Upishi na Maandalizi ya Milo yenye Afya

Jinsi ya kupika Biskuti Ya Keki Kavu kwa kizungu Shortcake

Viamba upishi

Unga 2 Magi (vikombe vya chai)

Sukari iliyosagwa 2/3 Magi (kikombe cha chai)

Siagi โ€… 220ย g

Unga wa mchele ยฝ Magi

Yai 1

Vanilla 1 kijiko cha chai

Jinsi ya kuandaa na kupika

1. Changanya vitu vyote hivyo kwenye bakuli mpaka unga ushikamane.

2. Paka mafuta treya ya kuchomea kisha utandaze kwenye treya ya 20cm kwa 30ย cm au (8 in kwa 12 in)

3. Choma kwenye moto 325หšC kwa muda wa saa nzima au mpaka ibadilike kuwa rangi ya dhahabu.

4. Epua acha ipoe kisha kata vipande kama mstatili, weak kwenye sahani tayari kunywewa na chai.

Mapishi ya Wali Wa Mboga Na Mchuzi Wa Kuku wa Tanduri

Vipimo vya Wali:

Mchele basmati – 3 magi (kikombe kikubwa)

Mchanganyiko wa mboga za barafu

(Frozen vegetables) – 1 ยฝ mug

Chumvi – kiasi

Mafuta – 3 vijiko vya chakula

Kitungu maji (kilichokatwa) – 1

Bizari ya pilau (nzima) – 1 kijiko cha chakula

Namna Ya kutayarisha na kupika:

Osha mchele uroweke kwenye maji muda wa dakika 20.
Chemsha maji kwenye sufuria kama magi 6.
Tia chumvi.
Yakisha kuchemka unatia mchele, chemsha usiive sana, uive nusu kiini. Mwaga maji na kuchuja wali.
Unamimina Yale mafuta kwenye sufuria unakaanga bizari ya pilau kidogo na kitunguu kabla ya kugeuka rangi ya hudhurungi (brown).
Tia mchanganyiko wa mboga za barafu.,
Mimina wali, changanya vizuri, ufunike na uweke katika moto mdogo kwa dakika 20.
Pakua tayari kwa kuliwa.

Vipimo Vya Mchuzi

Kuku – 2 Ratili (LB)

Chumvi – Kiasi

Mafuta – ยผ Kikombe

Nyanya Kata vipande – 4

Nyanya kopo – 2 vijiko wa chakula

Tangawizi – 1 kijiko ya chakula

Kitunguu saumu(thomu/galic) – 1 kijiko ya chakula

Tanduri masala – 1 kijiko cha chakula

Kotmiri liliyokatwa – 3 vijiko vya chakula

Pilipili mbichi – 2

Pili masala – 1 kijiko cha chakula

Garam masala – ยฝ kijiko cha chakula

Bizari manjano – ยฝ kijiko cha chakula

Mtindi – 3 vijiko vya chakula

Pilipili boga (kata vipande virefu) – 1

Ndimu – 2 vijiko vya chakula

Namna ya kutayarisha na kupika:

Kwenye bakuli tia kuku na changanya vitu vyote pamoja isipokua mafuta.
Tia mafuta kwenye sufuria yakisha kupata moto mimina kuku umpike kwa muda ยฝ saa kwa moto kiasi.
Pakua kuku kwenye bakuli au sahani na ukate vitunguu maji duara na umpambie. Tayari kwa kuliwa.

Jinsi ya kupika Wali Wa Samaki Na Mboga

VIPIMO VYA SAMAKI

Samaki wa sea bass vipande – 1ย 1/2 LB (Ratili)
Kitunguu saumu(thomu/galic) -1 Kijiko cha supu
pilipili mbichi iliyosagwa – 1 Kijiko cha chai
Bizari ya manjano au ya pilau – 1/2 Kijiko cha chai
Paprika ya unga au pilipili ya unga – 1 kijiko cha chai
Chumvi – Kiasi
Ndimu
Mafuta – 3 Vijiko vya supu

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

Roweka samaki kwa viungo hivyo vyote kwa muda wa robo saa hivi.

Washa oven moto wa 400F.
Kisha weka samaki katika trea na choma kwa muda wa dakika 15 na weka moto wa juu dakika za mwisho ili ipate rangi nzuri.
Ikishaiva epua na itakuwa tayari kuliwa.

