Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
☰
AckyShine

Kisa cha kusisimua cha kijana na mke wake na mama yake

Featured Image

Kuna kijana mmoja daktari alikwenda kuposa. Binti aliyemposa akamuwekea masharti mazito. Akamwambia chagua mawili imma kunioa mimi au kukaa na mama yako, kwa sababu ukinioa mimi sitokubali mama yako aje hata harusini kwangu! Yule kijana aliemewa. Hakujua la kufanya. Mke anamtaka, lakini mama yake pia anampenda.


Hivyo aliamua kuomba ushauri kwa mwalimu wake wa chuo kikuu. Alimwambia: moyo wangu unampenda mno binti niliyekwenda kumposa, lakini pia siwezi kuishi mbali na mama yangu. Nifanye nini?


Yule mwalimu mwenye hekima ambaye alikuwa anajua tabu alizopitia mama wa kijana yule, alimjibu kwa kumwambia: Kabla ya kukueleza uchague yupi kati ya wawili hao, rudi nyumbani, na leo usifanye chochote, ila kuikosha mikono ya mama yako. Yule kijana alifanya kama alivyotakiwa na mwalimu wake. Alipofika nyumbani aliomba idhini kwa mama yake amruhusu kuikosha mikono yake, na yule mama alimkubalia bila ya ajizi yoyote.



Yule kijana alipoanza kuikosha mikono ya mama yake na kuona jinsi ilivyogugutaa kwa kazi za sulubu, alilia sana. Muda wote huu alikuwa hajawahi kuangalia viganja vya mama yake. *Je, na wewe umewahi kukaa na kuangalia viganja vya mama au baba yako kuona tabu walizopitia kukulea?* Kumbe baba wa yule kijana alifariki dunia yeye akiwa bado mdogo, yule mama aliamua kusamehe kila kitu kwa ajili ya mustakbali wa mwanawe. Alijitolea kufanya kazi za sulubu. Alikubali kuwa mtumishi wa ndani, kukosha nguo, kupiga deki na kila kazi ambayo alihisi ingelimletea chumo la halali bila ya kujali ugumu wa jkazu hiyo.



Juhudi zake zilizaa matunda na kufanikiwa kumlea na kumsomesha mwanawe hadi chuo kikuu na sasa ni daktari ambaye ana mustakbali mzuri. Baada ya yule kijana kukumbuka yote hayo, alifanya haraka kumpigia simu mwalimu wake huku macho yakiendelea kububujikwa na machozi akimwambia, siwezi kusubiri hadi kesho. Jibu nimeshalipata. Siwezi kumtupa mama yangu kwa ajili ya mtu asiyejua thamani ya mama. Ahsante sana kwa kunionesha njia sahihi! Kamwe siwezi kumuuza mama yangu kwa ajili ya leo yangu wakati yeye ameuza maisha yake yote kwa ajili ya mustakbali wangu.
NANI KAMA MAMA?!? Maa! Tabasamu lako ni ufunguo wangu wa ofanisi.
Kama umeipenda.


Share kwa wengine ili nao wazinduke.






Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE




[products columns="2" ids="30827"]


AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsi ya Kuelewa na kukabiliana na hofu na wasiwasi katika uhusiano na mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kukabiliana na hofu na wasiwasi katika uhusiano na mpenzi wako

Hofu na wasiwasi ni hisia za kawaida katika uhusiano wowote, na ni muhimu kujifunza jinsi ya kuziele... Read More
Jukumu la Kujielewa katika Kufanya Mapenzi: Kukuza Uhuru na Urahisi

Jukumu la Kujielewa katika Kufanya Mapenzi: Kukuza Uhuru na Urahisi

Mapenzi yana jukumu muhimu katika maisha ya mwanadamu. Ni kitendo cha kupenda na kuthamini mtu mw... Read More

Njia za Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii na Urafiki katika Mahusiano

Njia za Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii na Urafiki katika Mahusiano

Hakuna kitu kizuri kama kuwa na marafiki wengi na mahusiano bora ya kijamii. Uhusiano mzuri unahi... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kukuza na kudumisha afya ya kimwili na akili

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kukuza na kudumisha afya ya kimwili na akili

Kusaidiana na mpenzi wako katika kukuza na kudumisha afya ya kimwili na akili ni jambo muhimu kat... Read More

Ushawishi wa Vyombo vya Habari katika Maoni yetu ya Kufanya Mapenzi: Kuchambua na Kuelimisha

Ushawishi wa Vyombo vya Habari katika Maoni yetu ya Kufanya Mapenzi: Kuchambua na Kuelimisha

Ushawishi wa vyombo vya habari katika maoni yetu ya kufanya mapenzi ni suala ambalo limekuwa liki... Read More

Je, kuna umuhimu wa kujadili mipango ya uzazi na ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna umuhimu wa kujadili mipango ya uzazi na ngono/kufanya mapenzi?

  1. Kujadili mipango ya uzazi na ngono/kufanya mapenzi kuna umuhimu mkubwa sana katika kuha... Read More

Kukabiliana na Changamoto za Kufanya Mapenzi katika Uhusiano

Kukabiliana na Changamoto za Kufanya Mapenzi katika Uhusiano

Kukabiliana na Changamoto za Kufanya Mapenzi katika Uhusiano

Katika uhusiano wowote wa kim... Read More

Kukuza Ujuzi wa Kujitegemea na Kujiamini kwa Watoto katika Familia

Kukuza Ujuzi wa Kujitegemea na Kujiamini kwa Watoto katika Familia

  1. Kuwa mfano mzuri kwa watoto wako

Watoto ni kama sponji, wanapochukua kila kit... Read More

Vidokezo vya Kuwa na Mawasiliano ya Kuaminika na Msichana

Vidokezo vya Kuwa na Mawasiliano ya Kuaminika na Msichana

Leo kwenye makala hii, tutazungumzia vidokezo vya kuwa na mawasiliano ya kuaminika na msichana. N... Read More

Ishara 10 za mwanamke aliyekuzimia na anayekupanda

Ishara 10 za mwanamke aliyekuzimia na anayekupanda

Ishara hizi zinaweza zikakusaidia kumgundua msichana anayekupenda, wasichana wanatofautiana ila w... Read More

Njia za Kuimarisha Ushirikiano na Kukuza Maadili ya Familia

Njia za Kuimarisha Ushirikiano na Kukuza Maadili ya Familia

Kuwa na familia yenye ushirikiano mzuri na maadili ni muhimu sana katika kuhakikisha maisha yanak... Read More

WACHEPUKAJI WENGI WANATABIA HIZI

WACHEPUKAJI WENGI WANATABIA HIZI

1.Hachezi mbali na simu yake kila wakati.
2.Inbox na sending items hufutwa kila wakati.
Read More