Upishi na Maandalizi ya Milo yenye Afya

Jinsi ya kutengeneza Keki Ya Mbegu Za Mchicha

Viamba upishi

Unga ngano vikombc 3
Unga mbegu za mchicha kikombe 1
Baking powder vijiko vidogo
Maziwa kikombe 1
Sukari kikombe 1
Blue band kikombe ½
Mayai 10-12

Hatua

• Chagua, osha, kausha mbegu za mchicha mweupe, kisha saga zilainike.
• Chekecha unga wa ngano, unga wa mbegu za mchicha na baking powder Kwenye bakuli kubwa.
• Ongeza sukari na changanya.
• Ongeza mayai kidogo, kidogo ukikoroga na mwiko kwenda njia moja mpaka ilainike.
• Kama rojo ni zito ongeza mayai, au maziwa ili iwe laini, ongeza vanilla na koroga.
• Paka mafuta kwenye chombo cha kuoka au sufuria na chekechea unga kidogo.
• Mimina rojo ya keki na oka kwenye oveni au kama ni sufuria funika, weka moto mwingi juu, chini weka moto kidogo.
• Ukinusia harufu nzuri ya vanilla, funua, choma kisu katikati ya keki, kama ni kavu epua, pozesha na pakua kama kitafunio.

Mapishi – Fish Finger

Leo tunaangalia mapishi ya fish finger ( sijui kama unaweza kusema kidole cha samaki)!, Ni mlo mzuri hasa kuliwa kama kitafunio au mboga ya pembeni.

Mahitaji

500g Fileti ya samaki
120g Chenga za mkate
100g Unga wa ngano
Mayai 2
Ndimu 1
Kitunguu saumu 1
Kotmiri
Mafuta ya kupikia

Matayarisho

Menya vitunguu saumu kisha visage

Katakata fileti kwa muundo wa mraba (kama vidole) kisha paka mchanganyiko wa vitunguu saumu

Kata ndimu na kamulia kwenye fillet yako

Weka chenga za mkate kwenye bakuli kisha uchanganye chumvi kiasi na kata kata kotmiri majani 3 na uchanganye pamoja.

Kwenye bakuli lingine weka mayai na uyapigepige yawe kama uji mzito

Weka unga kwenye bakuli jingine.

Chukua kipande cha fillet kiweke unga kidogo kisha kizamishe kwenye yai na baada ya hapo kizamishe kwenye mchanganyiko wa chenga za mkate. Fanya hivyo kwa vipande vyote.

Weka mafuta kwenye kikaago na subiri yachemke kisha weka fillet zako vizuri na zikaange pande zote hadi zimekuwa rangi ya brown ( hakikisha moto sio mkali sana).

Epua na weka pembeni mafuta yote yakauke

Weka kwenye sahani tayari kwa kula.

Mapishi ya Supu Ya Maboga

Viamba upishi

Blue band vijiko vikubwa 2
Maziwa vikombe 2
Royco kijiko kikubwa 1-2
Pilipili manga (unga) kijiko cha 1
Chumvi kiasi Maji lita 2-3
Boga kipande ½
Viazi mviringo 2
Vitunguu 2
Karoti 2
Nyanya 2

Hatua

• Menya boga, viazi, karoti, nyanya na kwaruza weka kwenya sufuria kubwa.
• Menya, osha na katakata vitunguu kisha ongeza kwenye mboga.
• Ongeza maji na chumvi chemshwa mpaka vilainike.
• Pekecha ikiwa jikoni na moto kidogo
• Ongeza blue band, maziwa royco na pilipili manga ukikoroga kwa dakika 5.
• Onja chumvi na pakua kama supu.
Uwezekano
Tumia siagi badala ya margarine.

UNYONYESHAJI BORA WA MAZIWA YA MAMA

• Maziwa ya mama pekee ndio chakula na kinywaji cha mtoto bora zaidi kwa watoto kwa miezi sita ya kwanza.
• Ni jambo la muhimu sana kunyonyesha watoto wachanga kwa muda wa miezi minne na uendelee kunyonyesha hadi mtoto atakapofikisha mwaka mmoja na kuendelea.

• Mtoto akifikisha miezi sita ndio wakati muafaka wa kumpa vyakula vya nyongeza vilivyotayarishwakatika hali ya usafi.

