JEE NYAMA YA NGURUWE (KITI MOTO) NI SALAMA KWA BINADAMU???
Hapa huwa kuna mvutano wa kidini sana juu ya nguruwe, Ila Leo napenda kuliweka sawa, kitaalamu kwa mujibu waย MEDICINE (Science)!!
Nguruwe ni mnyama anaeliwa na 38% ya watu wote duniani Na walaji wake ni nchi Magharibi na Kusini mwa Asia, Europe, Sub-Saharan Africa, America ya kaskazini , kusini mwa America, na Oceania.
Nguruwe ni mnyama ambae, Ana umbo la pekee sana, tukiangalia kuhusu madhara yake au faida yake , tunangalia vitu vinavyopatikana ktk mwili wake, tukilinganisha Na Faida.
FAIDA ZA NYAMA YA NGURUWE KITAALAMU
๐๐พKunapatikna vitamini muhimu ktk mwili Wa binadamu; ambavyo ni B1, B6 and B12
๐๐พUnapata madini ya Chuma, ambayo husaidia kuimarisha mifupa.
๐๐พNyama ya nguruwe inaimarisha ngozi yako Na kuifanya iwe laini.
๐๐พNyama ya nguruwe ina magnesium kwa wingi ambayo ina faida ktk mwili Wa binadamu
๐๐พNyama ya nguruwe ina protein ya kutosha, ambayo husaidia ulinzi wa mwili
๐๐พNyama ya nguruwe ina mafuta ambayo hutupa nguvu mwilini
HASARA YA NYAMA YA NGURUWE
Licha ya faida tajwa hapo juu, vile vile kuna hasara ya kutumia nyama hii.
๐๐พNyama ya nguruwe ; ina sumu yaย carcinogenย ambayo inasababisha kansa; kwa mujibu wa utafiti uliofanyika Na shirika la afya duniani (ย WHO), Naย The International Agency for Research on Cancer!!ย Utafiti huo ukaonesha kuwa ukila kila siku 50gms basi uwezekano Wa wewe kupata kansa unaongezeka kwa 18%
๐๐พAnasababisha Swine Flu kwa binadamu; hivi ni virusi vinavyosababisha mafua kwa binaadamu. Kwa mujibu wa utafiti uliofanyika naย Centers for Disease Control and Preventionย inaonesha influenza virus H1N1 na H3N2 ambaye anatokana Na Nguruwe(kiti moto) imeripotiwa kusababisha maradhi ya mripuko kwa nchi zaย MAREKANI
๐๐พNyama ya nguruwe ina minyoo wajulilanao kwa jina la trichinella worm , ambao wadudu hawa ni vigumu sana kuweza kufa kwa joto Hata la 100C , utafiti uliofanyika 1998 Na WHO ukaonesha nyama ya Nguruwe iliopikwa kwa Joto la 104C , Huwa asilimia 52.37% ya trichinella worm wanabaki kuwa hai!! Wadudu hao wakiingia ktk mwili Wa binadamu husababisha ugonjwa ujulikanao kwa jina la trichinosis;ย ambao huwa Na dalili kama ifuatavyo:
โ
Homa kali sana
โ
Kichwa kuuma
โ
Kukosa nguvu
โ
Maumivu ya nyama za mwili
โ
Macho kuwa rangi ya pink(conjunctivitis)
โ
Kuvimba uso Na kope
โ
Kudhuriwa Na mwanga
๐๐พNyama ya nguruwe ina virus aina ya Hepatitis E virus (HEV); ambaye husababisha homa ya ini aina E
๐๐พWadudu wengine ni kama;
๐ฅNipah virus
๐ฅMenangle virus
๐ฅViruses Ktk kundi Paramyxoviridae
Ambao wote hao; huwa wanaleta madhara kwa mwili Wa binadamu!!
๐๐พNyama ya nguruwe husababisha Maradhi ambayo Yana resistance(ukinzani) Naย ANTIBIOTICS
๐๐พNyama ya nguruwe ina minyoo aina ya Taenia solium. Kwa mujibu ya shirika la Afya duniani(WHO) – Referenceโฆ.open_http://www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/taeniasis-cysticercosis
Wanasema; minyoo hii huwa;
๐Unaweza kuipata ikiwa hautapika nyama vizuri au Ukila nyama ya kuruwe ilioathirika(infected): Kwa hyo sio kila nyama ya Nguruwe iliopikwa vizuri, huwezi kupata minyoo hii.
๐Minyoo hii ikiingia ktk mwili Wa binadamu husababisha matatizo ya mfumo Wa fahamu (central nervous system) iitwayo neurocysticercosis
Mfano wake ni kifafa
๐30% ya wagonjwa wenye kifafa huwa ni wale ambao hushambuliwa Na minyoo hii ipatikanayo kwenye nguruwe
๐๐พWatu milioni 50 duniani wanaopata kifafa , huwa ni walaji wazuuri Wa Nguruwe.
JEE NG’OMBE, MBUZI, KONDOO NA WANYAMA WENGINE WALIWAO NA WENGI HAWANA MINYOO??
Ukweli ni kwamba Hata wanyama wengine nyama zao huwa zina minyoo aina ya Taenia saginata.
Ila minyoo ya Taenia saginata ni tofauti Na Taenia solium kwa sababu; Saginata wanakufa kwa joto Dogo sana, lakini solium wanahitaji 71C bila Hata kupungua!!
Swali langu kwako wewe msomaji Wa nakala hii;
๐๐พNani anaepika huku akipima joto limefika au laa???
HITIMISHO
Tahadhari, sana Na nyama ya nguruwe , kwa sababu madhara yake ni makubwa kuliko faida yake!!!
Shared from;
Dr Isack
References:
Google ScholarResearchGate
Semantic Scholar
AckySHINE