Mapishi ya Pilau Ya Nyama ya Kusaga, Adesi Za Brauni Na Zabibu
Updated at: 2024-05-25 10:34:40 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele wa Par boiled au basmati - 5 vikombe
Nyama kondoo/mbuzi ya kusaga - 1 kikombe
Kitunguu - 2
Kitunguu saumu (thomu/galic) - 7 chembe
Adesi za brauni (brown lentils) - 1 kikombe
Zabibu - 1 kikombe
Baharaat/bizari mchanganyiko - 1 kijiko cha supu
Chumvi - kiasi
Pilipilii manga - ½ kijiko
Jiyra/bizari pilau/cummin - 1 kijiko cha chai
Supu ya nyama ng’ombe - Kiasi cha kufunikia mchele
Mafuta - ½ kikombe
Namna Ya Kutayarisha
Osha, roweka masaa 2 au zaidi.
Katakata (chopped)
Menya, saga, chuna
Osha, roweka, kisha chemsha ziive nusu kiini.
Osha, chuja maji
Namna Ya Kupika:
Tia mafuta katika sufuria, kaanga vitunguu hadi vianze kugeuka vyekundu. Tia kitunguu thomu, kaanga, tia baharati/bizari zote kaanga. Tia nyama uchanganye vizuri, ukaange iwive.. Tia mchele ukaange kidogo kisha tia supu, koroga kidogo, funika uivie mchele. Karibu na kuiva, tia adesi, zabibu, changanya, funika uendelee kuiva kama unavyopika pilau. Epua pakua katika chombo, ongezea zabibu kupambia ukipenda
Jinsi ya kutengeneza Slesi Za Chokoleti Na Karameli
Updated at: 2024-05-25 10:34:41 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga - 1 Magi (vikombe vya chai)
Sukari ya browni - ½ Magi
Siagi iliyoyayushwa - 125 g
Nazi iliyokunwa - ½ Magi
MJAZO WA KARMEL (Caramel filling)
Syrup - 1/3 kikombe cha chai
Siagi iliyoyayushwa - 125 g
Maziwa matamu ya mgando - 2 vikopo (condensed milk)
MJAZO WA CHOKOLETI (Chocolate filling)
Chokoleti - 185 g (dark chocolate)
Mafuta - 3 Vijiko vya chai
MAANDALIZI
Changanya unga, sukari, siagi na nazi iliyokunwa kwenye bakuli mpaka unga ushikamane. Paka mafuta treya ya kuchomea kisha utandaze kwenye treya ya 20cm kwa 30 cm au (8 in kwa 12 in) unaweza kuweka karatasi ya kuchomea chini ukipenda. Choma kwenye moto 325˚C kwa muda wa dakika 15 mpaka 18 au mpaka ibadilike kuwa rangi ya browni. Kwenye sufuria ndogo tia syrup siagi na maziwa matamu ya mgando na changanya kwa moto mdogo mpaka uwe mzito kasha mimina juu ya keki uliyochoma na choma tena kwa muda wa dakika 20 mpaka karameli iwe rangi ya dhahabu. Kwenye sufuria ndogo nyingine tia vipande vya chokoleti na mafuta na ukoroge kwa moto mdogo mpaka iyayuke kisha wacha ipoe kidogo mimina juu ya mjazo wa karameli kisha weka kwenye friji mpaka ishikamane. Kata vipande weka kwenye sahani tiyari kwa kuliwa
Tofauti kati ya yai la kuku wa kienyeji na la kuku wa kisasa
Updated at: 2024-05-25 10:34:45 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kilishe mayai yote ni sawa. Virutubishi vinavyopatikana kwenye yai la kuku wa kienyeji kama protini, vitamini A, madini ya chuma na virutubishi vya aina nyingine, ndivyo hivyo vinavyopatikana pia kwenye yai la kuku wa kisasa.
Tatizo linaweza kutokea pale ambapo wafugaji wa kuku wa kisasa hawafuati taratibu za ufugaji na pengine hawawapi kuku vyakula muhimu wanavyohitaji au wanawapa dawa na vyakula visivyo bora kiafya, hivyo wakati mwingine kiini cha yai la kuku wa kisasa huonekana kupungua rangi ya njano kuliko kiini cha yai la kuku wa kienyeji.