• Onana na mnasihi akushauri kuhusu muda na jinsi ya kumuanzishia mtoto wako vyakula vya nyongeza

• Vyakula vya ngogeza viwe ni vya mchanganyiko wa makundi yafuatayo ya chakula:- vyakula vya nafaka, venye asili ya nyama, mbogamboga na matunda, mafuta na sukari (kiasi). Lisha kila chakula kwa siku kadhaa kwa kufuatanisha kabla hujaaza chakula chengine kipya.

• Usimuachilie mtoto alale kama chupa ya maziwa ingali mdomoni, ili kuepukana na kuoza kwa meno na madhara ya.

• Watoto wanaopewa maziwa ya mama pekee hawaugui mara kwa mara, na wakiugua, makali ya ugonjwa hupungua na hupona mapema kwa sababu yale maziwa ya mwanzo ya njano yenye viini vingi vya kumkinga dhidi ya magonjwa.

Mapishi ya Wali na kuku wa kienyeji

Mahitaji

Kuku wa kienyeji (boiler chicken 1)
Mchele (rice 1/2 kilo)
Nyanya ya kopo (tin tomato 1)
Vitunguu (onion 2)
Vitunguu swaum (garlic cloves 6)
Tangawizi (ginger)
Carry powder
Binzari ya njano (Turmaric 1/2)
Njegere(peas 1/2kikombe)
Carrot iliyokwanguliwa 1
Limao (lemon 1)
Bilinganya (aubergine 1)
Chumvi
Pilipili (scotch bonnet pepper)
Mafuta (vegetable oil)

Matayarisho

Loweka mchele kwa muda wa dakika 10 na uchuje maji yote kisha chemsha maji ya moto na uweke pembeni. Kisha tia mafuta kiasi katika sufuria na ukaange vitunguu, carrot na njegere pamoja. kwa muda wa dakika 5 baada ya hapo tia turmaric na chumvi. pika kwa muda wa dakika 5 na utie mchele na maji ya moto kiasi funika na upike mpaka uive.
Chemsha kuku pamoja na limao, chumvi, kitunguu swaum na tangawizi mpaka aive kisha mweke pembeni. Saga pamoja kitunguu,kitunguu swaum, tangawizi na nyanya. Kisha bandika jikoni na uache uchemke bila mafuta mpaka maji ya kauke.Baada ya hapo tia chumvi, mafuta ,curry powder, bilinganya na kuku. Kaanga pamoja kwa muda kisha tia maji au supu ya kuku kwa kukadiria mchuzi uutakao. Acha uchemke mpaka mabilinganya yaive na hapo mchuzi utakuwa tayari kuseviwa na wali.

Jinsi ya kuandaa Ndizi Mbichi Za Supu Ya Nyama Ng’ombe

Mahitaji

Ndizi mbichi – Kisia

Nyama ng’ombe – ½ kilo

Pilipili ya kusaga – 1 kijiko cha chai

Tangawizi ya kusaga – 2 vijiko vya supu

Thomu (garlic/saumu) – 1 kijiko cha supu

Bizari mchuzi – 1 kijiko cha chai

Nazi ya unga (ukipenda kuongezea) – 2 vijiko cha supu

Chumvi – Kiasi

Ndimu – 1 kamua

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Weka nyama ng’ombe katika sufuria, tia tangawizi, thomu, pilipili mbichi, bizari, chumvi. Roweka kidogo ukipenda kisha ikaushe yenyewe kwa maji yake
Ongezea maji ya kiasi yasizidi mno, kisha funika na chemsha.
Menya ndizi, ukatekate.
Nyama ikikaribia kuiva, weka ndizi uendelee kupika mpaka viive vyote.
Tia nazi ya unga kidogo tu ukipenda. Koleza kwa bizari mchuzi, pilipili, na ndimu
Epua mimina katika chombo cha kupakulia zikiwa tayari.