VIPIMO VYA MBOGA

Gwaru (green beans) – 1 LB
Kitunguu saumu(thomu/galic) – 1 kijiko cha supu
Karoti – 4-5
Chumvi – Kiasi
Bizari ya manjano – 1/2 Kijiko cha chai
Pilipili manga – 1/4 kijiko cha chai
Mafuta ya zaituni – Kiasi

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

Kata kata karoti na toa sehemu ya mwisho za binzi.
Weka mafuta katika sufuria kisha kaanga karoti na gwaru
Kisha weka moto mdogo na funika ili ziwive na sio kuvurujika.
Karibu na kuiiva tia thomu kaanga kidogo,tia bizari ,chumvi na pilipili manga.
Ikisha changanyikana vizuri epua na tayari kuliwa na wali na samaki.

Mapishi ya Maini ya ng’ombe

Mahitaji

Maini (Cow liver) 1/4 kilo
Vitunguu (chopped onion) 2
Nyanya (chopped tomato) 1
Kitunguu swaum/tangawizi (ginger /garlic paste) 1 kijiko cha chai
Mafuta ya kupikia
Chumvi
Coriander
Curry powder 1 kijiko cha chai
Limao (lemon) 1/4
Pilipili (scotch bonnet ) 1

Matayarisho

Safisha maini na ukate vipande vidogovidogo na uweke pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu kidogo(visiwe vya brown) kisha tia ginger/ garlic paste,carry powder kaanga kidogo kisha tia nyanya. Kaanga nyanya mpaka zitoe mafuta kisha tia chumvi, pilipili na vimaji kidogo. Acha vichemke kidogo kisha tia maini na uyapike mpaka yaive. Malizia kwa kukamulia limao na kutia coriander kisha ipua na hapo yatakuwa tayari kwa kuliwa.

Jinsi ya kutengeneza Fagi Ya Kumumunyuka Mdomoni

VIAMBAUPISHI

Maziwa mazito matamu (condensed milk) – 2 vibati

Sukari – 1 kikombe

Samli 1 ยฝ kikombe

Vanilla 2 kifuniko cha chupa yake

Hiliki ilosagwa – 2 vijiko vya chai

Sinia kubwa ya bati Paka samli

MAANDALIZI

Changanya maziwa, sukari na samli katika sufuria isiyogandisha chakula (non-stick) uweke katika moto.
Koroga huku ikipikika hadi ianze kugeuka rangi na kuanza kuachana. Usiache mkono kuroga isije kufanya madonge.
Tia hiliki na vanilla, endelea kuipika.
Itakapogeuka rangi vizuri mimina katika sinia na haraka uitandaze kwa mwiko huku ukiuchovya katika maji na kuendelea kuitandaza hadi ikae sawa kote.
Pitisha kisu kuikataka ili ikipoa iwe wepesi kuitoa vipande.

Kila inapozidi kupoa na kukaa ndipo fagi inakauka na kumumunyuka.

Jinsi ya kupika pizza ya mboga mboga na cheese

MAHITAJI

1 kilo unga wa ngano
240 ml maji ya vugu vugu
2 olive oil kijiko kikubwa cha chakula
2 asali kijiko kidogo cha chai
1 chumvi kijiko kidogo cha chai
1 hamira ya chenga kijiko kidogo cha chai

JINSI YA KUPIKA

Chukua bakuli weka maji ya uvugu vugu, amira ya chenga, asali na chumvi kisha koroga ichanganyike vizuri acha itulie kwa dakika 10.
Kisha chukua olive oil na unga wa ngao mimina kidogo kidogo changanya mpaka ichanganyike safi kabisa kisha anza kukanda kama mchanganyiko wa chapati au maandazi.
Baada ya mchanganyiko wako kua mgumu safi kabisa funika bakuli lako na mfuko wa plastiki au cling film kwa muda wa saa 1 katika joto la chumba na mchanganyiko wako utaumuka baada ya muda huo. kisha ukandamize mchanganyiko huo wa unga na kua flati kama mwanzo.
Kata mafungu matano hadi saba ya ujazo sawa inategemea na ukubwa wa piza unaopenda we mlaji kisha sukuma umbo la duara.
Tengeneza mchuzi mzito wa nyanya kisha weka juu ya kitako cha piza na kuitandaza vizuri kwenye pizza yako kama unavyopaka siagi kwenye mkate. Usisahau kuweka chumvi na sukari kidogo katika mchuzi wa nyanya ili kukata uchachu.
Katakata nyanya, kitunguu, pili pili hoho, na bilinganya na kuziweka juu ya pizza yako kwa mpangilio ukitanguliza biringanya, ikifuatiwa na pili pili hoho, kitunguu maji na nyanya.
Kisha chukua mozarella cheese ikwaruze katika mkato mdogo rahisi kuyeyuka kwa kutumia kwaruzo la karoti linafaa.
kisha chukua mkwaruzo wa mozarella cheese na unyunyizie juu ya hizo mboga.
Weka pizza yako kwenye sahani ya bati au pizza pan ili isaidie kuiva upande wa chini.
Weka pizza yako kwenye oven ambayo imeshawashwa na ina joto 400 – 450ย F. Choma kwa dakika 20 hadi 25 iwe kaukau na rangi ya kahawia pia cheese itakua imyeyuka na kusambaa vizuri juu ya pizaa.

