Jinsi ya kutengeneza Biskuti Ya Keki Kavu (Shortcake)
Updated at: 2024-05-25 10:34:41 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga - 2 Magi (vikombe vya chai)
Sukari iliyosagwa - 2/3 Magi (kikombe cha chai)
Siagi - 220 g
Unga wa mchele - ½ Magi
Yai -1
Vanilla - 1 kijiko cha chai
MAANDALIZI
Changanya vitu vyote hivyo kwenye bakuli mpaka unga ushikamane. Paka mafuta treya ya kuchomea kisha utandaze kwenye treya ya 20cm kwa 30 cm au (8 in kwa 12 in) Choma kwenye moto 325˚C kwa muda wa saa nzima au mpaka ibadilike kuwa rangi ya dhahabu. Epua acha ipoe kisha kata vipande kama mstatili, weak kwenye sahani tayari kunywewa na chai.
NYONGEZA
Kwa unga huo huo unaweza kutengeneza vibiskuti vya duara duara.
Updated at: 2024-05-25 10:22:57 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga wa ngano (plain flour) ( 1/4 kilo) Yai (egg 1) Sukari (sugar 1/4 kikombe cha chai) Chumvi (salt 1/4 kijiko cha chai) Hiliki (ground cardamon 1/4 kijiko cha chai) Maji kiasi Mafuta (vegetable oil)
Matayarisho
Tia unga kwenye bakuli, kisha weka sukari, chumvi, hiliki na maji kiasi. Kisha koroga mpaka mchanganyiko wako uwe mzito. Baada ya hapo tia yai na ukoroge tena. hakikisha mchanganyiko hauwi mzito sana au mwepesi sana.Baada ya hapo onja kama kila kitu kimekolea. Injika chuma cha kupikia chapati (fry-pan) jikoni katika moto wa wastani. Baada ya hapo tia nusu kijiko cha chakula cha mafuta katika fry-pan na kisha yatandaze. Hakikisha chuma kinapata moto na weka upawa mmoja wa unga wa chapati na uutandaze mpaka uwe flat. Baada ya hapo subiri mpaka chapati ikauke juu na kisha igeuze upande wa pili tia mafuta kijiko 1 kikubwa cha chakula kwa upande wa chini na wa juu kisha uanze kuikandamiza kwa juu na kijiko ili iweze kuiva vizuri kwa chini. Ikisha kuwa ya rangi ya brown igeuze na upike upande wa pili kiasi kisha iipue na uiweke kwenye sahani yenye kitchen towel ili kukausha mafuta. Rudia hii process kwa unga wote uliobakia. Na chapati zitakuwa tayari
Updated at: 2024-05-25 10:22:57 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Kidali cha kuku 1 (chicken breast) Kitunguu maji 1/2 (onion) Kitunguu swaum/tangawizi (garlic and ginger paste) 1 kijiko cha chai Limao ( lemon)1/4 kijiko cha chai Curry powder 1/4 kijiko cha chai Pilipili ya unga kidogo (Chilli powder) Coriander powder 1/4 kijiko cha chai Soy sauce 1kijiko cha chai Mafuta 2 vijiko vya chai. Chumvi kiasi (salt) Vijiti vya mishkaki
Matayarisho
Osha kidali kisha kikaushe maji na kitchen towel na ukate vipande(cubes) vidogodogo na uweke pembeni. Baada ya hapo changanya vitu vyote (kasoro vijiti )na utie vimaji kidogo kisha visage katika breda kupata paste nzito. Baada ya hapo changanya hiyo paste na kuku na uache zimarinate kwa muda wa saa moja. Baada ya hapo zitunge kuku katika vijiti vya kuchomea na uzichome katika oven mpaka ziive (inaweza kuchukua kama dakika 10). Baada ya hapo chicken satay yako itakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:42 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Maini (Cow liver) 1/4 kilo Vitunguu (chopped onion) 2 Nyanya (chopped tomato) 1 Kitunguu swaum/tangawizi (ginger /garlic paste) 1 kijiko cha chai Mafuta ya kupikia Chumvi Coriander Curry powder 1 kijiko cha chai Limao (lemon) 1/4 Pilipili (scotch bonnet ) 1
Matayarisho
Safisha maini na ukate vipande vidogovidogo na uweke pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu kidogo(visiwe vya brown) kisha tia ginger/ garlic paste,carry powder kaanga kidogo kisha tia nyanya. Kaanga nyanya mpaka zitoe mafuta kisha tia chumvi, pilipili na vimaji kidogo. Acha vichemke kidogo kisha tia maini na uyapike mpaka yaive. Malizia kwa kukamulia limao na kutia coriander kisha ipua na hapo yatakuwa tayari kwa kuliwa.