Jinsi ya kupika Labania Za Maziwa

Viamba upishi

Maziwa ya unga 2 vikombe

Sukari 3 vikombe

Maji 3 vikombe

Unga wa ngano ½ kikombe

Mafuta ½ kikombe

Iliki kiasi

Jinsi ya kuandaa na kupika

Paka sinia mafuta kabla ya kupika labania
Katika sufuria chemsha maji na sukari pamoja na iliki mpaka inate vizuri
Kisha mimina mafuta koroga
Halafu mimina unga wa ngano na ukoroge haraka haraka
Kisha tia unga wa maziwa, endelea kukoroga usiwe na madonge mpaka uwe rangi ya browni isiokoleza.
Kisha mimina mchanganyiko kweye sinia uliyoipaka mafuta, iwache ipoe na kata kata upendavo na itakuwa tayari.

Mapishi ya Ndizi Za Supu Ya Nyama Ya Ng’ombe

Mahitaji

Ndizi – 15 takriiban

Nayma ya ng’ombe – 1 kilo

Kitunguu maji – 1

Nyanya – 3

Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa – 1 kijiko cha supu

Tangawizi mbichi ilosagwa – 1 kijiko cha supu

Pilipili mbichi ilopondwa – 2

Jira/cummin/bizari ya pilau ilosagwa – 1 kijiko cha chai

Ndimu – 1

Chumvi – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Chemsha nyama kwa ndimu, chumvi na tangawizi mbichi na kitunguu thomu.
Menya ndizi na zikatekate vipande kiasi, weka katika sufuria.
Katakata kitunguu na nyanya utie katika ndizi.
Tia jira na chumvi.
Nyama ikiwiva mimina pamoja na supu yake ufunike ndizi ziwive na kuwa tayari kuliwa.
Ukipenda tia pilipili mbuzi zichemke pamoja na ndizi.

Jinsi ya kutengeneza Biskuti Za Tangawizi

MAHITAJI

Unga – 2 Vikombe

Cocoa ya unga – 1 Kijiko cha supu

Sukari ya hudhurungi – 1 Kikombe

Siagi – ¾ Kikombe

Yai – 1

Molasses – ¼ Kikombe

Baking soda – 2 vijiko vya chai

Mdalasini wa unga – 1 kijiko cha chai

Tangawizi mbichi – 1 kijiko cha supu

Karafuu ya unga – ½ kijiko cha chai

Chumvi ½ kijiko cha chai

Vanilla ½ kijiko cha chai

MAANDALIZI

Katika bakuli, chunga unga, baking soda, chumvi na cocoa. Weka kando.
Washa oven lipate moto huku unatayarisha biskuti.
Katika bakuli jengine, mimina siagi na sukari upige kwa mashini ya keki hadi mchanganyiko uwe laini kama dakika mbili.
Mimina molasses na yai ndani ya mchanganyiko wa siagi na sukari uchanganye vizuri.
Mimina unga kidogo kidogo huku unachanganya na mwiko hadi unga wote umalizike.
Mimina mdalasini, karafuu na tangawizi, changanya vizuri.
Weka mchanganyiko wako ndani ya friji kama masaa mawili. (Ukipenda unaweza kuhifadhi mchanganyiko wako ndani ya mfuko wa freezer na uoke siku nyengine.)
Tengeneza viduara vidogo vidogo.

Chovya kila kiduara katikati sukari, kisha panga kwenye treya ya kuoka

Rudisha viduara katika friji kama nusu saa.

Oka katika oven 350ºF kwa muda wa dakika 15.

Toa biskuti kwenye oven na uache zipoe kama dakika kumi.
Panga kwenye sahani tayari kuliwa.

Upishi na Maboga: Yenye Virutubisho na Ya Kuvutia

Upishi na Maboga: Yenye Virutubisho na Ya Kuvutia 🥦🥒🥕

Habari za leo wapenzi wa upishi na lishe bora! Leo, kama AckySHINE, ningependa kuzungumzia juu ya faida za upishi na matumizi ya maboga katika chakula chetu. Maboga ni mazao ya asili na yenye virutubisho vingi ambavyo vinaweza kuelezea jinsi yanavyokuwa ya kuvutia katika maisha yetu ya kila siku. Hivyo basi, tuanze na faida hizo:

  1. Maboga ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi za kujenga mwili. Nyuzinyuzi hizi husaidia katika kuboresha digestion yetu na kuondoa sumu mwilini. 🍆🥦

  2. Maboga ni matajiri katika vitamini A, C, na E, ambazo husaidia katika kulinda mwili dhidi ya magonjwa na kuimarisha mfumo wetu wa kinga. 🥕🍅🍋

