Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
AckyShine

Jifunze kitu kupitia kisa hiki cha mume na mke

Featured Image

Mwanaume mmoja alimuoa mwanamke mrembo. Alikuwa akimpenda sana. Siku moja mwanamke alipatwa na maradhi ya ngozi. Kidogokidogo alianza kupoteza urembo wake.
.
.
.

Mume alipata safari na wakati akirudi alipata ajali iliyomfanya apoteze uwezo wake wa kuona. Hata hivyo, maisha yao ya ndoa yaliendelea kama kawaida. Lakini kadiri siku zilivyosonga mbele ndivyo mke alivyoendelea kupoteza urembo wake. Kwa kuwa mume alikuwa kipofu hakulijua hilo na hivyo hakuna kilichobadilika kwenye upendo wao. Aliendelea kumpenda, na mke alimpenda sana mumewe.
.
.
.

Siku moja mke alifariki dunia. Ilikuwa huzuni kubwa sana kwa mume.
Baada ya kumaliza taratibu zote za maziko, mazishi na kutandua msiba, alipanga kuhama kwenye mji huo na kwenda kuishi kwenye mji mwingine.
.
.
.

Mtu mmoja aliposikia habari hiyo alimwendea na kumuuliza: “Sasa utawezaje kutembea peke yako? Maana siku zote hizi mkeo alikuwa akikusaidia kukuonesha njia.”

Akajibu: “Mimi si kipofu. Nilifanya ionekane hivyo kwa sababu angejua kwamba ninauona mwili wake ulivyobadilika kuwa mbaya angepata maumivu makubwa zaidi kuliko ugonjwa wake wenyewe. Alikuwa mke mwema sana. Nilitaka aendelee kuwa na furaha.”
.
.
.

FUNZO:

Wakati fulani ni vizuri ukajifanya kipofu na kuyapuuza mapungufu ya mwenzako ili kumfanya awe mwenye furaha.

Meno huung’ata ulimi mara nyingi, lakini vinaendelea kuishi pamoja kinywani. Huo ndio moyo wa KUSAMEHEANA. Macho hayaonani, lakini yanatazama na kuona vitu kwa pamoja, hupepesa na kulia pamoja. Huo unaitwa UMOJA.

1. Ukiwa peke yako unaweza kuongea, lakini ukiwa pamoja na mwenzako mnaweza KUZUNGUMZA.

2. Ukiwa peke yako unaweza KUFURAHI, lakini ukiwa na mwenzako unaweza KUFURAHIA.

3. Ukiwa peke yako unaweza KUTABASAMU, lakini ukiwa na mwenzako mnaweza KUCHEKA.

Huo ndio UZURI wa mahusiano yetu kama binadamu. Tunategemeana.

Kiwembe kina ukali lakini hakiwezi kukata mti; shoka lina nguvu na imara lakini haliwezi kukata nywele.

*Kila mtu ni muhimu kulingana na kusudio na lengo la uwepo wake. Usimdharau mtu yeyote kwa hali yoyote, kwa sababu huwezi kuwa yeye.

Mwenyezi Mungu atujaalie nguvu na moyo wa kusamehe, kustahmiliana na kuishi kwa umoja.
.
Tafakari
Mm na ww tunaweza kufanya haya!!!

Yafahamu Mambo Mbalimbali kuhusiana na Wanawake kwa Ku-Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

Kitabu hiki kina topiki Zifuatazo;
1. Mambo anayohitaji mwanamke kutoka kwa Mwanaume
2. Mambo yanayowavutia wanawake kutoka kwa wanaume
3. Mambo wanayoyapenda wanawake wakati wa kufanya mapenzi
4. Dalili za mwanamke kicheche
5. Maswali ya kujiuliza kama mwanamke anakupenda kwa dhati au anakudanganya
6. Tabia za mwanamke anayekupenda lakini hawezi kusema
7. Ishara za mwanamke aliyevutiwa na wewe
8. Dalili za mwanamke anayeelekea kukukubali
9. Mambo ambayo mwanamke hawezi kukwambia
10. Njia za kudumisha na kuamsha mapenzi na mwanamke

Kitabu hiki ni Soft copy [pdf] kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa moja kirahisi kabisa hata kwenye simu yako. Utatumiwa Kopi ya kitabu hiki kwenye email yako na utaweza kukihifadhi na kusoma wakati wowote utakaotaka.

