SMS ya kumtumia mpenzi wako kumuahidi kuendelea kumpenda daima
Updated at: 2024-05-25 15:22:36 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Moyo wangu umehifadhi hisia zako, nakuahidi kamwe sintopunguza upendo kwako, tunza sms hii ya ahadi kwenye simu yako, iwe kumbukumbu kila uisomapo! "NAKUPENDA MALAIKA WANGU"
Dah! Safari yetu ilikuwa ngumu kweli ila hatimaye tumefika japo ni usiku sana hebu tupige hodi tusije kabwa na vibaka hapa nje. Hodiiiiii, Hodiiiii,
Updated at: 2024-05-25 15:37:09 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Dah! Safari yetu ilikuwa ngumu kweli ila hatimaye tumefika japo ni usiku sana hebu tupige hodi tusije kabwa na vibaka hapa nje.
Hodiiiiii, Hodiiiii,
Tunaomba tufungulie Mlango,, sisi tunaitwa FURAHA, AMANI na UPENDO. Tumebeba HEKIMA, BUSARA na MAFANIKIO. Tulikuwa wengi HURUMA na UPOLE wanakuja nyuma. CHUKI na WIVU hawana nauli. TABU ni mahututi. SHIDA yuko jela. MATATIZO amepigwa shoti ya umeme. MIKOSI amefariki njiani. LAANA ameliwa na mamba. UVIVU ameungua na maji ya moto hajiwezi. Tutakuwa nawe daima maana tumefika kwa NEEMA . Mungu akulinde na mabaya yote katika dunia hii. ucku mwema.
Ujumbe wa meseji wa kumsihi mpenzi wako mdumishe mapenzi yenu
Updated at: 2024-05-25 15:25:12 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ni vigumu kumpata mwenye mapenzi ya kweli na zaidi yule atakayekuwa tayari kukupenda zaidi, hivyo nafasi inapopatika si busara kuichezea tudumishe penzi letu laazizi wangu.
SMS ya kumshukuru mpenzi wako na kumwambia kuwa unampenda
Updated at: 2024-05-25 15:26:15 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
nakupenda sana mpenzi wangu ,we ndo wa pekee mwenye kujua furaha ya moyo wangu nikiwa na majonzi huwa upo karibu nami,nikiwa na furaha huja kushea nami,ahsante wangu tabibu ,we ndo wangu wa manani.
Ujumbe wa mahaba wa kumwambia mpenzi wako penzi lake ni tamu sana
Updated at: 2024-05-25 15:36:38 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
utamu wa penzi hunogeshwa na pendo la dhati pia utamu wa penzi ni uwepo wangu na wako,ladha yake ni zaidi ya nazi kwenye wali au royco kwenye mchuzi au pilipili kwenye kachumbari, utamu wake ni zaidi ya asali au jam kwenye mkate ,blueband kwenye uji.penzi tamu halina kifani