Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
☰
AckyShine

Jinsi ya kumfanya mwanamke afurahi na akupende kwa kumfanyia mambo anayoyataka

Featured Image

Kuna mambo ya msingi ambayo mwanamke anahitaji kutoka kwa mwanamme ili kufurahi na kutulia katika mahusiano japokuwa sio rahisi kukwambia mojakwa moja.


Mambo hayo ni kama ifuatavyo;


Kupewa nafasi na kipaumbele.


Wanawake wanapenda kuwa namba moja au kupendwa kuliko yeyote. Kumpenda mwanamke haikuishii kwenye kumpata na kumliki, kisha kujisahau kwa kisingizio kuwa umemuoa au umemvisha pete ya uchumba, ni zaidi ya hapo. Wanawake wanapenda watangulizwe katika mapenzi na kusiwepo na mwingine wa kuchukua nafasi yao katika mazungumzo na mapenzi kwa ujumla na katika maisha yao.


 

Kuheshimiwa


Wanawake wanapenda kueshimiwa kwa maneno na matendo. Wanawake hawapendi kuitwa majina mabaya kwa mfano mjinga, Malaya au kulinganishwa na wanawake wenzao wabaya. Wanawake hawapendi kukosewa heshima hasa mbele za watu, hata kama ni kwa mambo madogo madogo.


Kuridhishwa Kwenye tendo la ndoa


Mwanamke anapenda aridhishwe Kwenye tendo la ndoa. Hata kama utakuwa na kiwango kikubwa cha mapenzi juu ya mpenzi wako kwa kiwango gani, ukiwa dhaifu katika tendo la ndoa utayumbisha penzi lako. Utundu na ufundi unahitajika ili kumkata kiu mpenzi wako. Mwanamme anatakiwa kuhakikisha kuwa anamtosheleza mpenzi wake katika tendo hilo.


 

Nafasi ya kuongea na kujieleza


Wanawake wanapenda wapewe nafasi ya kuongea na kujieleza vile watakavyo. Mpe uhuru mpenzi wako kuzungumza na kumsikiliza bila kumkatiza kwa ukali pale anapoongea sana. Kwa kawaida wanawake wanatajwa kuzungumza maneno 25,000 kwa siku, wakati wanaume wakibaki na kiwango cha maneno 5,000 kwa siku, wanawake hupenda zaidi kujieleza walivyo mbele ya wengine. Kwa hiyo wakizuiwa wasiongee hujiona kama wanakosa nafasi muhimu ya kueleza mawazo yao.


 

Kusaidiwa katika shida na matatizo yao


Wanawake wengi hutegemea kuwa wanapokuwa na wapenzi watasaidiwa katika matatizo ya kimaisha na migogoro ya kimawazo. Kwa mfano ushauri juu ya maisha yao, kulindwa na hatari za kimaisha, kusaidiwa katika shida na kuongozwa pale wanapohisi kushindwa kufanya jambo. Kama mwanaume hatamfanyia mpenzi wake hili atakuwa amekosa sifa za kuteka penzi la mwanamke.


Kubembelezwa


Wanawake hupenda kubembelezwa hasa pale wanapokuwa na huzuni. Wanawake wengi hupenda kuelimishwa zaidi kuliko kufokewa. Wanawake hawapendi kukaripiwa, mara nyingi hupenda kuungwa mkono wanapokuwa na misuguano na wengine. Ili mwanaume amteke kimapenzi mwanamke lazima awe nyuma yake hata kama atakuwa na kosa.






Mfahamu zaidi Mwanamke kwa Kupitia Kitabu hiki kizuri cha SIRI ZA MWANAMKE




[products columns="2" ids="30827"]


AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za kiimani na dini na mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za kiimani na dini na mpenzi wako

Mapenzi ni hisia za kipekee ambazo huja na changamoto zake. Mojawapo ya changamoto kubwa katika u... Read More

Jinsi ya Kujenga Ushirikiano wenye Uaminifu katika Familia

Jinsi ya Kujenga Ushirikiano wenye Uaminifu katika Familia

  1. Kuwa na mawasiliano yenye wazi na ya kweli Ni muhimu kuwa na mawasiliano yenye wazi na ... Read More

Jinsi ya Kujenga Misingi Thabiti ya Ndoa ya uaminifu na mke wako

Jinsi ya Kujenga Misingi Thabiti ya Ndoa ya uaminifu na mke wako

Kujenga misingi thabiti ya ndoa yenye uaminifu na mke wako ni muhimu katika kuimarisha mahusiano yen... Read More
Kuhamasisha Ushirikiano wa Kielimu na Kukuza Maarifa katika Familia

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kielimu na Kukuza Maarifa katika Familia

Kuhamasisha ushirikiano wa kielimu na kukuza maarifa katika familia ni muhimu sana katika kuhakik... Read More

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za kiutamaduni na mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za kiutamaduni na mpenzi wako

Kuelewa na kushughulikia tofauti za kiutamaduni na mpenzi wako ni muhimu katika kuimarisha uhusiano ... Read More
Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya usawa na haki za wafanyakazi katika mahusiano ya ajira

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya usawa na haki za wafanyakazi katika mahusiano ya ajira

Mahusiano ya ajira yanatofautiana na mahusiano mengine ya kimapenzi. Kwa kawaida, katika mahusian... Read More

Njia za Kujenga Uhusiano Imara na Msichana

Njia za Kujenga Uhusiano Imara na Msichana

Kujenga uhusiano na msichana ni jambo muhimu katika maisha ya kimapenzi. Uhusiano unapokuwa imara... Read More

Kuweka Kipaumbele cha Furaha na Ustawi wa Familia yako

Kuweka Kipaumbele cha Furaha na Ustawi wa Familia yako

Mafanikio ya maisha yako yanategemea sana furaha na ustawi wa familia yako. Familia yenye afya na... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha urafiki na jamaa

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha urafiki na jamaa

Mahusiano ya kimapenzi na ya kijamii ni muhimu sana katika maisha yetu ya kila siku. Lakini, inak... Read More

Kupata Urahisishaji na Kusaidia katika Masuala ya Kufanya Mapenzi: Njia za Kuomba Msaada

Kupata Urahisishaji na Kusaidia katika Masuala ya Kufanya Mapenzi: Njia za Kuomba Msaada

Kupata urahisishaji na kusaidia katika masuala ya kufanya mapenzi ni muhimu sana kwa wapenzi wote... Read More

Jinsi ya Kuelewa na kukabiliana na changamoto za kuwa wazazi na mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kukabiliana na changamoto za kuwa wazazi na mpenzi wako

Kuwa wazazi na mpenzi ni changamoto kubwa katika maisha yetu. Mawazo mengi yako kwenye familia na... Read More

Majukumu ya mke katika ndoa

Majukumu ya mke katika ndoa

Katika ndoa, jukumu la mke ni jukumu muhimu na linajumuisha majukumu mengi. Hapa kuna baadhi ya maju... Read More