Updated at: 2024-05-25 10:37:41 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Filigisi (chicken gizzard) 1/2 kilo Carrot iliyokwanguliwa 1 Nyanya 1/2 kopo Vitunguu maji 1 kikubwa Tangawizi/swaum 1 kijiko cha chai Hoho 1 iliyokatwakatwa Limao 1/2 Chumvi Curry powder 1/2 kijiko cha chai Turmaric 1/2 kijiko cha chai Chilli powder 1/4 kijiko cha chai Mafuta Chopped coriander
Matayarisho
Safisha filigisi kisha zikate vipande vidogo vidogo.Zichemshe pamoja na chumvi, limao na nusu ya tangawizi na swaum mpaka ziive (hakikisha unabakiza supu kidogo). Baada ya hapo kaanga vitunguu mpaka viwe vya brown kisha tia tangawizi na swaum iliyobakia na kaanga kidogo kisha tia nyanya. Zipike mpaka ziive kisha tia spice zote pamoja na chilli. Zipike kidogo kisha tia filigisi (bila supu kwanza) Zichanganye vizuri na uzipike kidogo. Baada ya hapo tia carrot na hoho na supu iliyobakia. Vipike pamoja mpaka viive na supu ibakie kidogo sana. Malizia kwa kutia coriander na uipue na hapo firigisi zako zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:34:46 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Wakati mwingine mtu unakuwa umechoka na usingependa kupoteza muda jikoni, so mlo wa chapchap unakuwa ni wazo zuri, Mlo huu ni rahisi kuuanda na hata haikuchukui zaidi ya dakika ishirini chakula kinakuwa tayari mezani.
Mahitaji
Salmon fillet 2 Potatao wedge kiasi Lettice kiasi Cherry tomato Limao 1 Swaum Chumvi Olive oil
Matayarisho
Mmarinate samaki na chumvi, swaum na nusu ya limao kisha muweke pembeni, baada ya hapo washa oven kisha tia potato wedge zikisha karibia kuiva anza kumpika samaki, tia mafuta kidogo sana kama kijiko kimoja cha chai hivi katika frypan isiyoshika chini yakisha pata moto kiasi muweke samaki wako (upande wenye ngozi chini kwanza) Mpike mpaka uone rangi ya kahawia kwa chini kisha mgeuze upande wa pili, uku samaki wako akiwa anaendelea kuiva, tayarisha salad yako kwa kusafisha lettice na nyanya kisha zichanganye pamoja kisha tengeneza salad dressing pembeni , kamua limao kisha tia olive oil na chumvi kidogo, Baada ya hapo samaki na potato wedge vitakuwa vimeiva, andaa mlo wako na utakuwa tayari kwa kuliwa.
Upishi na Karanga na Mbegu: Vyakula vya Virutubishi
π± Upishi na Karanga na Mbegu: Vyakula vya Virutubishi! π₯π₯π½ π Haijui hii siri ya afya? Tuna furaha kukushirikisha! π½οΈ Tukutane katika makala hii kujifunza mapishi ya vyakula vya virutubishi na ladha tele!π€€ π Tuna mengi ya kukuonyesha,π hivyo tunakukaribisha kusoma zaidi!π π₯ Jiunge nasi kwa safari hii tamu ya kula vizuri na kuishi vizuri! ππ ππ½π Bofya hapa sasa kusoma zaidi na kujifunza mapishi ya ajabu! π«ππͺ
Updated at: 2024-05-25 10:22:20 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Upishi wa vyakula vya virutubishi kama vile karanga na mbegu ni muhimu sana kwa afya yetu. Kwa bahati nzuri, vyakula hivi vina ladha tamu na virutubishi vingi, ambavyo vinaweza kuboresha afya yetu kwa njia nyingi. Kwa hiyo, leo, katika makala hii, nataka kuzungumzia faida za upishi wa vyakula hivi na jinsi unavyoweza kuyatayarisha ili kuwa na chakula bora zaidi.
