Sidebar with Floating Button
Vichekesho vya AckySHINE
☰
AckyShine

Kisa cha kusisimua: Funzo kwa mabinti

Featured Image

Kijana maskini na mwenye maisha duni alimpenda msichana mmoja
Baada ya kutumia muda mwingi kumfikiria msichana huyo,
Siku moja akaamua kumwita na kumwambia ukweli ya kwamba amempenda na angehitaji kumuoa.

Msichana kwa nyodo na jeuri akasema "sikiliza tena unisikilize kwa makini wewe maskini mshahara wako unaopokea kwa mwezi hautoshi hata kwa matumizi yangu ya siku moja sasa utawezaje kunitunza mm!

Kwaufupi mm sio levo zako hivyo basi sahau kabisa kuhusu kunipata mimi
Nenda katafute maskini mwenzio atakae endana na maisha yako,
Mwisho akamwangalia kwa dharau na kisha akaenda zake.

Kwanzia siku ile kijana hakubahatika tena kumuona msichana yule lkn kwakuwa alimpenda basi hakuweza kumsahau kirahisi rahisi siku zilienda na miezi ikasonga,
Miaka 10 baadae wawili hawa walikuja kukutana katika supermarket moja hivi mjini

Kijana alipomwona msichana alitabasamu lakin kabla hajasema chochote msichana kama kawaida yake kwa dharau akasema "we maskin upo! hivi na ww unaingiaga supermarket eh!

Akaongeza huku akisema walau sasahivi nakuona umependeza inaonekana boss wako kakuongeza mshahara
ila kwa kifupi naomba nikwambie sasahivi nimeshaolewa mume wangu anafanya kazi kwenye kampuni moja hivi ya mtu binafsi kampuni maarufu sana na mshahara wa mume wangu ni shilingi milioni moja na laki mbili kwa mwezi na malupulupu mengine kibao,
Unafikiri ww na umaskini wako kuna siku utakuja kufikia kiwango cha mshahara anachopokea mume wangu!

Macho ya kijana yalitokwa na machozi kwa kuona msichana hajabadilika na anaendelea kuwa na maneno ya kejeri na dharau.

Mara hii mume wa yule dada akaingia ktk supermarket
Ile kumuona yule kijana mume akasema "ooh! Kiongozi upo hapa! Leo imekuwa bahati umekutana na mke wangu!" Kisha akamgeukia mke wake na kusema "mke wangu huyu ndo boss wangu

Na unajua nn mke wangu usishangae kumuona boss wangu anakuja kununua vitu mwenyewe hapa supermarket ukweli ni kwamba boss wangu hana mke, anasema alisha wahi kumpenda msichana mmoja lakini hakufanikiwa kumpata na amekuwa na ndoto ya kuja kukutana tena na msichana huyo ndio maana mpaka sasa bado hajaoa.

Akaendelea kusema hebu fikiria ni bahati kiasi gani alikuwa nayo msichana huyo kama angekubali kuolewa na boss wangu leo hii siangekuwa
maisha!

Muda wote msichana alikuwa kimya hajui hata ajibu nn kwa dharau alizomuonyesha kijana tangu mwanzo.

UJUMBE WANGU
Kwenye maisha mambo huweza kubadilika kama vile upepo unavoweza kubadili mwelekeo kulingana na masaa Hivyo basi usimdharau na kumbeza mtu yeyote kwa sababu ya hali aliyonayo,
Maana kila mtu anafungu lake alilopangiwa na Mungu,

Lakini pia kumbuka hakuna ajuaye kesho
Wakati mwingine mtu unayemdharau leo ndiye huyohuyo ambaye kesho utasimulia mafanikio yake.

Kwako unayesoma ujumbe huu nakuombea Mungu akakufungulie milango ya baraka na kuyapa thamani maisha yako ili pale ulipozomewa ukashangiliwe na wale wote waliokudharau punde wakapate kukupigia magoti kwa uweza wa Mungu.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

Director J (User) on May 15, 2025

Good story πŸ’ͺ

Related Posts

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kukuza na kudumisha talanta na vipaji

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kukuza na kudumisha talanta na vipaji

Jinsi ya Kusaidiana na Mpenzi Wako Katika Kukuza na Kudumisha Talanta na Vipaji

Kama wapen... Read More

Je, kuna umuhimu wa kujadili haki na usawa katika uhusiano wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna umuhimu wa kujadili haki na usawa katika uhusiano wa ngono/kufanya mapenzi?

Kila siku, tunaishi katika jamii ambayo ina maadili na kanuni za kufuata katika uhusiano wa ngono... Read More

Jinsi ya Kuwa na Tarehe ya Ushirikiano na Msichana

Jinsi ya Kuwa na Tarehe ya Ushirikiano na Msichana

  1. Anza kwa Kujijenga Kimaumbile Kabla ya kumwomba msichana tarehe ya ushirikiano, ni muhi... Read More

Vidokezo vya Kufanya Msichana Ahisi Anapendwa na Kuthaminiwa

Vidokezo vya Kufanya Msichana Ahisi Anapendwa na Kuthaminiwa

Habari za asubuhi wapendwa! Leo, tutajadili vidokezo muhimu ambavyo vitamsaidia msichana ahisi an... Read More

Jinsi ya Kufurahia maslahi na shughuli za pamoja na mpenzi wako

Jinsi ya Kufurahia maslahi na shughuli za pamoja na mpenzi wako

Kufurahia maslahi na shughuli za pamoja na mpenzi wako ni njia nzuri ya kuimarisha uhusiano wenu na ... Read More
Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya teknolojia na maendeleo ya kidijitali

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya teknolojia na maendeleo ya kidijitali

Katika maisha yetu ya kisasa, teknolojia imekuwa sehemu muhimu sana ya maisha yetu ya kila siku. ... Read More

Je, unyenyekevu una jukumu muhimu katika uhusiano wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, unyenyekevu una jukumu muhimu katika uhusiano wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, unyenyekevu una jukumu muhimu katika uhusiano wa ngono/kufanya mapenzi?

Kwa wengi, ngo... Read More

Kuhamasisha Heshima na Uwiano katika Mahusiano ya Familia

Kuhamasisha Heshima na Uwiano katika Mahusiano ya Familia

Mahusiano ya familia ni muhimu sana katika maisha yetu ya kila siku. Kuwa na heshima na uwiano ka... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya haki za wanyama na utunzaji wa mazingira

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya haki za wanyama na utunzaji wa mazingira

Jinsi ya Kuwasiliana na Mpenzi Wako Kuhusu Masuala ya Haki za Wanyama na Utunzaji wa MazingiraRead More

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha urafiki wa kijamii

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha urafiki wa kijamii

Kujenga na kudumisha urafiki wa kijamii ni muhimu sana katika uhusiano. Hapa kuna njia kadhaa za kus... Read More
Je, watu wanasemaje kuhusu kutumia manjonjo na manukato wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, watu wanasemaje kuhusu kutumia manjonjo na manukato wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Kutumia manjonjo na manukato wakati wa ngono/kufanya mapenzi ni mada ambayo ina debate kubwa. Wap... Read More

Njia za Kupunguza Mazoea ya Kutoelewana na Kukosa Ufahamu katika Familia

Njia za Kupunguza Mazoea ya Kutoelewana na Kukosa Ufahamu katika Familia

Leo tutazungumzia kuhusu njia za kupunguza mazoea ya kutoelewana na kukosa ufahamu katika familia... Read More