Updated at: 2024-05-25 10:34:45 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Tambi za mayai ni moja kati ya vyakula ambavyo napenda kuandaa pale ninapokua ninaharaka au sina muda mrefu wakukaa jikoni.pishi hili huchukuca muda mfupi sana na nimlo uliokamilika.
Mahitaji
Tambi ½ paketi
Vitunguu maji 2 vikubwa
Karoti 1
Hoho 1
Vitunguu swaumu(kata vipande vidogo) kijiko 1 cha chakula
Carry powder kijiko 1 cha chai
Njegere zilizochemshwa ½ kikombe
Mafuta kwa kiasi upendacho
Mayai 2
Chumvi kwa ladha upendayo
Njia
1.Chemsha maji yamoto yanayotokota,ongeza chumvi na mafuta kidogo,weka tambi kwenye maji hayo chemsha adi ziive.Chuja maji yote ili kupata tambi kavu 2.Katika bakuli piga mayai kisha weka pembeni 3.Katika kikaango,weka mafuta,vitunguu maji ,vitunguu swaumu,hoho, karoti na carry powder,kaanga kwa pamoja katika moto mdogo kwa muda mfupi kwani mboga hazitakiwi kuiva. 4.Ongeza tambi na njegere katika kikaango,geuza kila mara ili kuchanganya . 5.Ongeza mayai kwenye tambi kisha geuza kwa haraka bila kupumzika adi mayai yaive na tambi ziwe kavu.Tayari kwa kula
Katika hatua hii ongeza moto uwe wa wastani,moto ukiwa mdogo mayai yatafanya tambi zishikane na kufanya mabonge.
Updated at: 2024-05-25 10:35:26 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIPIMO
Unga wa mchele 500g
Samli 250g
Sukari 250g
Hiliki iliyosagwa 1/2 kijiko cha chai
Arki (rose flavour) 1/2 kijiko cha chai
Baking powder 1 kijiko cha chai
Mayai 4
Maji ya baridi 1/2 kikombe cha chai
NAMNA YA KUTAYRISHA NA KUPIKA
1. Saga sukari iwe laini kiasi, changanya unga wa mchele, baking powder, hiliki na sukari.
2. Pasha moto samli mpaka iwe nyepesi kama maji mimina kwenye ule mchanganyiko wa unga wa mchele, kisha uchanganye pamoja na arki.
3. Ongeza mayai yaliopigwa endelea kuchanganya mpaka unga umeanza kuchanganyika vizuri.
4. Ongeza maji ya baridi sana kama nusu kikombe tu ili uchanganyike vizuri.
5. Kata kwa design unayotaka viwe vinene visiwe kama cookies za kawaida kama ilivyo kwenye picha na ukipenda utaweka kidoto kwa kutumia zaafarani katikati ya kileja kama inavyoonesha hapo juu.
6. Choma kwa moto wa baina ya 300F na 350F kwa dakika 15 mpaka 20 visiwe vyekundu toa na tayari kwa kuliwa
Updated at: 2024-05-25 10:23:02 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga wa ngano (plain flour) 1/4 Kitunguu kikubwa (chopped/slice onion) 1 Yai (egg) 1 Chumvi (salt) Mafuta (cooking oil)
Matayarisho
Tia unga, chumvi na maji kiasi katika bakuli kisha koroga mpaka madonge yote yaondoke. Baada ya hapo tia yai na vitunguu kisha koroga tena mpaka mchanganyiko wote uchanganyike vizuri. baada ya hapo choma chapati zako kama kawaida (jinsi ya kuchoma unaweza kuangalia kwenye recipe yangu ya chapati za maji katika older posts) na baada ya hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:34:51 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Unga 1 Magi (vikombe vya chai)
Sukari ya browni ½ Magi
Siagi iliyoyayushwa 125 g
Nazi iliyokunwa ½ Magi
Mjazo wa karameli (Caramel filling)
Syrup 1/3 kikombe cha chai
Siagi iliyoyayushwa 125 g
Maziwa matamu ya mgando 2 vikopo (condensed milk)
Mjazo wa chokoleti (Chocolate filling)
Chokoleti 185 g (dark chocolate)
Mafuta 3 Vijiko vya chai
Jinsi ya kuandaa na kupika
1. Changanya unga, sukari, siagi na nazi iliyokunwa kwenye bakuli mpaka unga ushikamane.
2. Paka mafuta treya ya kuchomea kisha utandaze kwenye treya ya 20cm kwa 30 cm au (8 in kwa 12 in) unaweza kuweka karatasi ya kuchomea chini ukipenda.
3. Choma kwenye moto 325˚C kwa muda wa dakika 15 mpaka 18 au mpaka ibadilike kuwa rangi ya browni.
4. Kwenye sufuria ndogo tia syrup siagi na maziwa matamu ya mgando na changanya kwa moto mdogo mpaka uwe mzito kasha mimina juu ya keki uliyochoma na choma tena kwa muda wa dakika 20 mpaka karameli iwe rangi ya dhahabu.
