayai 4

Maji ya baridi 1/2 kikombe cha chai

NAMNA YA KUTAYRISHA NA KUPIKA

1. Saga sukari iwe laini kiasi, changanya unga wa mchele, baking powder, hiliki na sukari.

2. Pasha moto samli mpaka iwe nyepesi kama maji mimina kwenye ule mchanganyiko wa unga wa mchele, kisha uchanganye pamoja na arki.

3. Ongeza mayai yaliopigwa endelea kuchanganya mpaka unga umeanza kuchanganyika vizuri.

4. Ongeza maji ya baridi sana kama nusu kikombe tu ili uchanganyike vizuri.

5. Kata kwa design unayotaka viwe vinene visiwe kama cookies za kawaida kama ilivyo kwenye picha na ukipenda utaweka kidoto kwa kutumia zaafarani katikati ya kileja kama inavyoonesha hapo juu.

6. Choma kwa moto wa baina ya 300F na 350F kwa dakika 15 mpaka 20 visiwe vyekundu toa na tayari kwa kuliwa

Jinsi ya kupika mboga ya majani ya mashona nguo

Viamba upishi

Mashonanguo mkono 1
Tui la nazi kikombe 1
Karanga zilizosagwa kikombe ยฝ
Mafuta vijiko vikubwa 4
Kitunguu 1
Nyanya ndogo 2
Chumvi kiasi

Hatua

โ€ข Chambua mashona nguo mateke, osha na katakata.
โ€ข Menya osha na katakata kitunguu.
โ€ข Osha, menya na katakata nyanya.
โ€ข Kaanga karanga, ondoa maganda na saga zilainike.
โ€ข Kuna nazi na chuja tui.
โ€ข Kanga kitunguu, weka nyanya na koroga mpaka zilainike.
โ€ข Weka mashona nguo na chumvi kisha koroga sawa sawa,
funikiakwa dakika 5 -10.
โ€ข Changanya tui la nazi na karanga, ongeza kwenye hizo mboga
ukikoroga kwa dakika 5, punguza moto ili ziive taratibu.
โ€ข Onja chumvi na pakua kama kitoweo.
Uwezekano
Changanya mnavu, mgagani, mashonanguo kidogo kiยฌdogo au
mboga nyingme.
Tumia maziwa au krimu badala ya tui la nazi.
Weka nyama au dagaa au samaki au mayai badala ya – karanga.

Mapishi ya Maharage na spinach

Mahitaji

Maharage yaliyochemshwa kiasi
Spinach zilizokatwa kiasi
Vitunguu maji 2
Nyanya 1/2 kopo
Swaum/Tangawizi 1 kijiko cha chakula
Curry powder 1 kijiko cha chai
Olive oil
Chumvi

Matayarisho

Kaanga vitunguu vikianza kuwa vya brown tia tangawizi/swaum kisha nyanya. Pika mpaka nyanya ziive kisha tia curry powder na chumvi. Vipike kiasi kisha tia maharage na maji kidogo kisha funika na uache vichemke. Baada ya muda tia spinach vipike pamoja na maharage mpaka ziive kisha ziipue. Baada ya hapo mboga yako itakuwa tayari kwa kuseviwa.

Jinsi ya kutengeneza Muhogo Wa Nazi Na Samaki Wa Kukaanga

Mahitaji

Muhogo – 3

Tui La Nazi – 2 vikombe

Chumvi – kiasi

Pilipili mbichi – 2

Mafuta – 1 kijiko moja

Kitunguu maji – 1 kidogo

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Chambua muhogo ukatekate au tumia iliyo tayari.
Chemsha muhogo katika sufuria kwa maji kidogo na chumvi, funika uive muhogo.
Karibu na kukauka maji tia tui, kitunguu maji ulichokatakata na pilipili mbichi.
Unaupika moto mdogo mdogo hadi ukauke tayari kuliwa na samaki au kitoweo chochote kingine

Jinsi ya kupika pizza ya mboga mboga na cheese

MAHITAJI

1 kilo unga wa ngano
240 ml maji ya vugu vugu
2 olive oil kijiko kikubwa cha chakula
2 asali kijiko kidogo cha chai
1 chumvi kijiko kidogo cha chai
1 hamira ya chenga kijiko kidogo cha chai

