Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Kwa nini vijana wanakatazwa kujamiiana?

Featured Image

Ujana ni kipindi cha mabadiliko kutoka utotoni kuelekea utu uzima, wakati wa kipindi hiki kijana hupata mabadiliko ya kimwili, kiakili na kimtazamo. Mwili na akili hupevuka. Ni kipindi muhimu cha kuweka msingi wa maisha ya baadaye. Vijana wanakatazwa kujamiiana kwa sababu matatizo mengi yanaweza kutokea kutokana na tendo hilo.

Kwanza kabisa kwa kujihusisha na kitendo cha kujamiiana vijana wanapoteza nguvu na muda ambao wangeweza kutumia kwa shughuli za maendeleo. Kwa mfano, kusoma, kufanya kazi, kushiriki katika shughuli za vikundi katika jamii au kucheza michezo.
Pili, matatizo ya mimba katika umri mdogo ni mengi. Mojawapo ni msichana kufukuzwa shule, au hata jamii kumtenga. Matatizo mengine ni ya kiafya kutokana na mwili wa msichana bado kuwa haujakomaa vyema.
Tatu, vijana wanakuwa bado hawajajiandaa kwa uzazi au kujitegemea. Sababu nyingine ya kuwakataza vijana kujamiiana ni ile ya hatari ya kuambukizana magonjwa ya zinaa ikiwa ni pamoja na Virusi vya UKIMWI. Magonjwa haya ni mabaya sana yanaweza kusababisha maumivu makali, ugumba au hata kifo.
Unapofikiria sababu zote hizo utaona kwamba kujamiiana katika umri mdogo kunaweza kuleta madhara mengi kwa afya yako na malengo yako maishani. Hivyo basi unapokatazwa kujamiiana ni kwa sababu ya matatizo haya. Hata hivyo, kama kwa vyovyote huwezi kuacha kujamiiana, hakikisha kwamba unajikinga wewe na mpenzi wako kwa kutumia kondomu.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Mwanamume au mvulana anaweza kubakwa?

Mwanamume au mvulana anaweza kubakwa?

Ndiyo, mtu yoyote anayelazimishwa
kujamiina atakuwa
amebakwa, haijalishi kama
mtu ... Read More

Je, kama wazazi watawapa dawa za kulevya watoto wao watashitakiwa kisheria?

Je, kama wazazi watawapa dawa za kulevya watoto wao watashitakiwa kisheria?

Ndiyo, watashtakiwa! Wakati mwingine wazazi huwatuma
watoto wao kuchukua au kununua pombe au... Read More

Watu wanaamini kuwa Albino wana joto katika mapenzi kuliko watu weusi, Je, hiyo ni kweli?

Watu wanaamini kuwa Albino wana joto katika mapenzi kuliko watu weusi, Je, hiyo ni kweli?

Hii siyo kweli,
tofauti
baina ya Albino
na mtu a s i
ekuwa na ualbino
i ... Read More

Bikira na ubikira

Bikira na ubikira

Ubikira ni nini?:Β Maana halisi ya neno β€œbikira” ni mwanamke au mwanaume amb... Read More

Njia za Kujenga Hisia za Usalama katika Uhusiano wako na Msichana

Njia za Kujenga Hisia za Usalama katika Uhusiano wako na Msichana

Njia za Kujenga Hisia za Usalama katika Uhusiano wako na Msichana

Hakuna kitu kizuri kama ... Read More

Je, ngono/kufanya mapenzi ni sehemu muhimu ya uhusiano wa kimapenzi?

Je, ngono/kufanya mapenzi ni sehemu muhimu ya uhusiano wa kimapenzi?

Je, ngono/kufanya mapenzi ni sehemu muhimu ya uhusiano wa kimapenzi?

Kwa wengi, kufanya ma... Read More

Jinsi ya Kukabiliana na Hisia za Kufadhaika na Utendaji wa Ngono

Jinsi ya Kukabiliana na Hisia za Kufadhaika na Utendaji wa Ngono

Jinsi ya Kukabiliana na Hisia za Kufadhaika na Utendaji wa Ngono πŸ’†πŸŒ‘οΈ

Karibu kijana... Read More

Kwa nini mara nyingine mimba inatungwa kwenye mrija wa kupitisha mayai badala ya kwenye tumbo la uzazi?

Kwa nini mara nyingine mimba inatungwa kwenye mrija wa kupitisha mayai badala ya kwenye tumbo la uzazi?

Mara nyingi utunguaji mimba nje ya mfuko wa uzazi hutokea kwa sababu ya maradhi kwenye via vya uz... Read More

Mambo usiyoyajua kuhusu mimba na wasichana

Mambo usiyoyajua kuhusu mimba na wasichana

Je, mimba hupatikanaje?

Ukitaka kuelewa jinsi mimba i inavyopatikana, lazima uelewe mzung... Read More

Je, kuna madhara kama mtu akikaa muda mrefu bila kufanya mapenzi?

Je, kuna madhara kama mtu akikaa muda mrefu bila kufanya mapenzi?

Ukweli ni kwamba hakuna madhara yoyote ya kiafya ukikaa muda mrefu bila kujamii ana. Hakuna madha... Read More

Umri unaofaa kuoa

Umri unaofaa kuoa

Kuoana maana yake ni kuwajibika kwa maisha yako na mke au mume wako. Mara nyingi kuoana kunaambatana... Read More
Inakuwaje, baadhi ya Albino wana macho yanayochezacheza?

Inakuwaje, baadhi ya Albino wana macho yanayochezacheza?

Wapo baadhi ya Albino wenye macho ya kuchezacheza na
ambayo hayawezi kulenga pamoja. Hii ina... Read More