Mbegu kama vile alizeti, ufuta, na maboga ni matajiri katika asidi ya mafuta muhimu, ambayo ni muhimu kwa afya ya moyo na mishipa ya damu.π»π°
Karanga nazo zina protini nyingi, mafuta yenye afya, na nyuzinyuzi, ambazo zinaweza kusaidia kudhibiti kisukari na kukidhi mahitaji ya protini ya mwili.π₯πͺ
Vyakula hivi vinaweza kuongezwa kwenye sahani za mboga, kachumbari au hata katika smoothies za asubuhi ili kuongeza ladha na virutubishi.ππ₯π₯€
Kwa upande mwingine, unaweza pia kutumia karanga na mbegu kama vitafunio vya afya kati ya milo yako.πΏπ°
Kwa kuwa karanga na mbegu hazina cholesterol, zinaweza kuwa chaguo bora badala ya vitafunio vingine vyenye mafuta mabaya.π«π
Upishi wa vyakula hivi kunaweza kufanywa kwa njia nyingi tofauti. Kwa mfano, unaweza kuchoma karanga kwenye sufuria kavu au kuzipika kwa maji chumvi.π°π₯
Kwa mbegu, unaweza kuzikaanga kwenye mafuta kidogo au kuzitumia kama kiungo katika mikate, keki, au saladi.π₯π₯
Vyakula vya virutubishi kama vile karanga na mbegu vinafaa kwa watu wa kila umri na wanaweza kusaidia kuboresha afya ya watoto, vijana, watu wazima na wazee.πΆπ΅
Kwa mfano, watoto wanaweza kula mlo ulio na karanga na mbegu kwa kutengeneza sandwich ya karanga au kuongeza mbegu kwenye tambi au supu.π₯ͺπ
Watu wazima wanaweza kujaribu kuchanganya karanga na mbegu katika sahani za mboga au kwenye saladi ili kuongeza ladha na virutubishi.π₯π₯
Na kwa watu wazee, vyakula hivi vinaweza kusaidia kuboresha afya ya akili na kusaidia kuzuia magonjwa ya kuzeeka kama vile ugonjwa wa Alzheimer's.π§ π‘
Karanga na mbegu pia zinaweza kuwa chaguo bora kwa watu ambao wanahitaji kupata nguvu zaidi, kama vile wanariadha au watu wanaofanya kazi ngumu kimwili.πͺπββοΈ
Kwa kuwa karanga na mbegu zina kiwango cha juu cha kalori, ni muhimu kuzingatia kiasi unachokula ili kuepuka kuongeza uzito kupita kiasi.βοΈπ
Kwa hiyo, kwa kumalizia, nataka kukuhimiza kuongeza vyakula vya virutubishi kama vile karanga na mbegu katika lishe yako ya kila siku. Chakula chako kitakuwa si tu kitamu zaidi, lakini pia kitajaa virutubishi muhimu kwa afya yako. Kumbuka tu kula kwa kiasi na kuzingatia lishe yenye usawa.π°π½οΈ
Kwa maoni yako, je, wewe hula karanga na mbegu mara ngapi kwa wiki? Je, unapenda kuzipika vipi? Ningependa kusikia kutoka kwako! π°π½οΈπ€
Piga piga mayai vizuri kwenye bakuli na weka chumvi kidogo kisha weka kikaango kwenye moto na mafuta kidogo.
Kikisha pata moto miminia mchanganyiko wa mayai na uanze kukorogo pale tu unapomiminia, endelea kukoroga hadi uone yanakuwa magumu na kuanza kuiva. Pika kwa kiwango unachopendelea na kusha epua na weka kwenye sahani.
Weka mafuta kijiko kimoja kwenye kikaango na kisha weka soseji zako na uzipike kiasi pande zote kisha epua na weka pembeni.
Weka slesi za mikate kwenye toster na zikiwa tayari unaweza weka siagi ili kuongeza ladha na mvuto. Andaa mlo wako pamoja na juice, maziwa au chai.