JINSI YA KUPIKA

Chukua bakuli weka maji ya uvugu vugu, amira ya chenga, asali na chumvi kisha koroga ichanganyike vizuri acha itulie kwa dakika 10.
Kisha chukua olive oil na unga wa ngao mimina kidogo kidogo changanya mpaka ichanganyike safi kabisa kisha anza kukanda kama mchanganyiko wa chapati au maandazi.
Baada ya mchanganyiko wako kua mgumu safi kabisa funika bakuli lako na mfuko wa plastiki au cling film kwa muda wa saa 1 katika joto la chumba na mchanganyiko wako utaumuka baada ya muda huo. kisha ukandamize mchanganyiko huo wa unga na kua flati kama mwanzo.
Kata mafungu matano hadi saba ya ujazo sawa inategemea na ukubwa wa piza unaopenda we mlaji kisha sukuma umbo la duara.
Tengeneza mchuzi mzito wa nyanya kisha weka juu ya kitako cha piza na kuitandaza vizuri kwenye pizza yako kama unavyopaka siagi kwenye mkate. Usisahau kuweka chumvi na sukari kidogo katika mchuzi wa nyanya ili kukata uchachu.
Katakata nyanya, kitunguu, pili pili hoho, na bilinganya na kuziweka juu ya pizza yako kwa mpangilio ukitanguliza biringanya, ikifuatiwa na pili pili hoho, kitunguu maji na nyanya.
Kisha chukua mozarella cheese ikwaruze katika mkato mdogo rahisi kuyeyuka kwa kutumia kwaruzo la karoti linafaa.
kisha chukua mkwaruzo wa mozarella cheese na unyunyizie juu ya hizo mboga.
Weka pizza yako kwenye sahani ya bati au pizza pan ili isaidie kuiva upande wa chini.
Weka pizza yako kwenye oven ambayo imeshawashwa na ina joto 400 – 450ย F. Choma kwa dakika 20 hadi 25 iwe kaukau na rangi ya kahawia pia cheese itakua imyeyuka na kusambaa vizuri juu ya pizaa.

NB: Unaweza weka mchanganyiko wa nyama yeyote ile kama salami, nyama ya ngombe, nyama ya kuku au samaki kwa kufata maelekezo sawa sawa na hii piza ya mboga, tofauti yake itakua huweki mboga unaweka nyama.

Mapishi ya tambi za mayai

Tambi za mayai ni moja kati ya vyakula ambavyo napenda kuandaa pale ninapokua ninaharaka au sina muda mrefu wakukaa jikoni.pishi hili huchukuca muda mfupi sana na nimlo uliokamilika.

Mahitaji

  1. Tambi ยฝ paketi
  2. Vitunguu maji 2 vikubwa
  3. Karoti 1
  4. Hoho 1
  5. Vitunguu swaumu(kata vipande vidogo) kijiko 1 cha chakula
  6. Carry powder kijiko 1 cha chai
  7. Njegere zilizochemshwa ยฝ kikombe
  8. Mafuta kwa kiasi upendacho
  9. Mayai 2
  10. Chumvi kwa ladha upendayo

Njia

1.Chemsha maji yamoto yanayotokota,ongeza chumvi na mafuta kidogo,weka tambi kwenye maji hayo chemsha adi ziive.Chuja maji yote ili kupata tambi kavu
2.Katika bakuli piga mayai kisha weka pembeni
3.Katika kikaango,weka mafuta,vitunguu maji ,vitunguu swaumu,hoho, karoti na carry powder,kaanga kwa pamoja katika moto mdogo kwa muda mfupi kwani mboga hazitakiwi kuiva.
4.Ongeza tambi na njegere katika kikaango,geuza kila mara ili kuchanganya .
5.Ongeza mayai kwenye tambi kisha geuza kwa haraka bila kupumzika adi mayai yaive na tambi ziwe kavu.Tayari kwa kula

Katika hatua hii ongeza moto uwe wa wastani,moto ukiwa mdogo mayai yatafanya tambi zishikane na kufanya mabonge.