NB: Unaweza weka mchanganyiko wa nyama yeyote ile kama salami, nyama ya ngombe, nyama ya kuku au samaki kwa kufata maelekezo sawa sawa na hii piza ya mboga, tofauti yake itakua huweki mboga unaweka nyama.

Mapishi ya Wali Wa Kichina Wa Kuku Na Mboga Mchanganyiko

Vipimo

Mchele wa basmati/pishori – 4 vikombe vikubwa (mugs)

Kuku – 2

Vitnguu vya kijani (sprin onions) katakata – 5 miche

Maharage machanga (spring beans) katakata – kiasi kujaza mug moja

Pilipili boga la (capsicum) katakata – 1

Karoti katakata vipande virefu – 1

Kitunguu thomu (garlic) kuna (grate) – 1 kubwa

Tangawizi mbichi kuna (grate) – 1 kubwa

Sosi ya soya (soy sauce) – 2 vijiko vya supu

Kidonge cha supu – 1

Mafuta ya kupikia – ยผ kikombe cha chai

Chumvi – kiasi

Pilipili manga – 1 kijiko cha supu

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Osha kuku vizuri, katakata vipande, weka katika sufuria, tia chumvi, pilipili manga, mfunike, umkaushe motoni huku ukimgeuza geuza.

Roweka mchele kisha uchemshe uive nusu. Chuja maji, tia siagi kidogo ili usigandane.

Weka karai ya kupika mboga (wok) au sufuria kisha tia mafuta yashite moto.

Tia kitunguu thomu, tangawizi, kaanga kidogo.

Tia mboga zote, ulizokatakata.

kaanga kidogo, kisha tia sosi ya soya na kidonge cha supu. Usizipike sana mboga mpaka zikalainika mno. Sababu zitaiva katika mchele

Changanya kuku na mboga kisha changanya vyote katika mchele, urudishe katika moto.

Funika upike hadi uive kamilifu.

Pakua kwenye sahani.

Mapishi ya Biriani Ya Samaki Nguru, Njegere Na Snuwbar (UAE)

Mahitaji

Mchele wa basmati – 4 cups

Samaki nguru (king fish) – 7 vipande au zaidi

Kitunguu – 5

Nyanya/tungule – 3

Njegere – 1 kikombe

Snuwbar (njugu za pine) – 1 kikombe

Viazi – 2 kata kata mapande makubwa

Tangawizi mbichi – 1 kijiko cha supu

Kitunguu saumu – 1 kijiko cha supu

Pilipili nyekundu – 1 kijiko cha chai

Bizari ya biriani/garama masala – 1 kijiko cha supu

Namna Ya Kupika:

Kaanga samaki mbali kwa viungo upendavyo umkoleze vizuri. Au choma (bake/grill) katika oveni ukipenda.
Weka mafuta katika sufuria, tia vitunguu kaanga hadi vigeuka rangi. Gawa sehemu mbili.
Sehemu moja bakisha katika sufuria kisha tia tangawizi mbichi na kitunguu thomu ukaange.
Tia nyanya kaanga kisha tia bizari zote endelea kukaanga, tia njegere, njugu za snuwbar na ndimu kavu.
Tia viazi ulivyokwishakaanga, na vitunguu vilobakia.
Tia mapande ya samaki, changanya na masala bila ya kumvuruga samaki.
Chemsha wali kisha mwagia juu yake, funika upike ndani ya oveni au mkaa hadi wali uive kama unavyopika kawaida ya biriani.
Epua pakua huku ukichanganya na masala ya samaki.

