Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMS๐Ÿ’Œ๐Ÿ’•
โ˜ฐ
AckyShine

Kuna aina ngapi za dawa za kulevya?

Featured Image

Tunatofautisha dawa za kulevya katika makundi mawili. Zile zinazokubalika na zile zisizokubalika kisheria. Tanzania, dawa za kulevya zinazokubalika kisheria ni pamoja na tumbaku na pombe, pia dawa zilizothibitishwa kwa maandishi na daktari. Dawa zinazotolewa kwa udhibitisho wa madaktari ni zile dawa za kutibu. Pale zinapotolewa kwa sababu nyingine mbali na matibabu au maelezo ya daktari zinakuwa dawa za kulevya. Miongoni mwa dawa zinazotumika vibaya hapa Tanzania ni valium, asprin na panado. Vimiminika kama petroli pia hutumiwa kama dawa za kulevya. Vitu hivi hutumiwa kwa njia ya kuvuta hewa yake kwa pua au mdomo.
Pia kuna vileo visivyoruhusiwa ambavyo hutengenezwa kienyeji kama vile gongo. Dawa za kulevya ambazo hutumika sana Tanzania ni pamoja na bangi, mirungi, mandrax, heroini na kokaini. Kokaini ambayo hupatikana katika hali ya ungaunga ulio mweupe, hutumiwa kwa njia ya kuvuta kwa pua au kuchanganywa na maji na baadaye kujidunga mwilini kwa kutumia sindano. Heroini pia hupatikana kama unga mweupe. Unaweza kuvuta heroini kama sigara au kuvuta hewa yake kwa ndani na pia kwa kujidunga sindano. Katika hali i i isiyo ya kawaida heroini vilevile inaweza kupatikana katika vipande vidogovidogo vya kahawia vijulikanavyo kama โ€œsukari ya kahawiaโ€.
Njia nyingine ya kuzungumzia dawa za kulevya ni kutokana na madhara yake. Yapo madawa ambayo hupagawisha au yanayozubaisha au kupoozesha kama vile kileo, nikotini, dawa za usingizi, kwa mfano valium na heroini. Dawa hizo zinamfanya mtumiaji kujisikia shwari, lakini pia huhuzunisha. Dawa zinazochamngamsha ni i kama mirungi, kokaini na zile za kuvuta, kwa mfano petroli, zina madhara ya kukufanya uhamasike na kujisikia kuwa na nguvu. Dawa zinazopagawisha zinaleta hisia, sauti, taswira, harufu kwa mtu japokuwa vyote hivyo havipo kweli. Bangi ni mojawapo ya dawa hizi.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Je, kuna madhara kama mtu akikaa muda mrefu bila kufanya mapenzi?

Je, kuna madhara kama mtu akikaa muda mrefu bila kufanya mapenzi?

Ukweli ni kwamba hakuna madhara yoyote ya kiafya ukikaa muda mrefu bila kujamii ana. Hakuna madha... Read More

Je, ni tabia zipi zinazochangia kuenea kwa virusi vya UKIMWI?

Je, ni tabia zipi zinazochangia kuenea kwa virusi vya UKIMWI?

Virusi vya UKIMWI kwa kiasi kikubwa vinaenea kwa njia ya kujamii ana. Kama mtu ana wapenzi wengi ... Read More

Ualbino husababishwa na nini?

Ualbino husababishwa na nini?

Watu wenye ualbino hawana uwezo kabisa au wana uwezo mdogo wa kuwa na rangi kwenye ngozi zao, nywele... Read More
Utoaji wa zawadi kwa kubadilishana na kujamiiana

Utoaji wa zawadi kwa kubadilishana na kujamiiana

Kutoa zawadi kwa mtu kwa kubadilishana ili kujamiiana
ni unyanyasaji mbaya. Iwapo mpokeaji w... Read More

Ualbino unarithiwa vipi?

Ualbino unarithiwa vipi?

Watoto wengi wanaozaliwa na ualbino, wazazi wao wana rangi
ya ngozi, nywele na macho inayafa... Read More

Je, watu wanaoishi na ualbino wanafanana wote?

Je, watu wanaoishi na ualbino wanafanana wote?

Hapana. Albino wote hawafanani, wanatofautiana kufuatana na
kiasi cha melanini walicho nacho... Read More

Jinsi ya Kuzungumza na Mwenzi Wako kuhusu Matumizi ya Vidonge vya Kuzuia Mimba

Jinsi ya Kuzungumza na Mwenzi Wako kuhusu Matumizi ya Vidonge vya Kuzuia Mimba

Jinsi ya Kuzungumza na Mwenzi Wako kuhusu Matumizi ya Vidonge vya Kuzuia Mimba ๐Ÿ˜Š

Karibu... Read More

Je, watu wanapendelea kutumia vitu kama vile nguo za ndani za kimapenzi wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, watu wanapendelea kutumia vitu kama vile nguo za ndani za kimapenzi wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Karibu tena kwenye blogu yetu ya mapenzi. Leo tutaangazia swali linaloulizwa mara kwa mara kuhusu... Read More

Nini maana ya Ualbino?

Nini maana ya Ualbino?

Albino wana ngozi nyeupe, nywele nyeupe au nyekundu na macho
ya kijivu au ya bluu. Ngozi yao... Read More

Nani anavalisha kondomu ya kiume, je ni mwanamke au mwanaume?

Nani anavalisha kondomu ya kiume, je ni mwanamke au mwanaume?

Katika kufanya mapenzi iwe mwanaume anayeweka kondomu uumeni au iwe mwanamke anayeshugulika kuwek... Read More

Ubakaji ni nini?

Ubakaji ni nini?

Ubakaji ni tendo la kutumia nguvu katika ngono ambapo mbakaji anatumia nguvu kuonyesha ubabe wake... Read More

Je, watumiaji wa dawa za kulevya wanaweza kupata watoto?

Je, watumiaji wa dawa za kulevya wanaweza kupata watoto?

Ndiyo, hii i ii inawezekana. Lakini ujue kwamba watu wanaotumia dawa za kulevya huwa dhaifu kisai... Read More