Updated at: 2024-05-25 10:37:42 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Bamia (okra) 20 Nyanya chungu (garden eggs) 5 Magadi soda (Bicabonate soda) 1/4 ya kijiko cha chai Nyanya (fresh tomato) 1 Chumvi (salt) kidogo Pilipili 1/4
Matayarisho
Osha bamia, nyanya chungu na nyanya kisha vikatekate katika vipande vidogovidogo. Baada ya hapo vitie kwenye sufuria na vitu vyote vilivyobakia na kisha tia maji kidogo.Chemsha mpaka bamia na nyanya chungu ziive na vimaji vibakie kidogo sana. Baada ya hapo ziponde na mwiko kidogo kisha zikoroge na uipue na mlenda utakuwa tayari kwa kuliwa na ugali.
Updated at: 2024-05-25 10:37:48 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Makongoro (miguu ya ng'ombe) kiasi Limao 1 kubwa Kitunguu swaum Tangawizi Chumvi Pilipili
Matayarisho
Safisha makongoro kisha yatie kwenye pressure cooker. Kisha tia kitunguu swaum, tangawizi, chumvi,limao na maji kiasi. Baada ya hapo yachemshe mpake yaive na yawe malaini na pia ubakize supu kiasi inaweza kuchukua kama dk 45 au saa 1 hivi. Baada ya hapo yaipue na upakue supu yako kwenye bakuli katia pilipili kiasi kisha itakuwa tayari kwa kuliwa.
Note: Ukiwa unanunua makongoro hakikisha unachukuwa yale yasiyokuwa na manyoya na pia hakikisha usiyachemshe kupitiliza kwani yakiwa malaini sana utashindwa kuyaenjoy.
Jinsi ya kupika Cookies Za Jam Ya Peach Na Raspberry
Updated at: 2024-05-25 10:34:43 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Unga kikombe 1 Β½
Siagi Β½ kikombe
Sukari Β½ kikombe
Yai 1
Vanilla 1 kijiko cha chai
Jam ya peach na raspberry
MAANDALIZI
Wash oven moto wa takriban 180 β 190 Deg F Piga siagi na sukari katika mashine mpaka iwe laini na nyororo (creamy) kisha weka yai na vanilla. Tia unga kidogo kidogo uchanganye kwa mwiko wa mbao (wooden spoon). Pakaza mkononi unga uchukue vidonge ubonyeze kufanya vishimo vya kuwekea jam. Panga katika treya uliyopakaza siagi. Tia nusu yake jam ya peach na nusu jam ya raspberry Bake katika oven kiasi robo saa mpaka ziwive na kugeuka rangi ya brown light. Epua vikiwa tayari
Updated at: 2024-05-25 10:23:12 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viambaupishi Vya Masala
Nyama vipande - 3 LB
Mtindi - Β½ kopo
Kitunguu (thomu/galic) - 1Β½ kijiko cha supu
Tangawizi - 1Β½ kijiko cha supu
Nyanya - 2
Pilipili mbichi - kiasi
Nyanya kopo - 4 vijiko vya supu
Vidonge supu - 2
Pilipili nyekundu paprika - kiasi
Bizari zote saga - 2 vijiko vya supu
Viazi - 4
Mafuta - 2 mug
Samli - Β½ kikombe
Vitungu - 6
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika masala
Kwenye sufuria tia nyama, saga nyanya na thomu, pilipili mbichi, tangawizi. Mimina kwenye nyama na mtindi, tia na nyanya kopo, bizari paprika, vidonge vya supu, chumvi kisha changanya vyote pamoja weka motoni. Katika sufuria nyengine tia mafuta na samli kaanga vitungu mpaka viwe rangi ya hudhurungi toa weka pembeni. Kanga viazi weka pembeni. Chukua mafuta kidogo uliyokangia tia kwenye nyama acha katika moto wa kiasi mpaka nyama iwive na maji ya punguke. Tia viazi na vitunguu vivunje vunje tia ndani ya nyama acha moto mdogo.