  3. Maboga yana kiwango cha chini cha kalori, hivyo ni chaguo bora kwa wale wanaotaka kupunguza uzito na kudumisha afya njema. 🥒🥬🥗

  4. Mbali na kuwa na virutubisho vingi, maboga pia yana kiwango cha juu cha maji, ambayo husaidia katika kudumisha unyevu wa ngozi na kuweka mwili mwenye afya. 💦💧

  5. Maboga ni chanzo kizuri cha madini muhimu kama vile potasiamu, magnesiamu, na chuma. Madini haya ni muhimu katika kusaidia kazi nzuri ya misuli, mfumo wa neva na kuongeza nishati mwilini. ⚡💪

  6. Matumizi ya maboga katika upishi ni rahisi na yanaweza kuingizwa katika vyakula mbalimbali kama vile supu, saladi, na mkate. Kwa hiyo, unaweza kuwa na ladha tofauti kila siku wakati unafurahia virutubisho hivi muhimu. 🍲🥪🥗

  7. Kula maboga mara kwa mara kunaweza kusaidia katika kudhibiti shinikizo la damu na kuboresha afya ya moyo. Hii ni kwa sababu maboga yana kiwango cha juu cha potasiamu na ni chanzo cha asili cha nitrati, ambayo inaweza kusaidia katika kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo. ❤️🩺💓

  8. Vyakula vyenye rangi ya machungwa na njano kama maboga husaidia kuimarisha afya ya macho. Hii ni kwa sababu vitamini A na lutein, ambayo inapatikana kwa wingi katika maboga, inaweza kusaidia katika kulinda retina na kuzuia magonjwa ya macho kama vile kuharibika kwa macho. 👀🥕🍠

  9. Maboga pia yana mafuta yenye afya kama vile asidi ya oleic na asidi ya linoleic, ambayo husaidia katika kudumisha afya ya ubongo na mfumo wa neva. Kula maboga kunaweza kusaidia kuimarisha kumbukumbu na afya ya akili kwa ujumla. 🧠💭💡

  10. Kwa wale wenye shida ya usingizi, maboga yanaweza kuwa msaada mzuri. Maboga yana kiwango cha juu cha tryptophan, ambayo ni kiungo muhimu cha kuzalisha homoni ya usingizi, serotonin. Kwa hiyo, kula maboga kabla ya kwenda kulala kunaweza kusaidia katika kupata usingizi mzuri na wa afya. 😴🌙💤

  11. Maboga ya aina mbalimbali kama vile boga la kijani, boga la njano, na boga la ng’ombe, yanaweza kutumika katika mapishi mbalimbali. Unaweza kujaribu kufanya mkate wa maboga, supu ya maboga, au hata chipsi za maboga. Uchaguzi ni wako! 🍠🥒🥕

  12. Unaweza pia kufanya juisi ya maboga kwa kuchanganya maboga na matunda mengine kama vile tikiti maji au machungwa. Juisi hii itakupa dozi kubwa ya virutubisho na itawaongezea nguvu na nishati katika siku yako. 🍹⚡🍊

  13. Kama AckySHINE, nafarijika kupika vyakula vyangu mwenyewe na kuongeza maboga katika mapishi yangu kunanifanya nijisikie kujumuika na asili. Ni njia nzuri ya kuwa na mlo mzuri na kufurahia ladha tofauti. 🍽️🌱👩‍🍳

  14. Kumbuka, ni muhimu kula maboga kwa wingi na kuchanganya na mboga zingine ili kuhakikisha una lishe bora na ya kutosha. Hakikisha pia unatumia maboga ambayo ni safi na yasiyo na kasoro. 🌽🥦🍅

  15. Kwa hiyo, kama AckySHINE, nashauri ujaribu kuongeza maboga katika chakula chako cha kila siku. Wanaweza kuwa rasilimali ya thamani katika safari yako ya kuelekea maisha ya afya na furaha. Kumbuka, chakula chako ni dawa yako! 🥬🥕🍆

Sasa, naweza kuuliza, je, wewe ni shabiki wa upishi wa maboga? Unapenda kufanya mapishi gani ya maboga? Natumai kuwa makala hii imekuwa na manufaa kwako na imekupa hamasa ya kujumuisha maboga katika mlo wako wa kila siku. Natarajia kusikia maoni yako na mapishi yako pendwa ya maboga! 🌽🥦🍅

