Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Ndoa sio utani. Soma stori hii

Featured Image

"Mkeo amefariki. Rudi nyumbani kwako haraka sana" Hezron alimwambia Daniel katika simu.

"Mke wangu amekufa? Nini kimetokea? Amekufaje?" Daniel aliuliza huku akionekana kuchanganyikiwa vibaya.

"Daktari amesema ni shinikizo la moyo lililosababishwa na stress kali. Daktari na polisi wapo hapa nyumbani kwako. Njoo haraka" Hezron akaongea kidogo na akakata simu.

Muda anapigiwa simu na Hezron, Daniel alikuwa mtoko na mwanamke mwingine mrembo katika moja ya hoteli kubwa iliyoko maeneo ya Kunduchi. Alikuwa akifurahi nae huku wakinywa vinywaji ghali na chakula cha hadhi ya nyota tano. Lakini baada ya kupokea tu ile simu ya taarifa ya kifo cha mkewe, Daniel alichanganyikiwa, uso wake ukabadilika.

Hezron ni rafiki yake wa karibu.

Daniel akainuka na kuondoka katika ile Hotel akimwacha yule mwanake Mrembo.

"Kuna tatizo gani?" Yule mrembo aliuliza.

"Siwezi kuzungumza" Daniel alijibu na kuondoka haraka.

Daniel akaenda alikopaki gari yake, akaingia, akaiwasha na kukanyaga mafuta, akaiondoa kwa kasi ya ajabu.

Akiwa anaendesha, Daniel akakumbuka jinsi yeye na mkewe anaeambiwa amefariki walivoenda pamoja Showroom ya magari na kununua hilo gari pamoja.

Akiwa anakata kona, akakumbuka jinsi alivyokuwa akimfundisha mkewe kuendesha gari. Hizo zilikua nyakati njema kabisa katika maisha yao ya ndoa.

"Mke wangu amekufa! Kweli mke wangu amekufa! Mungu wangu.." alilia sana huku akiendesha.

Akakumbuka siku ya ndoa yao. Agano waliloliweka pamoja. Akiwa anabadilisha gia, akaangalia vidole vyake asiione pete yake ya ndoa. Pete ya ndoa aliitoa ili kudanganya wanawake wengine kwamba hajaoa.

Daniel akakumbuka ni jinsi gani alivyokuwa akimjibu mkewe hovyo, kwamba anayo kila sababu ya kufurahia maisha na kuponda raha. Akakumbuka maneno ya kuchoma aliyokuwa akimwambia mkewe kwamba yeye amezaa na amezeeka!

"Mke wangu amefariki! Kwanini umefariki Lisa! Kwanini Mungu? Alijiuliza maswali lukuki.

Jibu likamjia. Akakumbuka ni nini Hezron alimwambia. Kwamba mkewe yawezekana amekufa kwa shinikizo la damu kutokana ma stress. Kwa hali hiyo Daniel nimemuua mke wangu.

"Nimemuua mke wangu mwenyewe. Mungu nisamehe…" alijutia huku akiendesha gari kwa kasi.

Daniel akakumbuka jinsi mambo yalivyoenda vibaya katika ndoa yake. Jinsi gani upendo ulikimbia katika ndoa yao. Jinsi gani walivyoanza mabishano na ugomvi. Takribani mara nne ameshampiga mkewe vibao. Alikuwa mtu mbaya kwa mkewe na kwa watoto wake wadogo wawili.

Alifikiri aache kuhudumia familia, hitaji lake likaja kuwa kutomheshimu mkewe, kutomheshimu mkewe kukaleta dharau na maneno ya kejeli kwa mkewe, maneno ya kejeli yakasababisha vidonda vya tumbo kwa mke mwema Lisa kutokana na mawazo na kutokula.

Naam, Lisa aliugua vidonda vya tumbo kutokana na maumivu ya mawazo aliyosababishiwa na mumewe. Afya yake ilikongoroka, umbo lake zuri namba nane lilipotea, Lisa alionekana kama mzee, wakati ni mwanamke wa miaka 29 tu. Ila Daniel hakujali, alimzarau. Alijibadili kutoka mume aliyempenda mkewe kuwa mtu msaliti, anayemuumiza mkewe. Lisa amefariki!!?

Akiwa bado anaendesha akakumbuka jinsi alivyomfuata Lisa na kumuomba wafunge ndoa, Lisa alikuwa mzuri, akijitegemea na mwenye furaha na maisha. Yeye kumuoa tu ndio ikawa kumharibu, kumuumiza na mwishowe kumuua kwa stress!

Atakufaje? Hawezi kujua kwa sababu hajarudi nyumbani wiki moja sasa imepita, hajui watoto wanakula nini, wanavaa nini. Mke wake alikuwa akimtumia texts na kumpigia akimsisitizia arudi nyumbani, ila kilio cha mkewe kilitua katika masikio yake ambayo hayasikii. Mkewe alikuwa akilia, akipiga kelele mumewe arudi nyumbani, yote hayo ni kwa ajili ya kuokoa ndoa yake. Lakini mimi Daniel sikusikia. Sasa amefariki!