Mtu anashauriwa kula yai bila kujali ni la kuku gani, kwa kutegemea ni yai lipi linapatikana kwa urahisi. Lakini nivizuri kula mayai ambayo yapo salama.
Updated at: 2024-05-25 10:23:12 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo
Wali:
Mchele - 3 Vikombe
Kitunguu kiichokatwa - 1
Pilipili boga nyekundu iliyokatwa vipande - 1
Mafuta - ¼ Kikombe
Zaafarani - 1 kijiko cha chai tia kwenye kikombe na maji robo roweka
Chumvi - 1 kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Katika sufuria, tia mafuta, kaanga kitunguu mpaka kiwe kidogo rangu ya udongo (brown) Tia pili pili boga. Tia mchele, kaanga kwa muda wa dakika 3, tia zaafarani na chumvi. Tia supu uliyochemshia kuku iwe imoto. Pika wali katika moto mdogo hadi uwive.
Kuku
Kuku Mzima -1
Mayai ya kuchemsha - 6
Namna Ya Kupika Kuku
Mchemshe kuku mzima na chumvi mpaka uhakikishe ameiva vizuri. Mtowe na muweke pembeni. Supu yake tumia katika wali kama ilivyo hapo juuu. Chemsha mayai, menya na kata vipande viwili kila yai moja weka kando
Vipimo Vya Sosi Ya Kuku Ya Nazi
Kitunguu - 1
Nyanya iliyokatwa vipande - 1
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi - 1 kijiko cha supu
Garam Masala - ½ kijiko cha supu
Bizari ya manjano - ½ kijiko cha chai
Chumvi - kiasi
Pilipili masala ya unga - ½ kijiko cha chai
Nyanya ya kopo - 1 kijiko cha supu
Nazi ya unga - 1 kikombe
Maji ya ukwaju - ¼ kikombe cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Tia Mafuta vijiko 2 vya supu katika sufuria Kaanga kitunguu maji mpaka kiwe rangi ya udongo (brown). Tia thomu na tangawizi. Tia nyanya nzima iliyokatwa katwa. Tia garam masala, manjano, pilipili ya unga, nyanya ya kopo, kaanga vizuri. Changanya kwenye sufuria na ukwaju. Iache ichemke vizuri. Changanya nazi ya unga na maji vikombe viwili. Mtie kuku mpike vizuri na hilo tui. Mtie kwenye oveni kidogo.
Kupakuwa katika Sinia
Pakuwa wali kwanza katika sinia Muweke kuku juu ya wali. Pambia mayai
Updated at: 2024-05-25 10:34:44 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Blue band vijiko vikubwa 2 Maziwa vikombe 2 Royco kijiko kikubwa 1-2 Pilipili manga (unga) kijiko cha 1 Chumvi kiasi Maji lita 2-3 Boga kipande ½ Viazi mviringo 2 Vitunguu 2 Karoti 2 Nyanya 2
Hatua
• Menya boga, viazi, karoti, nyanya na kwaruza weka kwenya sufuria kubwa. • Menya, osha na katakata vitunguu kisha ongeza kwenye mboga. • Ongeza maji na chumvi chemshwa mpaka vilainike. • Pekecha ikiwa jikoni na moto kidogo • Ongeza blue band, maziwa royco na pilipili manga ukikoroga kwa dakika 5. • Onja chumvi na pakua kama supu. Uwezekano Tumia siagi badala ya margarine.