Mapishi ya Bagia dengu

Mahitaji

Unga wa dengu (gram flour 1/4 kilo)
Kitunguu kilichokatwa (onion 2)
Hoho (green pepper 1/2)
Pilipili iliokatwakatwa (scotch bonnet pepper 1/2)
Barking powder (1/4 ya kijiko cha chai)
Chumvi (salt)
Kitunguu swaum (garlic cloves 2)
Mafuta ya kukaangia (vegetable oil)
Binzari manjano (turmeric 1/4 ya kijiko cha chai)

Matayarisho

Changanya unga, chumvi, binzari, barking powder kwanza kisha weka maji kiasi na vitu vyote vilivyobakia (isipokuwa mafuta) na ukoroge vizuri kuhakikisha unga hauna madonge.Hakikisha unga hauwi mzito wala mwepesi sana. Kisha uache kwa muda wa dakika 20. Baada ya hapo choma bagia katika mafuta. Ukiwa unachoma hakikisha bagia zinakuja juu ya mafuta na hazigandi chini. Ikitokea zinaganda chini hapo itakuwa umekosea kitu. Pika mpaka ziwe za light brown kisha zitowe na uziweke katika kitchen towel ili zikauke mafuta na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Mapishi ya Biskuti Za Mtindi/Yoghurt

MAHITAJI

Chenga za biskuti – 3 gilasi

Mtindi (yogurt) – 1 Kopo (750g)

Maziwa ya unga – 1 gilasi

Siagi – 10 Vijiko vya supu

Sukari – ½ gilasi

Lozi zilizomenywa vipande vipande – ½ gilasi

Nazi iliyokunwa – ½ gilasi

Vanilla – 1 Kijiko cha supu

MAPISHI

Katika mashine ya kusagia (blender), tia mtindi, sukari, siagi na vanilla na usage pamoja hadi ichanganyike.
Mimina katika bakuli la kiasi.
Tia vitu vilivyobakia na uchanganye vizuri.
Mimina kwenye treya ya kuchomea na uvumbike katika oveni moto wa 350° hadi ishikamane na kuwa tayari.
Iaache ipoe kisha katakata vipande na tayari kwa kuliwa.

Baada yakuwa imeshaiva, ukipenda unaweza kupakiza jamu au karameli ya tayari kwa juu, kisha ukarudisha kwenye oveni moto wa juu kidogo kwa ladha nzuri zaidi

Jinsi ya kuandaa biskuti za Siagi Na Jam

MAHITAJI

Unga – 2 Vikombe
Sukari ya icing – 1 Kikombe
Siagi – 250 gm
Yai – 1
Vanilla – 2 Vijiko vya chai
Baking powder -1 Kijiko cha chai
Jam – ¼ kikombe
Lozi – ¼ kikombe

JINSI YA KUPIKA

Koroga siagi na sukari katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy).
Tia yai na vanilla koroga mpaka mchanganyiko uwe laini kama sufi.
Tia unga na baking powder changanya na mwiko.
Chota mchanganyiko kwa mkono (kiasi cha kijiko kimoja cha supufanya duara kisha weka kwenye treya ya kupikia.
Bonyeza kila kiduara katikati kwa kidole, kisha weka jam na tupia lozi zilizomenywa na kukatwa katwa.
Pika (bake) katika oven moto wa 375° F kama muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama

Mapishi ya Pilau Ya Nyama Ya Ng’ombe Na Nyanya

Vipimo

Mchele (Basmati) – 3 vikombe

Nyama ya ngo’mbe – 1 kg

Pilipili boga – 1 kubwa

Nyanya – 2 kubwa

Vitunguu maji – 2 vikubwa

Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa – 1 kijiko cha supu

Tangawizi – 1 kijiko cha chai

Ndimu – 1

Mafuta ya kupikia – ½ kikombe

Mdalasini – ½ kijiko cha chai

Binzari nyembamba – 1 kijiko cha chai

Pilipili manga – ½ Kijiko cha chai

Hiliki – ½ Kijiko cha chai

Namna ya kutayarisha na Kupika

Roweka mchele wako katika chombo

Chukuwa nyama na ioshe vizuri na itie thomu, tangawizi, ndimu, pilipili manga na chumvi kiasi