"Mimi nitafanya nini na watoto wangu?" alifikiria nafsini kwake. Watoto wawili alionao ambao alikuwa hawajali kwa sababu ya kuwa busy na warembo wa jiji la Makonda. Akakubali kwamba kweli mke wake alikuwa na moyo wa ajabu, kuwatunza watoto wale wawili bila msaada wake.

"Nani atanisaidia kuwalea? " Wanawake ambao amekuwa akila nao bata hawawezi kumsaidia kulea watoto, sio wife material wale, wife material hawezi kuvunja ndoa ya mwanamke mwenzake. Alifikiria nafsini mwake.

Wazazi wa mkewe watafikiri nini?
Watu watafikiri nini? Mungu ananifikiriaje?
Hii ndio inaishaje ishaje? Ndoa yangu ndio imeishia hivi? Mke wangu kafariki?

Daniel akapaki gari, akatoka na kukimbia ndani ya nyumba.

Akafungua geti, akafungua mlango. Akamuona Hezron, rafiki yake akiwa amesimama katika korido ya nyumba yake.

"Kimetokea nini? Haiwezekani kuwa amekufa. Hawezi kufa. Mimi nitafanya nini Hezron?" Daniel aliongea akiwa amekata tamaa.

Hezron akamkumbatia Daniel.

"Uko sawa Daniel?" Hezron aliuliza.

"Nitakuaje sawa wakati mke wangu amekufa? Mama wa watoto wangu! Uko wapi mwili wake?" Daniel aliuliza.

"Upo sebuleni" Hezron alijibu.

Daniel akakimbia kuelekea sebuleni.

Mshangao!!

Akamwona mkewe akiwa hai. Amekaa katika sofa akiwa na mke wa Hezron ambae ni daktari wa saikolojia pembeni.

"Haujafa?!" Daniel aliuliza akiwa na mshangao

"Ndio hajafariki. Ila kama ukiendelea na hii tabia atafariki siku moja. Mkeo hajawa sawa kabisa. Amekuwa akijaribu kukutafuta na kukurudisha nyumbani ila umempuuza. Taarifa za kifo chake zimekufanya ukimbie kama mwehu. Ulitakiwa ukimbie kwa ajili ya maisha yake na si kwa ajili ya kifo." Mke wa Hezron aliongea.

Daniel akakaa katika kochi mbele ya mkewe na akamshika uso wake. Mkewe akarudishwa kichwa nyuma.

"Natumaini kwamba safari yako ya uchungu kuja hapa ukifikiri mkeo amekufa itakukumbusha ni nini cha muhimu kinachotakiwa kufanywa. Usisubiri mpaka uchelewe ndio ufanye jambo jema. Unayo nafasi ya pili." Aliongea mke wa Hezron

Daniel akanyanyua mkono wa mkewe machozi yakimtiririka, asiamini juu ya kile anachoshuhudia.

"Ndoa sio lelemama nyie wawili. Acheni kucheza michezo ya kipumbavu na maisha. Kesho sio garantii" aliongeza mke wa Hezron.

"Nyie wawili mna matatizo. Mmeridhika na matatizo ya kuumizana hasa wewe shemeji yangu Daniel. Kesho haiwezi kuwa pale kwa ajili yako kwa ajili ya kuomba msamaha. Mkewe Hezron aliongea.

"Na siku ya kiama tutakapokutana na mwenyezi Mungu, Daniel kitu ambacho Mungu atauliza ulimtendaje mke wako ambae ni ubavu wako? Huyu ni binti wa Mungu. Unavomuumiza yeye na Mungu anaumia pia" Akaongezea Hezron.

Mke wa Daniel akamgeukia Hezron na mkewe akasema "Nashukuruni sana kwa kupanga hii idea ya kumuamsha mume wangu, sio siri nilitamani kufa hata leo. Ninampenda sana ila nimechoka na maumivu. Ninyi ni marafiki bora wa familia yetu.

Daniel akamkumbatia mkewe tightly na akasema "Nisamehe sana Lisa wangu, sitaki kukupoteza. Leo nimeshuhudia familia yangu ikivunjika vipande vipande. Nilikuwa kipofu tena katikati ya giza tororo ila sasa ninaona. Usife tafadhali. Nitafanya yale yaliyo bora kuanzia sasa.

Rafiki yangu Hezron na shemeji yangu Julieth ninyi ni marafiki bora kabisa, rafiki aliye bora hukuondoa katika kiza na kukuweka katika nuru. Mmedhihirisha hilo. Naomba niwaahidi tukio hili limekuwa funzo kubwa kwangu. Naanza sasa kuwa mume na baba bora wa familia. Ila siku nyingine msinitishie kifo, naweza kufa kwa pressure na mimi. Nawashukuruni sana. Mwenyezi Mungu awajazi.

