Huyu bwana leo kapatikana, Jamani nyodo nyingine mbaya
Baada ya kumaliza Degree yake ya sheria Bwana Rwegashora aliamua kurudi nyumbani Bukoba mjini na kufungua ofisi yake kwa ajili ya huduma kwa wateja.
Siku moja akiwa ndani ya ofisi yake alimuona mtanashati na mdada mmoja mrembo anakuja ofisini kwake akajua ni mteja anamletea kesi.
Ndipo akanyanyua mkoni wa wa simu ya TTCL na kuanza kuongea huku anajizunguusha kwenye kiti cha kuzunguuka.
Updated at: 2023-04-29 22:52:17 (3 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
Baada ya kumaliza Degree yake ya sheria Bwana Rwegashora aliamua kurudi nyumbani Bukoba mjini na kufungua ofisi yake kwa ajili ya huduma kwa wateja. Siku moja akiwa ndani ya ofisi yake alimuona mtanashati na mdada mmoja mrembo anakuja ofisini kwake akajua ni mteja anamletea kesi.
Ndipo akanyanyua mkoni wa wa simu ya TTCL na kuanza kuongea huku anajizunguusha kwenye kiti cha kuzunguuka. Wakati mdada alipokaribia Rwegashora alimkaribisha kwa ishara maana alijifanya yupo busy na kuongea na simu ya umuhimu. Wakati anaongea na simu akisikika akisema No, No, Noโฆ.. Absolutely No. Wajuulishe hao lay person wa New York kua siwezi kushuhulika na kesi ambayo itanilipa chini ya 50 million. Mimi ni profesional lawyer and im crossing the border to sarve international community.
Aka pose kidogo na akanywa maji kisha akaendeleaโฆ.. Naweza kuanza kukusanya primary evidence next weak but tell them watume kwanza ten million kwa kuanzaโฆ Hahahahaha you dont know my Account Mr Roger. Ok waambie watume kwenye Account ileile walionitumia million 100 last monthโฆ
Aka pose tena akameza fundo la maji na kurekebisha tai yake kisha akaendeleaโฆ Ok usisahau kumueleza muendesha mashtaka mkuu wa marekani kua nitakuja New York mwezi ujao maana nitapita kwanza Amsterdam kuwasilisha utetezi wa yule mteja wangu mholanzi kisha nitaenda Tokyo kulipia ile gari yangu niloagiza.
Wakati anaongea hayo yote yule mdada alikua ametulia na anamuangalia Bwana Rwegashora anavyojizunguusha kwenye kiti chake huku akiongea kwa tambo kwenye ile simu ya TTCL. Baada ya kumaliza kuongea na simu Bwana Rwegashora aliweka mkono wa simu yake ya TTCL chini kisha akamgeukia mdada mrembo.
Samahan sana kwa kukupotezea muda wako unajua tena kazi zetu zinaumiza kichwa sana kama unavyoona mwenyewe yaani niko busy sana ninapokea simu sana mpaka nimechoka na simu nyingi ni za wateja wa njee ya nchi.
Anyway nikusaidie nn? Mdada akajibu mimi ni mfanyakazi wa kampuni ya TTCL nimekuja kuunganisha line yako ya simu kwani haipo hewani tangu wiki iliyopitaโฆ!!!