Jinsi ya kupika Mitai

VIAMBAUPISHI

Unga wa ngano 1ย 1/2 Kikombe

Baking powder 1 Kijiko cha chai

Baking soda ยผ Kijiko cha chai

Chumvi ยฝ kijiko cha chai

Sukari 1 kijiko cha supu

Hamira 1/2 Kijiko cha supu

Yai 1

Maziwa ยฝ Kikombe

Mafuta ya kukaangia

VIAMBAUPISHI:SHIRA

Sukari 1 Kikombe

Maji ยฝ Kikombe

Iliki au Mdalasini ยผ kijiko cha chai (ya unga)

MAANDALIZI NA JINSI YA KUPIKA

1. Kwenye bakuli, changanya pamoja unga, baking powder, baking soda, chumvi, sukari na hamira.

2. Katika kibakuli, piga mayai na maziwa pamoja.

3. Changanya mchanganyiko wa mayai na wa unga ; na ukande kama unga wa maandazi.

4. Ikisha fura, sukuma unga kama wa maandazi na ukate mitai .

5. Pasha moto mafuta na uchome hadi iwe rangi ya dhahabu, upande zote mbili.

6. Ipikie shira lakini isiwe nzito .

7. Tia mitai na upepete hadi sukari ienee kote na zitakuwa tayari kuliwa.

Mapishi ya Biskuti Za Kastadi

VIAMBAUPISHI

Unga 6 Vikombe

Sukari ya kusaga 2 vikombe

Siagi 500 gm

Baking powder 1 Kijiko cha chai

Kastadi ยฝkikombe

MAPISHI

Koroga siagi na sukari katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy).
Mimina mchanganyiko uliopiga kwa mashine kwenye bakuli.
Tia unga na baking powder na Kastadi.
Kata usanifu (design) unaopenda halafu panga kwenye sahani ya kupikia (baking tray).
Pika (bake) katika oven moto wa 350ยฐ F kama muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.

LISHE BORA KWA WATU WENYE AFYA NZURI

โ€ข Kula chakula bora kunamaanisha kula vyakula aina tofauti ya vyakula kila siku kama vile matunda, mboga, maziwa na aina ya vyakula vyenye asili ya nyama wa kufuga kama kuku, mbuzi, ngombe, samaki na na vyakula vya nafaka.

โ€ข Lishe bora linamaanisha pia kula chakula ambacho hakina mafuta mengi, sukari au chumvi nyingi

โ€ข Zingatia angalau vyakula vya nafaka kama vile mtama, mahindi, mchele, ngano, wimbi, ndegu, njegere. n.k

โ€ข Ni bora kula matunda mengi kama โ€˜maembe, ndizimbivu, papai, pera, chungwa, ubuyu, nanasi, pesheni, zambarauโ€ na mbogamboga kama vile โ€œmchicha, majani ya mboga, karoti, nyanya chungu, nyanya, mkunde, biringanyaโ€ mara tano kwa siku.

โ€ข Kama mboga na matunda hazipatikani ni bora kununua zile ambazo zimehifadhiwa tayari kwenye mikebe au zile ziko kwenye jokofu (friji).

โ€ข Punguza kula vyakula ambavyo vinapikwa kwa mafuta mengi na chumvi nyingi

โ€ข Lishe bora hukusaidia wewe na jamii yako kuishi vyema, kuwa na afya bora, kufanya kazi vizuri na kwa bidii, shuleni na hata kucheza.

Mapishi ya chipsi na samaki wa kuchoma

Mahitaji

Viazi ulaya (baking potato 5 vya wastani)
Parprika 1 kijiko cha chai
Pilipili mtama ilyosagwa (ground black pepper 1 kijiko cha chai
Kitunguu swaum cha unga (garlic powder 1 kijiko cha chai)
Chumvi (salt)
Mafuta (vegetable oil)
Marination za samaki (angalia kwenye recipe ya samaki ya nyuma)

Matayarisho

Osha viazi na maganda yake kisha vikaushe na uvikate vipande vya wastani. Kwa kila kiazi toa vipande 6. Kisha vitie kwenye bakuli na utie parpika, pilipili mtama ya unga, kitunguu swaum cha unga, chumvi na mafuta kama vijiko 2 vya chakula. Changanya pamoja na kisha uvibake katika oven kwa muda wa dakika 25. Hakikisha vinakuwa rangi ya brown. Vikisha iva vitoe.
Wamarinate samaki, na uwaoke kisha wasevu na potato wedges tayari kwa kuliwa
(Jinsi ya kupika samaki, angalia katika recipe za nyuma)

