Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Kisa cha kusisimua cha kijana na mke wake na mama yake

Featured Image

Kuna kijana mmoja daktari alikwenda kuposa. Binti aliyemposa akamuwekea masharti mazito. Akamwambia chagua mawili imma kunioa mimi au kukaa na mama yako, kwa sababu ukinioa mimi sitokubali mama yako aje hata harusini kwangu! Yule kijana aliemewa. Hakujua la kufanya. Mke anamtaka, lakini mama yake pia anampenda.


Hivyo aliamua kuomba ushauri kwa mwalimu wake wa chuo kikuu. Alimwambia: moyo wangu unampenda mno binti niliyekwenda kumposa, lakini pia siwezi kuishi mbali na mama yangu. Nifanye nini?


Yule mwalimu mwenye hekima ambaye alikuwa anajua tabu alizopitia mama wa kijana yule, alimjibu kwa kumwambia: Kabla ya kukueleza uchague yupi kati ya wawili hao, rudi nyumbani, na leo usifanye chochote, ila kuikosha mikono ya mama yako. Yule kijana alifanya kama alivyotakiwa na mwalimu wake. Alipofika nyumbani aliomba idhini kwa mama yake amruhusu kuikosha mikono yake, na yule mama alimkubalia bila ya ajizi yoyote.



Yule kijana alipoanza kuikosha mikono ya mama yake na kuona jinsi ilivyogugutaa kwa kazi za sulubu, alilia sana. Muda wote huu alikuwa hajawahi kuangalia viganja vya mama yake. *Je, na wewe umewahi kukaa na kuangalia viganja vya mama au baba yako kuona tabu walizopitia kukulea?* Kumbe baba wa yule kijana alifariki dunia yeye akiwa bado mdogo, yule mama aliamua kusamehe kila kitu kwa ajili ya mustakbali wa mwanawe. Alijitolea kufanya kazi za sulubu. Alikubali kuwa mtumishi wa ndani, kukosha nguo, kupiga deki na kila kazi ambayo alihisi ingelimletea chumo la halali bila ya kujali ugumu wa jkazu hiyo.



Juhudi zake zilizaa matunda na kufanikiwa kumlea na kumsomesha mwanawe hadi chuo kikuu na sasa ni daktari ambaye ana mustakbali mzuri. Baada ya yule kijana kukumbuka yote hayo, alifanya haraka kumpigia simu mwalimu wake huku macho yakiendelea kububujikwa na machozi akimwambia, siwezi kusubiri hadi kesho. Jibu nimeshalipata. Siwezi kumtupa mama yangu kwa ajili ya mtu asiyejua thamani ya mama. Ahsante sana kwa kunionesha njia sahihi! Kamwe siwezi kumuuza mama yangu kwa ajili ya leo yangu wakati yeye ameuza maisha yake yote kwa ajili ya mustakbali wangu.
NANI KAMA MAMA?!? Maa! Tabasamu lako ni ufunguo wangu wa ofanisi.
Kama umeipenda.


Share kwa wengine ili nao wazinduke.






Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE




[products columns="2" ids="30827"]


AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsi ya Kuwa na Mawasiliano ya Wazi na Msichana Wako

Jinsi ya Kuwa na Mawasiliano ya Wazi na Msichana Wako

Jinsi ya Kuwa na Mawasiliano ya Wazi na Msichana Wako

Ndoa ni muunganiko wa wawili kuwa ki... Read More

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za kiimani na dini na mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kushughulikia tofauti za kiimani na dini na mpenzi wako

Mapenzi ni hisia za kipekee ambazo huja na changamoto zake. Mojawapo ya changamoto kubwa katika u... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya elimu na mafunzo

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya elimu na mafunzo

Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya elimu na mafunzo inaweza kuwa ngumu sana. Lakini hak... Read More

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kielimu na Kukuza Maarifa katika Familia

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kielimu na Kukuza Maarifa katika Familia

Kuhamasisha ushirikiano wa kielimu na kukuza maarifa katika familia ni muhimu sana katika kuhakik... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha ushiriki na jamii

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha ushiriki na jamii

Sisi sote tunajua kuwa mahusiano ya kimapenzi yanakuja na majukumu mengi, lakini jambo la muhimu ... Read More

Mbinu za Kujenga Upendo na Shukrani Ndani ya Familia: Mwongozo wa Mtaalamu

```html

Njia za Kujenga Utamaduni wa Upendo na Shukrani Ndani ya Familia: Msingi wa Furaha na Ms... Read More

Jinsi ya Kusikiliza kwa Uelewa na Kueleza Hisia

Jinsi ya Kusikiliza kwa Uelewa na Kueleza Hisia

Kusikiliza na kuelewa hisia za mke wako ni muhimu katika kujenga uhusiano wa karibu na wa kina. Hapa... Read More
Je, ni muhimu kuelewa na kuheshimu hisia za mwenza wako wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, ni muhimu kuelewa na kuheshimu hisia za mwenza wako wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

  1. Kujenga uhusiano wa kimapenzi wenye afya na mwenza wako ni muhimu sana. Hii ni kwa saba... Read More

Jinsi ya Kuwa na Mawazo Chanya katika Familia: Kujenga Mazingira ya Ustawi

Jinsi ya Kuwa na Mawazo Chanya katika Familia: Kujenga Mazingira ya Ustawi

Kama wazazi na familia, ni muhimu kujenga mazingira yenye mawazo chanya. Mawazo chanya ni muhimu ... Read More

Kujenga Mazingira ya Upendo na Kujali katika Familia Yako

Kujenga Mazingira ya Upendo na Kujali katika Familia Yako

Familia ni moja ya mazingira muhimu kuliko yote katika maisha yetu. Ni mahali ambapo tunakulia, t... Read More

Jinsi ya Kuunda Mazingira ya Kuwawezesha Watoto kufikia Malengo Yao

Jinsi ya Kuunda Mazingira ya Kuwawezesha Watoto kufikia Malengo Yao

Kuwawezesha watoto kufikia malengo yao ni jambo muhimu sana katika kuhakikisha kuwa wanakuwa na m... Read More

Jinsi ya Kuimarisha imani na kuaminiana katika uhusiano na mpenzi wako

Jinsi ya Kuimarisha imani na kuaminiana katika uhusiano na mpenzi wako

Kuimarisha imani na kuaminiana katika uhusiano wako na mpenzi wako ni muhimu sana kwa kujenga uhusia... Read More