Updated at: 2024-05-25 17:46:33 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MADENGE HAKOSI VISA
baada ya kumaliza form four baba akamwambia achague zawadi yoyote aipendayo MADENGE: naomba pesa nikamuoe bibi maana siku nyingi amekuwa akiniita mchumba wake. BABA: Shenzi, yule ni mama yangu mzazi huwezi kumuoa. MADENGE: Mbona wewe umemuoa mama yangu mzazi sijasema kitu ww inakuuma? lazima nilipize kisasi ikikuuma muache mama yangu kila mtu akae na mamayake. 😂😂😂
Updated at: 2024-05-25 16:59:56 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
JE WAJUA!…..
Msuli mrefu kuliko yote kwenye mwili wa binadamu unaunganisha kope za macho na sehemu ya kutolea haja kubwa ndo mana kila ukijaribu kubana jicho moja sehemu ya haja kubwa hufunguka bila kutarajia?
Updated at: 2024-05-25 17:12:11 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Eti kuna mkaka alitembelewa na mama yake mzazi. Wakiwa sebuleni yeye, mama na mke wake, mke wake akaanza kuonekana tofauti kama vile anajiskia vibaya. Akaenda chumbani. Baada ya muda mfupi yule mkaka akamfuata. Wakakaa sana huko kisha mkaka akarudi sebuleni kuendelea kuongea na mama yake. Lakini zipu ya suruali yake ilikuwa wazi. Mama akamuuliza, mkeo anaendeleaje? Akamuambia, anajisikia vzr sasa. Nimempa panadol. Mama akatabasamu na kumwambia mwanaye, sawa. Lakini siku nyingine ukishatoa panadol ukumbuke kufunga pharmacy😂😂
Updated at: 2024-05-25 18:09:37 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mchaga baada ya kufa akaulizwa na malaika anayetoa roho: Mangi hapa ni njiapanda kulia ni Mbinguni na kushoto ni Jehanamu, Je unachagua kwenda wapi?
MANGI: Bwashee, mi nabaki hapa hapa njiapanda aisee. MALAIKA: Kwa nini? MANGI: Aisee, nikifungua duka hapa si nitapata wateja wa Mbinguni na Jehanam. Yani patakuwa senta ya hatari, supu na nyama choma muda wote. Hata we utafaidi, unavyoenda kuchukua roho unaniletea stock nakupa hela yako cash mkononi. Na kila ukipita hapa unapiga mchemsho wako wa ulimi na bia mbili chap kabla ya kuingia mbinguni. Kwanza nashangaa Shirima alipitaje hapa bila kushika ploti, au alikufa amelewa sana?
Updated at: 2024-05-25 17:15:27 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Et jana usiku mwiz kavunja mlango kwangu akaanza kutafuta kitu kila kona ikabid na mie niamke namuuliza unatafuta nini ananijibu hela ndipo nilipoanza na mie kutafuta nae maana hta hela ya kula Jana sikua nayo alichoka zaid nilipomuliza una uhakika uliweka humu? sipendagi ujinga🚶🏻 na kitu hela mm!
Updated at: 2024-05-25 18:10:15 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kakubaliana vizuri na msichana fulani hivi kuwa aibuke gheto, mchizi kajipanga vizuri kabisa…. mara saa nne hivi mdada kasema hana nauli. Mshkaji kajikunja kamtumia Elfu tano maana mwenye shida alikuwa ni yeye…… Baada ya nusu saa yule dada akamtumia meseji. "Jamani mpenzi, kumbe baba hatoki nilijua atatoka… sorry bae sitaweza kuja kwa leo… sooo sorry!" Mshkaji jiii! hajajibu kitu…..
Baada ya muda kidogo meseji ikaingia katika simu ya binti, akajua mchizi kajibu. Mh! kutazama ni meseji kutoka Mpesa.
"CA90F0511 IMETHIBITISHWA Tshs 5000 ILIYOTUMWA KIMAKOSA KATIKA ACCOUNT YAKO IMETOLEWA SALIO LAKO NI Tshs 5"
Halafu ndo ikaingia meseji ya mshkaji. "BASI POA SIKU NYINGINE KAMA VIPI"
#dada wa watu mashavu yakamshuka… hakuamini kilichotokea…. yaani jamaa keshawapigia Voda na pesa fasta imezuiliwa……
Updated at: 2024-05-25 18:11:20 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
BONGO USANII UMEZIDI DAAH!!
…yani nakupeleka dinner unakula sana vipaja vya kuku na chips yai halafu nakupeleka bar unakunywa sana tu, tukitoka hapo nakupeleka club, Masaa yote hayo hakumbuki kuniambia upo periods hadi mdaa wakwenda kulala ndo beiby nipo kwenye siku zangu!! jamani jamani… Hapo ndo unaanza kupiga hesabu pesa iliyopotea buree😂😂😂😂