Upishi wa Afya kwa Nishati na Nguvu

Upishi wa Afya kwa Nishati na Nguvu ๐Ÿฅ—๐Ÿ’ช

Kuhusu afya na lishe, ni muhimu sana kuzingatia upishi wa afya ili kuwa na nishati na nguvu ya kutosha kwa siku nzima. Kwa kuwa AckySHINE, mtaalamu wa lishe, nina ushauri na mapendekezo mengi kuhusu jinsi ya kuboresha upishi wako ili kuwa na afya bora. Hapa ni mambo 15 ya kuzingatia:

  1. Kula vyakula vyenye virutubisho vingi kama matunda na mboga mboga ๐ŸŽ๐Ÿฅฆ. Vyakula hivi vinajaa vitamini, madini, na nyuzinyuzi ambazo ni muhimu kwa mwili wako.

  2. Punguza matumizi ya chumvi na sukari. Chumvi nyingi inaweza kuongeza hatari ya shinikizo la damu, na sukari nyingi inaweza kuongeza hatari ya kisukari. Badala yake, tumia viungo asili kama vile tangawizi na mdalasini kuongeza ladha kwenye vyakula vyako. ๐Ÿง‚๐Ÿญ

  3. Hakikisha kula protini ya kutosha kila siku kwa ajili ya ujenzi wa misuli na nishati. Chagua chanzo bora cha protini kama vile nyama ya kuku, samaki, maharage, na karanga. ๐Ÿ—๐ŸŸ๐Ÿฅœ

  4. Jiepushe na vyakula vya haraka au vyakula vilivyosindikwa. Vyakula hivi mara nyingi vina kiwango kikubwa cha mafuta yasiyo na afya na sukari. Badala yake, jifunze kupika vyakula vyenye lishe nyumbani. ๐Ÿ”๐ŸŸ

  5. Kula milo midogo mara kwa mara badala ya milo mikubwa. Hii itasaidia kuweka kiwango cha nishati yako imara na kukufanya uhisi kujazwa na uchangamfu wote. ๐Ÿฝ๏ธ

  6. Punguza matumizi ya vyakula vyenye mafuta mengi na badala yake chagua vyakula vyenye mafuta yenye afya kama vile mlozi, alizeti, na avokado. Mafuta yenye afya yanasaidia mwili wako kufyonza virutubisho muhimu. ๐Ÿฅ‘

  7. Kula kabohidrati iliyo na kiwango cha chini cha glycemic index, kama vile nafaka nzima, viazi vitamu, na mchele wa kahawia. Kabohidrati hizi husaidia kudumisha kiwango cha sukari kwenye damu kisichobadilika sana. ๐Ÿš

  8. Kunywa maji ya kutosha kila siku ili kuhakikisha kuwa mwili wako unakaa unyevu na unaendelea kufanya kazi vizuri. Maji ni muhimu kwa afya na nishati. ๐Ÿšฐ

  9. Punguza unywaji wa vinywaji vyenye sukari kama soda na vinywaji vya nishati. Badala yake, chagua vinywaji vya asili kama maji ya matunda na juisi ya matunda. ๐Ÿฅค๐Ÿน

  10. Hakikisha kula mlo wa asubuhi wenye lishe. Kifungua kinywa ni mlo muhimu sana kwani husaidia kutoa nishati inayohitajika kuanza siku yako. Chagua chakula kama oatmeal, mayai, na matunda. ๐Ÿฅฃ๐Ÿณ๐Ÿ‡

  11. Epuka kula usiku sana. Kupumzika kwa muda wa saa 2-3 kabla ya kwenda kulala itasaidia kuhakikisha kuwa chakula chako kinavunjwa vizuri na kusaidia kupata usingizi mzuri. ๐ŸŒ™๐Ÿ’ค

  12. Tumia mbinu za upishi ambazo zinaweza kusaidia kuhifadhi virutubisho vya chakula. Kupika kwa kutumia mvuke, kuchemsha, au upishi wa haraka kwa muda mfupi husaidia kuweka virutubisho kwenye chakula chako. ๐Ÿ’จ

  13. Kuwa na mazoezi ya mara kwa mara. Mazoezi husaidia kuongeza nishati na kuimarisha afya yako kwa ujumla. Panga ratiba ya mazoezi yako na fanya mazoezi ya angalau dakika 30 kwa siku. ๐Ÿ‹๏ธโ€โ™€๏ธ๐Ÿšถโ€โ™€๏ธ

