Updated at: 2024-05-25 15:22:11 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Hakika sikutaraji kulikosa lako penzi, wataka kuniacha kuniacha ningali nakuhitaji, mpenzi tambua nahitaji yako hifadhi na niko radhi kukupeleka hadi kwa wangu wazazi, amini kwenda kwa mwingine sihitaji. Nakupenda.
Updated at: 2024-05-25 15:36:19 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Pokea sms yangu iliyojaa utamu, nimeipamba kwa maneno laini yenye ladha adimu, utamu wake ni kama apple haufanani na ndimu, nimeituma kwako sms hii ikuletee salamu "UHALI GANI MPENZI?"
SMS kali ya kimahaba kumwambia mpenzi wako unavyoogopa kwa kuwa unampenda sana
Updated at: 2024-05-25 15:22:53 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mpenzi kwa mara ya kwanza nilipokuana niliogopa kukuambia, hata nilipokuambia niliogopa kukupenda, nilipokupenda sasa naogopa mno kukupoteza. Kusema kweli siko tayari kukukosa katika maisha yangu.
SMS nzuri ya mapenzi ya kimahaba ya kutuma kwa mpenzi wako umpendaye
Updated at: 2024-05-25 15:36:39 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Fikra hutawala mtima wangu, Kwa madhila yalojaa duniani, Kwa muhali wa yanayojiri, Kwa machweo na mawio, Kwa totoro ama nuruni, Nao moyo hukosa ukamilifu, Kwa utashi wa zake hisia, Zinipazo sababu kuu, Ya upendo juu yako, Ya kukufanya daima uwe, Mawazoni mwangu. Mawazoni ama ndotoni, Daima wewe hutawala, Kila asubuhi niamkapo, Nao usiku nilalapo, U chakula changu akilini, Nalo tulizo langu moyoni, Daima huuwaza upekee, Wewe uliojaaliwa, Na hivyo naihisi furaha, Daima wewe uwapo, Mawazoni mwangu.