Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
☰
AckyShine

Kisa cha kusisimua: Funzo kwa mabinti

Featured Image

Kijana maskini na mwenye maisha duni alimpenda msichana mmoja
Baada ya kutumia muda mwingi kumfikiria msichana huyo,
Siku moja akaamua kumwita na kumwambia ukweli ya kwamba amempenda na angehitaji kumuoa.

Msichana kwa nyodo na jeuri akasema "sikiliza tena unisikilize kwa makini wewe maskini mshahara wako unaopokea kwa mwezi hautoshi hata kwa matumizi yangu ya siku moja sasa utawezaje kunitunza mm!

Kwaufupi mm sio levo zako hivyo basi sahau kabisa kuhusu kunipata mimi
Nenda katafute maskini mwenzio atakae endana na maisha yako,
Mwisho akamwangalia kwa dharau na kisha akaenda zake.

Kwanzia siku ile kijana hakubahatika tena kumuona msichana yule lkn kwakuwa alimpenda basi hakuweza kumsahau kirahisi rahisi siku zilienda na miezi ikasonga,
Miaka 10 baadae wawili hawa walikuja kukutana katika supermarket moja hivi mjini

Kijana alipomwona msichana alitabasamu lakin kabla hajasema chochote msichana kama kawaida yake kwa dharau akasema "we maskin upo! hivi na ww unaingiaga supermarket eh!

Akaongeza huku akisema walau sasahivi nakuona umependeza inaonekana boss wako kakuongeza mshahara
ila kwa kifupi naomba nikwambie sasahivi nimeshaolewa mume wangu anafanya kazi kwenye kampuni moja hivi ya mtu binafsi kampuni maarufu sana na mshahara wa mume wangu ni shilingi milioni moja na laki mbili kwa mwezi na malupulupu mengine kibao,
Unafikiri ww na umaskini wako kuna siku utakuja kufikia kiwango cha mshahara anachopokea mume wangu!

Macho ya kijana yalitokwa na machozi kwa kuona msichana hajabadilika na anaendelea kuwa na maneno ya kejeri na dharau.

Mara hii mume wa yule dada akaingia ktk supermarket
Ile kumuona yule kijana mume akasema "ooh! Kiongozi upo hapa! Leo imekuwa bahati umekutana na mke wangu!" Kisha akamgeukia mke wake na kusema "mke wangu huyu ndo boss wangu

Na unajua nn mke wangu usishangae kumuona boss wangu anakuja kununua vitu mwenyewe hapa supermarket ukweli ni kwamba boss wangu hana mke, anasema alisha wahi kumpenda msichana mmoja lakini hakufanikiwa kumpata na amekuwa na ndoto ya kuja kukutana tena na msichana huyo ndio maana mpaka sasa bado hajaoa.

Akaendelea kusema hebu fikiria ni bahati kiasi gani alikuwa nayo msichana huyo kama angekubali kuolewa na boss wangu leo hii siangekuwa
maisha!

Muda wote msichana alikuwa kimya hajui hata ajibu nn kwa dharau alizomuonyesha kijana tangu mwanzo.


UJUMBE WANGU
Kwenye maisha mambo huweza kubadilika kama vile upepo unavoweza kubadili mwelekeo kulingana na masaa Hivyo basi usimdharau na kumbeza mtu yeyote kwa sababu ya hali aliyonayo,
Maana kila mtu anafungu lake alilopangiwa na Mungu,

Lakini pia kumbuka hakuna ajuaye kesho
Wakati mwingine mtu unayemdharau leo ndiye huyohuyo ambaye kesho utasimulia mafanikio yake.

