Updated at: 2024-05-25 10:34:46 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Wakati mwingine mtu unakuwa umechoka na usingependa kupoteza muda jikoni, so mlo wa chapchap unakuwa ni wazo zuri, Mlo huu ni rahisi kuuanda na hata haikuchukui zaidi ya dakika ishirini chakula kinakuwa tayari mezani.
Mahitaji
Salmon fillet 2 Potatao wedge kiasi Lettice kiasi Cherry tomato Limao 1 Swaum Chumvi Olive oil
Matayarisho
Mmarinate samaki na chumvi, swaum na nusu ya limao kisha muweke pembeni, baada ya hapo washa oven kisha tia potato wedge zikisha karibia kuiva anza kumpika samaki, tia mafuta kidogo sana kama kijiko kimoja cha chai hivi katika frypan isiyoshika chini yakisha pata moto kiasi muweke samaki wako (upande wenye ngozi chini kwanza) Mpike mpaka uone rangi ya kahawia kwa chini kisha mgeuze upande wa pili, uku samaki wako akiwa anaendelea kuiva, tayarisha salad yako kwa kusafisha lettice na nyanya kisha zichanganye pamoja kisha tengeneza salad dressing pembeni , kamua limao kisha tia olive oil na chumvi kidogo, Baada ya hapo samaki na potato wedge vitakuwa vimeiva, andaa mlo wako na utakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:34:38 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Viazi - 3lb
Nyama - 1lb
Kitunguu - 1
Nyanya - 2
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 kijiko cha chai
Manjano - ½ kijiko cha chai
Curry powder - ½ kijiko chai
Nyanya kopo - 1 kijiko cha chai
Pilipili ya unga - kiasi upendavyo
Chumvi - kiasi
Kidonge cha supu - 1
Tui la nazi - 1 kopoau zaidi
Mtindi ukipenda - 3 vijiko vya supu
Kotmiri - kiasi ya kupambia
Nazi ya unga - 4 vijiko vya supu
Mafuta - 2 vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Kata nyama vipande vipande kisha chemsha na chumvi mpaka iive. Menya maganda viazi na ukate slice kubwa weka pembeni Kata kata kitunguu kisha kaanga na mafuta mpaka vibadilike rangi Tia thomu, bizari ya manjano, pilipili ya unga, nyanya kopo Kata kata nyanya nzima vipande vidogo tia na kidonge cha supu. Kisha tia viazi, nyama na tui la nazi finika mpaka viazi viwive lakini visiwe vikavu. Tia mtindi na nazi ya unga kama vijiko 4 vya supu iache motoni kidogo kisha pakua, tupia kotmiri juu na itakuwa tayari kuliwa.
Mapishi ya Pilau Ya Nyama Ng'ombe Karoti Na Zabibu
Updated at: 2024-05-25 10:37:34 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo - Nyama
Nyama ng’ombe ya mifupa ilokatwa vipande - 1 kilo
Tangawizi na thomu (somu/garlic) ilosagwa - 2 vijiko vya supu
Bizari mchanganyiko/garama masala - 1 kijiko cha chai
Chumvi - Kiasi
Vipimo - Wali
Mchele - 4 glass
Mbatata/viazi menya katakata - 3 kubwa
Vitunguu katakata - 5
Kitunguu thomu kilosagwa (garlic/somu) - 1 kijiko cha supu
Hiliki ya unga - 1 kijiko cha chai
Bizari nzima ya pilau/cumin - 1 mti
Samli au mafuta - 2 Vijiko vya supu
Karoti zilokatwakatwa nyembamba - 6-7
Zabibu - Kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Katika sufuria weka mafuta kijiko kimoja cha supu tia nyama na viungo vyake. kaushe katika moto hadi ikaribie kukauka kisha tia maji kiasi cha kuivisha na kubakisha supu ya mchele. Katika sufuria ya kupikia weka samli au mafuta ishike moto. Tia mbatata/viazi kaanga, tia vitunguu kaanga kidogo. Tia kitunguu thomu, hiliki, bizari ya pilau endelea kukaanga hadi viwe rangi ya brown kidogo. Tia mchele kaanga kidogo, kisha mimina nyama na supu yake. Funika wali uwive. Weka kikaangio katika moto, tia samli kijiko kimoja kisha tia karoti na zabibu, kaanga kwa sekunde chache tu kwa ajili ya kulainisha karoti na zabibu. Utakapopakuwa wali, pambia juu karoti na zabibu.
Mapishi ya Haliym Ya Nyama Mbuzi -Bokoboko La Pakistan
Updated at: 2024-05-25 10:23:16 (2 years ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Nyama ya mbuzi au ng’ombe ya mafupa - 2 LB
Mchanganyiko wa dengu (hadesi, mchele, chooko, ngano, dengu n.k au nunua ya tayari iliyokwisha changanywa - 2 Vikombe
Kitungu maji (vikate vidogo) - 1
Mafuta - ¼ Kikombe
Nyana kata ndogo ndogo - 1
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawazi iliyosagwa - 1 Kijiko cha supu
Bizari ya haliym - 2 vijiko vya supu
Nyanya ya kopo - 2 vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Chemsha nyama na chumvi ½ kijiko mpaka iive, toa mafupa. Chemsha mchanganyiko wa dengu mpaka ziive. Katika sufuria weka mafuta, kaanga vitunguu vilainike, tia thomu na tangawizi, bizari ya haliym, nyanya ya kopo. Kaanga mpaka iwive. Tia nyama iliyowiva na supu yake kidogo. Tia mchanganyiko wa dengu tia kwenye mashine ya kusaga (blender), saga na ile supu ya nyama isagike vizuri Mimina kwenye sufuria changanya, tia ndimu kidogo, acha moto mdogo mdogo kwa muda wa dakika 15. Tia katika bakuli, pambia kwa vitunguu vilivyokaangwa vya rangi ya hudhurungi vikavu, pilipili mbichi (ukipenda) na kotmiri, ikiwa kuliwa.