Jinsi ya kutengeneza biskuti za Matunda Makavu Na Cornflakes
Updated at: 2024-05-25 10:23:08 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga - 4 Vikombe
Sukari - 1 Kikombe
Baking powder 1 kijiko cha chai mfuto
Siagi - 454 gms
Mayai - 2
Matunda makavu (tende, zabibu, lozi) - 1 Kikombe
Vanilla - 2 Vijiko vya chai
Cornflakes - ½ kikombe
JINSI YA KUANDAA
Changanya sukari na siagi katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy) Tia yai moja moja huku unachanganya mpaka iwe laini kama sufi. (fluffy) Tia unga, baking powder, matunda makavu, changanya na mwiko. Chota mchanganyiko wa biskuti kwa mkono kama (kiasi cha kijiko kimoja cha supu) fanya duara na uchovye katika cornflakes iliyopondwa kwa mkono (crushed) Zipange katika treya ya kupikia na zipike (bake) katika moto wa 375°F kwa muda wa kiasi dakika 15 huku unazitazama tazama.
Updated at: 2024-05-25 10:23:07 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga 2 ½ gilasi
Sukari ¾ gilasi
Samli 1 gilasi
Mayai 2
Baking powder 2 kijiko vya chai
Vanilla 1 ½ kijiko cha chai
Maganda ya chungwa 1
MAPISHI
Tia kwenye machine ya kusagia (blender) mayai, sukari, vanilla, samli na maganda ya chungwa, saga vizuri. Tia unga kwenye bakuli pamoja na baking powder, mimina vitu ulivyosaga kwenye bakuli, changanya. Punguza unga uliochanganya kidogo weka pembeni. Unga uliobakia tia kwenya tray ya kuchomeya, utandaze vizuri, tia jam juu yake. Chukua la kukwaruzia carrot (grater) ukwaruze unga uliuopunguza juu ya jam. Choma kwa muda dakika 20 moto wa 180 C.
Acha ipowe kidogo, zikate vipande vya mraba (square) Tayari kwa kula.
Safisha samaki kisha mmarinate na tangawizi, kitunguu swaum, chumvi na limao kwa muda wa masaa mawili. Baada ya hapo menya viazi na uvikate vipande vidogo kisha vioshe na viweke kwenye sufuria yenye maji kiasi kwa ajili ya kuvichemsha. Viinjike jikoni na uviache vichemke kwa dakika 7. Vikisha chemka tia samaki, katia kitunguu,pilipili, chumvi, limao, vegetable oil na nyanya na uache supu ichemke mpaka samaki na viazi vitakapoiva. baada ya hapo supu itakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:41 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Maharage yaliyochemshwa kiasi Spinach zilizokatwa kiasi Vitunguu maji 2 Nyanya 1/2 kopo Swaum/Tangawizi 1 kijiko cha chakula Curry powder 1 kijiko cha chai Olive oil Chumvi
Matayarisho
Kaanga vitunguu vikianza kuwa vya brown tia tangawizi/swaum kisha nyanya. Pika mpaka nyanya ziive kisha tia curry powder na chumvi. Vipike kiasi kisha tia maharage na maji kidogo kisha funika na uache vichemke. Baada ya muda tia spinach vipike pamoja na maharage mpaka ziive kisha ziipue. Baada ya hapo mboga yako itakuwa tayari kwa kuseviwa.
Updated at: 2024-05-25 10:23:10 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Unga - 4 Vikombe vya chai Sukari ya laini (icing sugar) - 1 Kikombe cha chai Baking powder - 2 Vijiko vya chai Mayai - 2 Siagi au margarine - 1 Kikombe cha chai Vanilla -1 Kijiko cha chai Maziwa ya kuchanganyia - kiasi Tende iliyotolewa koko - 1 Kikombe ufuta (sasame) kiasi 1/4 kikombe
MAANDALIZI
Changanya unga, siagi, baking powder, na sukari katika mashine. Kisha tia mayai, vanilla na halafu maziwa kidogo kidogo hadi mchanganyiko ushikamane. Gawanya madonge mawili na usukume kama chapati, lakini sio nyembamba sana. Tandaza tende robo ya duara na unyunyize ufuta duara zima: kisha kunja hadi mwisho na ukate kate, kisha upange katika trei ya kuvumbika. Vumbika (bake) moto wa 350°F kwa muda wa dakika 20 au hadi vigeuke rangi na viwive. Zikisha iiva ziache zipowe na zitakuwa tayari kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:34:43 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Yai bichi linaweza kuwa na vijidudu viitwavyo kwa kitaalamu “SALMONELLA” vinavyoweza kusababisha tumbo kuuma, kichefuchefu na pia kuharisha. Vijidudu ya “Salmonella” vinaweza kusababisha madhara makubwa kwa watoto, wazee na wale wenye hali dhaifu ya kimwili kama wagonjwa wa UKIMWI.
Pia yai bichi lililowazi linaweza kuwa zalio zuri la vimelea vya maradhi mbalimbali. Inashauriwa kupika yai mpaka liive kabisa, na kuhakikisha kwamba hakuna ute unaoteleza.
