Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Matatizo yanayotokana na ujauzito katika umri mdogo

Featured Image

Wataalamu wanashauri kwamba msichana anastahili kuanza kubeba mimba kuanzia umri wa miaka 18 hadi 20. Kabla ya umri huu, mwili wa msichana bado haujakomaa vizuri. Viungo vya uzazi bado ni vidogo na ngozi ni laini. Vilevile mfupa wa nyonga bado mwembamba kiasi cha kumwezesha mtoto kupitia wakati wa kuzaliwa.
Wasichana chini ya miaka 18 wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata matatizo, hasa wakati wa kujifungua. Matatizo hayo ni pamoja na mapigo ya moyo kuwa juu, kuumwa uchungu kwa muda mrefu, kukwama kwa mtoto, kujifungua kwa njia ya operesheni, kujifungua kabla ya wakati na watoto kuzaliwa na uzito mdogo. Mwili huwa na mahitaji makubwa wakati wa ujauzito na kujifungua na mwili wa wasichana wenye umri chini ya miaka 18 huwa haujakomaa vya kutosha kwa kazi ya kubeba mimba.
Mbali ya shida za kiafya, kuna matatizo mengine yatokanayo na kupata mimba mapema. Mara nyingi msichana na mwenzie wanakuwa bado wanasoma shule, msichana hufukuzwa shule na hata hutengwa katika jamii . Vijana mara nyingi hawana mapato ya kumlea na kumtunza mtoto, na mahali pa kuishi huwa hawana. Vilevile mvulana mara nyingi hayuko tayari kuchukua jukumu la kuwa baba. Kwa sababu hizi zote, ni vizuri zaidi mimba zitungwe baada ya msichana kufikia umri wa miaka 18.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Vidonge vya kuzuia mimba vinasababisha vidonda vya tumbo?

Vidonge vya kuzuia mimba vinasababisha vidonda vya tumbo?

Wanawake wengine wanapata vidonda vya tumbo, lakini haya hayana uhusiano na vidonge vya kuzuia mi... Read More

Je, ni muhimu kuelewa na kuheshimu hisia za mwenza wako wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, ni muhimu kuelewa na kuheshimu hisia za mwenza wako wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

  1. Kujenga uhusiano wa kimapenzi wenye afya na mwenza wako ni muhimu sana. Hii ni kwa saba... Read More

Je, kuna umuhimu wa kujadili maoni na mitazamo yako kuhusu ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna umuhimu wa kujadili maoni na mitazamo yako kuhusu ngono/kufanya mapenzi?

Habari zenu wapenzi wa Mapenzi! Kuna umuhimu mkubwa sana wa kujadili maoni na mitazamo yako kuhus... Read More

Je, watu wanapendelea kujaribu mbinu za kuleta msisimko wa kihisia wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, watu wanapendelea kujaribu mbinu za kuleta msisimko wa kihisia wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Leo, tutazungumzia kuhusu mbinu za kuleta msisimko wa kihisia wakati wa ngono/kufanya mapenzi. Ni... Read More

Madhara ya pombe kwa mwili na akili

Madhara ya pombe kwa mwili na akili

Pombe huingia kwenye damu na kuzunguka mwili mzima pamoja
na kwenye ubongo wako. Ina madhara... Read More

Ubikira ni nini?

Ubikira ni nini?

Maana halisi ya neno β€œbikira” ni mwanamke au mwanaume ambaye hajawahi kabisa kujamii ana. Kuj... Read More

Utumiaji nguvu katika mahusiano ya ujinsia kama sehemu ya utamaduni

Utumiaji nguvu katika mahusiano ya ujinsia kama sehemu ya utamaduni

Utumiaji wa nguvu
katika mahusiano ya
ujinsia unavunja haki
za uzazi na haki zaRead More

Je, kuna mambo ya haramu katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna mambo ya haramu katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna mambo ya haramu katika ngono/kufanya mapenzi? Hili ni swali ambalo linaweza kuwa na maji... Read More

Je, kuna madhara msichana akifanya mapenzi wakati akiwa katika hedhi (siku zake)?

Je, kuna madhara msichana akifanya mapenzi wakati akiwa katika hedhi (siku zake)?

Kufanya mapenzi wakati msichana yuko katika hedhi hakuna madhara yoyote kiafya kwa mwanaume wala ... Read More

Je, watu wanaamini nini katika kuongeza mchezo wa hisia wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, watu wanaamini nini katika kuongeza mchezo wa hisia wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, watu wanaamini nini katika kuongeza mchezo wa hisia wakati wa ngono/kufanya mapenzi? Kufanya ... Read More

Je, watu wanaamini katika kutumia dawa za kuongeza hamu ya ngono/kufanya mapenzi?

Je, watu wanaamini katika kutumia dawa za kuongeza hamu ya ngono/kufanya mapenzi?

Je, watu wanaamini katika kutumia dawa za kuongeza hamu ya ngono/kufanya mapenzi? Hili ni swali a... Read More

Je, Ni Lazima Kutumia Kinga (Condom) Kila Wakati?

Je, Ni Lazima Kutumia Kinga (Condom) Kila Wakati?

Je, ni lazima kutumia kinga (condom) kila wakati? 🌍

Leo nataka kuzungumzia jambo muhimu... Read More