Mapishi ya Firigisi za kuku

Mahitaji

Filigisi (chicken gizzard) 1/2 kilo
Carrot iliyokwanguliwa 1
Nyanya 1/2 kopo
Vitunguu maji 1 kikubwa
Tangawizi/swaum 1 kijiko cha chai
Hoho 1 iliyokatwakatwa
Limao 1/2
Chumvi
Curry powder 1/2 kijiko cha chai
Turmaric 1/2 kijiko cha chai
Chilli powder 1/4 kijiko cha chai
Mafuta
Chopped coriander

Matayarisho

Safisha filigisi kisha zikate vipande vidogo vidogo.Zichemshe pamoja na chumvi, limao na nusu ya tangawizi na swaum mpaka ziive (hakikisha unabakiza supu kidogo). Baada ya hapo kaanga vitunguu mpaka viwe vya brown kisha tia tangawizi na swaum iliyobakia na kaanga kidogo kisha tia nyanya. Zipike mpaka ziive kisha tia spice zote pamoja na chilli. Zipike kidogo kisha tia filigisi (bila supu kwanza) Zichanganye vizuri na uzipike kidogo. Baada ya hapo tia carrot na hoho na supu iliyobakia. Vipike pamoja mpaka viive na supu ibakie kidogo sana. Malizia kwa kutia coriander na uipue na hapo firigisi zako zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Mapishi ya Tambi na nyama ya kusaga

Mahitaji

Tambi (Spaghetti)
Nyama ya kusaga
Kitunguu maji
Nyanya ya kopo
Kitunguu swaum
Tangawizi
Carrot
Hoho
Lemon
Chumvi
Curry powder
Mafuta
Fersh coriander

Matayarisho

Katakata vitunguu maji, carrot, hoho, kisha weka pembeni. Saga vitunguu swaum na tangawizi pamoja kisha weka pembeni. Baada ya hapo injika sufuria jikoni, tia mafuta. Yakisha pata moto tia vitunguu maji kaanga mpaka vigeuke rangi ya kahawia kisha tia kitunguu swaum na tangawizi.baada ya hapo tia nyanya ya kopo na iache ichemke mpaka iive. Baada ya nyanya kuiva tia curry powder na chumvi. Geuza mpaka mchanganyiko uchanganyike vizuri kisha tia nyama ya kusaga na uiache ichemke mpaka iive.Baada ya nyama kuiva tia Corrot na hoho na uzipike kwa muda wa dakika 2.Na baada ya hapo mboga itakuwa imeivaa, iipue na katia fresh coriander. Baada ya hapo injika sufuria yenye maji jikoni. Yaache yachemke na kisha tia chumvi na mafuta ya mzaituni (olive oil) na tambi. Acha zichemke mpaka ziive kisha zichuuje maji na chujio na baada ya hapo zitakuwa tayari kuseviwa na nyama.

Mapishi ya Wali Wa Kukaanga Kwa Nyama Mbuzi Ilichomwa Ya Sosi Ya Ukwaju

Vipimo Vya Wali

Mchele Basmati – 4 vikombe

Vitunguu vya majani (Spring onions) – 5 miche

Pilipili mboga nyekundu (capsicum) – 1

Pilipili mboga manjano (capscimu) – 1

Nyanya kubwa – 1

Supu ya kidonge – 2

Siagi – 2 vijiko vya supu

Chumvi – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Osha mchele kisha roweka kiasi masaa matatu takriban.
Katakata vitunguu majani, mapilipili boga, nyanya vipande kiasi.
Weka siagi katika sufuria ya kupikia, weka katika moto iyayuke.
Tia vitunguu majani, mapilipili boga, nyanya, kaanga kidogo tu.
Tia mchele kaanga kidogo, kisha tia maji kiasi ya kuivisha mchele.
Tia supu ya kidogo au supu yoyote, funika wali upikike moto. mdogodogo.