"Hahaaa Okey yaishi maneno yako, Mke wangu na mimi tunawaacha, tuwaache mfanye yale ambayo wanandoa wawili wanaopendana kweli hufanya." Hezron aliongea.

Na wakaondoka!

Mpende mwanandoa mwenzako, waheshimu wazazi, wabariki watoto wako, wapende rafiki zako, wote wakiwa bado wako hai.

Kabla hujachelewa!

Busara yangu,.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Njia za Kupunguza Mazoea ya Kutokuelewana na Kukosa Msamaha katika Familia Yako

Njia za Kupunguza Mazoea ya Kutokuelewana na Kukosa Msamaha katika Familia Yako

Familia ni nguzo muhimu sana katika maisha yetu na tunapaswa kuilinda kwa gharama yoyote ile. Hat... Read More

Njia za Kupunguza Mazoea ya Kukosa Uwiano na Kuunda Amani na Furaha katika Familia

Njia za Kupunguza Mazoea ya Kukosa Uwiano na Kuunda Amani na Furaha katika Familia

Familia ni kitu muhimu sana katika maisha ya kila mtu. Ni katika familia ndipo tunapopata upendo,... Read More

Je, unyenyekevu una jukumu muhimu katika uhusiano wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, unyenyekevu una jukumu muhimu katika uhusiano wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, unyenyekevu una jukumu muhimu katika uhusiano wa ngono/kufanya mapenzi?

Kwa wengi, ngo... Read More

Je, kuna tofauti ya kiumri katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna tofauti ya kiumri katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna tofauti ya kiumri katika ngono/kufanya mapenzi? Ndio! Kuna tofauti kubwa sana kati ya wa... Read More

Je, nini imani ya watu katika kujifunza kutoka kwa mwenza wako kuhusu ngono/kufanya mapenzi?

Je, nini imani ya watu katika kujifunza kutoka kwa mwenza wako kuhusu ngono/kufanya mapenzi?

Karibu kwenye nakala hii ambayo tunaangazia imani ya watu katika kujifunza kutoka kwa mwenza wako... Read More

Je, umri unaathiri ngono/kufanya mapenzi katika uhusiano?

Je, umri unaathiri ngono/kufanya mapenzi katika uhusiano?

Je, umri unaathiri ngono/kufanya mapenzi katika uhusiano?

Hakuna jibu moja sahihi kwa swal... Read More

Je, kuna umuhimu wa kujadili mipaka ya faragha katika uhusiano wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna umuhimu wa kujadili mipaka ya faragha katika uhusiano wa ngono/kufanya mapenzi?

Leo tutaongelea kuhusu umuhimu wa kujadili mipaka ya faragha katika uhusiano wa ngono au kufanya ... Read More

Jinsi ya Kusaidia Watoto kujenga Ujuzi wa Kujitunza na Kuwa na Heshima

Jinsi ya Kusaidia Watoto kujenga Ujuzi wa Kujitunza na Kuwa na Heshima

Karibu kwenye makala hii! Leo, tutajadili jinsi ya kusaidia watoto kujenga ujuzi wa kujitunza na ... Read More

Jinsi ya Kujenga Ushirikiano wenye Ubunifu katika Mahusiano yako

Jinsi ya Kujenga Ushirikiano wenye Ubunifu katika Mahusiano yako

Mahusiano ni muhimu sana katika maisha yetu ya kila siku. Hata hivyo, mahusiano hayawezi kuwa ya ... Read More

Jinsi ya Kuunga Mkono Watoto katika Kufuata Ndoto zao: Kuwa Mlezi wa Kuhamasisha

Jinsi ya Kuunga Mkono Watoto katika Kufuata Ndoto zao: Kuwa Mlezi wa Kuhamasisha

Kama mzazi au mlezi, unaweza kuunga mkono watoto wako ili wafuate ndoto zao kwa kuwa mlezi wa kuh... Read More

Jinsi ya Kuwezesha Ushirikiano wa Kifedha katika Familia: Kukuza Ustawi na Utulivu

Jinsi ya Kuwezesha Ushirikiano wa Kifedha katika Familia: Kukuza Ustawi na Utulivu

Kuwezesha ushirikiano wa kifedha katika familia ni jambo muhimu sana katika kukuza ustawi na utul... Read More

Jinsi ya Kukuza Uhusiano wa Marafiki katika Familia: Kuwa Rafiki wa Kweli

Jinsi ya Kukuza Uhusiano wa Marafiki katika Familia: Kuwa Rafiki wa Kweli

Uhusiano wa marafiki katika familia ni muhimu sana kwani unaleta amani na furaha kwenye familia. ... Read More