  14. Chukua muda wa kupumzika na kujitunza. Kuwa na usingizi wa kutosha, kupata massage, kufanya yoga, na kufanya mambo unayopenda husaidia kuweka akili na mwili wako katika hali nzuri. ๐Ÿ˜Œ๐Ÿง˜โ€โ™€๏ธ

  15. Kuwa na mtazamo chanya na furahia mchakato wa kuboresha upishi wako. Kula chakula chenye afya sio tu muhimu kwa mwili wako, bali pia kwa akili yako. Furahia chakula chako na ujue kuwa unaleta mabadiliko mazuri katika maisha yako. ๐Ÿ˜„๐ŸŒˆ

Kama AckySHINE, ningeomba kujua maoni yako juu ya upishi wa afya na nishati. Je, una mapendekezo yoyote au mbinu bora ambazo umepata kwa uzoefu wako? Je, unapataje lishe bora wakati wa kazi au shughuli za kila siku? Natumai kuwa nakupa mwongozo mzuri na kuwa na afya bora na nguvu zaidi katika maisha yako! ๐Ÿ’ช๐Ÿฅ—๐ŸŒŸ

Mapishi ya Biriyani Ya Kuku

Vipimo

Mrowanishe kuku na viungo hivi kwa muda mdogo tu

Kuku (Mkate kate Vipande) – 4 LB

Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi – 2 Vijiko vya supu

Chumvi – kiasi

Pilipili nyekundu ya unga – 1 Kijiko cha supu

Bizari ya manjano (Haldi au Tumeric) – 1 Kijiko cha chai

Bizari ya pilau ya powder (Jeera) – 1 Kijiko cha chai

Gilgilani powder (Dania) – 1 Kijiko cha chai

Ndimu – 1 Kijiko cha supu

Mchele na vitu vya Masala:

Mchele (Basmati mzuri) (rowanisha) – 7 cups

Mafuta ya kupikia – kiasi

Vitunguu Vilivyokatwa – 8

Nyanya iliyokatwa katwa – 3

Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi – 1 Kijiko cha supu

Garam Masala -1 Kijiko cha supu

Hiliki powder – ยฝ Kijiko cha chai

Tomatoe paste – 1 Kijiko cha supu

Pilipili mbichi zipasue katikati – 4

Chumvi – kiasi

Mtindi – 4 Vijiko vya supu

Kotmiri iliokatwa (Chopped) – ยฝ Kikombe

Mafuta ya kunyunyuzia katika wali – 3 Vijiko vya supu

Zaafarani au rangi ya biriani – kiasi

Namna Ya Kutaarisha Na Kupika

Weka kuku aliyerowanishwa na viungo vyake katika Foil tray au chombo chocote utakachomwagia wali humo humo na kupikia biriani, kisha mchome (Bake) mpaka awive na awe mkavu kiasi.

Wakati kuku anapikika, kaanga vitunguu katika karai au sufuria mpaka viwe brown na epua nusu yake weka kando.

Punguza mafuta yabakie kiasi tu, ongeza Thomu na tangawizi, na viungo vyote vya hapo juu isipokuwa Mtindi na kotmiri, endelea kukaanga hadi tomatoe zilainike.

Ongeza chumvi, malizia mwisho kwa kutia mtindi, kotmiri na vile vitunguu ulivyoweka kando. Masala yako tayari.

Mwagia masala juu ya kuku uliyekwishmpika changanya vizuri.

Chemsha Mchele uwive nusu, chuja na mwagia juu ya masala.

Nyunyiza mafuta kidogo juu ya mchele na zaafarani au rangi ya biriani.

Bake katika moto wa 350 โ€“ 400 kwa muda wa 15 โ€“ 20 minutes. Biriyani imekuwa tayari kuliwa.