Vipimo Vya Nyama Mbuzi Na Sosi Ya Ukwaju

Nyama mbuzi mapande makubwa kiasi – 7/8 vipande

Kitunguu saumu(thomu/galic) kilosagwa – 1 kijiko cha supu

Pilipili mbichi ilosagwa – 1 kijiko cha supu

Ukwaju mzito ulokamuliwa – 1 kikombe cha chai

Jiyra/cummin/bizari pilau – 1 kijiko cha chai

Nyanya kopo – 2 vijiko vya supu

Siki – 2 vijiko vya supu

Mafuta – ยฝ kikombe cha chai

Chumvi – kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

Changanya vitu vyote pamoja katika kibakuli kidogo.
Weka nyama katika bakuli kubwa kisha tia mchanganyiko wa sosi, ubakishe sosi kiasi pembeni.
Roweka kwa muda wa masaa 3 โ€“ 5
Panga nyama katika bakuli au treya ya kuchomea katika oven.
Pika (bake) kwa moto wa kiasi kwa muda wa saa takriban.
Karibu na kuiva, epua, zidisha kuichangaya na sosi ilobaki.
Rudisha katika jiko uendelee kuipika muda kidogo tu.
Epua ikiwa tayari, weka juu ya wali uliopakuwa kisha mwagia sosi ya nyanya pilipili (chilii tomato sauce) ukipenda.

Jinsi ya kutengeneza juisi ya nyanya

Viamba upishi

Nyanya 1ย kg
Maji Iita ยฝ
Chumvi kijiko kidogo 1
Sukari

Hatua

โ€ข Osha nyanya, katakata na chemsha na maji mpaka zilainike.
โ€ข Chuja juisi.
โ€ข Pima juisi – vikombe 2 vya juisi kwa kikombe 1 cha sukari, weka
kwenya sufuria safi .
โ€ข Ongeza chumvi, chemsha ukikoroga mpaka ichemke.
โ€ข Mara ikichemka epua, pozesha na weak kwenya chombo safi kwa
kunywa.

Jinsi ya kupika Pilau Ya Nafaka Na Nyama Ya Kusaga

Viambaupishi

Mchele 3 vikombe

Nyama ya kusaga 1 LB

Mchanganyiko wa Nafaka (upendavyo) 1 kikopo

(maharagwe, njegere, mbaazi, na kadhalika)

Vitunguu maji kata vipande vipande 3 vya kiasi

Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi 2 vijiko vya supu

Mafuta ยฝ Kikombe

Mchanganyiko wa bizari (Garam Masala) 2 vijiko vya chai

Vipande vya supu (Maggi cubes) 3

Maji (inategemea mchele) 5

Chumvi Kiasi

Jinsi ya kuandaa na kupika

1) Osha mchele na roweka.

2) Weka mafuta katika sufuria na kaanga vitunguu mpaka viwe brown.

3) Tia Thomu na tangawizi, kaanga kidogo.

4) Weka nyama ya kusaga, chumvi na garam masala, endelea kukaanga mpaka nyama iwive.

5) Mwaga maji yaliomo katika kopo la nafaka na utie nafaka pekee humo.

6) Tia maji na vipande vya supu (Maggi cubes) huku unavivuruga, koroga kidogo.

7) Tia mchele, koroga kidogo.

8) Funika na pika kwa moto mdogo mpaka karibu na kukauka ukikorogoka kidogo. (kama unavyopika pilau ya kawaida)

9) *Epua uipike katika moto wa oven 350-400 Deg kwa muda wa dakika 15.

*Kama sufuria uliyotumia sio ya kupikia katika oven, mimina katika chombo chochote kinachotumika kwa oven kama bakuli la pyrex au treya za foil.

10) Pakua katika sahani na iko tayari kuliwa.

Jinsi ya kupika Biryani ya mbogamboga

Biriani ni miongoni mwa vyakula ambavyo ni nadra sana kupikwa katika familia nyingi tofauti na vyakula vingine. Inawezekana ni kutokana na watu wengi kutoelewa namna ya kuoika chakula hiki kutokana na kuhitaji viungo vingi ambavyo huwapa usumbufu wapishi.
Kuna aina mbalimbali za upishi wa biriani ambapo mara nyingi hutofautiana kutokana na viungo vinavyotumika katika upishi.
Biriani la mbogamboga ni miongoni mwa aina hizo za upishi. Chakula hiki kinaweza kuliwa na kila mtu hususan wale wasiotumia nyama wala samaki.

