Ujumbe wa kumsifia mpenzi wako kumwambia kuwa hakuna anayemfikia yeye
Updated at: 2024-05-25 15:26:31 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Baadhi ya watu huzaliwa na vipaji. Huweza kufanya mambo mazuri kwa ujuzi wao, lakini hamna anayekufikia wewe, kwani ukinisogelea tu kila kitu huwa kizuri.
Ujumbe mzuri wa kumwambia mpenzi wako kuwa yeye tuu mdiye kakutawala
Updated at: 2024-05-25 15:36:48 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Fikra hutawala mtima wangu, Kwa madhila yalojaa duniani, Kwa muhali wa yanayojiri, Kwa machweo na mawio, Kwa totoro ama nuruni, Nao moyo hukosa ukamilifu, Kwa utashi wa zake hisia, Zinipazo sababu kuu, Ya upendo juu yako, Ya kukufanya daima uwe, Mawazoni mwangu.
Mawazoni ama ndotoni, Daima wewe hutawala, Kila asubuhi niamkapo, Nao usiku nilalapo, U chakula changu akilini, Nalo tulizo langu moyoni, Daima huuwaza upekee, Wewe uliojaaliwa, Na hivyo naihisi furaha, Daima wewe uwapo, Mawazoni mwangu.
Meseji nzuri ya kumwambia mpenzi wako asichoke kukupenda
Updated at: 2024-05-25 15:23:12 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Thamani ya Mapenzi yako nikubwa kwangu, haifanani nachochote kwenye huu ulimwengu, sina budi kumshukuru mungu, kwa kunijaalia mpenzi mwema unaejali hisia zangu, USICHOKE KUNIPENDA MPENZI
Updated at: 2024-05-25 15:36:40 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Nitaenda mbali Zaidi ya maono yako Safarini nitajenga hekalu la pendo letu Nitapuliza filimbi kama ishara ya utambulisho wako Na mwanzo wa sherehe ya ndoa yetu
Updated at: 2024-05-25 15:36:30 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Katika maisha nimejifunza mambo mengi ikiwemo,. Kupendwa, kupenda, kusamehe, kuvumilia, lakini nimeshindwa kujifunza kukusahau wewe kwa sababu umekuwa ukinikumbuka sana.. nakutakia ASUBUHI NJEMA
Ujumbe mzuri wa SMS wa kumfariji mpenzi wako maisha yake yanapokuwa magumu
Updated at: 2024-05-25 15:36:58 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Furaha yangu kubwa ni kuliona tabasamu lako, kujua uko na furaha, na kuhisi upendo wako. Najua kuwa maisha mara nyingine huwa ni makatili, na hiyo ni sababu niko hapa kukuonyesha kuwa maisha yanaweza kuwa mazuri kama kuna mtu anayekujali.