Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
AckyShine

BADILIKA: Anza kupiga hatua ya maendeleo sasa

Featured Image

Ili kutoka hapo ULIPO uweze kwenda HATUA inayofuata kuna SWALI muhimu sana unahitaji kujiuliza.
Watu ambao huwa wanashindwa kupiga hatua katika maisha yao ni kwa sababu huwa wanajiuliza kinyume cha swali hili.
Swali hili ndilo wanalojiuliza watu wote waliofanikiwa:

Swali: "Hivi kwa sasa nina nini ambacho naweza kuanza kukitumia kama mtaji wa kwanza kuanza kufanya ninachotaka"?

Siku moja wakati nasoma biblia niliona Mungu alipotaka kumtumia Mussa kuokoa wana wa Israel akamuuliza-

“Una nini mkononi mwako”-

Mussa akajibu
kwa kudharau alichonacho kuwa “Nina fimbo kavu tu ya kuchungia mifugo”.

Ndipo Mungu alianza kumuonyesha miujiza kutumia fimbo ambayo siku zote
alikuwa nayo na kujidharau ndiyo ambayo ikatumika kwenda kuokoa wana wa Israel.

Watu wengi sana wanashindwa kuanza kwa sababu huwa wanajiuliza-

"Hivi ninakosa nini ili niweze kuanza"
badala ya 'Hivi nina nini cha kuanzia'.

Cha kuanzia sio lazima iwe pesa-Inawezekana ni uwezo wa kufanya jambo fulani la kipekee,inawezekana ni
mahusiano mazuri uliyonayo na watu fulani(mtandao wako),inawezekana ni uzoefu ulionao,inawezekana ni kipaji n.k
Leo unapoanza siku yako naomba ijiulize-

“Nina nini mkononi mwangu ambacho naweza kutumia katika
hatua ya kwanza”?.

Kumbuka hakuna mtu ambaye hana
kitu kabisa-KITAFUTE HADI UKIPATE NA ANZA KUKITUMIA KUCHUKUA HATUA.

Share ili wengine wajifunze…..uwe na Jumatatu njema……..

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Unashangaa kwa nini hufanikiwi?

Unashangaa kwa nini hufanikiwi?

Sikiliza, hakuna haja ya kuketi chini ili kuelewa ujumbe huu: Ukweli unabak... Read More

Wewe ni mshindi: Mambo yakuzingatia ili uweze kushinda chochote katika maisha

Wewe ni mshindi: Mambo yakuzingatia ili uweze kushinda chochote katika maisha

Mshindi ni mtu aliyeshinda, Hivyo wewe ni mshindi kwa kuwa umeshinda, kuwa hai leo ni ushindi, ku... Read More

Ushauri wangu kwa leo: Zingatia hili, hamasika, badilika

Ushauri wangu kwa leo: Zingatia hili, hamasika, badilika

Tupo kwenye dunia ambayo tulikuta watu na tutawaacha watu.
Vyote tulivyovikuta vilianzishwa ... Read More

Ujumbe kwa leo

Ujumbe kwa leo

Kuna baadhi ya LEVEL huwezi kufika…Kuna MAFANIKIO huwezi kuyafikia…Kuna HELA huwezi kuzipata... Read More

Elimu ya biashara

Elimu ya biashara

Jifunze kujikagua, jifunze kujiuliza je hapa ndipo napotakiwa kuwa? Usifurahie tu kwamba upo hapo... Read More

Je, Wewe unayesoma huu ujumbe una ndoto?

Je, Wewe unayesoma huu ujumbe una ndoto?

KILA mtu duniani ana ndoto ingawa haijalishi ni ndoto gani uliyonayo.
Nd... Read More

Ilinde ndoto yako

Ilinde ndoto yako