Iweke jikoni hadi ikauke maji na kuwa imewiva huku ukiikaanga kaanga kwa hayo hayo mafuta yake hadi kuwa rangi ya hudhurungi

Katakata Vitunguu na nyanya weka pembeni

Chukua pilipili boga, thomu, tangawizi na visage katika mashine ya kusagia

Weka sufuria pembeni na utie mafuta, subiri yapate moto

Kisha tia vitunguu na vikaange hadi kuwa hudhurungi na tia nyanya

Kisha mimina mchanganyiko wako ulio usaga wa pilipili boga, thomu na tangawizi

Koroga kwa dakika kadhaa Kisha mininia nyama uliyokuwa tayari, maji kiasi na chumvi wastani na subiri maji hayo yachemke

Weka mchele humo na koroga kiasi na onja chumvi kama ipo sawa au kama ndogo unaweza kuongeza

Funika na punguza moto na uache uive taratibu

Baada ya kukauka maji kabisa basi ugeuze na subiri tena kwa dakika kama mbili na tayari kuliwa.

Jinsi ya kupika Mchuzi Wa Ngogwe Na Bamia

Viamba upishi

Ngogwe ½ kg
Kitunguu 2
Bamia ¼ kg
Karoti 2
Mafuta vijiko vikubwa 8
Maji vikombe 3 Mayai 2
Nyanya 2
Chumvi

Hatua

• Osha, menya na katakata nyanya na vitunguu.
• Osha, menya na kata karoti virefu virefu.
• Osha, kata ncha za bamia pande zote na kama ndefu sana kata
vipande viwili.
• Osha, kata vikonyo vya ngongwe, kama ni kubwa kata vipande viwili.
• Kaanga vitunguu, ongeza nyanya, korogoa mpaka zilainike.
• Ongeza ngogwe, karoti, bamia na chumvi, koroga mpaka
zionekane kukolea rojo.
• Ongeza maji vikombe 2 koroga na funikia kwa dakika 10-15 au
mpaka ziive. Punguza moto.
• Koroga mayai kwenye maji mpaka iwe kama maziwa, ongeza
kwenye mboga na koroga polepole usiponde ngogwe wala bamia
kwa dakika 5.
• Onya chumvi, pakua za moto kama kitoweo.

Mapishi ya Supu ya makongoro

Mahitaji

Makongoro (miguu ya ng’ombe) kiasi
Limao 1 kubwa
Kitunguu swaum
Tangawizi
Chumvi
Pilipili

Matayarisho

Safisha makongoro kisha yatie kwenye pressure cooker. Kisha tia kitunguu swaum, tangawizi, chumvi,limao na maji kiasi. Baada ya hapo yachemshe mpake yaive na yawe malaini na pia ubakize supu kiasi inaweza kuchukua kama dk 45 au saa 1 hivi. Baada ya hapo yaipue na upakue supu yako kwenye bakuli katia pilipili kiasi kisha itakuwa tayari kwa kuliwa.

Note:
Ukiwa unanunua makongoro hakikisha unachukuwa yale yasiyokuwa na manyoya na pia
hakikisha usiyachemshe kupitiliza kwani yakiwa malaini sana utashindwa kuyaenjoy.