Updated at: 2024-05-25 16:54:13 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kuoa vijijini raha sana Hata ukiulizwa unafanya kazi gani ukiwaambia mimi ni admin basi daaaah wanaona wewe ni bonge la boss๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Updated at: 2024-05-25 16:55:49 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ukioa mke asiyesoma hata hili unaweza kufanya
KUOA MKE AMBAE HAJASOMA RAHA SANA LEO NIMEMUAMBIA MWEZI HUU HATUTOLIPWA MSHAHARA KWAKUA HAUNA TR 30 KAENDA KUNGALIA KARENDA KARUDI ANANIAMBIA HAMNA SHIDA MME WANGU TUTAVUMILIA TU
Nilichomfanyia huyu aliyenizingua nilipomuazimisha pasi
Updated at: 2024-05-25 17:03:53 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
๐๐๐๐๐๐ Jana nimeenda kuazima pasi chumba jirani, ili ninyooshe nguo zangu, Jamaa wakaniambia nichukue nguo nikanyooshe room kwao maana hawataki pasi yao itoke. Sasa leo amekuja mmoja wao kuazima mopper akasafishe room, nimemwambia aje adekie humu humuโฆ
Jamaa ameondoka nadhani atakua ameenda kuchukua maji ๐ค๐ค๐ค
Mzee kaingia pharmacy,
MZEE: Mambo mwanangu, kuna kitu naomba uonje nitakulipa
MFAMASIA: Kitu gani?โฆ.Mzee akatoa kichupa na kijiko akaweka โฆmajimaji yaliyomo kwenye
kichupa kwenye kijiko na kumwambia mfamasia aonje, mfamasia akatia yale maji mdomoni na kuyazungusha zungusha mdomoni akionja;
Updated at: 2024-05-25 18:05:01 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mzee kaingia pharmacy,
MZEE: Mambo mwanangu, kuna kitu naomba uonje nitakulipa
MFAMASIA: Kitu gani?โฆ.Mzee akatoa kichupa na kijiko akaweka โฆmajimaji yaliyomo kwenye
kichupa kwenye kijiko na kumwambia mfamasia aonje, mfamasia akatia yale maji mdomoni na kuyazungusha zungusha mdomoni akionja;
MZEE: Nipe jibu, ina utamu wa sukari au chumvi au pilipili?
MFAMASIA: Kama chumvichumvi
MZEE: Hakuna sukari
MFAMASIA: Sukari hakuna kabisa
MZEE: Loh asante chukua hii alfu tano nashukuru sana, dokta alinambia nipime mkojo wangu kama nina kisukari, kumbe sina asante bwana mdogo
Watoto wa siku hizi ni shida! Angalia huyu mtoto anachomwambia baba yake
Ka ni wewe?
DOGO: baba mi siendi tena shule inaonekana walimu hawana uhakika na majibu yao.
BABA: Kwanini unasema hivyo?
Updated at: 2023-04-29 22:53:48 (3 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
Ka ni wewe?
DOGO: baba mi siendi tena shule inaonekana walimu hawana uhakika na majibu yao.
BABA: Kwanini unasema hivyo?
DOGO: juzi walisema 3+4= 7, jana wakasema 1+6=7, halafu leo wanasema 5+2=7 sasa huoni kama wanatuchanganya.
ungekua wewe ungemjibu nini
Alichojibu dalali baada ya kufumwa na mke wa mtu ndani ya nyumba ya kupanga
Dalali aliwatafutia jamaa chumba Buguruni karibu na reli, nyumba nzuri sana. Jamaa na mkewe wakahamia kwa furaha, lakini furaha yao iliisha walipokuja gudundua nyumba ile iko karibu mno na reli treni ikipita mpaka kitanda kinacheza.
Siku hiyo dalali akapita mke akamwita na kumwambia tatizo wakati treni inapita, wakaanza kubishana, yule mama akamwambia dalali kwa kuwa kuna treni itapita sasa hiviโฆ njoo ndani uone mwenyewe.
Updated at: 2024-05-25 18:05:28 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Dalali aliwatafutia jamaa chumba Buguruni karibu na reli, nyumba nzuri sana. Jamaa na mkewe wakahamia kwa furaha, lakini furaha yao iliisha walipokuja gudundua nyumba ile iko karibu mno na reli treni ikipita mpaka kitanda kinacheza.
Siku hiyo dalali akapita mke akamwita na kumwambia tatizo wakati treni inapita, wakaanza kubishana, yule mama akamwambia dalali kwa kuwa kuna treni itapita sasa hiviโฆ njoo ndani uone mwenyewe.
Bahati mbaya wakiwa wamejilaza kitandani ili dalali aone adhabu wanayopata, Mzee mwenye mali alirudi ghafla, akauliza,
'Nyie mnafanya nini hapa?'
Masikini dalali kwa woga mkubwa akajibu' Tunangoja treni'