Mahitaji:

ยฝ kg mchele wa basmati
Kitunguu maji kikubwa 1
Nyanya 1 kubwa
Karoti 1 kubwa
Njegere robo kikombe
Kiazi ulaya 1 kikubwa
Tangawizi za kusaga kijiko 1
Kitunguu swaumu cha kusaga kijiko 1
Karafuu kijiko 1
Majani ya kotimili fungu 1
Maziwa ya mtingi ยผ kikombe
Chumvi na pilipili kiasi
Unga wa dhani kijiko 1 cha mezani
Juisi ya limao kijiko 1 cha mezani
Mafua ยผ lita

Maandalizi:

Chemsha mchele na kisha weka pembeni
Osha mbogamboga zote isipokuwa vitunguu na nyanya
Changanya mtindi na tangawizi pamoja na kitunguu swaumu viache vikae kwa muda wa saa moja
Chukua sufuria weka mafuta na kisha kaanga vitunguu maji, weka nyanya, chumvi, kotimili na limao halafu weka karafuu na kanga hadi vichanganyike vizuri
Miminia mchanganyiko wa mtindi na baadaye weka pilipili na baadaye weka unga wa dhania
Chukua mchele uliochemshwa changanya na mchanganyiko huo
Palia moto juu ya chakula chako na acha kwa muda wa dakika 30
Baada ya hapo chakula chako cha biriani kitakuwa tayari kwa kuliwa

Jinsi ya kupika Visheti Vyeupe Na Vya Kaukau

VIPIMO:

Unga wa Visheti

Unga 4 Vikombe vya chai

Siagi 1 Kikombe cha chai

Hiliki ยฝ Kijiko cha chai

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

1. Tia unga kwenye bakuli pamoja na siagi na hiliki.

2. Changanya vizuri isiwe na madonge.

3. Tia maji baridi vikombe viwili kasoro vya chai changanya ukiona bado ongeza maji kidogo, iwe kama chapati usikande uchanganye tu.

4. Halafu utakata sampuli unayopenda mwenyewe.

5. Unaweka karai ya mafuta yakisha kupata moto unaanza kuchoma moto usiwe mkali sana, kiasi, baadae unaweza kuongeza moto na vikaange hadi viwe rangi ya dhahabu, kisha viepue vichuje mafuta. .

6. Ukipenda gawa visheti sehemu mbili, na shira pia igawe sehemu mbili

7. Changanya nusu ya visheti kwa shira nyeupe.

8. Nusu ya shira nyingine ibandike tena motoni na tia cocoa vijiko viwili vidogo vya chai. Inapochanganyika cocoa vizuri changanya nusu ya visheti ulivyogawa kupata visheti vya shira ya cocoa.

Shira:

Sukari 2 Vikombe vya chai

Maji 1 Kikombe cha chai

Vanilla ยฝ Kijiko cha chai

(cocoa ukipenda kugawa visheti aina mbili) 2 Vijiko vya chai.

Mapishi ya Supu ya makongoro

Mahitaji

Makongoro (miguu ya ng’ombe) kiasi
Limao 1 kubwa
Kitunguu swaum
Tangawizi
Chumvi
Pilipili

Matayarisho

Safisha makongoro kisha yatie kwenye pressure cooker. Kisha tia kitunguu swaum, tangawizi, chumvi,limao na maji kiasi. Baada ya hapo yachemshe mpake yaive na yawe malaini na pia ubakize supu kiasi inaweza kuchukua kama dk 45 au saa 1 hivi. Baada ya hapo yaipue na upakue supu yako kwenye bakuli katia pilipili kiasi kisha itakuwa tayari kwa kuliwa.

Note:
Ukiwa unanunua makongoro hakikisha unachukuwa yale yasiyokuwa na manyoya na pia
hakikisha usiyachemshe kupitiliza kwani yakiwa malaini sana utashindwa kuyaenjoy.

Jinsi ya kupika Biskuti Nyembamba (Wafer Bar) Za Chokoleti Na Njugu

MAHITAJI

Wafer Powder/gram wafer (unga wa biskuti uliosagwa wa tayari) – vikombe 2

Maziwa ya Mgando Matamu ya Kopo – 2 vikombe

Nazi iliyokunwa – ยฝ Kikombe

Chokoleti vipande vipande – 1 Kikombe

Njugu vipande vipande – ยฝ Kikombe

Siagi – 227ย g

MAPISHI

Yeyusha siagi motoni kisha changanya na unga wa wafer acha kidogo motoni
Mimina katika treya unayochomea itandaze vizuri, kisha mimina maziwa juu yake pamoja na njugu vipande , nazi iliyokunwa na vipande vya chokoleti.
Choma (bake) kwenye oveni kwa moto wa 350ยบC kwa dakika 20.
Katakata tayari kwa kuliwa

