Sidebar with Floating Button
AckySHINE SMSπŸ’ŒπŸ’•
☰
AckyShine

Madhara yanayotokea kwa unyanyasaji wa jinsia kwa mtu

Featured Image

Unyanyasaji wa ujinsia una matatizo mabaya ya kimwili na
yanayochukua muda mrefu kwa mwathiriwa kupona. Unyanyasaji
wa jinsia mara nyingi humuumiza mwathiriwa, matendo ya
ubakaji, majaribio ya ubakaji, unyanyasaji wa kijinsia kwa mtoto,
na ukeketaji kwa wanawake yanamhusu moja kwa moja mwili
wa mwathiriwa. Mwathiriwa anaweza kupata maumivu makali
wakati wa kitendo, viungo vyake vya uzazi akiwa mwanamume
au mwanamke kuna uwezekano ukapata majeraha wakati wa
ubakaji. Zaidi ya hayo mbakaji anaweza kumuumiza mwathiriwa
katika sehemu nyingie za mwili. Na jambo baya zaidi ukatili
wa kijinsia wakati mwingine unaweza kusababisha ulemavu wa
maisha na mara nyingine hata kifo cha mwathiriwa. Ubakaji
unaweza kusababisha mimba, na uenezaji wa magonjwa hatari
kama Virusi vya Ukimwi.
Watoto wanadhuriwa zaidi na vitendo vya ukatili wa ujinsia
katika miili yao kwa sababu ukubwa wa viungo vyao vya sehemu
za siri ni vidogo kuliko vile vya watu wazima.
Athari za kisaikolojia kwa mwathiriwa pia ni hatari sana. Uonevu
wa ujinsia kwa mwathirika unaweza kusababisha kuchanganyikiwa
na kupata kiwewe na hali ya hatari sana inayoweza kusababisha
mtu akapata kichaa katika miezi ya kwanza. Baada ya uonevu
wa ujinsia na hata baada ya miaka, mwathiriwa bado atakuwa
na kumbukumbu ya maumivu aliyopata na hivyo kukumbuka
katika akili yake. Waathiriwa wengi wa ubakaji wana matatizo
ya kutokuwa na uhusiano mzuri wa kujamiiana, kwani kila mara
atahusisha kujamiiana na alipobakwa. Ndiyo maana waathiriwa
wa ubakaji wanahitaji msaada, uelewa na uvumilivu toka kwa
wazazi wao, wenzi wao na marafiki.

AckySHINE Solutions

Comments

Please Join AckySHINE to Participate in Discussion.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Je, kuna dawa yoyote ya kutibu ugumba?

Je, kuna dawa yoyote ya kutibu ugumba?

Hakuna jibu la ujumla kwa swali hili, kwa sababu tiba ya ugumba inategemea chanzo maalum cha ugum... Read More

Je, zipo sheria zinazolinda watu wenye ulemavu hapa Tanzania?

Je, zipo sheria zinazolinda watu wenye ulemavu hapa Tanzania?

Ndiyo, zipo sheria
hapa T a n z a n i a
z i n a z o w a l ... Read More

Jinsi ya kujikinga na ubakaji

Jinsi ya kujikinga na ubakaji

Hata kama utafanya kila kitu usibakwe bado inaweza ikatokea. Ubakaji na unyanyasaji wa ujinsia unawe... Read More
Je, kuna tofauti za kimwili katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna tofauti za kimwili katika ngono/kufanya mapenzi?

Mapenzi ni sehemu muhimu katika maisha ya binadamu na inaweza kuwa njia ya kujifunza, kufurahia, ... Read More

Je, magonjwa ya zinaa yanaweza kuenea ukitoa uume kabla ya kumwaga mbegu?

Je, magonjwa ya zinaa yanaweza kuenea ukitoa uume kabla ya kumwaga mbegu?

Ndiyo, magonjwa ya zinaa yanaweza kuenea, hata ukitoa uume kabla ya kumwaga mbegu. Mwenye magonjw... Read More

Je, mbegu za kiume zinaweza kupita kwenye kondomu?

Je, mbegu za kiume zinaweza kupita kwenye kondomu?

Hapana, mbegu za kiume haziwezi kupita kwenye kondomu. Kondomu zimetengenezwa ili kuzuia mbegu za... Read More

Je, ni muhimu kujadili haki na usawa wa kijinsia katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, ni muhimu kujadili haki na usawa wa kijinsia katika ngono/kufanya mapenzi?

Kujadili haki na usawa wa kijinsia katika ngono/kufanya mapenzi ni muhimu sana katika jamii yetu.... Read More

Je, ni madhara gani atapata mama mjamzito endapo atajamiiana na mwenzi wake?

Je, ni madhara gani atapata mama mjamzito endapo atajamiiana na mwenzi wake?

Kama kati ya mwanamke na mwanaume hakuna mwenye magonjwa ya zinaa, hakuna madhara yoyote kwa mwan... Read More

Je, watu wanapendelea kujaribu kufanya mapenzi?

Je, watu wanapendelea kujaribu kufanya mapenzi?

Habari za leo wapendwa wasomaji! Leo, tunajadili kuhusu je, watu wanapendelea kujaribu kufanya ma... Read More

Je, inafaa kuzungumzia kuhusu historia ya ngono/kufanya mapenzi ya kila mmoja katika uhusiano?

Je, inafaa kuzungumzia kuhusu historia ya ngono/kufanya mapenzi ya kila mmoja katika uhusiano?

Je, kuna haja ya kuzungumzia historia ya ngono/kufanya mapenzi ya kila mmoja katika uhusiano? Jib... Read More

Ukeketaji ni nini?

Ukeketaji ni nini?

Katika baadhi za jamii viungo vya uzazi vya nje vya msichana,
yaani kisimi au sehemu ya ndan... Read More

Je, unaweza kufa ukitumia dawa za kulevya?

Je, unaweza kufa ukitumia dawa za kulevya?

Ndiyo, unaweza. Kifo kinaweza kuwa cha ghafla au
kutokana na madhara ya muda mrefu katika vi... Read More