Kama ni yai la kuchemsha, lichemshwe kwa dakika kumi zaidi baada ya maji kuchemka. Pia ni muhimu kuhakikisha kwamba vyombo vilivyotumika k u k o rogea yai bichi vinaoshwa kwa maji na sabuni kabla ya kuvitumia tena kwa matumizi mengine ili kuepuka maradhi.
Updated at: 2024-05-25 10:34:48 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Matunda ni mojawapo wa kundi la vyakula, ni muhimu sana kwa afya bora. Matunda yakitengenezwa vizuri yanavutia sana na yanakuwa ni chakula kizuri sana.
Mahitaji
Embe iliyoiva kiasi Nanasi Tango Tikiti maji Zabibu Papai
Matayarisho
1. Ondoa maganda kwenye embe, nanasi, tango, papai na tikiti maji kisha kata kata vipande vidogo vidogo vya mraba
2. Changanya vipande vya matunda kwenye bakuli safikisha weka na zabibu zilizotolewa kwenye kikonyo chake.
3. Weka kwenye friji yapate ubaridi kidogo
4. Saladi yako tayari kwa kuliwa
Waweza kula saladi hii kama mlo wa kati au kama mlo kamili wa usiku.
Mapishi ya Chai ya maziwa, mandazi, uyoga na mayai
Updated at: 2024-05-25 10:22:58 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mandazi (angalia jinsi ya kupika katika recipe ya mandazi ya nyuma) Uyoga (mashroom kikombe 1 cha chai) Mayai (eggs 4) Hoho (greenpepper 1/4 ya hoho) Nyanya (fresh tomato 1) Kitunguu (onion 1/4 ya kitunguu) Chumvi (salt) Mafuta (vegetable oil) Hiliki nzima (cardamon 4) Masala ya chai (tea masala 1 kijiko cha chai) Pilipili mtama iliyosagwa (ground black pepper 1/4 ya kijiko cha chai) Maziwa (fresh milk 1 kikombe cha chai) Majani ya chai (tea leaves) Maji kiasi. Sukari (sugar)
Matayarisho
Jinsi ya kupika chai, weka maziwa, maji kiasi,hiliki, masala ya chai, pilipili mtama na majani katika sufuria. Chemsha kwa muda wa dakika 10 na chai itakuwa tayari. Jinsi ya kupika mayai, weka mafuta kiasi katika fry pan na utie vitunguu, vikaange kidogo kisha tia nyanya, chumvi na hoho. Pika kwa muda wa dakika 4 kisha tia mayai na uyaache yaive mpaka yakauke kisha geuza upande wa pili na uyapike mpaka ya ive kisha ipua. Jinsi ya kupika uyoga, weka mafuta kidogo katika fry pan kisha tia uyoga na chumvi na ukaange mpaka uive katika moto wa wastani. Ukisha iva breakfast yako itakuwa teyari kwa kuseviwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:46 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Ndizi laini (Matoke 6) Viazi mbatata (potato 3) Samaki wabichi wa wastani ( Fresh tilapia 2) Kitunguu swaum (garlic 6 cloves) Tangawizi (fresh ground ginger vijiko 2 vya chai) Nyanya ya kopo (tin tomato 1/2 kopo) Vitunguu (onion 1) Pilipili (chilli 1 nzima) Chumvi (salt to your taste) Mafuta (vegetable oil) Limao (lemon 1/2) Curry powder (1/2 kijiko cha chai)
Matayarisho
Safisha samaki kisha wakate vipande vitatu. Wakaushe maji kisha wamarinate na kitunguu swaum,tangawizi, chumvi, na limao kwa muda wa masaa 2. baada ya hapo waoke kwenye oven kwa muda wa dakika 30. baada ya hapo andaa ndizi na viazi kwa kuzimenya na kuziosha kisha ziweke pembeni. Kisha katakata vitunguu maji, Tangawizi, vitunguu swaum na nyanya kisha vitie kwenye blenda na usage mpaka mchanganyiko usagike vizuri. Baada ya hapo tia mchanganyiko katika sufuria na ubandike jikoni, acha uchemke mpaka maji yote yakauke. Maji yakisha kauka punguza moto na utie mafuta, curry powder, pilipili na chumvi. Kaangiza mpaka mchanganyiko uive na baada ya hapo tia viazi na maji kiasi na uache viazi vichemke mpaka vikaribie kuiva kisha tia ndizi na samaki na ufunike. Pika mpaka ndizi na viazi viive. Baada ya hapo chakula kitakuwa tayari kwa kuseviwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:55 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Nyanya 1 kg Maji Iita ½ Chumvi kijiko kidogo 1 Sukari
Hatua
• Osha nyanya, katakata na chemsha na maji mpaka zilainike. • Chuja juisi. • Pima juisi - vikombe 2 vya juisi kwa kikombe 1 cha sukari, weka kwenya sufuria safi . • Ongeza chumvi, chemsha ukikoroga mpaka ichemke. • Mara ikichemka epua, pozesha na weak kwenya chombo safi kwa kunywa.