Vipimo Vya Wali
Mchele - 5 mug
Maji - kiasi
Chumvi - kiasi
Mafuta uliyokaanga vitungu - kiasi
Rangi ya biriani - ΒΌ kijiko cha chai
*Zafarani - Β½ kijiko cha chai
*roweka rangi na zafarani
Namna Ya Kutarisha Na Kupika Wali
Osha mchele roweka muda wa saa. Chemsha maji kama magi 10 hivi na chumvi tia mchele. Uache uchemke ukishaiva kiini nusu, mwaga maji chuja. Mimina juu ya nyama tia rangi na mafuta kwa juu funika. Aacha kidogo katika oveni kwa muda wa dakika 20 hivi kisha epua ikiwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:23:12 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo
Wali:
Mchele - 3 Vikombe
Kitunguu kiichokatwa - 1
Pilipili boga nyekundu iliyokatwa vipande - 1
Mafuta - ΒΌ Kikombe
Zaafarani - 1 kijiko cha chai tia kwenye kikombe na maji robo roweka
Chumvi - 1 kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Katika sufuria, tia mafuta, kaanga kitunguu mpaka kiwe kidogo rangu ya udongo (brown) Tia pili pili boga. Tia mchele, kaanga kwa muda wa dakika 3, tia zaafarani na chumvi. Tia supu uliyochemshia kuku iwe imoto. Pika wali katika moto mdogo hadi uwive.
Kuku
Kuku Mzima -1
Mayai ya kuchemsha - 6
Namna Ya Kupika Kuku
Mchemshe kuku mzima na chumvi mpaka uhakikishe ameiva vizuri. Mtowe na muweke pembeni. Supu yake tumia katika wali kama ilivyo hapo juuu. Chemsha mayai, menya na kata vipande viwili kila yai moja weka kando
Vipimo Vya Sosi Ya Kuku Ya Nazi
Kitunguu - 1
Nyanya iliyokatwa vipande - 1
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi - 1 kijiko cha supu
Garam Masala - Β½ kijiko cha supu
Bizari ya manjano - Β½ kijiko cha chai
Chumvi - kiasi
Pilipili masala ya unga - Β½ kijiko cha chai
Nyanya ya kopo - 1 kijiko cha supu
Nazi ya unga - 1 kikombe
Maji ya ukwaju - ΒΌ kikombe cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Tia Mafuta vijiko 2 vya supu katika sufuria Kaanga kitunguu maji mpaka kiwe rangi ya udongo (brown). Tia thomu na tangawizi. Tia nyanya nzima iliyokatwa katwa. Tia garam masala, manjano, pilipili ya unga, nyanya ya kopo, kaanga vizuri. Changanya kwenye sufuria na ukwaju. Iache ichemke vizuri. Changanya nazi ya unga na maji vikombe viwili. Mtie kuku mpike vizuri na hilo tui. Mtie kwenye oveni kidogo.
Kupakuwa katika Sinia
Pakuwa wali kwanza katika sinia Muweke kuku juu ya wali. Pambia mayai
Tofauti kati ya yai la kuku wa kienyeji na la kuku wa kisasa
Updated at: 2024-05-25 10:34:45 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kilishe mayai yote ni sawa. Virutubishi vinavyopatikana kwenye yai la kuku wa kienyeji kama protini, vitamini A, madini ya chuma na virutubishi vya aina nyingine, ndivyo hivyo vinavyopatikana pia kwenye yai la kuku wa kisasa.
Tatizo linaweza kutokea pale ambapo wafugaji wa kuku wa kisasa hawafuati taratibu za ufugaji na pengine hawawapi kuku vyakula muhimu wanavyohitaji au wanawapa dawa na vyakula visivyo bora kiafya, hivyo wakati mwingine kiini cha yai la kuku wa kisasa huonekana kupungua rangi ya njano kuliko kiini cha yai la kuku wa kienyeji.
Mtu anashauriwa kula yai bila kujali ni la kuku gani, kwa kutegemea ni yai lipi linapatikana kwa urahisi. Lakini nivizuri kula mayai ambayo yapo salama.