Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
AckyShine

Jinsi ya kutumia kondomu ya kike

Featured Image

Kondomu ya kike inafahamika kwa jina la „care“ na “Lady Peteta”. Hapa Tanzania hazipatikani sehemu zote na bei yake ni kubwa kidogo.
Kondomu ya kike huingizwa ukeni kabla ya kujamiiana. Kama unatumia kondomu ya kike, chana kwa uangalifu pembezoni mwa pakiti. Kondomu ina pete mbili za plastiki na uwazi upande wa juu. Pete moja imelegea ni ndogo na iko kwa ndani, upande usio na uwazi. Pete ya pili ni kubwa zaidi, imeshikiliwa na iko upande wa tundu. Shikilia kondomu upande uliozibwa na minya pete ya ndani kwa dole gumba na kidole cha pili na cha kati. Mara nyingine inaweza ikakuponyoka, (kuteleza) lakini endelea kujaribu hadi umeiminya vizuri. Tafuta mkao mzuri na ingiza kondomu ya kike. Huku bado unaminya kwa vidole vyako iongoze kondomu ndani ya uke wako. Ukiiachia pete ya ndani itashikilia kondomu ndani ya uke. Sasa ingiza kidole chako kwenye kondomu, sukuma pete mpaka inapogota kwenye mlango wa uzazi.
Kondomu ya kike inaweza kuvaliwa saa kadhaa kabla ya kufanya ngono na pia inaweza kuvuliwa baada ya muda wa kufanyika ngono kupita. Ili kuhakikisha kuwa uume umeingia sehemu husika, msaidie mwenzi wako kuongoza uume kuingia kwenye uke ili usipenye pembeni.
Baada ya kujamiiana, vua kondomu kwa uangalifu. Tupa kondomu iliyotumika kwenye choo cha shimo au uichome. Usitupe kondomu iliyotumika ovyo.
Kama ilivyo kwa kondomu ya kiume, kondomu ya kike itatumika kwa mafanikio zaidi pale ambapo wahusikia wanakuwa na makubaliano na maelewano juu ya matumizi yake.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Kwa nini vijana wanakatazwa kujamiiana?

Kwa nini vijana wanakatazwa kujamiiana?

Ujana ni kipindi cha mabadiliko kutoka utotoni kuelekea utu uzima, wakati wa kipindi hiki kijana ... Read More

Vidokezo vya Kuchagua Tarehe ya Kuvutia na Msichana

Vidokezo vya Kuchagua Tarehe ya Kuvutia na Msichana

Kuchagua tarehe ya kuvutia na msichana inaweza kuwa changamoto sana, lakini kwa bidii na uwezo wa... Read More

Je, unaweza kufa kutokana na kuvuta sigara na kunywa pombe?

Je, unaweza kufa kutokana na kuvuta sigara na kunywa pombe?

Ndiyo. Unaweza kufa kutokana na kuvuta sigara au kunywa
pombe. Lakini pale tu utakapozidisha... Read More

Inatokeaje, katika baadhi ya mazingira baba anakataa kuwa mtoto si wake?

Inatokeaje, katika baadhi ya mazingira baba anakataa kuwa mtoto si wake?

Katika mazingira fulani, baba anapomuona mtoto ana ngozi
nyeupe anakataa ya kwamba mtoto si ... Read More

Je, watu wanapendelea kujaribu kufanya mapenzi?

Je, watu wanapendelea kujaribu kufanya mapenzi?

Habari za leo wapendwa wasomaji! Leo, tunajadili kuhusu je, watu wanapendelea kujaribu kufanya ma... Read More

Jinsi ya Kuzungumza na Mwenzi Wangu kuhusu Kujikinga na Mimba

Jinsi ya Kuzungumza na Mwenzi Wangu kuhusu Kujikinga na Mimba

Jinsi ya Kuzungumza na Mwenzi Wako kuhusu Kujikinga na Mimba

Karibu sana marafiki zangu! L... Read More

Utumiaji nguvu katika mahusiano ya ujinsia kama sehemu ya utamaduni

Utumiaji nguvu katika mahusiano ya ujinsia kama sehemu ya utamaduni

Utumiaji wa nguvu
katika mahusiano ya
ujinsia unavunja haki
za uzazi na haki zaRead More

Jinsi ya Kuwa na Mazungumzo ya Kina na Msichana

Jinsi ya Kuwa na Mazungumzo ya Kina na Msichana

Wanaume wengi huwa na shida katika kuongea na wanawake, hasa katika mazungumzo ya kina. Hii mara ... Read More

Je, ni kweli kwamba kuvuta bangi kunaongeza akili na uwezo wa kufikiri?

Je, ni kweli kwamba kuvuta bangi kunaongeza akili na uwezo wa kufikiri?

Hapana, hii si kweli! Vijana wanaoamini kwamba wana uwezo wa kufikiri baada ya kuvuta bangi kwa s... Read More

Je, unaweza kufa ukitumia dawa za kulevya?

Je, unaweza kufa ukitumia dawa za kulevya?

Ndiyo, unaweza. Kifo kinaweza kuwa cha ghafla au
kutokana na madhara ya muda mrefu katika vi... Read More

Mapenzi salama ni yapi?

Mapenzi salama ni yapi?

Mapenzi salama ni yale yanayofanyika bila wasiwasi wa kupata mimba zisizotarajiwa, magonjwa ya zi... Read More

Je, watu wanasema ni muhimu kuelewa na kuheshimu upendeleo wa kingono/kufanya mapenzi wa mwenza wako?

Je, watu wanasema ni muhimu kuelewa na kuheshimu upendeleo wa kingono/kufanya mapenzi wa mwenza wako?

Habari yako! Leo, tutaangazia umuhimu wa kuelewa na kuheshimu upendeleo wa kingono/kufanya mapenz... Read More