[products columns="2" ids="30827"]

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsi ya Kujenga Ushirikiano wenye Furaha na Matarajio ya Muda Mrefu katika Familia

Jinsi ya Kujenga Ushirikiano wenye Furaha na Matarajio ya Muda Mrefu katika Familia

Familia ni chombo muhimu sana katika maisha yetu. Lakini, ili familia iweze kuishi kwa furaha na ... Read More

Jinsi ya KusaidiaWatoto Kukabiliana na Mabadiliko ya Familia: Kuwa na Uthabiti na Msaada

Jinsi ya KusaidiaWatoto Kukabiliana na Mabadiliko ya Familia: Kuwa na Uthabiti na Msaada

Jinsi ya Kusaidia Watoto Kukabiliana na Mabadiliko ya Familia: Kuwa na Uthabiti na Msaada

... Read More

Jinsi ya Kuwa na Mazungumzo ya Heshima na Uwazi katika Familia

Jinsi ya Kuwa na Mazungumzo ya Heshima na Uwazi katika Familia

Kama unataka kuwa na familia yenye amani na furaha, mazungumzo ya heshima na uwazi ni muhimu sana... Read More

Mambo 7 ambayo mwanamme hapaswi kumfanyia mke wake

Mambo 7 ambayo mwanamme hapaswi kumfanyia mke wake

Mambo 7 ambayo mwanaume apaswi kumfanyia mke wake..
1. Usimpige.
2. Usimtukane na kumshushi... Read More

Njia za Kufanya Tarehe ya Kwanza Iwe ya Kusisimua na Msichana

Njia za Kufanya Tarehe ya Kwanza Iwe ya Kusisimua na Msichana

Unapokwenda kwenye tarehe ya kwanza na msichana, ni muhimu sana kufikiria njia za kufanya tarehe ... Read More

Nini imani ya watu katika ngono/kufanya mapenzi ya mara moja au watu wanapendelea uhusiano wa kudumu?

Nini imani ya watu katika ngono/kufanya mapenzi ya mara moja au watu wanapendelea uhusiano wa kudumu?

Kuna mjadala mkubwa kuhusu imani ya watu katika ngono au kufanya mapenzi ya mara moja ikilinganis... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya maendeleo binafsi na ukuaji

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya maendeleo binafsi na ukuaji

Wakati mwingine haifai kuwa mzaha kuhusu kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya maendeleo b... Read More

Uhusiano wa Kufanya Mapenzi na Mazoea ya Kijamii: Kuathiri na Kubadilisha Mtazamo wetu

Uhusiano wa Kufanya Mapenzi na Mazoea ya Kijamii: Kuathiri na Kubadilisha Mtazamo wetu

Uhusiano wa Kufanya Mapenzi na Mazoea ya Kijamii: Kuathiri na Kubadilisha Mtazamo wetu

Map... Read More

Kuweka Mipaka na Kujihami katika Kufanya Mapenzi: Kuimarisha Usalama na Faragha

Kuweka Mipaka na Kujihami katika Kufanya Mapenzi: Kuimarisha Usalama na Faragha

  1. Kuweka mipaka na kujihami katika kufanya mapenzi ni muhimu kwa wote wanaojihusisha kati... Read More

Umri na Kufanya Mapenzi: Athari Zake katika Uhusiano wa Kimapenzi

Umri na Kufanya Mapenzi: Athari Zake katika Uhusiano wa Kimapenzi

Mara nyingi, watu wanafikiri kuwa kufa katika mapenzi kunaweza kuwa jambo la kupendeza, lakini ku... Read More

Jinsi ya Kuweka mipango ya likizo na mapumziko pamoja na mpenzi wako

Jinsi ya Kuweka mipango ya likizo na mapumziko pamoja na mpenzi wako

Kuweka mipango ya likizo na mapumziko pamoja na mpenzi wako ni njia nzuri ya kujenga uhusiano thabit... Read More
Jinsi ya Kuimarisha Upendo na Kuunda Maisha ya Ndoa yenye Maana na mke wako

Jinsi ya Kuimarisha Upendo na Kuunda Maisha ya Ndoa yenye Maana na mke wako

Kuimarisha upendo na kuunda maisha ya ndoa yenye maana na mke wako ni muhimu katika kudumisha uhusia... Read More