Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Jinsi ya kumfanya mwanamke afurahi na akupende kwa kumfanyia mambo anayoyataka

Featured Image

Kuna mambo ya msingi ambayo mwanamke anahitaji kutoka kwa mwanamme ili kufurahi na kutulia katika mahusiano japokuwa sio rahisi kukwambia mojakwa moja.

Mambo hayo ni kama ifuatavyo;

Kupewa nafasi na kipaumbele.

Wanawake wanapenda kuwa namba moja au kupendwa kuliko yeyote. Kumpenda mwanamke haikuishii kwenye kumpata na kumliki, kisha kujisahau kwa kisingizio kuwa umemuoa au umemvisha pete ya uchumba, ni zaidi ya hapo. Wanawake wanapenda watangulizwe katika mapenzi na kusiwepo na mwingine wa kuchukua nafasi yao katika mazungumzo na mapenzi kwa ujumla na katika maisha yao.

Kuheshimiwa

Wanawake wanapenda kueshimiwa kwa maneno na matendo. Wanawake hawapendi kuitwa majina mabaya kwa mfano mjinga, Malaya au kulinganishwa na wanawake wenzao wabaya. Wanawake hawapendi kukosewa heshima hasa mbele za watu, hata kama ni kwa mambo madogo madogo.

Kuridhishwa Kwenye tendo la ndoa

Mwanamke anapenda aridhishwe Kwenye tendo la ndoa. Hata kama utakuwa na kiwango kikubwa cha mapenzi juu ya mpenzi wako kwa kiwango gani, ukiwa dhaifu katika tendo la ndoa utayumbisha penzi lako. Utundu na ufundi unahitajika ili kumkata kiu mpenzi wako. Mwanamme anatakiwa kuhakikisha kuwa anamtosheleza mpenzi wake katika tendo hilo.

Nafasi ya kuongea na kujieleza

Wanawake wanapenda wapewe nafasi ya kuongea na kujieleza vile watakavyo. Mpe uhuru mpenzi wako kuzungumza na kumsikiliza bila kumkatiza kwa ukali pale anapoongea sana. Kwa kawaida wanawake wanatajwa kuzungumza maneno 25,000 kwa siku, wakati wanaume wakibaki na kiwango cha maneno 5,000 kwa siku, wanawake hupenda zaidi kujieleza walivyo mbele ya wengine. Kwa hiyo wakizuiwa wasiongee hujiona kama wanakosa nafasi muhimu ya kueleza mawazo yao.

Kusaidiwa katika shida na matatizo yao

Wanawake wengi hutegemea kuwa wanapokuwa na wapenzi watasaidiwa katika matatizo ya kimaisha na migogoro ya kimawazo. Kwa mfano ushauri juu ya maisha yao, kulindwa na hatari za kimaisha, kusaidiwa katika shida na kuongozwa pale wanapohisi kushindwa kufanya jambo. Kama mwanaume hatamfanyia mpenzi wake hili atakuwa amekosa sifa za kuteka penzi la mwanamke.

Kubembelezwa

Wanawake hupenda kubembelezwa hasa pale wanapokuwa na huzuni. Wanawake wengi hupenda kuelimishwa zaidi kuliko kufokewa. Wanawake hawapendi kukaripiwa, mara nyingi hupenda kuungwa mkono wanapokuwa na misuguano na wengine. Ili mwanaume amteke kimapenzi mwanamke lazima awe nyuma yake hata kama atakuwa na kosa.

Mfahamu zaidi Mwanamke kwa Kupitia Kitabu hiki kizuri cha SIRI ZA MWANAMKE

[products columns="2" ids="30827"]

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsi Mwanamme Unavyoweza kubobea katika Mapenzi na Mahusiano

Jinsi Mwanamme Unavyoweza kubobea katika Mapenzi na Mahusiano

Read More
Jinsi ya Kuunga Mkono Kazi na Mafanikio ya Mke wako

Jinsi ya Kuunga Mkono Kazi na Mafanikio ya Mke wako

Kuunga mkono kazi na mafanikio ya mke wako ni muhimu sana katika kujenga uhusiano imara na kuimarish... Read More
Kukabiliana na Matarajio ya Jamii katika Kufanya Mapenzi: Kujitambua na Kujieleza

Kukabiliana na Matarajio ya Jamii katika Kufanya Mapenzi: Kujitambua na Kujieleza

Mapenzi ni jambo muhimu katika maisha yetu na yanahusisha mambo mengi sana, ikiwemo kukabiliana n... Read More

Njia za Kuboresha Stamina ya Kufanya Mapenzi: Mazoezi na Vyakula

Njia za Kuboresha Stamina ya Kufanya Mapenzi: Mazoezi na Vyakula

  1. Njia ya kwanza ya kuboresha stamina ya kufanya mapenzi ni kufanya mazoezi ya mwili. Maz... Read More

Kuweka Kipaumbele cha Kuendeleza Ushirikiano wa Kujenga katika Mahusiano

Kuweka Kipaumbele cha Kuendeleza Ushirikiano wa Kujenga katika Mahusiano

Kuweka Kipaumbele cha Kuendeleza Ushirikiano wa Kujenga katika Mahusiano

Kuwa na mahusiano... Read More

Kuweka Kipaumbele cha Uhusiano wa Karibu na Kuweka Nafasi ya Wakati wa Familia

Kuweka Kipaumbele cha Uhusiano wa Karibu na Kuweka Nafasi ya Wakati wa Familia

Kuweka Kipaumbele cha Uhusiano wa Karibu na Kuweka Nafasi ya Wakati wa Familia

Kuweka kipa... Read More

Jinsi ya Kudumisha Umoja na Kuishi kwa Amani katika Familia

Jinsi ya Kudumisha Umoja na Kuishi kwa Amani katika Familia

Jinsi ya Kudumisha Umoja na Kuishi kwa Amani katika Familia

Kuishi katika familia yenye um... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya haki za binadamu na usawa

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya haki za binadamu na usawa

Kuwa na mazungumzo ya dhati na mpenzi wako kuhusu masuala ya haki za binadamu na usawa ni muhimu ... Read More

Jinsi ya Kuwa na Sala na Ibada ya Pamoja na mke wako

Jinsi ya Kuwa na Sala na Ibada ya Pamoja na mke wako

Kuwa na sala na ibada ya pamoja na mke wako ni njia nzuri ya kuimarisha uhusiano wenu wa kiroho na k... Read More
Kuishi na Tofauti za Kijinsia katika Uhusiano: Kuelewa na Kuheshimu

Kuishi na Tofauti za Kijinsia katika Uhusiano: Kuelewa na Kuheshimu

Kuishi na Tofauti za Kijinsia katika Uhusiano: Kuelewa na Kuheshimu

  1. Kuelewa Tofa... Read More

Je, kuna tofauti ya kiumri katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna tofauti ya kiumri katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna tofauti ya kiumri katika ngono/kufanya mapenzi? Ndio! Kuna tofauti kubwa sana kati ya wa... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu malengo ya elimu na ukuaji binafsi

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu malengo ya elimu na ukuaji binafsi

Kuwa na mpenzi ambaye anaelewa umuhimu wa elimu na ukuaji binafsi ni zawadi kubwa sana. Kwa sabab... Read More