Upishi wa Afya kwa Ajili ya Afya ya Moyo: Kitamu na Kilainishi

Upishi wa Afya kwa Ajili ya Afya ya Moyo: Kitamu na Kilainishi ๐Ÿ๐Ÿ’š๐ŸŒฝ

Leo, tutazungumzia juu ya jambo muhimu sana katika maisha yetu – afya ya moyo. Kama AckySHINE, ninapenda kushiriki na wewe njia ambazo unaweza kula chakula kitamu na cha kufurahisha wakati huo huo kuhakikisha kuwa unalinda afya yako ya moyo. Sasa twende tukashiriki njia hizi kumi na tano za upishi wa afya kwa ajili ya afya ya moyo wako! ๐Ÿ’ชโค๏ธ

  1. Kula Matunda na Mboga: Matunda na mboga mboga ni chanzo kizuri cha vitamini, madini, na nyuzi ambazo zinaweza kusaidia kudumisha afya bora ya moyo. ๐ŸŽ๐Ÿฅฆ

  2. Kupunguza Matumizi ya Chumvi: Chumvi nyingi inaweza kuongeza shinikizo la damu na hatari ya magonjwa ya moyo. Jaribu kutumia viungo vingine vya kitamu kama vile pilipili, tangawizi, au vitunguu. ๐ŸŒถ๏ธ๐Ÿง„

  3. Kula Nafaka Zisizochakatwa: Nafaka zisizochakatwa kama vile mchele mzuri, ngano nzima, na tambi za ngano nzima zina nyuzi nyingi na virutubisho vingine muhimu kwa afya ya moyo wako. ๐ŸŒพ๐Ÿš

  4. Punguza Matumizi ya Mafuta Yasiyo na Lishe: Mafuta mengi ya wanyama na ya nazi ni mafuta yenye mafuta mengi ambayo yanaweza kuathiri afya ya moyo wako. Badala yake, tumia mafuta yenye afya kama vile mafuta ya zeituni au ya alizeti. ๐Ÿฅฅ๐Ÿซ’

  5. Kupunguza Matumizi ya Sukari: Sukari nyingi inaweza kuongeza hatari ya kisukari na shida ya moyo. Badala yake, tumia asali au matunda kuongeza ladha tamu kwenye vyakula vyako. ๐Ÿฏ๐Ÿ“

  6. Ongeza Samaki kwenye Lishe yako: Samaki kama vile samaki wa maji baridi na mafuta kama vile samaki wa tuna, salmoni, na sardini, ni matajiri katika asidi ya mafuta omega-3 ambayo inaweza kusaidia kudumisha afya ya moyo. ๐ŸŸ๐Ÿ 

  7. Kula Vyakula vya Lishe: Kula vyakula vyenye lishe kama vile karanga, maharage, na mbegu za chia ambazo zina protini, nyuzi, na viinilishe vingine muhimu kwa afya ya moyo wako. ๐Ÿฅœ

  8. Kuepuka Vyakula Vyenye Mafuta Mengi: Vyakula vyenye mafuta mengi kama vile nyama ya nguruwe, nyama ya ng’ombe, na bidhaa za maziwa zilizochakatwa zina mafuta mengi ya wanyama ambayo yanaweza kuathiri afya ya moyo wako. Chagua nyama nyepesi kama vile kuku au nyama ya ng’ombe iliyokatwa mafuta. ๐Ÿ–๐Ÿท

  9. Kupika Kwa Kutumia Njia za Kupikia Zisizo za Mafuta Mengi: Jaribu kupika kwa kutumia njia kama kupika kwa mvuke, kuchemsha, au kupika kwenye grill badala ya kukaanga au kuchoma moto. Hii itapunguza matumizi ya mafuta mengi na kuifanya chakula chako kiwe afya zaidi. ๐Ÿณ๐Ÿฅฆ

  10. Punguza Matumizi ya Vyakula Vilivyosindikwa: Vyakula vilivyosindikwa mara nyingi huwa na viungo vingi vya kemikali na mafuta mengi ambayo yanaweza kuwa na athari mbaya kwa afya ya moyo. Chagua vyakula vya asili na visindikwe kwa wingi. ๐Ÿ”๐ŸŸ

  11. Kula Chakula kidogo mara kwa mara: Badala ya kula milo mikubwa mara chache, jaribu kula milo midogo mara kwa mara. Hii itasaidia kudumisha kiwango cha sukari na cholesterol kwenye damu yako. ๐Ÿฝ๏ธโฐ