Kwako unayesoma ujumbe huu nakuombea Mungu akakufungulie milango ya baraka na kuyapa thamani maisha yako ili pale ulipozomewa ukashangiliwe na wale wote waliokudharau punde wakapate kukupigia magoti kwa uweza wa Mungu.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

Director J (User) on May 15, 2025

Good story πŸ’ͺ

Related Posts

Jinsi ya Kuelewa na kukabiliana na changamoto za kusaidia na kuwajali watu wenye makundi ya kijamii

Jinsi ya Kuelewa na kukabiliana na changamoto za kusaidia na kuwajali watu wenye makundi ya kijamii

Kusaidia na kuwajali watu wenye makundi ya kijamii ni wajibu wa kila mmoja wetu. Kwa bahati mbaya... Read More

Njia Rahisi za Kufanya Msichana Awe na Hamu ya Kuwa na Wewe

Njia Rahisi za Kufanya Msichana Awe na Hamu ya Kuwa na Wewe

Wapenzi, kama unapenda msichana fulani na unataka kuwa na uhusiano naye, inaweza kuwa ngumu kumsh... Read More

Jinsi ya Kufanya mipango ya baadaye na ndoto za pamoja na mpenzi wako

Jinsi ya Kufanya mipango ya baadaye na ndoto za pamoja na mpenzi wako

Kufanya mipango ya baadaye na ndoto za pamoja na mpenzi wako ni njia nzuri ya kujenga malengo ya pam... Read More
Jinsi ya Kujenga Furaha na Amani katika Ndoa na mke wako

Jinsi ya Kujenga Furaha na Amani katika Ndoa na mke wako

Kujenga furaha na amani katika ndoa na mke wako ni muhimu sana kwa ustawi wa uhusiano wenu. Hapa kun... Read More
Kuweka Mazingira ya Amani na Furaha katika Maisha ya Kila Siku ya Familia

Kuweka Mazingira ya Amani na Furaha katika Maisha ya Kila Siku ya Familia

Kuweka mazingira ya amani na furaha katika maisha ya kila siku ya familia ni muhimu sana kwa usta... Read More

Namna ya Kujenga Nia na Ndoto za Pamoja na mke wako

Namna ya Kujenga Nia na Ndoto za Pamoja na mke wako

Kujenga nia na ndoto za pamoja na mke wako ni muhimu katika kukuza uhusiano imara na kufikia malengo... Read More
Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha mipaka ya faragha

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha mipaka ya faragha

Kujenga na kudumisha mipaka ya faragha katika uhusiano ni muhimu kwa usalama, heshima, na ustawi wa ... Read More
Jinsi ya Kusaidiana na Kuunga Mkono katika Familia: Nguvu ya Ushirikiano

Jinsi ya Kusaidiana na Kuunga Mkono katika Familia: Nguvu ya Ushirikiano

Familia ni kitu muhimu sana katika maisha yetu. Inatupa nguvu, faraja, na upendo. Hata hivyo, kun... Read More

Jinsi ya Kukuza Heshima na Uaminifu katika Mahusiano ya Familia

Jinsi ya Kukuza Heshima na Uaminifu katika Mahusiano ya Familia

Mahusiano ya familia ni muhimu sana kwani ndiyo yanayotufanya tuwe na furaha na amani katika mais... Read More

Jinsi Kuweka Usawa kati ya Kazi na Maisha ya Familia

Jinsi Kuweka Usawa kati ya Kazi na Maisha ya Familia

Kuweka usawa kati ya kazi na maisha ya familia ni muhimu sana ili kuwa na afya na furaha katika mais... Read More
Muda wa Kufanya Kufanya Mapenzi

Muda wa Kufanya Kufanya Mapenzi

Muda wa Kufanya Kufanya Mapenzi

Wapenzi wote duniani wana nia ya kufanikiwa katika mapenzi... Read More

Jinsi ya Kuzungumza na mpenzi wako kuhusu masuala ya uzazi na uzazi wa mpango

Jinsi ya Kuzungumza na mpenzi wako kuhusu masuala ya uzazi na uzazi wa mpango

Kuzungumza na mpenzi wako kuhusu masuala ya uzazi na uzazi wa mpango ni muhimu katika kujenga uelewa... Read More