Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
AckyShine

Mizigo tuliyoibeba ambayo haina faida

Featured Image

1.💥Umejipa jukumu la kuwa "mpelelezi" wa maisha ya wengine na umesahau maisha yako.

2.💥Umebeba vinyongo na visasi moyoni vinavyokufanya uwafikirie waliokuumiza zaidi kuliko kufikiria furaha na maendeleo yako.

3.💥 Una marafiki wengi ambao ni kama kupe, wapo kukutumia tu na hawachangii lolote katika maendeleo zaidi ya kujifanya ndio watu wako karibu lakini kumbe wapo kwa maslahi yao!

4.💥Umeweka mbele zaidi "watu watanichukuliaje" kuliko kuangalia maisha yako.Watu ndio wanakuchagulia aina ya maisha unayoishi na unajilazimisha kuishi kama wao hata kama huna uwezo huo.

5.💥Unaongea zaidi ya kasuku lakini vitendo hakuna. Unatamani mafanikio tu moyoni lakini huna mipango ya kuyafikia.
6.💥Maisha yako yote umeyaweka kwenye mitandao ya kijamii. Huna siri hata moja! Hivyo unalazimika kuishi aina ya maisha ambayo yataendelea kufanana na yale uliyoyaweka kwenye mitandao ya jamii kwa sababu ukibadilika tu watasema "umefulia"

7.💥Kila aliefanikiwa ni rafiki yako au utasema ni mtu wako wa karibu na unaishia kuwasifia tu na kupiga nao picha lakini hujifunzi kutokana na mafanikio yao na wala hutumii fursa hiyo ya kujuana nao.

8.💥Upo sahihi kila siku(you are always right). Huambiliki, hushauriki na kila wazo atakalotoa mwenzako basi si zuri ila la kwako ndio sahihi na utataka litekelezwe hilo hilo. Mwisho wa siku kila mtu anakukimbia hakuna wa kukuambia "hapa umekosea" kwa sababu ya ujuaji wako.

9.💥Hujifunzi maarifa mapya.Mara ya mwisho kusoma kitabu ilikuwa ni "Ngoswe, penzi kitovu cha uzembe" Tena ni kwa sababu ilikuwa ni kwa ajili ya kujibia mtihani. Hujifunzi "life skills" wala ujuzi mwingine.

10.💥Unazurura mno mitandaoni bila faida. Kwako wewe intaneti ni kwa ajili ya kuchati tu na kufuatilia habari za mjini ambazo tangu umeanza kuzifuatilia hujawahi kuingiza hata shilingi moja, zaidi unateketeza tu hela yako ya vocha.

ISHUSHE hiyo mizigo kama kweli inahitaji kusonga mbele!

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Elimu ya biashara

Elimu ya biashara

Jifunze kujikagua, jifunze kujiuliza je hapa ndipo napotakiwa kuwa? Usifurahie tu kwamba upo hapo... Read More

Jinsi ya kutengeneza mishumaa

Jinsi ya kutengeneza mishumaa

MALIGHAFI ZINAZO HITAJIKA WAKATI WA UTENGENEZAJI WA MISHUMAA.

1. Paraffin Wax
2. Uta... Read More

Uhusiano uliopo kati ya pesa na muda

Uhusiano uliopo kati ya pesa na muda

Bila shaka upo uhusiano mkubwa kati ya pesa na muda..

-Ndio maana nauli ya ndege ni kubwa k... Read More

Kwa ushauri huu jitambue upate mafanikio

Kwa ushauri huu jitambue upate mafanikio

Ukiona unalala masaa 9 wakati Donald Trump analala manne tu. Afu unaamka huna nauli na bado kesho... Read More

Kukosa hela sio tatizo bali ndio kigezo ya kutafuta hela

Kukosa hela sio tatizo bali ndio kigezo ya kutafuta hela

Ukimonyesha mtu fursa akakwambia hana hela mwambie hiyo ndio sababu ... Read More

FUNZO: Maisha ni kuchagua

FUNZO: Maisha ni kuchagua

Siku hizi kuna tangazo moja la kampuni ya simu za mikononi, Tigo, likimuonesha mama akiwa _busy_ ... Read More

Jinsi Muda Unavyopotea, Jifunze kitu hapa

Jinsi Muda Unavyopotea, Jifunze kitu hapa

Kila mtu ambaye ni hai amepewa muda Wa masaa 24 kila siku,168 kwa wiki,672 kwa mwezi,8064 kwa mie... Read More

Jipe moyo kamwe usikate tamaa

Jipe moyo kamwe usikate tamaa

Nilikuwa naangalia mpira wa miguu katika uwanja wa
shule.
Nilipokaa, Nilimuuliza kijana... Read More

UJASIRIAMALI NA CHANZO CHA MTAJI

UJASIRIAMALI NA CHANZO CHA MTAJI

UJASIRIAMALI