  12. Kunywa Maji ya Kutosha: Maji ni muhimu kwa afya ya moyo wako. Kunywa angalau lita mbili za maji kwa siku ili kudumisha mwili wako vizuri. ๐Ÿ’ง๐Ÿ’ฆ

  13. Kufanya Mazoezi: Mazoezi ni muhimu kwa afya ya moyo wako. Fanya mazoezi angalau dakika 30 kwa siku, kama vile kutembea au kukimbia ili kuweka moyo wako mwenye nguvu. ๐Ÿƒโ€โ™‚๏ธ๐Ÿ‹๏ธโ€โ™€๏ธ

  14. Kupunguza Mafadhaiko: Mafadhaiko yanaweza kuathiri afya ya moyo wako. Jaribu kufanya mazoezi ya kupumua, yoga, au kutafakari ili kupunguza mafadhaiko yako na kuweka akili yako na moyo wako vizuri. ๐Ÿง˜โ€โ™€๏ธ๐Ÿ˜Œ

  15. Pima Afya ya Moyo wako: Fanya uchunguzi wa afya ya moyo mara kwa mara ili kugundua mapema shida yoyote au hatari ambayo inaweza kuathiri afya ya moyo wako. ๐Ÿฉบโค๏ธ

Kwa kumalizia, kula chakula kitamu na cha kufurahisha haimaanishi kuwa unapaswa kuhatarisha afya yako ya moyo. Kwa kufuata kanuni hizi za upishi wa afya, unaweza kufurahia chakula chenye ladha nzuri wakati ukihakikisha kuwa moyo wako unaendelea kuwa na afya bora. Kumbuka, afya ya moyo ni muhimu sana kwa maisha yetu ya kila siku, na kula vyakula vyenye afya ni hatua ya kwanza ya kuhakikisha tunadumisha moyo mzuri. Kwa hivyo, jiunge nami katika safari hii ya kusisimua ya upishi wa afya kwa moyo wako! ๐Ÿฅ—โค๏ธ

Na wewe je, una maoni gani kuhusu njia hizi za upishi wa afya kwa ajili ya afya ya moyo? Je, umewahi kujaribu njia hizi au una njia nyingine za kuongeza kitamu na kilainishi kwenye lishe yako ya moyo? Nimependa kusikia maoni yako! ๐Ÿ’ฌ๐Ÿ˜Š

Madhara ya nyama nyekundu kwa mtu mwenye VVU

Kuna nyama za aina mbili, nazo ni nyama nyeupe na nyama nyekundu.

Nyama nyeupe

Hizi ni nyama zitokanazo na samaki, kuku, ndege wa aina zote, bata, wadudu

Nyama nyekundu

Hutokana na ngโ€™ombe, mbuzi, kondoo,nguruwe na wanyama wa porini.

Nyama ina virutubishi vingi muhimu kwa afya ya binadamu kama protini, vitamini na madini. Madini ya chuma yanayopatikana kwenye nyama ni rahisi sana kusharabiwa (kufyonzwa) mwilini na ni muhimu kwa kuongeza wekundu wa damu.
Uwezo wa miili ya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI kuyeyusha chakula na kusharabu (kufyonza) virutubishi hupungua. Utumiaji wa nyama nyekundu kwa wingi unaweza kuwaletea matatizo hasa katika uyeyushwaji tumboni kwani nyama nyekundu si rahisi kuyeyushwa ukilinganisha na nyama nyeupe.

Hata hivyo katika nchi yetu watu walio wengi wanatumia nyama kwa kiasi kidogo sana na mara chache. Si vyema watu hawa waache kabisa nyama nyekundu. Jambo la muhimu ni kutumia njia mbalimbali ili kuifanya nyama hii iyeyushwe kwa urahisi tumboni.

Namna ya kusaidia uyeyushwaji ni pamoja n a : –

โ€ข Kutafuna vizuri au kutumia nyama ya kusaga (kwa wanaoipata).
โ€ข Kupika nyama na viungo vinavyosaidia kulainisha kama vile papai bichi, limao, vitunguu saumu n.k.
โ€ข Kula nyama pamoja na papai

Kwa hiyo, kwa anayepata nyama nyekundu kwa wingi, kupunguza kiasi cha nyama hiyo na kuongeza kiasi cha nyama nyeupe. Na kwa yule asiyepata nyama nyeupe, apatapo nyama nyekundu asiache kutumia kwani ina umuhimu mwilini mwake.

Shopping Cart
25
    25
    Your Cart
    ๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About