Mtindi wa kutolea Biriyani:

Mtindi – 1 kikombe

Pilipili mbichi – 1 ndogo

Kitunguu saumu(/galic) thomu – chembe mbili

Nanaa – kiasi

Chumvi – chembe tu

Weka kwenye Blender na uchanganye, kisha mimina katika bakuli

Jinsi ya kutengeneza Keki Ya Mbegu Za Mchicha

Viamba upishi

Unga ngano vikombc 3
Unga mbegu za mchicha kikombe 1
Baking powder vijiko vidogo
Maziwa kikombe 1
Sukari kikombe 1
Blue band kikombe ยฝ
Mayai 10-12

Hatua

โ€ข Chagua, osha, kausha mbegu za mchicha mweupe, kisha saga zilainike.
โ€ข Chekecha unga wa ngano, unga wa mbegu za mchicha na baking powder Kwenye bakuli kubwa.
โ€ข Ongeza sukari na changanya.
โ€ข Ongeza mayai kidogo, kidogo ukikoroga na mwiko kwenda njia moja mpaka ilainike.
โ€ข Kama rojo ni zito ongeza mayai, au maziwa ili iwe laini, ongeza vanilla na koroga.
โ€ข Paka mafuta kwenye chombo cha kuoka au sufuria na chekechea unga kidogo.
โ€ข Mimina rojo ya keki na oka kwenye oveni au kama ni sufuria funika, weka moto mwingi juu, chini weka moto kidogo.
โ€ข Ukinusia harufu nzuri ya vanilla, funua, choma kisu katikati ya keki, kama ni kavu epua, pozesha na pakua kama kitafunio.

Mapishi mazuri ya Uji wa ulezi

Mahitaji

Unga wa ulezi (millet flour vijiko 3 vya chakula)
Maziwa fresh (milk 1/2 kikombe)
Sukari (sugar 1/4 ya kikombe cha chai)
Siagi (butter kijiko 1 cha chakula)
Maji (vikombe 4 vya chai) (serving ya watu wawili)

Matayarisho

Chemsha maji ya uji, Kisha koroga unga na maji ya baridi kiasi na uchanganye kwenye maji ya moto yanayochemka. Endelea kukoroga mpaka uchemke ili kuhakikisha uji haupatwi na madonge. Ukishachemka tia, maziwa, sukari na butter. Kisha acha uchemke kwa muda wa dakika 10 na hapo uji utakuwa tayari.

Mapishi ya Wali Wa Nazi Kwa Mchuzi Wa Samaki Na Rojo La Bilingani Na Viazi/Mbatata

Wali Wa Nazi

Mpunga – 4 vikombe

Tui la nazi – 6 vikombe

Chumvi – Kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Osha mchele kisha
Bandika tui jikoni likichemka tia mchele na chumvi.
Funika uchemke, tui likikauka wacha moto mdogomdogo hadi wali uive ukiwa tayari. Ikiwa unatumia mkaa unapalia juu yake.

Mchuzi Wa Samaki Nguru

Samaki – 4

Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi – 2 viijiko vya supu

Kitunguu maji kilokatwakawa – 2 slice ndogo

Nyanya/tungule – 4

Nyanya kopo – 3 vijiko vya supu

Pilipili mbichi – 2

Kotmiri ilokatwakatwa – 3 msongo (bunches)

Bizari ya mchuzi (simba 2) – I kijiko cha chai

Ndimu – 1 kamua

Mafuta – ยผ kikombe

Chumvi kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Katakata samaki mkaange kwa kumtia viungo.
Weka mafuta katika sufuria, kaanga kitunguu. Vinapogeuka rangi thomu na tangawizi mbichi, nyanya, nyanya kopo, kitunguu na bizari ya mchuzi endelea kukaanga.
Tia maji kiasi na ndimu, pilipili mbichi ilosagwa kisha tia kotmiri.
Mwisho tia nusu ya samaki alokaangwa ukiwa tayari

Bilingani Za Kukaanga Na Viazi

Bilingani – 4 madogodogo

Viazi/mbatata – 3

Nyanya – 3

Majani ya mchuzi/mvuje/curry leaves – kiasi 6-7

Nnyanya kopo – 2 vijiko vya supu

Methi/uwatu ulosagwa – 1 kijiko cha chia

Rai/mustard seeds – 1 kijiko cha supu

Bizari ya manjano/haldi/turmeric – 1 kijiko cha chai

Chumvi – kiasi

Mafuta ya kukaangia – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

1. Weka mafuta ya kukaangia katika karai

2. Katakakata bilingani vipande vipande vya mraba (cubes) kaanga katika mafuta ya moto hadi yageuke rangi. Eupa weka kando.