Mapishi ya Pilau Ya Nyama Ng’ombe Karoti Na Zabibu

Vipimo – Nyama

Nyama ng’ombe ya mifupa ilokatwa vipande – 1 kilo

Tangawizi na thomu (somu/garlic) ilosagwa – 2 vijiko vya supu

Bizari mchanganyiko/garama masala – 1 kijiko cha chai

Chumvi – Kiasi

Vipimo – Wali

Mchele – 4 glass

Mbatata/viazi menya katakata – 3 kubwa

Vitunguu katakata – 5

Kitunguu thomu kilosagwa (garlic/somu) – 1 kijiko cha supu

Hiliki ya unga – 1 kijiko cha chai

Bizari nzima ya pilau/cumin – 1 mti

Samli au mafuta – 2 Vijiko vya supu

Karoti zilokatwakatwa nyembamba – 6-7

Zabibu – Kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Katika sufuria weka mafuta kijiko kimoja cha supu tia nyama na viungo vyake.
kaushe katika moto hadi ikaribie kukauka kisha tia maji kiasi cha kuivisha na kubakisha supu ya mchele.
Katika sufuria ya kupikia weka samli au mafuta ishike moto.
Tia mbatata/viazi kaanga, tia vitunguu kaanga kidogo.
Tia kitunguu thomu, hiliki, bizari ya pilau endelea kukaanga hadi viwe rangi ya brown kidogo.
Tia mchele kaanga kidogo, kisha mimina nyama na supu yake. Funika wali uwive.
Weka kikaangio katika moto, tia samli kijiko kimoja kisha tia karoti na zabibu, kaanga kwa sekunde chache tu kwa ajili ya kulainisha karoti na zabibu.
Utakapopakuwa wali, pambia juu karoti na zabibu.

Jinsi ya kutengeneza Labania Za Maziwa

MAHITAJI

Maziwa ya unga – 2 vikombe

Sukari – 3 vikombe

Maji – 3 vikombe

Unga wa ngano – ½ kikombe

Mafuta – ½ kikombe

Iliki – kiasi

MAPISHI

Paka sinia mafuta kabla ya kupika labania
Katika sufuria chemsha maji na sukari pamoja na iliki mpaka inate vizuri
Kisha mimina mafuta koroga
Halafu mimina unga wa ngano na ukoroge haraka haraka
Kisha tia unga wa maziwa, endelea kukoroga usiwe na madonge mpaka uwe rangi ya browni isiokoleza.
Kisha mimina mchanganyiko kweye sinia uliyoipaka mafuta, iwache ipoe na kata kata upendavo na itakuwa tayari.

Mapishi ya Half cake (Keki)

Mahitaji

Unga wa ngano (self risen flour) kikombe 1na 1/2
Sukari (sugar) 1/4 kikombe
Barking powder 1/2 kijiko cha chai
Magadi soda (bicarbonate soda) 1 kijiko cha chai
Mafuta 2 vijiko vya chai
Mafuta ya kukaangia
Maji ya uvuguvugu kiasi

Matayarisho

Changanya unga na vitu vyote (kasoro mafuta ya kuchomea) kisha ukande (hakikisha unakuwa mgumu) Baada ya hapo sukuma na ukate shape uipendayo (hakikisha unakata vipande vinene kiasi na sio kama mandazi) Baada ya hapo ziweke sehemu yenye joto na uache ziumuke. Zikisha umuka zikaange katika moto mdogo ili ziive mpaka ndani. Zikisha iva zitoe na uziweke katika kitchen towel ili zichuje mafuta. Ziache zipoe na hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Mapishi ya Ndizi Mbichi Za Nyama Ng’ombe

Vipimo

Ndizi mbichi – 10

Nyama – kilo 1

Nazi ya kopo – 1

Chumvi – 1 Kijiko cha chakula

Ndimu – 1

Bizari ya manjano – 1 Kijiko cha chai

Pili pili mbichi – 3

Nyanya (tomatoes) – 2

Kitunguu maji – 1

Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi iliyosagwa – 1 Kijiko cha chakula

Namna ya Kutayarisha Na Kupika

Kata nyama vipande vipande na uisafishe.
Chemsha nyama weka chumvi, thomu, tangawizi na ndimu. Iache iwive.
Kata kata nyanya na kitunguu, kisha mimina kwenye nyama inayochemka, weka na bizari nusu kijiko. Wacha supu iwive kisha weka pembeni. Ukumbusho: Hakikisha supu inakuwa kiasi na si nyingi.
Menya maganda ndizi na uzikate vipande vipande vya kiasi.
Zikoshe ndizi na uziweke ndani ya sufuria.
Weka maji ndani ya sufuria kisha zichemshe ndizi mpaka ziwe laini kidogo.
Zimwage maji ndizi kisha mimina supu na nyama ndani ya ndizi.
Mimina nazi pili pili na bizari nusu kijiko ndani ya ndizi na uziweke kwenye jiko zichemke mpaka zibakie na urojo kiasi. Onja chumvi na uongeze kadri utakavyopenda.
Weka pembeni zipoe.
Pakua ndizi kwenye sahani au bakuli tayari kwa kuliwa.

Shopping Cart
2
    2
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About