Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Kisa cha kusisimua: Funzo kwa mabinti

Featured Image

Kijana maskini na mwenye maisha duni alimpenda msichana mmoja
Baada ya kutumia muda mwingi kumfikiria msichana huyo,
Siku moja akaamua kumwita na kumwambia ukweli ya kwamba amempenda na angehitaji kumuoa.

Msichana kwa nyodo na jeuri akasema "sikiliza tena unisikilize kwa makini wewe maskini mshahara wako unaopokea kwa mwezi hautoshi hata kwa matumizi yangu ya siku moja sasa utawezaje kunitunza mm!

Kwaufupi mm sio levo zako hivyo basi sahau kabisa kuhusu kunipata mimi
Nenda katafute maskini mwenzio atakae endana na maisha yako,
Mwisho akamwangalia kwa dharau na kisha akaenda zake.

Kwanzia siku ile kijana hakubahatika tena kumuona msichana yule lkn kwakuwa alimpenda basi hakuweza kumsahau kirahisi rahisi siku zilienda na miezi ikasonga,
Miaka 10 baadae wawili hawa walikuja kukutana katika supermarket moja hivi mjini

Kijana alipomwona msichana alitabasamu lakin kabla hajasema chochote msichana kama kawaida yake kwa dharau akasema "we maskin upo! hivi na ww unaingiaga supermarket eh!

Akaongeza huku akisema walau sasahivi nakuona umependeza inaonekana boss wako kakuongeza mshahara
ila kwa kifupi naomba nikwambie sasahivi nimeshaolewa mume wangu anafanya kazi kwenye kampuni moja hivi ya mtu binafsi kampuni maarufu sana na mshahara wa mume wangu ni shilingi milioni moja na laki mbili kwa mwezi na malupulupu mengine kibao,
Unafikiri ww na umaskini wako kuna siku utakuja kufikia kiwango cha mshahara anachopokea mume wangu!

Macho ya kijana yalitokwa na machozi kwa kuona msichana hajabadilika na anaendelea kuwa na maneno ya kejeri na dharau.

Mara hii mume wa yule dada akaingia ktk supermarket
Ile kumuona yule kijana mume akasema "ooh! Kiongozi upo hapa! Leo imekuwa bahati umekutana na mke wangu!" Kisha akamgeukia mke wake na kusema "mke wangu huyu ndo boss wangu

Na unajua nn mke wangu usishangae kumuona boss wangu anakuja kununua vitu mwenyewe hapa supermarket ukweli ni kwamba boss wangu hana mke, anasema alisha wahi kumpenda msichana mmoja lakini hakufanikiwa kumpata na amekuwa na ndoto ya kuja kukutana tena na msichana huyo ndio maana mpaka sasa bado hajaoa.

Akaendelea kusema hebu fikiria ni bahati kiasi gani alikuwa nayo msichana huyo kama angekubali kuolewa na boss wangu leo hii siangekuwa
maisha!

Muda wote msichana alikuwa kimya hajui hata ajibu nn kwa dharau alizomuonyesha kijana tangu mwanzo.

UJUMBE WANGU
Kwenye maisha mambo huweza kubadilika kama vile upepo unavoweza kubadili mwelekeo kulingana na masaa Hivyo basi usimdharau na kumbeza mtu yeyote kwa sababu ya hali aliyonayo,
Maana kila mtu anafungu lake alilopangiwa na Mungu,

Lakini pia kumbuka hakuna ajuaye kesho
Wakati mwingine mtu unayemdharau leo ndiye huyohuyo ambaye kesho utasimulia mafanikio yake.

