Updated at: 2024-05-25 15:26:53 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Hii ni mbegu bora inaitwa UPENDO ipande kwa ndg zako,na pale utakapokuta imeota imwagilie maji ya FURAHA,iwekee kivuli cha USHIRIKIANO, ipalilie kwa jembe la KUSAMEHE, iwekee mbolea ya AMANI, ipige dawa ya NENO LA MUNGU, itakayoua wadudu wote waharibifu kama ubinafsi, chuki, wivu, dharau, unafki, kiburi, choyo, tamaa na fitna kwenye mmea huu, MMEA HUU (UPENDO) UENDELEE KUWA MCHE BORA KULIKO YOTE KTK MAISHA YAKO SIKU ZOTE.
Updated at: 2024-05-25 15:24:52 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
nimetuma ndege wangu auzunguke ''moyo'' wako kwa '' upendo '' auguse ''uso'' wako kwa ''faraja'' na mwisho akunong'oneze sikioni taratibu kuwa nakupenda.
Ujumbe wa mahaba wa kumwambia mpenzi wako penzi lake ni tamu sana
Updated at: 2024-05-25 15:36:38 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
utamu wa penzi hunogeshwa na pendo la dhati pia utamu wa penzi ni uwepo wangu na wako,ladha yake ni zaidi ya nazi kwenye wali au royco kwenye mchuzi au pilipili kwenye kachumbari, utamu wake ni zaidi ya asali au jam kwenye mkate ,blueband kwenye uji.penzi tamu halina kifani
Updated at: 2024-05-25 15:36:04 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mungu akupe umri wa mnazi uishi mingi miaka. Akupe thamani ya mnazi kila kitu chatumika. Kuanzia kuti lake mpaka kwenye kidaka. Kitale katikati yake ukila utaridhika. Matamu na maji yake hukata kiu haraka. Weupe watui lake lina ladha ukipika. Kupaka mafuta yake mwili hulainika. Na kwenye machicha yake kazi nying hufanyika. Hata na upepo wake uvumapo utacheka. Sikijui kitu chake kipi kisichotumika.usiku mwema
Ujumbe wa kimahaba wa kumuuliza mpenzi wako anayatumiaje mapenzi
Updated at: 2024-05-25 15:23:29 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
pendo ni silaha kali zaidi duniani hu uwa wasio na hatia na hujeruhi bila kutarajia,wengine hujitolea muhanga nayo ,silaha hiyo itumikapo vizuri huleta marafiki na kuongeza furaha,je we unaitumiaje silaha hiyo?
Ujumbe wa kimahaba wa kumtumia msichana umpendaye kumwambia kuwa utampenda daima
Updated at: 2024-05-25 15:36:23 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
nashtumiwa kwa kumpenda mcchana mmoja aliyeutesa moyo wangu mahakama imenihukumu kifo kwa kunyongwa na kamba upendo lkn kwa msamaha wa raisi mapenzi nmehukumiwa kuwa mwaminif kwake nakumpenda zaidi ya hapo daima milele. nakupenda mpz