5. Kwenye sufuria ndogo nyingine tia vipande vya chokoleti na mafuta na ukoroge kwa moto mdogo mpaka iyayuke kisha wacha ipoe kidogo mimina juu ya mjazo wa karameli kisha weka kwenye friji mpaka ishikamane.
6. Kata vipande weka kwenye sahani tiyari kwa kuliwa
Updated at: 2024-05-25 10:37:41 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Maharage yaliyochemshwa kiasi Spinach zilizokatwa kiasi Vitunguu maji 2 Nyanya 1/2 kopo Swaum/Tangawizi 1 kijiko cha chakula Curry powder 1 kijiko cha chai Olive oil Chumvi
Matayarisho
Kaanga vitunguu vikianza kuwa vya brown tia tangawizi/swaum kisha nyanya. Pika mpaka nyanya ziive kisha tia curry powder na chumvi. Vipike kiasi kisha tia maharage na maji kidogo kisha funika na uache vichemke. Baada ya muda tia spinach vipike pamoja na maharage mpaka ziive kisha ziipue. Baada ya hapo mboga yako itakuwa tayari kwa kuseviwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:40 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga wa ngano (self risen flour 2 vikombe vya chai) Hamira (yeast kijiko 1 cha chai) Sukari (sugar 2 vikombe vya chai) Hiliki (cardamon 1/4 ya kijiko cha chai) Maji kikombe1 na 1/2 Mafuta
Matayarisho
Changanya unga, hamira, maji na mafuta kijiko 1. Koroga vizuri mpaka upate uji mzito usiokuwa na madoge Baada ya hapo uache uumuke kisha zichome kalmati katika moto wa wastani. Baada ya hapo tia sukari, hiliki na maji 1/2 kikombe katika sufuria na ichemshe uku unakoroga mpaka iwe tayari.(ukitaka kujua kama iko tayari chovya mwiko kisha gusa na vidole utaona iko kama nta au gundi) Baada ya hapo tia kalmati na uzichange pamoja mpaka zikolee kisha zitoe na uziache mpaka zipoe tayari kwa kuliwa.
Jinsi ya kupika Pilau ya Mpunga Na Nyama Ya Ng’ombe
Updated at: 2024-05-25 10:23:15 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mpunga - 4 vikombe
Nyama - 1 kilo moja
Kitunguu maji - 3
Mbatata/viazi - 7 vidogodogo
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi ilosagwa 3 vijiko cha supu
Bizari nzima/ya pilau/uzile/cumin - 3 vijiko vya supu
Mdalasini - 3 vipande
Hiliki - 7 punje
Pilipili manga nzima - 1 kijiko cha supu
Chumvi kiasi
Mafuta - ½ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Osha mchele weka kando Katakataka vitunguu slice ndogo ndogo. Weka mafuta katika sufuria kisha ukaange vitunguu pamoja na mdalasini, hiliki pilipilimanga. Vitunguu vikigeuka rangi unatia kitunguu thomu na tangawizi. Tia supu kidogo na nyama, kisha tia bizari ya pilau/uzile, na viazi/mbatata. Maliza kutia supu yote, na ikiwa ni kidogo ongeze maji kiasi cha kuivisha mchele. kisha tia mchele ufunike hadi wali uwe tayari. Ikiwa unatumia mkaa palia juu yake, ikiwa hutumii uache uive kwa moto mdogo mdogo.
Menya viazi na kisha vikate katika vipande. Tia mafuta kwenye chuma cha kukaangia, yakisha pata moto tia viazi nauviache vikaangike mpaka upande mmoja uwe wa brown na kisha geuza upande wa pili na upike mpaka uwe wa brown. Vikisha iva ipua na uweke kwenye kitchen towel ili vikauke mafuta. Kachumbali: Katakata vitunguu katika bakuli na kisha tia chumvi kwa ajili ya kuondoa ukali wa vitunguu. Baada ya hapo vioshe mpaka chumvi yote iishe. osha nyanya, Pilipili tango na kisha katakata slice nyembamba na uchanganye na vitunguu. Baada ya hapo tia chumvi, kamulia limao na uchanganye zote pamoja .Baada ya hapo viazi na kachumbali vitakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:34:42 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Maziwa mazito matamu (condensed milk) - 2 vibati
Sukari - 1 kikombe
Samli 1 ½ kikombe
Vanilla 2 kifuniko cha chupa yake
Hiliki ilosagwa - 2 vijiko vya chai
Sinia kubwa ya bati Paka samli
MAANDALIZI
Changanya maziwa, sukari na samli katika sufuria isiyogandisha chakula (non-stick) uweke katika moto. Koroga huku ikipikika hadi ianze kugeuka rangi na kuanza kuachana. Usiache mkono kuroga isije kufanya madonge. Tia hiliki na vanilla, endelea kuipika. Itakapogeuka rangi vizuri mimina katika sinia na haraka uitandaze kwa mwiko huku ukiuchovya katika maji na kuendelea kuitandaza hadi ikae sawa kote. Pitisha kisu kuikataka ili ikipoa iwe wepesi kuitoa vipande.
Kila inapozidi kupoa na kukaa ndipo fagi inakauka na kumumunyuka.