Updated at: 2024-05-25 10:22:57 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga wa ulezi (millet flour vijiko 3 vya chakula) Maziwa fresh (milk 1/2 kikombe) Sukari (sugar 1/4 ya kikombe cha chai) Siagi (butter kijiko 1 cha chakula) Maji (vikombe 4 vya chai) (serving ya watu wawili)
Matayarisho
Chemsha maji ya uji, Kisha koroga unga na maji ya baridi kiasi na uchanganye kwenye maji ya moto yanayochemka. Endelea kukoroga mpaka uchemke ili kuhakikisha uji haupatwi na madonge. Ukishachemka tia, maziwa, sukari na butter. Kisha acha uchemke kwa muda wa dakika 10 na hapo uji utakuwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:34:54 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Unga 2 Magi (kikombe kibuwa cha chai)
Sukari 1/3 Kikombe cha chai Mayai 5
Siagi 4 Vijiko vya chakula
Hamira 1 Kijiko cha chakula
Baking Powder 1 Kijiko cha chai
Vanilla 1 Kijiko cha chai
Hiliki zilizosagwa 1 Kijiko cha chai
Sukari ya laini ya unga
(icing sugar) 1 Magi
Jinsi ya kuandaa na kupika
Unavunja mayai, unatia sukari, hamira, baking powder, vanilla na hiliki ikisha unapiga kwa kutumia mchapo wa kupigia keki. Unapiga mchanganyiko kwa muda wa dakika tano.
Unatia siagi kwenye sufuria na unaiyayusha na kuipasha moto mpaka iwe moto ikisha unaimimina kwenye mchanganyiko na unapiga tena kwa dakika mbili tu.
Unatia unga kwenye sinia au bakuli kubwa ikisha unamimina ule mchanganyiko kwenye unga na unaukanda kutumia mkono, mpaka ulainike.
Ukiona unga mwingi basi ongeza maziwa kidogo mpaka uwe sawa, na ukiona unga mwepesi sana basi unaweza kuongeza unga kidogo pia mpaka ukae sawa mfano wa unga wa maandazi.
Sukuma na ukate madonge kama unavyoyaona hapo juu. Tumia kifuniko cha chupa kwa kukatia kiduara kidogo katikakti ya madonge. Ukimaliza kukata madonge yote, yaweke kidogo yavimbe halafu teleka mafuta na uyachome. Ukitoa kwenye mafuta yachuje moto na kabla ya kupoa yawe moto moto yarovye kwenye icing sugar na uhakikishe yote yameenea sukari juu. Ukimaliza tia kwenye sahani acha zipowe na zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Jinsi ya kupika Cookies Za Jam Ya Peach Na Raspberry
Updated at: 2024-05-25 10:34:43 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Unga kikombe 1 ½
Siagi ½ kikombe
Sukari ½ kikombe
Yai 1
Vanilla 1 kijiko cha chai
Jam ya peach na raspberry
MAANDALIZI
Wash oven moto wa takriban 180 – 190 Deg F Piga siagi na sukari katika mashine mpaka iwe laini na nyororo (creamy) kisha weka yai na vanilla. Tia unga kidogo kidogo uchanganye kwa mwiko wa mbao (wooden spoon). Pakaza mkononi unga uchukue vidonge ubonyeze kufanya vishimo vya kuwekea jam. Panga katika treya uliyopakaza siagi. Tia nusu yake jam ya peach na nusu jam ya raspberry Bake katika oven kiasi robo saa mpaka ziwive na kugeuka rangi ya brown light. Epua vikiwa tayari
Updated at: 2024-05-25 10:23:00 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga wa ngano ( self risen flour) kikombe 1 na 1/2 Hamira (yeast) 1 kijiko cha chai Sukari (sugar) 1 kijiko cha chakula Chumvi (salt) 1/2 kijiko cha chai Siagi iliyoyeyushwa (melted butter) 1 kijiko cha chakula Maji ya uvuguvugu ( warm water) kiasi
Matayarisho
Changanya vitu vyote katika bakuli kubwa kisha aanza kukanda mpaka upate donge laini.Baada ya hapo liweke hilo donge kwenye bakuli la plastic na weke katika sehemu yenye joto ili unga uumuke. Hakikisha unga unaumuka zaidi (yani unaji double size) unaweza kuchukua kama saa 1 na nusu hivi. Baada ya hapo ukande tena na uache uumuke tena kwa mara ya pili, Ukisha umuka pakaza butter katika baking tin (chombo cha kuokea) na upakaze mkate butter kwa juu,kisha uoke katika oven kwa muda wa dakika 30 (katika moto wa 200C) (hakikisha juu na chini unakuwa wa brown Na hapo mkate wako utakuwa tayari