Kilichotokea baada ya kichaa kumfumania mke wake na mwanamme mwingine
Jay akaruhusiwa kwenda nyumbani kutoka hospital ya Vichaa, akapakiwa ktk ambulance hadi karibu na nyumbani kwake, akaulizwa unapakumbuka? akajibu ndio nyumba yangu ileee, mara wakatoka watoto wawili wamevaa uniform akasema
Updated at: 2024-05-25 18:01:23 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Jay akaruhusiwa kwenda nyumbani kutoka hospital ya Vichaa, akapakiwa ktk ambulance hadi karibu na nyumbani kwake, akaulizwa unapakumbuka? akajibu ndio nyumba yangu ileee, mara wakatoka watoto wawili wamevaa uniform akasema watoto wangu walee wanakwenda shule.. akatoka mwanamke akasema na mke wangu yulee, ghafla akatoka mwanaume Jay akasema na mimi yule naenda kazini. hivi Jay kweli kapona?
Updated at: 2023-04-29 22:52:35 (2 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
Baba- : Halloo mke wangu.. yaani ni shida sitaweza kurudi nyumban, daraja limevunjika na kutoka morogoro kurudi dar haiwezekani MAMA:- Mme wangu morogoro ulienda bila kuniaga! ? BABA:- Ilikuwa ni ghafla sana mke wangu sikuweza kukwambia MAMA:- kha! Sasa watoto nani atawaangalia BABA:- Unasemaje! We uko wapi kwan MAMA:- Niko bagamoyo na daraja limeondolewa na maji sitaweza kurudi. BABA:- Unasemaje we mwanamke.. nakwambia nikukute nyumban ndani ya dk 15 Baada ya dk 15 Baba kafika nyumban. MAMA:- Haya umefkaje kutoka morogoro? BABA:- Nimepewa lift na helkopta ya Mbowe..
Updated at: 2024-05-25 18:09:48 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kuna maprofesa 40 walipanda AIR TANZANIA ili wasafari. Kabla ndege haijaanza kuondoka, Lilipita tangazo kama ifuatavyo:
Ndugu wasafiri wote, ndege unayotarajia kusafiri nayo imetengenezwa na wanafunzi wa Kitanzania. Baada ya tangazo maprofesa wote waliteremka isipokuwa mmoja alibaki kwenye kiti chake Walipomuuliza ni kwanini hakuondoka akajibu kwa haraka na furaha kuwa: Kama ndege hii imetengenezwa na watanzania, hata kuwaka haitawaka!
Updated at: 2024-05-25 17:01:44 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mke: Unampango gani na pasaka hii mmewangu.. Mume: Nitafanya kama yesu.. Mke: Unamaanisha Nini?
Mume: Nitaondoka ijumaa na Kurudi j3.. Mke: Unanishangaza, kama utafanya hivi nami nitafanya kama Maria.. Mume: Unamaanisha Nini? Mke: Nitapata mimba bila ya kuingingiliwa na wewe mume wangu.. Mume: π³π³π³
Mke anamwambia mme wake kuwa angetamani mme wake awe tajiri cheki alichojibiwa
Updated at: 2024-05-25 17:03:41 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mke; mme wangu ungekuwa tajiri ningefurahi Mimi; kwa nini? Mke; ungekuta na sisi tuna gari nzuri hatutembeu kwa mguu Mimi; ah wap,unadhani ningekuwa tajiri ningekuwa na wewe?ungekuta natoka na kina wema,zariβ¦ πππ naona anakusanya nguo zake itakuwa anaenda kufua
Updated at: 2024-05-25 17:48:42 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Tukiwa kanisani mdada alikuwa amelala , akaamka akasikia Pastor anasema " SIMAMA" Yule dada akasimama akashangaaa kanisa zima linamtizima kwa mshangao akiwemo mumewe, akaangalia kanisa zima akashtuka kujiona yeye peke yake ndiye aliesimama Pastor akaendelea vizur endelea kusimama, tumepata mmoja hadi sasa aliyesimama narudia kwa mara ya mwisho kama hujasikia vizuri " kama wew umewahi kumsaliti au bado unasaliti ndoa yako SIMAMA" Binti akazimia