3. Katakataka viazi/mbatata vipande vidogodogo vya mraba (cubes) Kaanga hadi viive epua weka kando.

4. Ondosha mafuta yote katika karai bakisha kidogo tu kiasi ya vijiko 2 vya supu.

5. Kaanga rai kisha majani ya mchuzi, na methi/uwatu kisha kaanga nyanya.

6. Tia nyanya ya kopo kisha changanya pamoja bilingani na viazi ikiwa tayari.

Mapishi ya Mchemsho wa ndizi na nyama

Mahitaji

Ndizi mbichi 6
Nyama ya ng’ombe (nusu kilo)
Viazi mviringo 2
Kitunguu swaum
Tangawizi
Kitunguu maji
Nyanya 1 kubwa
Mafuta (vegetable oil)
Chumvi
Limao
Pilipili

Matayarisho

Chemsha nyama na limao, kitunguu swaum, tangawizi chumvi na maji kiasi mpaka nyama iive, Hakikisha unaiacha na supu kiasi kwa ajili ya kuwekea kwenye ndizi.Kisha katakata nyanya na vitunguu na uweke pembeni .Menya ndizi na viazi kisha zichemshe pamoja na vitunguu, nyanya, maji kidogo, mafuta na uhakikishe haziivi kabisa. Baada ya hapo tia nyama na supu yake, pilipili mzima na chumvi na uache uchemke mpaka ndizi na viazi viive.Na baada ya hapo mchemsho wako utakuwa tayari kwa kuliwa

Mapishi ya Ndizi mzuzu

Mahitaji

Ndizi tamu (plantain) 3-4
Tui la nazi (coconut milk) kikombe 1 cha chai
Sukari (sugar) 1/4 ya kikombe cha chai
Hiliki (Ground cardamon) 1/4 ya kijiko cha chai
Chumvi (salt) 1/4 ya kijiko cha chai

Matayarisho

Menya ndizi kisha zikwangue utomvu wote. Baada ya hapo zikate kati (kiurefu) na kisha kata tena kati katika kila ndizi vitoke vipande 4. baada ya hapo toa moyo wa katikai wa ndizi. Zioshe na kisha zikaushe maji na uziweke kwenye sufuria ya kupikia. Baada ya hapo tia tui la nazi, sukari, chumvi na hiliki. Ziinjike jikono na uziache zichemke uku ukiwa unalikoroga tui ili lisikatike. Baada ya dakika 10 tui la nazi litakuwa limepungua na kubaki kidogo na hapo ndizi zitakuwa zimeshaiva. Ziache zipoe na zitakuwa tayari kwa kuliwa. Zinaweza kuliwa kama mlo (main meal) au kitinda mlo (dissert) au mlo wa pembeni (side dish) haswa kwa futari.

Jinsi ya kupika Wali Wa Samaki Na Mboga

VIPIMO VYA SAMAKI

Samaki wa sea bass vipande – 1ย 1/2 LB (Ratili)
Kitunguu saumu(thomu/galic) -1 Kijiko cha supu
pilipili mbichi iliyosagwa – 1 Kijiko cha chai
Bizari ya manjano au ya pilau – 1/2 Kijiko cha chai
Paprika ya unga au pilipili ya unga – 1 kijiko cha chai
Chumvi – Kiasi
Ndimu
Mafuta – 3 Vijiko vya supu

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

Roweka samaki kwa viungo hivyo vyote kwa muda wa robo saa hivi.

Washa oven moto wa 400F.
Kisha weka samaki katika trea na choma kwa muda wa dakika 15 na weka moto wa juu dakika za mwisho ili ipate rangi nzuri.
Ikishaiva epua na itakuwa tayari kuliwa.

VIPIMO VYA MBOGA

Gwaru (green beans) – 1 LB
Kitunguu saumu(thomu/galic) – 1 kijiko cha supu
Karoti – 4-5
Chumvi – Kiasi
Bizari ya manjano – 1/2 Kijiko cha chai
Pilipili manga – 1/4 kijiko cha chai
Mafuta ya zaituni – Kiasi

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

Kata kata karoti na toa sehemu ya mwisho za binzi.
Weka mafuta katika sufuria kisha kaanga karoti na gwaru
Kisha weka moto mdogo na funika ili ziwive na sio kuvurujika.
Karibu na kuiiva tia thomu kaanga kidogo,tia bizari ,chumvi na pilipili manga.
Ikisha changanyikana vizuri epua na tayari kuliwa na wali na samaki.

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About