Kwako unayesoma ujumbe huu nakuombea Mungu akakufungulie milango ya baraka na kuyapa thamani maisha yako ili pale ulipozomewa ukashangiliwe na wale wote waliokudharau punde wakapate kukupigia magoti kwa uweza wa Mungu.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

Director J (User) on May 15, 2025

Good story πŸ’ͺ

Related Posts

Kusisimua Hisia katika Kufanya Mapenzi: Njia za Kuchochea Hamu na Ushirikiano

Kusisimua Hisia katika Kufanya Mapenzi: Njia za Kuchochea Hamu na Ushirikiano

Kusisimua Hisia katika Kufanya Mapenzi: Njia za Kuchochea Hamu na Ushirikiano

Mapenzi ni h... Read More

Kukabiliana na Matarajio ya Jamii katika Kufanya Mapenzi: Kujitambua na Kujieleza

Kukabiliana na Matarajio ya Jamii katika Kufanya Mapenzi: Kujitambua na Kujieleza

Mapenzi ni jambo muhimu katika maisha yetu na yanahusisha mambo mengi sana, ikiwemo kukabiliana n... Read More

Njia za Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii na Urafiki katika Mahusiano

Njia za Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii na Urafiki katika Mahusiano

Hakuna kitu kizuri kama kuwa na marafiki wengi na mahusiano bora ya kijamii. Uhusiano mzuri unahi... Read More

Msaada na Ushirikiano katika Familia: Kuweka Wanafamilia Kwanza

Msaada na Ushirikiano katika Familia: Kuweka Wanafamilia Kwanza

  1. Msaada na Ushirikiano Katika Familia Ni Muhimu Sana

Katika jamii yetu, famili... Read More

Kuhamasisha Ushirikiano na Maendeleo ya Kibinafsi katika Mahusiano yako

Kuhamasisha Ushirikiano na Maendeleo ya Kibinafsi katika Mahusiano yako

Mahusiano ni jambo muhimu sana katika maisha yetu, hasa yale ya kimapenzi. Ndio maana ni muhimu s... Read More

Jinsi ya Kusimamia Mipaka na Kanuni katika Familia: Kuwa na Muongozo

Jinsi ya Kusimamia Mipaka na Kanuni katika Familia: Kuwa na Muongozo

Kusimamia mipaka na kanuni katika familia ni muhimu sana kwa ustawi wa familia yako. Ili kuwa na ... Read More

Jinsi ya Kuonyesha Utambulisho Wako kwa Msichana

Jinsi ya Kuonyesha Utambulisho Wako kwa Msichana

Jinsi ya Kuonyesha Utambulisho Wako kwa Msichana

Kuonyesha utambulisho wako kwa msichana n... Read More

Jinsi ya Kuunganisha Kupitia Mchezo: Furaha na Uhusiano wa Familia

Jinsi ya Kuunganisha Kupitia Mchezo: Furaha na Uhusiano wa Familia

Karibu kwenye makala hii ambayo itakufundisha jinsi ya kuunganisha kwa furaha na uhusiano wa fami... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu ndoto na malengo ya kazi na kazi ya kila mmoja

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu ndoto na malengo ya kazi na kazi ya kila mmoja

Kwa wapenzi wengi, kuwa na ndoto za kazi na malengo ni sehemu muhimu ya maisha yao. Kwa hiyo, ni ... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kushughulikia matatizo ya kifamilia

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kushughulikia matatizo ya kifamilia

Karibu sana katika makala hii ambapo tutaangalia jinsi ya kusaidiana na mpenzi wako katika kushug... Read More

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Ushirikiano katika Familia: Kuhamasisha Ushirikiano wa Timu

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Ushirikiano katika Familia: Kuhamasisha Ushirikiano wa Timu

  1. Shughulikia masuala yako ya kibinafsi kabla ya kujihusisha na familia yako. Unapojihusi... Read More

Jinsi ya Kupambana na Mawazo na Hisia Hasi za mke wako

Jinsi ya Kupambana na Mawazo na Hisia Hasi za mke wako

Kupambana na mawazo na hisia hasi za mke wako ni muhimu katika kujenga na kuimarisha uhusiano wenye ... Read More