Huyu mchungaji ni noma, cheki alichomwambia pedeshe
Mchungaji kamfuata pedeshe moja maarufu kwa kumwaga pesa kwenye kumbi za muziki; MCHUNGAJI: Kijana, tuko katika harakati za kujenga kanisa, jitafutie nafasi katika ufalme wa mbingu kwa kuchangia ujenzi huu. Na Mungu atakubariki zaidi
Updated at: 2024-05-25 18:06:14 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mchungaji kamfuata pedeshe moja maarufu kwa
kumwaga pesa kwenye kumbi za muziki;
MCHUNGAJI: Kijana, tuko katika harakati za
kujenga kanisa, jitafutie nafasi katika ufalme wa
mbingu kwa kuchangia ujenzi huu. Na Mungu
atakubariki zaidi
PEDESHE: Samahani Mchungaji haitakuwa vizuri
mimi kuchangia kanisa, fedha zangu ni haramu,
huwa nazipata kwa utapeli na kuuza madawa ya
kulevya.
MCHUNGAJI: Yote ni heri, pesa yako tutatumia
kwa kujenga eneo la choo we toa tu!!!
Updated at: 2024-05-25 17:14:55 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Chizi kakaa ukingoni mwa bahari analia kwa masikitiko na huku kakamata kijiko cha chai. Mwezake akamuuliza mbona unalia mwenzangu. Chizi akajibu nimetia vijiko vitatu vya sukari baharini, kila nikionja bado ina chumvi. Mwenzake akacheka sanaaaaaa akamwambia. Hujakoroga!!!!😂😂😂😂😂😂
Updated at: 2024-05-25 17:06:14 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mwenzenu nilikatiwa umeme jana basi leo si nikaamua kwenda kununua luku ya 10,000. Kufika njiani nikatamani fursana nikaingia kijisupermarket mara sindo nakutana na ex wangu! Mshenzi yule kaniona mimi sijui alikua na mpango wa kununua vocha ya jero eti kabadili kanunua vocha ya buku tano ilimradi nione maisha yake safi tangu tuachane. Mambo ya kijinga spendi kudadeky nimetoa buku kumi nikanunua mipampers nami nijifanye nimeowa nina mtoto halafu huyoo nikashika njia yangu.
Sasa washkaji zangu tafadhalini mwenye mtoto au shida ya pampers naomba anunue kwangu maana leo nalala tena kiza 🙆♂